SoC04 Tusijaze maji ya mkopo kwenye mtungi unaovuja tukitegemea mtungi utajaa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Genius Man

Member
Apr 7, 2024
27
25
Hivi umeshawai kujaribu au kuona nini kinachotokea baada yakujaribu kujaza maji kwenye mtungi unaovuja, kwa hakika kitakachotokea ni kwamba maji yatakuwa yanaingia tu kwenye mtungi kisha yana penya pale panapo vuja na kumwagika nje ya mtungi, alafu baada ya hapo mtungi unabakiwa mkavu, inamaana maji yalikuwa yanajazwa tu bure kwenye mtungi, alafu ukute hapo labda maji yenyewe yalikuwa ya mkopo wala siyo yako hapo lazima hilo litakuwa ni tatizo kubwa sana. Kwa kweli kujaza maji ya mkopo kwenye mtungi unaovuja nisawa na kujiingiza kwenye matatizo na kupoteza tu nguvu zako bure. Lakini pamoja na hayo hivi unajua kuwa hata Tanzania kwasasa ni kama vile inafanya kujaza maji ya mkopo kwenye mtungi unaovuja.

Kwa hakika kwa sasa Tanzania, nikama vile tunajaza maji ya mkopo kwenye mtungi unaovuja na cha kushangaza zaidi ni kwamba baada ya kugundua kuwa mtungi wetu unavujisha, sisi badala ya kuuziba usivuje sisi ndo kwanza tumekazana kuujaza, tena tumezidisha idadi mara mbili na zaidi kujaza maji hayo ya mkopo kwenye mtungi wetu mbovu. Alafu huku tukitegemea labda maji yatajaa mtungini wakati tunaona kabisa kuwa mtungi wenyewe unavujisha, alafu itafika mwisho wa siku mtungi tuliokuwa tunaujaza maji ya mkopo unakuwa umeshavujisha maji yote, hapo sasa ndiyo tunakuwa tumeingia kwenye matatizo mazito.

Nchi yangu ya Tanzania, kwa kweli ni kama vile tumekuwa tukijaza maji kwenye mtungi unaovuja kusudi tuujaze mtungi huo, lakini huku tukiwa tunatambua kwamba mtungi huo kwa sasa ni mbovu hatuwezi kuujaza unavujisha maji yote na kumwagika nje. Lakini sisi wala hatujali wenyewe tumekomaa kuujaza hivyo hivyo tena tumeongeza kasi mara mbili na zaidi kuujaza mtungi mbovu, alafu mwisho wa siku matokeo yake maji yote ya mkopo yanakuwa yamesha mwagika yote na mtungi wetu utabakiwa tu mkavu, hapo sasa tunakuwa tumeshajiingiza kwenye matatizo makubwa, kwanza tunakuwa tumepoteza nguvu zetu bure wala hakuna tulicho kijaza na maji yote ya mkopo yalikuwa yanamwagika tu nje, yani kwa kazi yote tuliokuwa tunaifanya na juhudi zetu zote za kuujaza mtungi ni kwamba tulikuwa tunajisumbua bure.

Hivi unajua mfano wangu wa mtungi unaojazwa maji ya mkopo alafu unavujisha maji yote unamaanisha nini, ni kwamba mtungi huo naufananisha na uchumi wa Tanzania, na yule anaejaza maji kwenye mtungi namfananisha na serikali na yale maji yanayojazwa kwenye mtungi ni mikopo na pale panapovuja maji kwenye mtungi ni upetevu mkubwa wa fedha unaoendelea nchini.

Kwa kweli tumekuwa tukishuhudia serikali yetu ya Tanzania, imekuwa ikikopa mikopo mingi sana kwenye nchi yetu kusudi likiwa ni kukuza uchumi wetu, lakini pia huku kwa upande mwengine kumekuwa na upotevu mkubwa wa fedha nchini. Kwahiyo inamaana serikali inakuwa inafanya kazi ya kuingiza fedha kwa mikopo alafu fedha hizo zinapotea, mwisho wasiku tunakuwa kama tulikuwa tunajaza maji kwenye mtungi mbovu alafu matokeo yake tunakuwa tumejiingiza kwenye matatizo makubwa sana.

Kuna ushahidi mkubwa wa jambo hili kwamba linafanyika kwenye nchi yetu, hata kwenye ripoti zetu mbalimbali hapa nchini zimekuwa zikionyesha kuwa inchi yetu imekuwa na upotevu mkubwa sana wa fedha, inamaana hata mikopo hiyo inayoombwa na serikali inakuwa haina maana yoyote zaidi ya kuitumbukiza zaidi nchi yetu kwenye matatizo makubwa kwasababu fedha zinakuwa zinapotea tu. Yani inamaana kwamba serikali imekuwa ikikopa alafu fedha hizo zinapotea alafu na ukizingatia ni fedha za kukopeshwa, kwa hakika hapo ni lazima tunakuwa tunajiingiza kwenye matatizo makubwa sana.

Licha ya serikali kulifahamu jambo hili lakini badala ya kudhibiti upotevu huo, badala yake serikali imeongeza idadi ya mikopo ili kufidia upotevu wa fedha zinazopotea, yani badala ya serikali kudhibiti upotevu wa fedha serikali yetu tunaona imeendelea kukopa kwa kuzidisha kasi mara mbili yake. ambapo jambo hili nalichukulia kama ni kitendo cha kuamua kuzidisha kujaza maji ya mkopo kwenye mtungi ambao unavuja ili kufidia maji yanayovuja kitu ambacho hakisaidii kwamba tulitakiwa tu tupazibe panapovuja, lakini sisi tumeamua kuongeza idadi ya maji mara mbili kuujaza. Yani ni kama vile serikali inazani kwamba kuzidisha mikopo ndiyo suluhisho la kukuza uchumi badala ya kudhibiti upotevu wa fedha unaoendelea. kwa mwendo huu tunaweza kuzani labda tunakuza uchumi kumbe tunakuwa tunaliingiza taifa kwenye matatizo makubwa.

Yani serikali baada ya kuona ndani ya nchi kuna upotevu mkubwa wa fedha badala ya kukomesha upotevu huo serikali yetu imeamua kuongeza idadi ya mikopo ili uchumi upumue. Kwa kweli uchumi wetu wa Tanzania katika awamu hii kwa asilimia kubwa umekuwa ukitegemea mikopo ili uweze kupumua, inamaana hapo tunakuwa na uchumi wa mikopo na mikopo hiyo inapotea tu. tunakuwa tunakopa alafu lakini huku upotevu mkubwa wa fedha ukiendelea kama kawaida, kwahiyo nikama vile tunajaza maji ya mkopo kwenye mtungi unaovuja. Hapo mwisho wa siku tunakuwa kwenye madeni makubwa sana kuliko inavyozaniwa.

Mapendekezo

Kwa kweli tunataka kuujaza mtungi maji sharti ni moja tu, ni kuuziba pale panapovuja maji ili yasimwagike na sio kuongeza kasi ya utiaji maji kwenye mtungi kama tunavyofanya, kwasababu tusipouziba mtungi huo usivujishe hata tuongeze kasi vipi lazima maji yataendelea kuvuja tu, kwahiyo itabidi tuuzibe kwanza mtungi usivujishe. Kumbuka kamwe hatutoweza kuujaza mtungi kwa kuongeza idadi ya maji kwenye mtungi ni lazima tuuzibe pale panapovuja kwanza, kwani panapovuja situnapaona lakini, kwa bahati nzuri pale panapovuja sisi wote tunapajua. Basi sasa lazima tupazibe hapo pasivuje tena maji alafu baada ya hapo ndipo tutafanikiwa kuujaza mtungi mzima maji tena kwa urahisi kabisa.

Kwa kweli baada ya kupaziba pale panapovuja maji, ndipo mtungi tutafanikiwa kuujaza mtungi wetu maji tele, hata yule aliyekuwa anatukopesha hayo maji akija kutudai tunakuwa na uwezo mkubwa wa kumlipa na hata kama akitaka na yeye tumkopeshe sisi tunakuwa na uwezo wa kumkopesha, kwasababu mtungi wetu unakuwa unamaji mengi yani umejaa mpaka juu.

Unajua mtungi huo unamaanisha nini, mtungi huo ninaouongelea hapo naufananisha na uchumi wetu, kwa hakika serikali yetu inapaswa kugeukia kule pesa zinapo potea na kupadhibiti ili tuukuze uchumi wetu, kwasababu hatuwezi kuwa tunakopa alafu pesa nyingi zinakuwa zinapotea tu, alafu tutegemee kuwa tutaukuza uchumi wetu tunakuwa tunajidanganya. Alafu mwisho wa siku nchi yetu inakuwa kwenye madeni makubwa alafu na kilichokuwa kinafanyika hakionekani zaidi ya hasara na kujitwika matatizo makubwa.

Hitimisho

Tanzania bora tuitakayo ni ile isiyokuwa kama inajazamaji ya mkopo kwenye mtungi unaovuja, kwani kwa kufanya hivi kunaweza kupelekea ipatikane Tanzania tusiyoitaka.
 
Tanzania bora tuitakayo ni ile isiyokuwa kama inajazamaji ya mkopo kwenye mtungi unaovuja, kwani kwa kufanya hivi kunaweza kupelekea ipatikane Tanzania tusiyoitaka.
Sawa bro, sasaa ngoja tukakope maji ua mwishomwisho ili tuje tuyatumie kuchanganyia na huo udongomfinyanzi wa kuzibia mtungi😄😄..

Natania bro.

Ndivyo tunavyopaswa kudili na afya, uchumi na hata roho zetu. Unapaswa kuacha dhambi sambamba na kutenda mema sio kianza kushindanisha mema na mabaya kuangalia kipi kitamzidi mwenzie la. Pungiza hiki hapohapo unaongeza kile ili faida iwe maratatu ya vitendo.

Ngoja nifafanue kihesabu;
1 + -1 ni ziro = 0 ❌
1 - -1 ni 2 na zaidi na ndiyo Tanzania tuitakayo✔
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom