SoC03 Tanzania ya viwanda inawezekana

Stories of Change - 2023 Competition

saadala muaza

Member
May 12, 2023
38
37
TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA
Kuiga kizuri si dhambi.Ni vyema tukarudi nyuma mpaka katikati ya karne ya 18.Uingereza ilikuwa na uchumi wa kati na ni hata nyuma zaidi ya hapa tulipo sisi sasa.Si hili tu India pia ni nchi ambayo kwa kiasi kikubwa vijana wengi na familia nyingi zenye maisha ya kati zimejikita katika uzalishaji wa nguo kwa kutumia vifaa vya kitamaduni.

Je nini tufanye?

Kwanza: Ni lazima serikali ijipambanue na kujielekeza katika teknolojia ya kisasa kama matumizi ya matrector mashambani,mbolea na kujikita katika kilimo cha umwagiliaji.

Pili: Ni lazima pia serikali kuwekeza katika viwanda vya kisasa vya utengenezaji wa nguo.Tofauti na matumizi ya viwanda vyenye mifumo ya kizamani vilivyoachwa na waasisi wetu.

Tatu:Upatikanaji wa umeme na nishati ya uhakika.Hili ni vyema serkali ikajikita katika kuandaa na kutafuta vyanzo zaidi vya nishati tofauti na matumizi ya maji pekee.

Nne:Uzalishaji wa rasilimali bora ya watu katika nyanja tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na wabobezi katika sayansi na teknolojia ya kisasa.

Faida ya kuwa na maendeleo katika nyanja ya viwanda.

1. kuimaruka kwa uchumi wa taifa kwa ujumla.
2. Maisha bora kwa kila mtanzania .
3. Kuongezeka kwa pato cha taifa.
4. Maendeleo katika Nyanja tofauti tofauti zikisukumwa na viwanda.
5. Upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika.
6. Nchi kujitegemea katika bajeti na si kutegemea mikopo na misaada yenye masharti magumu.
7. kuongezeka kwa umri wa kuishi kwa Watanzania.

Changamoto mbalimbali katika kuyafikia malengo haya.

1.Uwepo wa Viongozi walarushwa.
2.Ukosefu wa uthubutu kwa viongozi wa ngazi za juu.
3.Ukoloni mamboleo.
4.Uwepo wa Viongozi wenye tamaa na mali pamoja na madaraka.
5.Uwepo wa sera mbovu na usimamizi mbovu wa maono ya raia wa nchi hii.
6.Ukiritimba na ubeberu wa baadhi ya viongozi wenye tamaa ya kujilimbikizia mali.
7.Uwepo wa viongozi vibaraka wa mabeberu katika nchi yetu.

Asanteni. By Saadala Muaza.
EnvisolInfrastructure-Arvind-Envisol-alwoFr2Sx1U5jM.jpg
 
Back
Top Bottom