TFF Ubabaishaji huu mpaka lini?.......Siasa mpaka kwenye Soka!!

Balantanda

JF-Expert Member
Jul 13, 2008
12,476
4,759
YANGA.PNG
 
Yanga kwa sasa inatakiwa ilie na FUFA pamoja Sc Villa ambao either kwa tamaa ya pesa au hawakuelewa maana ya Provisional permit! Ikawaingiza mkenge Yanga.Kwa Okwi kuzuiliwa CHAN kunajieleza hakuwa mchezaji huru!!!!
 
Sasa ilikuwaje TFF wakabariki usajili na CAF pia wakabariki usajili....Na TMS ikakubali?.....
 
Ah! We are tired of Yanga na Simba bana u guys can settle them out there. Timu zenyewe hakuna maendeleo ujinga tu.
 
TFF nao waliingizwa mkenge kwa kuangalia ushabiki na kujikomba, ila kimsingi Baba akishayumba familia nzima nayo itayumba hata kama mtoto ndiye aliyemyumbisha, but tangu mwanzo nilishasema TFF wanahusika na si mara ya kwanza TFF kuyumbisha
Sasa ilikuwaje TFF wakabariki usajili na CAF pia wakabariki usajili....Na TMS ikakubali?.....
 
TFF pale wanafanya mambo kama vile hawajui taratibu na sheria. Wanafanya kazi zao kiushabiki zaidi.
 
[h=1]Watunisia wamruhusu Okwi Yanga: Waondoa jina lake CAF[/h]
JAMBO ambalo linaiumiza kichwa Yanga sasa ni kutaka kuhakiki kama kweli Etoile du Sahel imewasilisha jina la straika, Emmanuel Okwi kwenye usajili wake kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Lakini katika orodha ya Etoile du Sahel, ambayo Mwanaspoti imepata nakala yake jana Ijumaa ni kwamba klabu hiyo imepeleka CAF majina 24 tu, na hakuna jina la Emmanuel Okwi.

Iwapo ikitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Etoile inaweza kuongeza majina sita kwani kila klabu inaruhusiwa kutuma majina 30.

Kwa kifupi ni kwamba, Etoile du Sahel haiwezi kumtumia Okwi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na sasa Yanga wanaweza kumtumia raia huyo wa Uganda kwani wametuma jina lake katika shirikisho hilo mjini Cairo, Misri.

Etoile kwenye usajili wake wa CAF imepeleka wachezaji 24 ambao pia hakuna jina la Okwi.

Waliosajiliwa CAF ni Aymen Mathlouthi, Saif Ghezal, Ghazi Abderrazzak, Radhouene Felhi, Marouene Tej, Hamza Lahmar, Alaya Brigui, Baghdad Bounedjah, Abdel Fadel Suanon, Issam Jebali, Franck Kom, Ahmed Mortadha na Ben Ouannes.

Wengine ni Hamouda Chatti, Marouene Troudi, Hamdi Nagguez, Aymen Ben Ayoub, Drame Michailou, Mohamed Slama, Zied Essoussi, Rami Bedoui, Aymen Trabelsi, Fehmi Kacem, Khaled Yahia na Youssef Mouihb

Ingawa, TFF imesimamisha kwa muda Yanga kumtumia Okwi, lakini jambo hilo inaelekea linakosa nguvu baada ya Etoile kuliondoa jina la mchezaji huyo CAF.

Yanga itacheza na Komorozine ya Comoro katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi ujao ikianza Dar es Salaam kabla ya kurudiana Comoro.

Okwi alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea SC Villa ya Uganda kwa mkataba wa miaka miwili huku ikidaiwa kuwa alipewa dola 100,000 (Sh 160 milioni).

SC Villa iliruhusiwa na Fifa kumtumia mchezaji huyo kwa mkataba wa miezi sita wakati sakata la madai ya mishahara na marupurupu yake Etoile yakifanyiwa kazi.

Mbali na madai ya Okwi kwa Etoile hata Simba ilikuwa ikidai dola 300,000 ambazo haijalipwa mpaka sasa na kesi ipo Fifa.

MWANASPOTI 25/1/2014
 
Hata kama wewe ni shabiki wa yanga kuwa mkweli, waandishi hasa ndio wanaopotosha hii habari, watandanzania wa sasa sio wa kudanganywa kama zamani, kila mtu ana simu na internet ipo hata kwenye simu tunaangalia jamani semeni ukweli jina la okwi lipo upnde gani. Sasa naomba kila mtanzania aingie mwenyewe kwenye hii web, The Football Portal for the Premier League and Transfer Rumour Forum - - transfermarkt.com. Ukisha fungua angalia kushoto kwako kuna sehemu imeandikwa Europe, america, Africa na zingine, fungua africa, ukisha fungua Africa utaona ramani, kwenye ile ramani utaona sehemu imeandikwa TUN manaake tunisia, Fungua pale utaona majina yooote ya virabu vya Tunisia, bofya pale palipo andikwa Etoile Sportive de Sahel, Utaona Squad of Etoile Sportive du Sahel in the season 2013/2014, Je? jina la Okwi lipo?????????????????????????????
na inakuonyesha mkataba wake unaisha lini?????????. tusidanganyene hapa kama wewe ni mwandishi za michezo unashindwa nini kuona haya mnabaki kwenda yanga na kuchukua habari za kufoji na kutoa kwenye maredio na mitandao yenu, acheni hizo mambo yako wazi, kama wewe ni shabiki acha kazi ya uandishi wa habari za michezo fanya ushabi wa club unaoipenda acheni kudanganya watanzania kisa ninyi ni waandishi wa michezo
aksanteni
 
Samahani angalieni kwenye karatasi iliyo tolewa jana kwa waandishi wa habari haionyeshi hata umri wa mchezaji, ina maana Caf kwao umri sio dili??????
 
Hata kama wewe ni shabiki wa yanga kuwa mkweli, waandishi hasa ndio wanaopotosha hii habari, watandanzania wa sasa sio wa kudanganywa kama zamani, kila mtu ana simu na internet ipo hata kwenye simu tunaangalia jamani semeni ukweli jina la okwi lipo upnde gani. Sasa naomba kila mtanzania aingie mwenyewe kwenye hii web, The Football Portal for the Premier League and Transfer Rumour Forum - - transfermarkt.com. Ukisha fungua angalia kushoto kwako kuna sehemu imeandikwa Europe, america, Africa na zingine, fungua africa, ukisha fungua Africa utaona ramani, kwenye ile ramani utaona sehemu imeandikwa TUN manaake tunisia, Fungua pale utaona majina yooote ya virabu vya Tunisia, bofya pale palipo andikwa Etoile Sportive de Sahel, Utaona Squad of Etoile Sportive du Sahel in the season 2013/2014, Je? jina la Okwi lipo?????????????????????????????
na inakuonyesha mkataba wake unaisha lini?????????. tusidanganyene hapa kama wewe ni mwandishi za michezo unashindwa nini kuona haya mnabaki kwenda yanga na kuchukua habari za kufoji na kutoa kwenye maredio na mitandao yenu, acheni hizo mambo yako wazi, kama wewe ni shabiki acha kazi ya uandishi wa habari za michezo fanya ushabi wa club unaoipenda acheni kudanganya watanzania kisa ninyi ni waandishi wa michezo
aksanteni

Kwa wale ambao hawajakuelewa ngoja nisaidie kuwawekea hapa.
 
Attachments

  • Okwi.doc
    209 KB · Views: 97

Kweli kabisa mkuu. Bahati mbaya imeshindikana kuweka picha (nadhani mods wanaishighulikia hali hii) ya gazeti tena la serikali la Spoti Leo toleo # 139 la Jan 9-11 2014 likisema 'Maximo atua Yanga rasmi. Kuungana na timu Uturuki'. Uandishi huu wa kishabiki ndio upo hata kwenye siasa, ni hatari mno na sijui kama mh naibu Juma Nkamia ataliona na kulikemea jambo hili.
 
safi sana.ndani ya tff wamegawanyika kiushabiki
Mkuu, si umeona uteuzi wa, nadhani makatibu, wa kutoka Yanga na Simba? Ili kuweka mambo sawa na pia rais na makamu wake wa TFF ni hivo hivo. Kumbuka hata wabunge wetu wana timu za Simba na Yanga, sasa kisoka ndio hatutaendelea kamwe.
 
Back
Top Bottom