Tatizo la Yanga

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,660
Wakuu, baada ya mechi ya jana ya Kombe la Shirikisho sasa ni dhahiri kuwa timu ya Yanga wana tatizo la mipira ya kutenga. Kumekuwa na matukio mfululizo ya kufungwa mabao yanayotokana na mipira hiyo. Hata mechi ya jana dhidi ya Prisons mapungufu hayo yameonekana. Kocha Prof Nabi ana kazi kubwa ya kufanya kwenye eneo hilo.
 
Hivi Manara Carrier Yake Ya Usemaji Wa Soka Vikiisha, ni Kitu gani Kitakachofanya Akumbukwe..?

Mimi nadhani ni Ile Kauli Yake Kuwa.. nanukuu " Yanga Wote ni Hamnazo isipokuwa Baba ake Na Mzee JK" Mwisho Wa Kunukuu..!
 
Mimi nashukuru ule wimbo wa kusema Aishi Manula anafungwa magoli yanayofanana sasa umeanza kupata majibu kwa kuhamia kwa waliokuwa wanamsema. Ingawa likifungwa huku inasemwa Yanga (sio Djigui Diara), likifungwa kule kule anasemwa Manula (sio Simba)
 
Wakuu, baada ya mechi ya jana ya Kombe la Shirikisho sasa ni dhahiri kuwa timu ya Yanga wana tatizo la mipira ya kutenga. Kumekuwa na matukio mfululizo ya kufungwa mabao yanayotokana na mipira hiyo. Hata mechi ya jana dhidi ya Prisons mapungufu hayo yameonekana. Kocha Prof Nabi ana kazi kubwa ya kufanya kwenye eneo hilo.
ni kweli,timu za ndani na za nje zinafunga hivyo
 
Na Aseno nao washaurini watafute dawa wanafungwa Sana seti pisezi.
 
Hivi Manara Carrier Yake Ya Usemaji Wa Soka Vikiisha, ni Kitu gani Kitakachofanya Akumbukwe..?

Mimi nadhani ni Ile Kauli Yake Kuwa.. nanukuu " Yanga Wote ni Hamnazo isipokuwa Baba ake Na Mzee JK" Mwisho Wa Kunukuu..!
Hivi kwa mfano mtu mgeni ambae unaJua kabisa pale Mlimani ambako Sisi tuliishi kama home kwetu tukisoma vitabu vigumu wakati yeye akisoma Madrasa mtu huyo wa Madrasa kwa mfano akija kwenye kikao chenu Cha ukoo Kimara akapayuka akasema "nyie wote mliokusanyika hapa ukoo mzima hamna akili isipokuwa mke wangu TU Yuko home na shoga yake wa Buza kwa Mpalanger " kwa kauli hiyo tayari nyie wote ukoo mzima mnakuwa Vilaza? Hivi kauli imekaaje kisayansi kwamba inatoa akili za watu?

Nawahurumia sana wanasimba waliovurugwa kwa kiwango kibovu wachezaji wazee kocha mnene mbumbumbu fc kwa kudandia kauli za kijinga na kutembea Nazo!!
 
Back
Top Bottom