Tra kutoza kodi kubwa bandari dar-es-salaam kwa manufaaa ya nani???

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,219
370
Wana JF,

Tanzania yetu hii jamani ina mambo, Tokea Majuzi kumekuwa na kasheshe la kufumuka kwa tozo la kodi hapo bandari dar-es-salaam, Kwa wafanya biashara wengi wamekuwa wakilia sana esp wale wa kariakaoo na kwingineko. Twashindwa kuwaelewa Tatizo kubwa ni nini hapo bandari je ni ugonvi wa mawakara wanagombania wateja au ni poor service za mawakara ndizo zinawafanya wafanya biashara wahamie kwa wakara mwingine au ni mbinu chafu zinatumika watu kukwepa kulipa kodi au ni nini?

Nchi hii imefika mahali haito tawalika tena au nao wafanyabiashara nao waandamane? kudai punguzo ta kodi hapo Costumes (bandarini)? Mfanya biashara mmoja kati ya waliohojiwa na Clouds FM jana alisema Contena alikuwa akitozwa 12M hadi 14M Tsh ghafla kodi imefika 80M Tsh sasa hapo ataendeshaje biashara atarudishaje mkopo na huyo mtu aliye mtumia mzigo toka nje atamlipaje?

Sielewi sisi watanzania esp Mfumo mzima wa serikali yetu hii tunafanya nini ni kuwa twajinyoga wenyewe? au?
Hivi hatuna source nyingine ya kukusanya kodi ndani ya nchi hii Bandarini ni shida, Gesi mtwara shida, Uranium nayo imeisha anza kuwa shida, Lamasi ndio tusiseme hatujuai tena hata wapi inapotelea watu wa mwadui maganzo ndio masikini wa kutupwa na shinyanga mjini, Geita ndio wilaya maskini yakuliko wilaya zote hapa nchini, Kahama uuuuwwiiiii shida fullllll, sasa Ukija Malia sili na utaliii ndio kabisaaaaa hovyooo, nchi hii itarudi lini kuwa na AMANI kama viongozi waliopo ndio wapindisha sheria na wameshindwa kuitawala nchi kila kukicha kimezuka hiki mara kile.

Kitilya hebu utufafanualie hizi kodi tunalipa zinakwenda wapi serikali inajigawia yenyewe na vikao vingi tuuu ewanafanya vya nini na hizo semina mnazo wapeleka watu nje ya nchi ili wakirudi waweze kuja na mbinu mpya ya kuboresha mifumo yetu ya kiuchumi matokeo yake ni kutunyoya watanzania.

My Take;

Serikali ina matabaka makubwa sasa esp hiki kipindi tuanacho pitia kwenda uchaguzi 2015 watu wana tafuta hela kwa kuwanyonya wananchi wenye kipato cha chini, na hapo ndipo wanapo ipeleka nchi kwa majanga.

Sioni Mantiki ya mawakala kupisha hapo bandarini wana zengwe gani ambalo mnaathri uchumi wa watu wa kipato cha chini. mbona mmekuwa waroho sana na tamaa ya pesa ????

Mwakyembe kama bandari wanakuundia zengwe waaachie watakuja huku kwa wananchi hapa ndipo wanatuamsha akili zetu zaidi si mwaka mmoja to 2015 umebaki wale na wakimbie kabisa maana hatutoa wabakisha ni ndani tuuu wote walio hujumu nchi.

Haya yote twajenga kwa kizazi kipi cha sasa au kijachooo?
 
Tatizo siyo mawakala wala Customs,hiki kilichotokea kwa sasa ni kosa la wafanya biashara wenyewe kukubali
kudanaganywa na baadhi ya mawakala wasio waaminifu na wakawa wanakwepa kulipa kodi halali,kwa kuandika
uongo kwenye nyaraka.Mnaleta suti mnaandika vyandarua,mnaleta makapeti mnaandika wayamesh,sasa imekula kwenu baada ya dili hili kubumbuluka customs wakali kama nyuki verification 100% Any way poleni'
 
Ingawa siitetei serikali lakini kusema kweli wafanyabiashara wengi hawalipagi kodi halali kama sisi wafanyakazi kwenye PAYE
 
halafu umenichekesha kwenye hiyo 'My take' yako
"Serikali ina matabaka makubwa sasa esp hiki kipindi tuanacho pitia kwenda uchaguzi 2015 watu wana tafuta hela kwa kuwanyonya wananchi wenye kipato cha chini, na hapo ndipo wanapo ipeleka nchi kwa majanga".

mwenye uwezo wa kuingiza kontena na kulipa ushuru wa M12-M14 ni wa kipato cha chini mkuu! kweli tuko tofauti!!
 
Bwana Jethro system yetu ya kodi ni ubabaishaji mtupu ningetumia maneno ya Kolimba (TRA haina dira wala mwelekeo)kodi watozazo ni makisiokisio tu ambayo wala hayaendani na ukweli,leo uta import hiki kodi ni hii kesho uta import kilekile kodi ni tofauti!!!Nigeria baada ya kuona tatizo kubwa la ajira kwa vijana wao walitumia bandari kuwasaidia waliwawekea kodi zinazoeleweka matokeo yake vijana wa kinigeria wananufaika sana na bandari yao,nenda miji yote ya kibiashara duniani utakutana nao wananunua bidhaa na kutuma kwao faida yake leo hii vijana wa nchi nyingine za afrika magharibi kama cameroon,guinea,senegal,chad nk hawaendi dubai/china kununua bidhaa wanakwenda Lagos Nigeria kununua bidhaa..Nenda showroom zetu kijigari kidogo used kama toyota Ist cha mwaka 2004 watakuanzia 12ml maana gharama ya kukitoa port ni around 4ml ukienda nchi zisizo na bandarani kama Rwanda utaipata chini ya hapo!!!hivyo vijana toka kwenye nchi yenye bandari wanakwenda kwenye nchi ambayo haina bandari kununua bidhaa!!!bwana mito kuna mzigo nimeutoa juzi nimewapa risit zangu hivyo nilitegemea kodi ya 3.6ml nilishangaa sana kodi ya Tra ilikuja 6.5ML sikuamini macho yangu!!!baiskeli ndogo nilinunua $100 wao katika makisio yao fake wakasema ni $300 ovyo kabisa,hawawaumizi wafanyabiashara wanawaumiza wananchi wote,baada ya kulipia bado unazungushwa ili storage iongezeke ukienda leo system ipo down vyoo kesho na ukienda kesho wana sababu nyingine ovyo sana!!wanataka ushindwe kutoa ili wauziane wenyewe kwa wenyewe..bwana mito yakikukuta ndio utawaelewa vizuri hawa TRA nadhani bado hujakutana nao ni very fake!!!lara 1 anasema wawezafanya biashara!!kama haupo connected hiyo nchi haina mazingira mazuri kwa biz ya import/export maana kodi hazieleweki labda kwa biz za ndani!!!
 
mkuu lucky sabasaba naona hukunielewa, nilisema sitetei serikali ila nimeenda mbele kidogo kwa kujaribu kulinganisha wafanyakazi na wafanyabiashara ktk suala zima la kulipa kodi.

mkuu madudu ya bandari yetu na TRA nayajua sana na yalishaniliza sana tu!
 
kimsingi faida ilitakiwa irudi kwa wananchi kwa kuweka mazingira mazuri ya shule ,afya , elimu ,miuondo mbinu ,maji n.k lakini bado kwenye bajeti yetu ni tegemezi kwa asilimia kubwa .hapa kuna kazi ya kufanya kuweka mambo sawa kodi hizi zinaishia wapi .
 
Tatizo siyo mawakala wala Customs,hiki kilichotokea kwa sasa ni kosa la wafanya biashara wenyewe kukubali
kudanaganywa na baadhi ya mawakala wasio waaminifu na wakawa wanakwepa kulipa kodi halali,kwa kuandika
uongo kwenye nyaraka.Mnaleta suti mnaandika vyandarua,mnaleta makapeti mnaandika wayamesh,sasa imekula kwenu baada ya dili hili kubumbuluka customs wakali kama nyuki verification 100% Any way poleni'
Nakubaliana nawe 100%. Wafanyabiashara ndiyo wajilaumu wenyewe.TRA haijapandishi kodi ila imeanza kuwatoza kodi halali.TRA walikuwa wanafanya 'homework' na sasa wamemaliza..
 
Hoja ya kwamba kodi zao wanakadiria na hakuna calculation maalum ni kwel,kwa maana unaweza ambiwa labda hyo kodi ya m80 mfano ni halali,tatzo linakuja imekujaje?,hakuna mahesabu ambayo yapo wazi yanayoönyesha jinsi kodi inavyokokotolewa mimi nadhani hili nalo lingeangaliwa kwa kina kupunguza malalamiko
 
Ni kweli. Ni tatizo kubwa. Rafiki yangu juzi katozwa kodi 120,000/- kwa simu ya 200,000/-. Tena hapo baada ya kulalamika. Manake mwanzo walidai 200,000/-. Ingekuwa rate ya kodi ipo clear, wafanya biashara wangejua jinsi gani ya kujipanga kuleta mizigo. Mtihani ni kuwa wafanya biashara wengine wanatozwa kodi ndogo kuliko wengine. Na wengine wankwepa. There's no level plain field like developed countries. Bora kodi ijulikane ni kubwa kuliko kutokuwa wazi.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Dr. Said is a medical doctor (MD), Entrepreneur and a home based business coach. He's the current CEO of Strategic Marketing & Design, a company which helps business owners increase their profits using strategic marketing.

He spends most of his FREE time blogging about business, entrepreneurship and marketing on his blog site SaidSaid.Net.
To learn more from him, make sure you subscribe to his FREE Strategic Marketing Course.
 
Pale bandarini na TRA ni balaa tuliowahi deal nao tunajua,wale dawa yao ni kuhakikisha wafanyakazi hawana access na pesa au malipo yeyote maana ndio mwanzo wa rushwa zote na usumbufu wote tunaopata,make sure wanao process zile tax na customers hawajuani wala hawaingiliani kabisa...lakini still nashangaa why na technology na hizi software zote bado wanafanya mambo ya kukisia kisia tuu,kuna watu management pale ni watupu na hawafany kazi zao vizuri ndio maana tunahangaika bila sababu
 
Nakubaliana nawe 100%. Wafanyabiashara ndiyo wajilaumu wenyewe.TRA haijapandishi kodi ila imeanza kuwatoza kodi halali.TRA walikuwa wanafanya 'homework' na sasa wamemaliza..

yaani mkuu ndo unaweka msisitizo kabisa, loh! tutashindwa kufanya biashara sasa na nyie mkose mapato
 
Ni kweli. Ni tatizo kubwa. Rafiki yangu juzi katozwa kodi 120,000/- kwa simu ya 200,000/-. Tena hapo baada ya kulalamika. Manake mwanzo walidai 200,000/-. Ingekuwa rate ya kodi ipo clear, wafanya biashara wangejua jinsi gani ya kujipanga kuleta mizigo. Mtihani ni kuwa wafanya biashara wengine wanatozwa kodi ndogo kuliko wengine. Na wengine wankwepa. There's no level plain field like developed countries. Bora kodi ijulikane ni kubwa kuliko kutokuwa wazi.

----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Dr. Said is a medical doctor (MD), Entrepreneur and a home based business coach. He's the current CEO of Strategic Marketing & Design, a company which helps business owners increase their profits using strategic marketing.

He spends most of his FREE time blogging about business, entrepreneurship and marketing on his blog site SaidSaid.Net.
To learn more from him, make sure you subscribe to his FREE Strategic Marketing Course.
sasa huo ni ukusanyaji kodi au unyang'anyi?
 
Tatizo siyo mawakala wala Customs,hiki kilichotokea kwa sasa ni kosa la wafanya biashara wenyewe kukubali
kudanaganywa na baadhi ya mawakala wasio waaminifu na wakawa wanakwepa kulipa kodi halali,kwa kuandika
uongo kwenye nyaraka.Mnaleta suti mnaandika vyandarua,mnaleta makapeti mnaandika wayamesh,sasa imekula kwenu baada ya dili hili kubumbuluka customs wakali kama nyuki verification 100% Any way poleni'

umemaliza! No comment! Watz hatuishi kulalamika hawakusanyi kodi, wakikusanya wanatuonea.tra wanafanya kazi kwa kiasi, ila tatizo wakishakusanya wanaopelekewa na kupanga bajeti!
 
Ni kweli kabisa kwamba kodi Tanzania ulipaji wake unategemea sana huruma ya tax collector na huo ni mwanya wa upotevu wa mapato yetu. Ni kama vile hakuna uwazi sana kwa masuala ya kodi.
Hata hivyo kwa sababu wabongo tulisha kubali kufanya kazi kwa mtindo huo bila pingamizi kwa kipindi chote, ni lazima wote mlioleta bidhaa mzilipie kama mnavyodaiwa. Msitake kukwepa kodi. Bila kulipa kodi nchi yetu inayumba kiasi wanakopa kwenye mabenki ya kibiashara na inflation inaongezeka. LIPENI.
 
Ingawa siitetei serikali lakini kusema kweli wafanyabiashara wengi hawalipagi kodi halali kama sisi wafanyakazi kwenye PAYE

MKUU MITO, upo sahihi kabisa. Nchi hii ni wafanyakazi peke yao ndiyo wanalipa kodi stahiki na ndiyo wanabanwa saaana. Nakuapia WAFANYABIASHARA WOTE (100%) AU WANAOJIITA WAWEKEZAJI NI WAKWEPA KODI WAKUBWA period!. For the time being TRA Customs ya Masamaki wanajaribu kuamka ili kurekebisha unyanyasaji huu. My worry ni hawa wafanyabiashara kama hawatahujumu juhudi hizi takatifu!
 
Back
Top Bottom