TFF na Bodi ya ligi inapaswa kubadili sheria ya timu ya ligi kuu kucheza play off na timu ya championship

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,383
12,946
Kwanza nichukue fusa hii nikiwa mdau wa ball kupitia jukwaa hili la michezo la Jamiiforums kuzipongeza timu kutoka championship na kupanda ligi kuu.

KENGOLD FC NA PAMBA FC, Hakika timu hizi zinastahili pongezi maana siyo kazi nyepesi kutoka championship mpaka kupanda ligi kuu.

Na pia nichukue fursa hii kuwashauri (kuwasihi) ndugu KENGOLD FC NA PAMBA FC kuwa ligi kuu ya NBCPL haitaki mbwenbwe za huko mlikotoka bali ligi kuu inahitaji NIDHAMU, UONGOZI BORA, USAJILI MZURI NA BENCHI MAKINI, ligi kuu haitaki mambo ya kuchinja paka, kuchimba chimba uwanja bali ni usajili mzuri na kuwapa morali wachezaji.

Turudi kwenye kichwa cha habari kama kinavyojieleza hapo juu ligi yetu imekuwa ina kipengele cha play off, timu nne za mwanzo katika ligi ya championship timu mbili hupita moja kwa moja lakini mbili zilizobaki hucheza play off bingwa anakwenda kucheza na timu moja wapo ya ligi kuu iliyocheza play off na mwenzie nje ndani na kushinda

HOJA YANGU; timu za ligi kuu zinakuwa tayali zina uzoefu, msuli wa usajili pamoja msuli wa fedha tofauti na championship wanakuwa ni wa kuunga unga sasa ukiwakutanisha kwenye playoff kwa asilimia kubwa timu inayotoka championship lazima itapigwa tu na timu kutoka ligi kuu itarudi tena wa championship atarudi alikotoka.

MAONI YANGU; TFF na Bodi ya ligi inapaswa waliangalie hii sheria hii wa championship wamalizane wao kwa wao na wa ligi kuu pia wamalizane wao kwa wao kuliko wa championship kukutana na wa ligi kuu, hiyo ni ngumu na kwa upande mwingine ni uonevu tu.
 
Binafsi napingana na wewe. Hapa wameweka sheria hii ili zisije kupanda timu dhaifu kuliko zile zinazoshuka. Ndiyo maana wamezipa fursa na haki timu mbili za juu kupanda moja kwa moja wakati zile zingine zinapimwa na vibonde wenzao ili mwenye uafadhali kati yao ndiyo apande.

Tupe data za miaka 3 iliyopita, playoffs walicheza nani na nani na yupi alipita ili tupate mwanga zaidi kwenye hii mada.
 
Wewe ndiyo ulipaswa kuja na data za nyuma huko ili kusapoti hoja yako
 
Binafsi napingana na wewe. Hapa wameweka sheria hii ili zisije kupanda timu dhaifu kuliko zile zinazoshuka. Ndiyo maana wamezipa fursa na haki timu mbili za juu kupanda moja kwa moja wakati zile zingine zinapimwa na vibonde wenzao ili mwenye uafadhali kati yao ndiyo apande.

Tupe data za miaka 3 iliyopita, playoffs walicheza nani na nani na yupi alipita ili tupate mwanga zaidi kwenye hii mada.
Hakuna wa championship aliyetoboa kwenye playoff dhidi ya waligi kuu....tangu hii Kanuni ianze....
 
Pamba alicheza mtoano mara mbili

Alicheza msimu na Coastal Union akachezea
Alicheza msimu na Kagera Sugar akachezea

Msimu huu akatengeneza mikakati ya kupita moja kwa moja bila kucheza mtoano...

Makalla akatengeneza mkakati kwa kushirikisha wadau wa michezo mkoa wa mwanza ili pamba ipite

Na ndipo ikabadilishwa jina kuitwa Pamba Jiji FC ili iwe chini ya Jiji la Mwanza
 
Hii ni data ya misimu 4 iliyopita. Utaona data hizi hazisapoti hoja yako.

KMC, Mbeya City - KMC akabaki
Mtibwa, Prisons - zote zilibaki
JKT, Gwambina - zote zilishuka
Alliance, Lipuli - zote zilishuka
hivi umenielewa nilichokiandika hapo juu
 
Pamba alicheza mtoano mara mbili

Alicheza msimu na Coastal Union akachezea
Alicheza msimu na Kagera Sugar akachezea

Msimu huu akatengeneza mikakati ya kupita moja kwa moja bila kucheza mtoano...

Makalla akatengeneza mkakati kwa kushirikisha wadau wa michezo mkoa wa mwanza ili pamba ipite

Na ndipo ikabadilishwa jina kuitwa Pamba Jiji FC ili iwe chini ya Jiji la Mwanza
sawa lakini bado hujajikita kweny hoja yangu
 
Hii ni data ya misimu 4 iliyopita. Utaona data hizi hazisapoti hoja yako.

KMC, Mbeya City - KMC akabaki
Mtibwa, Prisons - zote zilibaki
JKT, Gwambina - zote zilishuka
Alliance, Lipuli - zote zilishuka
Mbeya ciyty alitolewa na mashjaatena kwa ujanja ujanja hadi kocha anapigwa na kuna baadhi ya wachezaji wa Mbeya city walirubuniwa na kuiacha timu kipindi cha playoff

mtibwa alikua ligi kuu alipambania nafasi akabaki katika mfumo huo huo wa play off kwa kua wao ni wakongwe walifanikiwa kubaki
 
Hii ni style ya kuzibeba timu zilizofeli ligi kuu, kwa mfano mtibwa haina jipya na hadhi ya kucheza ligi kuu ni huu uozo wa TFF na bodi yake ya ligi kuweka kanuni mbovu, play off za kucheza ligi kuu na championship duniani kote hamna hii kitu....only Tz!
 
Back
Top Bottom