johnsonmgaya
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 2,818
- 3,727
Nipo zangu feri kwenye kivuko cha Magogoni narudi nyumbani saa 7 mchana huu.
Kichwa hakiko Sawa maana “mchongo” niliofata town umebuma hivyo nikajiwazia zangu heri nirudi mapema nikacheze na watoto wangu tu atleast.
Mar pah macho yangu yanavutwa kutazama kundi la wauza madafu wengi wakiwa wamepaki baiskeli zao wakipiga story, kiukweli wanafuraha pengine kuliko mimi kwa siku ya leo
Nilichovutiwa zaidi ni kuwaona wakiwa na mabaki ya madafu mzigo wote waliopandisha nao town kwa siku ya leo wameshaumaliza na ndio kwanzaaa saa 7.
Sijawahi wahi vuka hapa muda kama huu pengine ndio maana nimejikuta nawashangaa hawa ndugu zangu leo pengine ndio maisha yao ya kila siku pengine saa 7 tu hivi wanakuwaga watamu wamemaliza Mali.
Swali nililo nalo hapa kichwani pengine nimesukumwa tu na wivu wangu kwao
Je, hawa jamaa wanaingiza bei gani?
Je, wanabeba madafu mengi kiasi gani?
Nafahamu bei moja ya Dafu mjini ni shilling 1000 tukijua kwa siku wanabeba madafu mangapi kwenye vikapu vyao tutajua wanajngiza kiasi gani kwa masaa 7 (sio siku)
Mwisho:
Vijana tuache ubishoo na upumbavu wa heri uwe chawa wa fulani wakati kuna kazi kama hizi fasta tu ukipiga au ukiwekeza ndani ya masaa yako 7 hukosi 50,000/- ya kuchagua na wewe chawa unaowataka.