Tumejiandaaje ufundishaji wa TEHAMA mashuleni ?

Maje Omary

New Member
Jun 20, 2012
4
0
Teknolojia ya Habari na Mawsiliano katika shule zote za msingi na Sekondari ni somo muhimu sana kwa karne hii ya sayansi na teknolojia. Nionavyo mimi utekelezaji wa mpango huu hauna kasi yokutosha kukidhi mahitaji ya dunia ya sasa hasa kwa nchi yetu Tanzania.

Katika pita pita yangu nimegundua kuwa TEHAMA imebakia katika nadharia tu kwani walimu wengi wanaofundisha somo hili hawana taaluma ya ICT na hivyo kinachofanyika ni kufundisha TEHAMA kwa nadharia tu iliyopo vitabuni hali inayomfanya mwanafunzi kutoelewa kinachoendelea darasani,

Anabakia kukariri misamiati migumu ya taaluma hii ili aweze kujibu maswali atakayoulizwa katika mtihani na siyo kumwandaa kwa kuitumia taaluma hii katika maishayake ya sasa na baadae.

Huku nikuwaandaa wataalamu wa ainagani? Wito wangu kwa wadau wote wa elimu ni kuwa tuwe na vipaumbele katika kutekeleza programu muhimu za kitaaluma!! Ninaamini kuwa, mwalimu ndiye aliyepaswakupewa taaluma hii kabla ya mwanafunzi.

Hali ilivyo sasa ni kuwa mwalimu na mwanafunzi wote wanafanana.

Bado hatujachelewa tuwape mafunzo ya kutosha walimu wetu ili waweze kuitendea haki TEHAMA.
Nawasilisha.:israel:
 
Tanzani inapenda kukurupuka sana bila kujipanga... kulikua na umuhimu gani wa kuanzisha hili somo shule za msingi wakati hata vifaa hakuna??
Computer mwalimu haijui mwanafunzi anayemfundisha ataijua?
 
TEHAMA kwa Tanzania bado tunacheza sana tena sana.Changamoto ni nyingi sana(Nishati ya uhakika,wataalam,computer+Internet).Walimu wamebaki kufundisha kwa kuchora ubaoni, kama lile tangazo la HAKI ELIMU......Hii ndiyo sipiyuu,sikirini,ukitaka kuzima........!Watoto wanachanganywa
 
Asante sana mkuu kwa kuliona hili... juzi nilikuwa napiga story na mtoto m1 jirani ye2..nikawa namuuliza matokeo yake akasema amekuwa wa 18 kati ya 73.. nikamuuliza maswali gani yanamshinda akasema Maswali Ya KWELI au SIKWELI..

Nikamuuliza somo gani akasema TEHAMA.. ni kamuuliza kwani tehama ni nini?? akacheka akasema hujui tehama Kuwa Ni AINA ZA SIMU?? dah nilibaki nashanga sana.. Mtoto yuko darasa la tatu..shule zetu za kayumba.. kazi ipo.
 
asante sana mkuu kwa kuliona hili... Juzi nilikuwa napiga story na mtoto m1 jirani ye2..nikawa namuuliza matokeo yake akasema amekuwa wa 18 kati ya 73.. Nikamuuliza maswali gani yanamshinda akasema maswali ya kweli au sikweli.. Nikamuuliza somo gani akasema tehama.. Ni kamuuliza kwani tehama ni nini?? Akacheka akasema hujui tehama kuwa ni aina za simu?? Dah nilibaki nashanga sana.. Mtoto yuko darasa la tatu..shule zetu za kayumba.. Kazi ipo.

kulingana na mazingira yetu ya tanzania,hatujafikia hatua ya kufindiaha tahama shule za msingi.mfano miundo mbinu ya umeme hata baadhi ya makao makuu ya wilaya hakuna.vifaa vyenyewe tani hizo kompyuta hazipo licha ya wataalamu .mtoto hajui hata bulbu ya umeme iweje komptuta.kuna vitabu tu vyenye picha za kompyuta.madarasa mengine hata fremu za madirisha hakuna.yaani vichekesho .
 
Back
Top Bottom