TISS kitengo cha Intellijensia ya uchumi mnakwama wapi?

Tanroad watakachojitetea ni Wakandarasi wa ndani, mtaji wa kufanya kazi hawana. Jambo ambalo ni kweli ukiangalia miradi mingi inayofanywa na wazawa changamoto kubwa ni ukwasi wa kuendesha mradi, ukimpa mzawa mradi wa miezi 24 atafanya kwa miezi 48 sababu alikuwa anasuasua kupata fedha za kuendesha mradi
Upuuzi,mtaji hawana nani kasema wakati banks zipo? Caspian construction waliojenga njia 8 hawana mtaji?

Hakuna kitu hapo ni kwamba Wachina wanatoa hongo ndefu
 
Anza sasa kuwaza kama mwananchi wa dunia nzima 'a global citizen'

Wazawa na wa kuja mtambue wananchi wanachotaka ni huduma bora ya bei nafuu tu bhaaaaas
Siku wachina wakianza kujaa humu na hizo biashara zenu za uchuuzi wa kuungaunga zikafirisika na mkakosa vipato na kupigwa na njaa ya umasikini ndio akili zitawakaa vizuri.
Unajua hii nchi watu ni wapuuzi sana , watanzania wengi wana akili finyu na huangalia pua zao tu ,hawaangalii consequences za maamuzi ya kipumbavu jinsi zinavyoweza athiri future
 
Na Wachina nao wakatalie vyao si ndio? Tanzania sio Kijiji, hiyo nadharia unayowaza kwa dunia ya leo haiwekaniki ni kujichimbia kaburi na kujifukia, Dunia ya sasa ili uweze kulinda maslahi yako unatakiwa kuwekeza kwa watu wako wawe na maarifa, ujuzi na stadi zitakazowafanya wawe na soko mahali popote pale duniani, wawe wenye ujuzi wa kutatua changamoto za kila mahali hapa duniani, ukifikiri kumzuia mchina ndo kumuokoa mtanzania ni kujidanganya, tunaihitaji mataifa mengine zaidi kuliko yanavyotuhitaji, ili tufanikiwe inabidi na sisi tuhitajike zaidi. Tujifunze kwa mataifa kama Marekani, Taifa limeundwa na binadamu kutoka pande zote za duniani na halina hizi sera za kuzuia wageni, kwao ni mgeni analeta nini. Ukiwa huna faida kwao huingii,
Protectionism haikwepeki , huwezi achilia nchi ikawa totally shamba la bibi na kunufaisha wageni tu ,haipo hiyo
Nenda Marekani nenda China nenda popote , kuna vitu vimewekwa kumnufaisha mzawa na kulinda maslahi ya kiujumla ya mzawa.
Wewe mtanzania na vibilioni vyako vya madafu nenda kajaribu kuwekeza China kwenye real estate au construction , uone kama inawezekana .
Au nenda Dubai au nchi yoyote ya kiarabu hapo middle east utake kuanzisha biashara ya uchuuzi , uone moto wake
Wananchofanya wachina kina implications mbaya kwa future ya kiuchumi kwa wananchi wa hizi nchi za kiafrika
Jua kwamba hizi nchi zetu hazina sekta komavu za viwanda za kuzalisha bidhaa ili kufanya export na kuhudumia masoko ya ndani , sasa tunaagiza bidhaa kwa wingi toka nje hasa China ,Kwa kufanya hivyo tunanufaisha China Kwa kuwapa ajira watu wao kupitia uzalishaji wa bidhaa viwandani ,sisi huku ni loosers na watu wanakosa ajira .
Pili , tunakuwa looser kama lundo la wachina wanakuja kufanya biashara za uchuuzi huku , ina maana wao wanafaidika kwa watu wao kupata kipato kupitia uchuuzi that's means Tanzania Au nchi za Afrika pesa zote zinavunwa na kwenda kunufaisha uchumi wa China ,so net results sisi ni loosers .

Sikubaliani na huu ujinga wa kuruhusu wa wahindi au wachina au waarabu kuruhusiwa kuja kufanya biashara za uchuuzi huku ,huu ni Upumbavu
 
Wapo Watanzania wengi tu wamefungua biashara nchi za nje, na hizo nchi hazijaja na hizi hoja za kulinda wazawa ikiwemo hiyo China, Je wachina nao wafukuze watanzania waliopo huko china wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na wachina?
Protectionism ina umuhimu wake kwenye uchumi hasa kuleta mizania na kunufaisha wananchi pale inapowezekana
Hakuna 100 percent free market dunia hii .
Huyo China mwenyewe kafungia kitambo kampuni za kimarekani za mitandao ya kijamii mfano facebook , instagram ,YouTube , WhatsApp , Google nk ,zote hizo hazipatikani China , na kafanya hivyo ili kuzipa kampuni zake za ndani wigo wa kukua na kukomaa na kujitanua kupitia soko la ndani ya China , hizo kampuni kama weibo ,wechatt nk
Leo hii zimekuwa giants na nyingine kama bytedance wameanza kutoka nje ya mipaka na kujitanua kupitia products kama tiktoks nk

Mmarekani naye anafungia tiktoks ili kulinda kampuni zake kama facebook nk ambazo zinacompete na bytedance ya mchina .
Protectionism haikwepeki
 
Wapo Watanzania wengi tu wamefungua biashara nchi za nje, na hizo nchi hazijaja na hizi hoja za kulinda wazawa ikiwemo hiyo China, Je wachina nao wafukuze watanzania waliopo huko china wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na wachina?
Kitu ambacho kilitakiwa kifanyike wachina waje wawekeze kwenye viwanda na technology na si uchuuzi ambao ndio shughuli inayofanywa na watanzania asilimia kubwa , tena watanzania wengi ambao ni masikini na wachuuzi wa mitaji midogo .
 
Wapo Watanzania wengi tu wamefungua biashara nchi za nje, na hizo nchi hazijaja na hizi hoja za kulinda wazawa ikiwemo hiyo China, Je wachina nao wafukuze watanzania waliopo huko china wanaofanya kazi zinazoweza kufanywa na wachina?
Hata kwenye boxing huwezi chukua bondia mwenye uzito wa pound 200 apigane na bondia mwenye uzito wa pound 100
 
Na hapo ndipo CCM watajikorigea sumu yao kwa raia maana sababu ya kuwaondoa itakuwa imepatikana shenzi sana hawa.
Dar ina almost 10 million people , unataka wote twende kariakoo, soko kubwa kwa kila mtu acheni wasiwasi wa kujitia umaskini, fungua hata kariakoo 100, supply and demand itaamua
 
Nchi yetu miaka michache ijayo tutaanza kupambana na Wachina. Inakuaje mchina anakuja nchini kufungua supermarket. Wachina wametapakaa kila kona ya hii nchi wanachukua fursa za Watanzania. Juzi bungeni mbunge wa Geita vijijini alitoa tahadhari kuhusu Wachina kupewa migodi wakati wana mitaji ambayo Watanzania wanaweza kuwa nayo. Nilisikitishwa sana na jibu la Mh Spika akidai kwamba mambo mengine ni kulinda diplomasia. Yaani mtu aje nchini kwako kuchukua fursa za wazawa wewe usite kuchukua hatua eti kisa diplomasia. Hii sio sahihi.

Pili kwanini tusirudishe sera ya Magufuli. Hakuna kuruhusu kampuni yeyote kuajiri zaidi ya raia wa 5 wakigeni. Hii itasaidia kujenga uwezo kwa raia wa Kitanzania. Magufuli aliweka kikomo kwenye vibali kwa raia wa Kigeni ili kuwezesha kujengewa uwezo. Hakuna kazi yeyote hapa nchini inashindwa kufanywa na wazawa . Imenichukua muda kuelewa kwanini Magufuli alichukua hii hatua. Hawa watu wanaipiga sana serikali kwa kupunguza makadirio ya mapato kwa sababu kuwaruhusu kwa wingi kwenye makampuni kunawawezesha kutengeneza mtandao wao vizuri. Ushahidi upo.

“Tusipoimarisha uwezo wa watu wetu kushiriki katika uchumi, tutajikuta tunagawana umaskini baadala ya kugawana utajiri. Ni kwa sababu watu wetu hawana ujuzi na elimu ndo maana tunapata wawekezaji uchwara ambao wanakuja kuchukua fursa za Watanzania……” Rostam Aziz
Lini tumekuwa na hicho kitengo?
Hao ni kitengo ki1 tu cha kulinda sisiemu na viongozi wake,baaasi.
 
Kitu ambacho kilitakiwa kifanyike wachina waje wawekeze kwenye viwanda na technology na si uchuuzi ambao ndio shuguli inayofanywa na watanzania asilimia kubwa , tena watanzania wengi ambao ni masikini na wachuuzi wa mitaji midogo .
Kila mtu anataka kula, kama wanafanya kihalali acha wawe wachuuzi tuu labda wabongo wataamka
 
Nchi yetu miaka michache ijayo tutaanza kupambana na Wachina. Inakuaje mchina anakuja nchini kufungua supermarket. Wachina wametapakaa kila kona ya hii nchi wanachukua fursa za Watanzania. Juzi bungeni mbunge wa Geita vijijini alitoa tahadhari kuhusu Wachina kupewa migodi wakati wana mitaji ambayo Watanzania wanaweza kuwa nayo. Nilisikitishwa sana na jibu la Mh Spika akidai kwamba mambo mengine ni kulinda diplomasia. Yaani mtu aje nchini kwako kuchukua fursa za wazawa wewe usite kuchukua hatua eti kisa diplomasia. Hii sio sahihi.

Pili kwanini tusirudishe sera ya Magufuli. Hakuna kuruhusu kampuni yeyote kuajiri zaidi ya raia wa 5 wakigeni. Hii itasaidia kujenga uwezo kwa raia wa Kitanzania. Magufuli aliweka kikomo kwenye vibali kwa raia wa Kigeni ili kuwezesha kujengewa uwezo. Hakuna kazi yeyote hapa nchini inashindwa kufanywa na wazawa . Imenichukua muda kuelewa kwanini Magufuli alichukua hii hatua. Hawa watu wanaipiga sana serikali kwa kupunguza makadirio ya mapato kwa sababu kuwaruhusu kwa wingi kwenye makampuni kunawawezesha kutengeneza mtandao wao vizuri. Ushahidi upo.

“Tusipoimarisha uwezo wa watu wetu kushiriki katika uchumi, tutajikuta tunagawana umaskini baadala ya kugawana utajiri. Ni kwa sababu watu wetu hawana ujuzi na elimu ndo maana tunapata wawekezaji uchwara ambao wanakuja kuchukua fursa za Watanzania……” Rostam Aziz
Hicho kitengo sijui kama kipo.

Kama kipo basi kimelala usingizi wa pono.

Nachojua uchumi ndiyo mhimili mkuu kwenye intelijensia.

Hawa jamaa sijui huwa wanafanya kazi gani?
 
Kwahiyo suluhisho la kukosa mtaji ni kukaribisha raia wa mataifa mengine kuja kujichotea hela kwenye taifa letu si ndio?
Wanakuja kufanya kazi sio kujichotea, kama wanafanya kazi vizuri na kupiga pesa jifunze kwao upate maendeleo sio kuwafanyia roho mbaya na kuwaona kama wezi, wahamiaji dunia nzima wanakuja na maarifa na mitaji, US unayoiona imeendelea sana sababu kubwa ni wahamiaji, wewe endelea kushindana locals ambao hata maji ya kuoga wameshindwa kujiwekea majumbani kwao huku wakizungukwa na mito safi kila kona
 
Wanakuja kufanya kazi sio kujichotea, kama wanafanya kazi vizuri na kupiga pesa jifunze kwao upate maendeleo sio kuwafanyia roho mbaya na kuwaona kama wezi, wahamiaji dunia nzima wanakuja na maarifa na mitaji, US unayoiona imeendelea sana sababu kubwa ni wahamiaji, wewe endelea kushindana locals ambao hata maji ya kuoga wameshindwa kujiwekea majumbani kwao huku wakizungukwa na mito safi kila
 
Attachments

  • DD553DF8-6482-4533-A0D5-3550C940265B.jpeg
    DD553DF8-6482-4533-A0D5-3550C940265B.jpeg
    216.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom