SoC04 Uanzishwaji wa Vituo vya kudumu kukabiliana na Maafa katika jamii

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jerry Farms

Member
Jul 18, 2022
59
41
Miaka ya karibuni na hadi sasa Tanzania na dunia kwa ujumla imekua ikikumbwa na majanga mbalimbali yakiwemo mafuriko, matetemeko, milipuko ya magonjwa, moto, vimbuga na maporomoko ya udongo. Matukio haya yamechagizwa kwa kiwango kikubwa na mabadiriko ya tabia nnchi.

Majanga haya punde yanapotokea huja na athari za vifo, uharibifu wa mali na miundombinu, kuharibu uchumi na mazingira. Mfano wa majanga haya ni janga la moto Morogoro 2019, maporomoko ya udongo Katesh, Manyara 2023 ambapo kaya zaidi ya 1000 ziliathirika na vifo zaidi ya 60 kuripotiwa, mlipuko wa kipindupindu mnamo mwezi Januari 2024 katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera, na Dar es salaam. Mvua za elnino zilizopelekea mafuriko, Pwani na Morogoro zikiathirika pakubwa kwa kaya 10839 kuharibiwa na vifo 58( M Matinyi,mkurugenzi Idara ya habari na msemaji wa serikali,14 April 2024). Maeneo mengine yaliyoathiriwa na mvua kubwa ni Geita, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Kigoma, Shinyanga , Dar, Iringa, Tabora, Dodoma, Lindi, Mtwara, Songwe ,Kagera na Rukwa.
Picha ya athari ya mafuriko yaliyotokea 2024.
IMG_20240524_133108.jpg

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Serikali imekua ikichukua hatua mbalimbali kukabiliana na maafa zikijumlisha; uanzishwaji wa kitengo cha maafa, utoaji wa mafunzo ya utayari, ukarabati wa miundombinu, utoaji misaada na kambi za muda za wahanga. Pamoja na jitihada hizi, taifa halina budi kujijengea uwezo zaidi wa kukabiliana na majanga na athari zake hivyo mpango mkakati wa uanzishwaji wa vituo vya kudumu vya maafa kwa ajili ya kutoa huduma za kidhalura baada ya maafa kutokea.

Hali ilivyo sasa katika kukabiliana na maafa.
Punde majanga yanapotokea serikali imekua ikilazimika kutumia njia zifuatazo kukabiliana nayo.
•Kupeleka misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathirika moja kwa moja.
•Matumizi ya maeneo ya umma mfano shule na hospitali kwa muda maalumu.
•Uanzishwaji wa kambi za muda kubeba wahanga.

Njia hizi kwa kiasi zinasaidia pindi cha dharula lakini sio njia bora ya kushughulikia na maafa. Matumizi ya njia hizi yana mapungufu yafuatayo;

•Kupunguza ufanisi wa huduma zilizokua zikitolewa kabla ya maafa. Mfano uanzishwaji wa kambi ya wahanga shuleni huzuia utolewaji wa huduma ya elimu katika eneo, huduma husitishwa kwa muda kupisha kambi.

•Msogamano na usumbufu katika utolewaji wa huduma za kijamii. Mara nyingine panapotokea mlipuko wa magonjwa hospitali hulazimika kuondoa wagonjwa wa kawaida na kupisha kwa muda aghalabu kipindi cha kipindupindu.

•Unzishwaji wa kambi za muda huisababishia gharama za mara kwa mara serikali ikiambatana na ufanisi mdogo katika utolewaji wa huduma kutokana na ukosefu wa bajeti na miundombinu hafifu katika makambi.

•Kutweza utu wa waathiriwa.
Waathiriwa wanamahitaji tofauti tofauti, mjumuisho wa wanaume na wanawake eneo moja lenye miundombinu michache huumiza hisia za waathiriwa.

•Hatari ya kukuza tatizo na uharibifu wa mazingira.
Matumizi ya shule kama kituo cha kuhifadhia waathiriwa si salama sana, kwani shule zetu zimejengwa zikiwa na miundombinu ya kukidhi idadi maalumu. Matharani shule yenye matundu 15 ya choo haiwezi kutimiza mahitaji ya wahanga mamia walioweka kambi shuleni hivyo hatari ya magonjwa na uharibifu wa mazingira.
Kwa kuzingatia methali ya "Ng'ombe hanenepi siku ya mnada" kwa maana ya 'ng'ombe'= mtoa huduma ya dharula+ uwezo wake+ huduma atoayo huku 'mnada'= janga.

Kambi ya muda inayoanzishwa wakati wa maafa haiwezi kuwa na miundombinu toshelezi ndani ya muda mfupi toka janga litokee hivyo utolewaji wa huduma chini ya viwango. Majanga huja pasi na taarifa hivyo maandalizi kabla ya janga ni bora zaidi. Serikali haina budi kuanzisha vituo vya kudumu katika halmashauri zake, vituo hivi vitakua na miundombinu toshelezi hivyo kuweza kustahimili matokeo ya janga( athari) na kubeba idadi kubwa ya waathiriwa.

Uanzishwaji wa vituo hivi ufanywe awamu kwa awamu kwa kufuata hatua zifuatazo:
•Utafiti kuchunguza historia ya maeneo na kukusanya taarifa za kitwakimu ya idadi ya majanga katika eneo husika.

•Utengaji wa maeneo maalumu kwa kuzingatia vigezo vya kiafya,gharama na vigezo vya kimazingira.

•Ujenzi wa vituo na miundombinu

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wafanye hima kuanzisha ujenzi wa vituo vya kudumu na miundombinu wezeshi katika vituo hivyo.

Matumizi ya vituo
Vituo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa tu.

Angalizo: Vituo hivi visigeuke kuwa makazi ya kudumu, serikali ipange utatatibu maalumu wa matumizi ya vituo hivi. Waathiriwa wa majanga wapatiwe taratibu za vituo ilinkuepusha sintofahamu.
Faida za uwepo wa vituo vya dharula vya kudumu.
Unzishaji wa vituo vya kudumu vya kukabiliana na maafa una manufaa mengi ikiwemo; •Utunzaji mazingira.
•Utolewaji wa huduma toshelevu pindi cha dharula na kupunguza gharama za mara kwa mara.
 Hitimisho
Serikali iandae mpango mkakati wa uanzishwaji wa vituo hivi katika halmashauri zake kwa kuangalia hali ya utokeaji wa majanga katika eneo husika.​
 
•Utafiti kuchunguza historia ya maeneo na kukusanya taarifa za kitwakimu ya idadi ya majanga katika eneo husika.
Sawa sawia. Tena utafiti uende mbali zaidi na kuyafanyia kazi yatakayogundulika kuwa ni chanzo cha maafa hayo. Kama ni kujenga mabwawa, kuhamisha watu na kusambaza maji safi basi hilo lifanyike. Tuwe na miundimbinu yenye utayari.

Yaani kimsingi tusisitize kuwepo na 'resilience' katika majanga ambayo hatujaweza kuwa na 'resistance' nayo.

..."Vituo vitumike kwa malengo yaliyokusudiwa tu.

Angalizo: Vituo hivi visigeuke kuwa makazi ya kudumu, serikali ipange utaratibu maalumu wa matumizi ya vituo hivi. Waathiriwa wa majanga wapatiwe taratibu za vituo ili kuepusha sintofahamu."....

Ndugu, unapendekeza kujengwe majengo yasiyokaliwa na watu kipindi choote hadi kutokee majanga tu🤯.

Ni kwa nini tusitafutie matumizi tunayohitaji sasa na inapotokea majanga basi wahanga watatumia hayo. Mfano:

1. Hiyo ya mashule ambayo umeikataza

2. Kuboresha maeneo ya wazi, masoko, au maeneo ya mikutano nk. Ili yaweze kubeba hema za dharula pindi janga linapotokea. Au yawe katika mfumo/muundo yanaweza kubadilishiwa matumizi fasta kwa dharula.

Kwa kweli suala la kuwepo majumba yasiyokaliwa na watu, wakati ambapo wapo watu wasio na nyumba hata sasa ni matumizi.... yaani tunafanyeje matumizi ya ziada wakati ambapo matumizi ya msingi hatujakamilisha!???
 
Kutumia shule kama mbadala kipind cha makazi!huko n kuingilia matumizi. Watoto wataaitishiwa masomo na hivyo ama wasimalize mtaala kwa wakati na mitihan ya kitaifa iko pale pale! Yaan tuzingatie matumizi.
 
Back
Top Bottom