Tetemeko la Ardhi Kagera: Serikali imeonesha udhaifu mkubwa sana

Wanasiasa ni wale waifanyao,waifuatiliao na wanaonufaika nayo siasa. Hawaishiwi maneno au matendo. Wanamaliza maneno au matukio haya,wanakwenda kwenye yake.

Lilipopatwa jua,hasa kule Rujewa Mbeya,ikasemwa na wanasiasa kuwa hiyo ni ishara ya kukubalika kwa Rais Dr. J.P.M. Jambo hilo likajadiliwa na kushangiliwa ikizingatiwa kuwa kulipatikana kipato pia. Wanasiasa wakaamini na kuaminisha kuwa ni dalili njema!

Limetokea tetemeko la ardhi na kusababisha vifo,majeruhi na uharibifu wa miundombinu. Taifa lipo pamoja kushughulikia hilo.Watu wote kimya. Hakukutokea wa kusema lolote. Ni kuogopa kuwa wachochezi au? Siasa ina vijimambo sana!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)

Umezificha kucha zako?Ah nimekumbuka kwa Mwanaccm hakuna shida ila ungekuwa mpinzani saa hizi Mzee wangu ningekuwa namtafuta Petro Kibatala
 
Serikali ya majanga hii Mkuu wako busy kuonyesha misuli yao dhidi ya wapinzani na hakuna chochote kinachoendelea ndani ya Serikali hii dhalimu. Ingekuwa CHADEMA/UKAWA wamefanya mkutano au maandamano mara moja wangeonyesha misuli yao lakini kwenye maafa ya Watanzania wenzetu hili halina kipaumbele kwao.

Pesa ya kuonyesha misuli dhidi ya CHADEMA/UKAWA wanayo nyingi sana kwenye maafa hawana hata senti moja wanapitisha bakuli kwanza.

Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaj katika ktuo cha redio huko Washington DC amesema

"Nyie TBC. Mnataka tuuu tuseme.
Nyie si ndio kituo cha TAIFA?
Nyie si ndio mnaoendeshwa kwa kodi ya wananchi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuhabarisha kinachotokea kule ambako radio za kibiashara haziendi?
Si ni nyinyi mnaostahili kuwa WAZALENDO zaidi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuweka maslahi ya nchi mbele?
Nyie si ndio mnaotakiwa kufanya coverage ya MATUKIO YA KITAIFA?
Iweje mnapuuza TUKIO hili la tetemeko?
Watu 16 wanaingizwa uwanja wa Kaitaba sasa, mamia wameumia na dazeni za nyumba hazifai kwa makazi, mnaendelea na vipindi vya MUZIKI. Seriously????
Mmewapuuza wahanga wa tetemeko hili kubwa.
Na mnaendelea kusema mnahimiza UZALENDO?"
 
Mpango wa maendeleo wa muda mfupi na muda mrefu ungejibu haya ya kagera na kwingineko kama yangepata muda wa kutosha kujadiliwa pamoja na wapinzani.

TUJIFUNZE KUWASIKILIZA HATA TUNAO DHANI HAWANA TIJA KWETU.
 
Sitochangia kampeni zozote zile za serikali kutaka wananchi wachangie haya mambo kwa sababu

Siamini kuwa serikali hii haina pesa za kuwasaidia wahana wa hili tetemeko la ardhi

Kama pesa zipo za kuthibiti wanaoikosoa serikali (last month alone wametumia close to 10 billion) then pesa za kuwasaidia waathirika zipo. Kodi nishakatwa za kila namna mpaka za kutumia JF sasa why nitoe tena pesa zingine?

Viongozi wa Serikali kuanzia rais mpaka wakurugenzi wa wilaya wakisamehe mishahara yao ya mwezi huu itatosha kabisa kuwasaidia waaathirika na kama hazitoshi watumie pesa za Mbio za mwenye kuwasaidia waathirika

Huo ndio msimamo wangu na naamini siko peke yangu mwenye kuamini hivyo.
 
Hata madiwani wa bukoba wakiachia posho zao za mwezi tu utakuwa ni mchango wa kutosha sana
 
Hauko peke yako, tupo wengi na huu ndio uzalendo wa kweli.

Red cross wameacha majukumu yao sasa wamekuwa Real estate agent na Viva tower yao halafu usawa huu mimi pangu pakavu unchangishe?

Nilimsikia kwa masikio yangu Mzee wa Chatu akisema hakuna msaada wa chakula kwa watakaokumbwa na baa la njaa.

Taifa ambalo halijajiandaa kwa majanga simply limejiandaa kwa maafa. wajuwauji na waendelee tu na ujuwaji wao.
 
Tulianza na madawati wakaomba sikuona mchango wa serikali

Jambo la dharula la tetemeko nalo wanaanza kwa kuomba omba..

nchi ya viwanda hii hawaombi bali wanailazimisha mifuko ya jamii kujenga viwanda...wapate faida au hasara its up to them.

Serikali msikimbie majukumu...haya ndio majukumu ya baba mwenye nyumba.
 
Magufuli si alisema kampeni yake haijachukua hata senti tano kutoka kwa mfanyabiashara? Sasa imekuwaje?
 
Tulianza na madawati wakaomba sikuona mchango wa serikali

Jambo la dharula la tetemeko nalo wanaanza kwa kuomba omba..

nchi ya viwanda hii hawaombi bali wanailazimisha mifuko ya jamii kujenga viwanda...wapate faida au hasara its up to them.

Serikali msikimbie majukumu...haya ndio majukumu ya baba mwenye nyumba.
Hawana Pesa Kwa sasa Pesa zote zilimalizikia kwenye UKUTA
 
Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaj katika ktuo cha redio huko Washington DC amesema

"Nyie TBC. Mnataka tuuu tuseme.
Nyie si ndio kituo cha TAIFA?
Nyie si ndio mnaoendeshwa kwa kodi ya wananchi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuhabarisha kinachotokea kule ambako radio za kibiashara haziendi?
Si ni nyinyi mnaostahili kuwa WAZALENDO zaidi?
Nyie si ndio mnaotakiwa kuweka maslahi ya nchi mbele?
Nyie si ndio mnaotakiwa kufanya coverage ya MATUKIO YA KITAIFA?
Iweje mnapuuza TUKIO hili la tetemeko?
Watu 16 wanaingizwa uwanja wa Kaitaba sasa, mamia wameumia na dazeni za nyumba hazifai kwa makazi, mnaendelea na vipindi vya MUZIKI. Seriously????
Mmewapuuza wahanga wa tetemeko hili kubwa.
Na mnaendelea kusema mnahimiza UZALENDO?"
Nadhani hii yote ni kwa sababu Bukoba mjini wallikataa Ccm. Hakuna kitu kingine hapo. Hakuna mantiki ya kutafanywa janga la Kitaifa.
 
TUMEKUWA tukiandika kuhusu ni jinsi gani TBC na ubunifu wa kurusha matangazo ya kwa muda muafaka lanini hawbadiliki. Wajifunze kwa CNN jinsi walivyo sharp kurusha live matukio ya ghafla pindi yanapotokea(Breaking News)
Tanzania ni nchi maskini sana. Kwa nini ulinganishe nà CNN? Hivi tutajitambua lini kwamba sisi ni maskini? Tuache utani, nchi ni maskini sana linapokuja suala la Tecnolojia. Kama tunashindwa kupack nyanya, kabechi, nyama, na vyakula mbalimbali vya kwaida, tunaweza kweli kuwa na vifaa vya kufanya kazi kama CNN? BBC? ALJAZEERA? FRANCE 24? SKY NEWS? Noooo... Big Noooo;;;;;;!!!!!
 
TUMEKUWA tukiandika kuhusu ni jinsi gani TBC na ubunifu wa kurusha matangazo ya kwa muda muafaka lanini hawbadiliki. Wajifunze kwa CNN jinsi walivyo sharp kurusha live matukio ya ghafla pindi yanapotokea(Breaking News)
Hawana hata huo uwezo wa kujifunza toka kwa yeyote isipokuwa mamlaka za uteuzi wa viongozi wakuu. Ukiuliza utaambiwa hawana pesa za kurusha ysnayojili eneo la tukio la dharura.
 
Back
Top Bottom