Tuipende Nchi yetu ukisikia popote wanatoa Mikopo mstueni aende akakope

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
13,535
10,035
1645547721650.png

This is what we do...
 
Mnawaza Upuuzi na upumbavu tu.. kwani akikopa anatumia kwenye mambo yake au ni kwa faida ya nchi..??
 
Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Aliyeanzisha "miradi ya kimkakati" ya matrilioni kafariki njiani, ukapewa wewe, njia alizokuwa anazitumia kuhudumia miradi huzijui au huzitaki lakini kila ukiamka unaskia sauti yake inadai "malizia miradi"
 
Hii lugha ya kuwa eti deni letu la taifa bado ni himilivu, na kuanza kujisifu kuwa bado tunakopesheka na bado pia tutaendelea kukopa, ina ukakasi mwingi sana. Hii ndiyo sababu kubwa inayopelekea viongozi wetu kutokutilia maanani kuongeza vyanzo na kupanua wigo wa kuongeza mapato ya nchi.

Mikopo ambayo baadhi yetu wanaishangilia, hivi sijui hata kama wanadadisi kuhusu masharti yanayoambatana nayo. Serikali ifikie wakati sasa ifanye "down sizing".

Ipunguze nafasi nyingi za watendaji wenye kofia za kisiasa tu ndani yake ili "government expenditure" zishuke angalau kwa 50%. Serikali imejaza watumishi wengi mno ambao wengi wao hata hawajui wanafanya nini, achilia mbali suala la uzalishaji wao kuwa wenye tija.

Badala ya kukopa, ni vyema serikali ikafikiria vitu vifuatavyo;
1. Iendeshe baadhi ya shughuli ama mashirika yaliyo chini yake kwa njia ya PPP.
2. Nafasi ya RC ama DC ziwe zinatokana na mmoja wapo wa wabunge waliochaguliwa katika majimbo yaliyopo ndani ya mkoa husika.
3. Idadi za wabunge zipunguzwe ili iendane na idadi ya wilaya
4. Ifute nafasi za wabunge wanawake wa viti maalum bungeni, kwa sababu huo umaalum wao wala haupo.
5. Iwakopeshe magari watendaji wa serikali ili wawajibike wao wenyewe katika kuyagharimia katika matengezo yake na kuajiri madereva.
6. Kupunguza marupurupu ya kufuru kwa viongozi wakisiasa wastaafu ili nao wawe kama wazee na wastaafu wengine.
7. Posho za vikao kwa wabunge ziondolewe, kwani kazi ya uwakilishi bungeni ni kazi, kwa hiyo wanapaswa kulipwa mishahara, "transport allowances" na "per diems" tu pale wanapoenda kuhudhuria vikao vya kamati za bunge ama vingine vya Bunge.
 
Hivi imagine mama angeipotezea miradi yote ya Mwendazake, ingekuaje?
 
Bora anayekopa anasema ili tufuatilie mahali hela zimeenda kuliko anayekopa kimya kimya tunashtuka tuna deni la kufa mtu
 
Hivi imagine mama angeipotezea miradi yote ya Mwendazake, ingekuaje?
Ni miradi iliyowekewa sera na nchi, ama ilikuwa miradi iliyoanzishwa kwa ajili ya ujiko? Kama aliyeanzisha miradi hakuianzisha kwa matakwa yake, bali alianzisha kulingana na dira ya nchi, basi haina budi kuendelezwa maana ni ya nchi si ya mtu binafsi.
 
Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Aliyeanzisha "miradi ya kimkakati" ya matrilioni kafariki njiani, ukapewa wewe, njia alizokuwa anazitumia kuhudumia miradi huzijui au huzitaki lakini kila ukiamka unaskia sauti yake inadai "malizia miradi"

Hapo lazima ukope. Ingawa pia ipo njia ya kujibana. Kiukweli matumizi ya serikali yako juu sana. Ifikie wakati na watu wa juu nao wafikirie kujibana walau kidogo.

Wapunguze kula kwa urefu wa kamba yao.
 
Hivi imagine mama angeipotezea miradi yote ya Mwendazake, ingekuaje?
Mwanasiasa YEYOTE dunian anfikiria afanye Nini aweze KUKUBALIKA
anatengeneza tatizo/anasolve
amalizie miradi au alete YAKE mipya
Na MDA unakimbia na wabunge WOTE KIJANI
2025 hiyo hapo
Full stress URAIS
KETE PEKEE NI HAKI BARABARA INGEKUWA NYEUPE AANZE NA BATIKA MPYAAAAA
 
Hii lugha ya kuwa eti deni letu la taifa bado ni himilivu, na kuanza kujisifu kuwa bado tunakopesheka na bado pia tutaendelea kukopa, ina ukakasi mwingi sana. Hii ndiyo sababu kubwa inayopelekea viongozi wetu kutokutilia maanani kuongeza vyanzo na kupanua wigo wa kuongeza mapato ya nchi.

Mikopo ambayo baadhi yetu wanaishangilia, hivi sijui hata kama wanadadisi kuhusu masharti yanayoambatana nayo. Serikali ifikie wakati sasa ifanye "down sizing".

Ipunguze nafasi nyingi za watendaji wenye kofia za kisiasa tu ndani yake ili "government expenditure" zishuke angalau kwa 50%. Serikali imejaza watumishi wengi mno ambao wengi wao hata hawajui wanafanya nini, achilia mbali suala la uzalishaji wao kuwa wenye tija.

Badala ya kukopa, ni vyema serikali ikafikiria vitu vifuatavyo;
1. Iendeshe baadhi ya shughuli ama mashirika yaliyo chini yake kwa njia ya PPP.
2. Nafasi ya RC ama DC ziwe zinatokana na mmoja wapo wa wabunge waliochaguliwa katika majimbo yaliyopo ndani ya mkoa husika.
3. Idadi za wabunge zipunguzwe ili iendane na idadi ya wilaya
4. Ifute nafasi za wabunge wanawake wa viti maalum bungeni, kwa sababu huo umaalum wao wala haupo.
5. Iwakopeshe magari watendaji wa serikali ili wawajibike wao wenyewe katika kuyagharimia katika matengezo yake na kuajiri madereva.
6. Kupunguza marupurupu ya kufuru kwa viongozi wakisiasa wastaafu ili nao wawe kama wazee na wastaafu wengine.
7. Posho za vikao kwa wabunge ziondolewe, kwani kazi ya uwakilishi bungeni ni kazi, kwa hiyo wanapaswa kulipwa mishahara, "transport allowances" na "per diems" tu pale wanapoenda kuhudhuria vikao vya kamati za bunge ama vingine vya Bunge.
yaani umeongea bonge la point kaka, ila cha kuongezea hapo wajitahidi kuziba na ile mianya ya upigaji maana taarifa za wafanyakazi hewa zimesharudi tena
 
Back
Top Bottom