"Tumeshaona nyingi"......

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,717
Wakati nilipokuwa na umri mdogo kule kijijini nilikuwa nimezoea mara nyingi sana wakati tukiwa kwenye harakati za shambani au kutafuta kuni huku nikiwa na baba na vijana wengine wakubwa,walipokuwa wanajisaidia haja ndogo halafu akatokea mwanamke au binti hurudi kwa kasi sana kule alikotoka ili asione utupu wa anaejisaidia haja ndogo

Leo nimejikuta nikijiuliza maswali mengi sana kuhusiana na hili

Ni kwamba,nilikuwa natoka eneo moja na kwenda lingine,huku nikiwa na safari yangu kwa miguu nilikuwa nimeongozana na wadada wawili,wao walikuwa mbele mimi nilikuwa nyuma na walikuwa wanaongea mambo tofauti tofauti,kama mjuavyo uswazi kuna vinjia vingi na vingine ni vya vichochoro sana,nasi tulipitia kwenye kichochoro kimoja na ghafla binti mmoja alistuka na kusimama na yule mwingine nae alisimama na kisha kumuuliza mwenzake "kuna nini"?

Yule binti mwingine alimuambia "humuoni huyo jamaa hapo anakojoa"?,yule mwingine akamwambia "sasa ndio ustuke hivyo? Mbona umesimama?,mwenzake akamjibu "Huoni anajisaidia"? mwingine akamuambia "sasa cha ajabu nini? Si twende"?,waliendelea na safari yao na wakati huo nilikuwa nimewapita baada ya kubishana pale njiani

Ilibidi sasa fikra zangu zihamia kwa hawa madada na mara kwa mara nilikuwa nageuka kuwaangalia,Wakati wanamkaribia yule jamaa aliyekuwa anajisaidia walimgeukia na kumuangalia kisha wakaendelea na mmoja wao alisema nadhani ni yule ambae alimshangaa mwenzake kusita kuendelea kutembea alipomuona huyu jamaa anajisaidia haja ndogo kwakuwa nilikuwa naangalia mbele na wao walikuwa nyuma yangu,huyu dada alimuambia mwenzake "mi nakushangaa sana kwa kushindwa kuendelea saa ile,mbona tumeshaona nyingi tu"?

Mwenzake alicheka na kuitikia "ni kweli lakini",nilijikuta natafakari mengi sana,hawa mabinti walikuwa ni wadogo sana kiumri na kama ni kweli wakisemacho basi huko beleni inaweza kuja kuwa ni hatari sana ,kama binti mdogo kama yule "ameshaona nyingi" vipi akikua?

Nimestaajabu sana jioni ya leo ....!!
 
Ndo mfumo tulio nao sasa,ila tusihukumu mapema labda wameziona za wadogo zao wakiwa wanawaogesha n.k
 
hii kauli kama inataka kuzoeleka siku hizi nimeshaisikia mara kadhaa
 
Mtakapoziona ishara hizi mjue ule mwisho umekaribia:
 
Ndo mfumo tulio nao sasa,ila tusihukumu mapema labda wameziona za wadogo zao wakiwa wanawaogesha n.k
Yaani za wadogo zao ni nyingi kiasi gani hadi ziwe nyingi?

Au familia yao ni kama timu ya mpira?
 
Yaani za wadogo zao ni nyingi kiasi gani hadi ziwe nyingi?

Au familia yao ni kama timu ya mpira?

Wameona za wa nyumbani mwao,jirani zao na za ndugu zao,bado zile walizocheza kipindi kile kibaba na kimamaa
 
Ukifuatilia mabinti wanaanza mapenzi katika umri mdogo mno tena wanatembea na hwa vijana wa sekondari wao wapo primary,kiukweli sijui haya mambo wanajifunzia wapi..
 
Watakua watu wa karibu na ziwani hao wakienda kuoga wanachunguliana.Au la sivyo wamejua wanaume katika umri mdogo.
 
Mi alishanikutaga mdada flani akaniambia kwa jazba we huogopi ntakuchungulia nikamjib niogope nn wakati jana umelala nayo
 
Za wadogo zao + walizotumitumia+ JLK + porno movies+ raha tupu blog+ walizoziona uchochoroni km hivyo...... List ya kuona itakuwa ni ndefu sana.
 
Tendo la ngono pasi na uhalali wa ndoa ni uzinzi na uasherati. Kusema ni "mapenzi" ni kutaka kupaka rangi uovu ili watu waone ni halali kutenda.
 
Back
Top Bottom