Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,726
- 29,962
- Thread starter
- #21
Nadhani TRA wakae na Wizara za Kisekta kuwaelimisha utendaji unaolinda uchumi wa TaifaUkiamka vizuri Huwa unakuwa na hoja ,usikilizwe
Ukiangalia rationale ya mgao na hata sababu za kukosa umeme wa uhakika asilimia kubwa ni ukiritimba kwenye taratibu za manunuzi.
Niwape mfano mmoja hai. TTCL imekuja na mradi maridhawa wa Fiber Mlangoni kwako. Maeneo mengi wameshaanza kutandaza miundombinu lakini mradi umesimama zaidi ya mwaka wamesimamisha ukamilishwaji wa mradi, ukiwauliza wanasema taratibu za manunuzi...
Tukija kwenye sekta ya maji, inakuwaje watu wanakosa maji ilihali serikali imewekeza mtandao wa maji katibu nchi nzima?
Hizi hujuma zitokanazo na uzembe ama makusudi zinakwamisha ukuaji wa mitaji hususan hupelekea uwekezaji kuwa mchungu zaidi