๐—ง๐—ญ ๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐—ผ ๐—ป๐—ฐ๐—ต๐—ถ ๐—ฝ๐—ฒ๐—ธ๐—ฒ๐—ฒ ๐—ถ๐—น๐—ถ๐˜†๐—ผ๐˜„๐—ฎ๐˜๐˜„๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—ธ๐—ผ๐—ฑ๐—ถ ๐—ธ๐˜‚๐—ฏ๐˜„๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ฐ๐—ต๐—ถ ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฒ ๐˜‚๐—ธ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ๐—ฎ ๐—ต๐˜‚๐˜‚ ๐˜„๐—ฎ ๐—˜๐—” ๐—ป๐—ฎ ๐—ฆ๐—”๐——๐—–

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
66
1,259
Jana niliandika katika mtandao wa X ambao zamani ulikuwa ukiitwa Twitter kuhusu kodi kubwa 150% zinazotozwa na serikali ya Samia Suluhu unapoagiza gari nje. Kuna watu waliibuka na kusema kodi kubwa inasababishwa na umri wa gari linalozidi miaka 10. Kwamba ukiagiza gari ambalo ni chini ya miaka 10 kodi yake inakuwa kidogo.

Baada ya kuibuka hoja hiyo kwamba gari nililokuwa nimeliweka katika bandiko hilo kodi yake ilikuwa kubwa kutokana na umri wake kuzidi miaka 10, niliamua kutafuta gari aina hiyohiyo ambayo bado halijafikisha umri wa miaka 10 tangu litoke kiwandani. Kumbuka kwamba gari nililoliweka katika bandiko hilo ni la mwaka 2010 na lilikuwa linauzwa pesa za madafu milion 6 kwa Ulaya lakini likifika Tanzania serikali ya Samia inatoza kodi milion 16 kwenye gari hilo ulilonunua milion 6 Ulaya.

Gari hilohilo toleo la 2015 ambalo liko chini ya miaka 10 linauzwa milion 23 na kodi yake ni milion 25. Yani bado kodi ni kubwa kuliko bei uliyonunua gari huko Ulaya pamoja na kwamba lipo chini ya umri wa miaka 10. Wakati nchi za jirani zote kodi ya vyombo vya moto ikiwemo magari wanatoza 15% mpaka 20% tu ya bei uliyonunulia gari huko Ulaya, Bongo serikali ya Samia inatoza 100% mpaka 200% mara mbili mpaka mara tatu ya gharama ulizonunulia hilo gari.

Kwa bahati mbaya pamoja na maumivu haya ya kodi pesa hizi zinaishia kuibiwa na kutapanywa hovyo na hakuna anayewajibika. Nchi hii tusipochukua hatua za haraka na lazima wananchi watakuwa na maisha magumu kuliko hata wasomali. Sijapata kuona nchi ambayo ina viongozi wenye viburi na wanaopenda kuabudiwa kama hawa wa TZ. Wananchi tunahitaji kuunganisha nguvu tukomeshe kiburi na ujambazi huu wa kodi kubwa kwenye bidhaa mbalimbali pamoja na wizi wa pesa na mali za Umma.

Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

Screenshot_20240505-121159_1.jpg
20240505_120847.jpg
 
Kodi huwa ni asilimia ndogo ya gharama. Sasa kuweka kodi sawa na gharama au zaidi ya gharama aiseee ni jambo la ajabu sana.
 
View attachment 2981265View attachment 2981266
"Any government is an organ of exploitation by nature."

Mikhail Bukhanin
 
Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono mwehu Mdude. Kumiliki gari Tanzania ni jambo zito mno. Serikali inakosea sana.
 
Mm na ushamba wangu nilitamani kigari nikawa naangalua google huko japan kanauzwa dolla 1500 kaliko bora zaidi mpaka dora buku 2 nikajiuliza kwa nn sasa gari inaubzwa dola 2000 lakini huku inafika unauzwa million 14 nikachoka nimebaka na boxer yangu acha mvua ininyeshee
 
Kuna watu waliibuka na kusema kodi kubwa inasababishwa na umri wa gari linalozidi miaka 10. Kwamba ukiagaza gari ambalo ni chini ya miaka 10 kodi yake inakuwa kidogo.

Kumbuka kwamba gari nililoliweka katika bandiko hilo ni la mwaka 2010 na lilikuwa linauzwa pesa za madafu milion 6 kwa Ulaya lakini likifika Tanzania serikali ya Samia inatoza kodi milion 16 kwenye gari hilo ulilonunua milion 6 Ulaya.

Gari hilohilo toleo la 2015 ambalo liko chini ya miaka 10 linauzwa milion 23 na kodi yake ni milion 25. Yani bado kodi ni kubwa kuliko bei uliyonunua gari huko Ulaya pamoja na kwamba lipo chini ya umri wa miaka 10. Wakati nchi za jirani zote kodi ya vyombo vya moto ikiwemo magari wanatoza 15% mpaka 20% tu ya bei uliyonulia gari huko Ulaya, Bongo serikali ya Samia inatoza 100% mpaka 200% mara mbili mpaka mara tatu ya gharama ulizonunulia hilo gari.

Kwa bahati mbaya pamoja na maumivu haya ya kodi pesa hizi zinaishia kuibiwa na kutapanywa hovyo na hakuna anayewajibika.

Mdude Mpaluka Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

View attachment 2981265View attachment 2981266
Zinatuumiza. Ila zinafanana kwa Afrika ya Mashariki. Zinapaswa zishushwe. Kule kwa ndugu zetu Ethiopia, huko ndio huwezi kabisa kununua gari kwa sababu ya ushuru mkuuubwa sana.
 
Wanataka tusiagize magari tuwe tunaendesha maskeli na pkpki...

Kuna muda najiuliza hv kweli hakuna njia za panya za kuingiza gari nchini bila haya makodi...!!?
 
Back
Top Bottom