NDUGU WAPENDWA WATEJA WETU MNAOTOA TAARIFA KUPITIA MITANDAO YETU YA KIJAMII TUNAWAOMBA MZINGATIE YAFUATAYO ILI KURAHISISHA UFAFANUZI NA UFUMBUZI WA TATIZO AU TAARIFA HUSIKA

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)

TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Kw mawasiliano Kituo cha Miito ya Simu (+255) 22194400 or (+255) 768 985 100 Mitandao ya kijamii Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter Facebook: Tanesco Yetu

IMETOLEWA NA:- Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makauu
Asante kiongozi. Hiyo namba ya simu uliyoweka ni 24 hours ili tukupigie?

Vv
 
TANESCO

Namba (06),,,,,me mmenifungia mita ambayo nashindwa hata kusoma kiasi cha Unit kilichobakia, ,huwa kila sekunde inakuja minamba namba tofauti, ,,msaada
 
Ukitoa taarifa ka mfumo uliotajwa hapo juu hata hapa jamii forum wataalamu wetu watifikish mkoa husik
Mkuu hujanijibu, unajibu ki-PR, hizo namba za simu zinajibiwa 24 hrs? Halafu nakuomba utuwekee namba za emergency kwa wilaya za mkoa wa Dar, mimi nahitaji namba za Wilaya ya Kigamboni.

Vv
 
Mbagara charambe why Tanesco mnatutesa na umeme badoshida mwezi sasa unakatika umeme haunataarifa haueleweki
 
Tunashukuru , naomba kuuliza hizo no zinapatikana wakati gani. Kwani hiyo no ya Voda nilishawahi kupiga zaidi ya mara kumi bila kupokelewa na nilikua na tatizo
Namba (06),,,,,me mmenifungia mita ambayo nashindwa hata kusoma kiasi cha Unit kilichobakia, ,huwa kila sekunde inakuja minamba namba tofauti, ,,msaada

kila mita ya tanesco inakuwa na namna inayoonyesha salio la umeme..kuna mita kila baada baada ya sekunde kadhaa inajibadilisha lakn unapojibadilisha kuna namba zinatokea kubwa na namba ndogo zinakuwa kama sio 00 ni 01 kama ukiona namba inatokea na kuandika 00 hio ni jumla ya umeme ulitumia hadi leo na ikijibadilisha na kuandika namba alafu juu inakuwa namba ndogo ikisomeka 01 inakuwa ni salio la unit ambalo lipo kwa sasa.

je mita yako ikibadilika ìnakuwa na maelezo kama hayo..
 
Mbagala mnakata sana umeme
mkuu Shirika siku zote linapenda kusikia wateja wake wanafurahia huduma zetu. hivyo basi sio ukiona TANESCO wamekata umeme sehemu jua tu kuna tatizo au ni dharura.

Tunaomba radhi kwa hilo na tutahakikisha tutakuwa tunatoa taarifa mapema kwa wateja wetu
 
Nahitaji umeme nyumbani kwangu lakin tanesco tanga wamekua na bla bla nyingi. Mtanksaidiaje nipo tanga mjini

mkuu tutaomba kujua kama umeshachukua fomu na kulipia. je umelipia gharama ya nguzo au bila nguzo bila kusaau ni tarehe ngapi kama ulilipia. tutafurah kama tutapata mawasiliano yako pia.

usiku mwema
 
mkuu tutaomba kujua kama umeshachukua fomu na kulipia. je umelipia gharama ya nguzo au bila nguzo bila kusaau ni tarehe ngapi kama ulilipia. tutafurah kama tutapata mawasiliano yako pia.

usiku mwema
kuunganisha mteja bila nguzo shilingi ngapi? ikiwa na nguZo shilingi ngapi?

baada ya kujaza form na kulipia mpaka kufungiwa huchukua wiki ngapi?
 
mkuu tutaomba kujua kama umeshachukua fomu na kulipia. je umelipia gharama ya nguzo au bila nguzo bila kusaau ni tarehe ngapi kama ulilipia. tutafurah kama tutapata mawasiliano yako pia.

usiku mwema

Nawashukru kwa huduma hii, Mi niko Mwanza nina tatizo kama la ndugu hapo juu nimelipia TANESCO-NYAKATO nguzo mbili tangu Tarehe 6 Septemba 2016 hadi leo sijaletewa nguzo, kila siku madai ni hakuna nguzo sasa mi kama mteja hamuoni kama mnanionea?

Ikumbukwe hadi kulipa hiyo pesa kuna huduma niliamua kutozifanya ili nipate huduma ya umeme, badala yake nimekosa huduma zote mpaka leo huku nyie pesa yangu mkiifanyia biashara.

Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu jambo hili.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Mimi Niko chanika Niko sehemu iliyoteuliwa kupata Umeme wa rea
Fomu nishajaza tangu January 2016 ila mpaka Leo sijapata hiyo huduma
Tanesco wanasema hiyo sio sehemu yao mpaka watakapokabidhiwa na REA
Swali je? Nilini mtakabidhiwa hilo eneo rasmi?
Pili, kwa Mimi nitaweza kupata hiyo huduma chini ya rea?
Maana kila nikienda pale kisarawe hawa jamaa siwakuti
 
Natumaini mnategemea kupokea details za watu humu kwa PM, na nyie kuwajibu na kuyatatua.

Wadau andikeni humu eneo na kuwaambia details zaidi za kwenu kama namba ya simu, unapoishi etc mnawaandikia PM. Hii ni kwa ajili ya usalama wako wewe mteja wao.

Ila mkiona hawafanyi kitu, basi unarusha humu kwenye uzi wao kuwasema chochotekama wamekushughulikia au la. Itasaidia wengi mkiweka updates kujua wanafanya kazi zao

Pamoja tutafika.
 
Mbagala mnakata sana umeme
Kuna miradi mikubwa inayofanyika ya uboreshaji Huduma ya umeme Jijini Dar es Salaam, Vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini vinapata umeme wa msongo wa kilovolti 33, kutokana na ongezeko la Watu na shughuli za Kiuchumi maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo kuzidiwa
ndio maana Serikali kupitia TANESCO inaviboresha vituo hvyo vya Kupoza na Kusambaza Umeme kwa kuviongezea uwezo mkubwa wa Kilovoti 132.

Maboresho hayo yanategemewa kukamilika mwaka huu hivyo kuondoa tatizo la umeme kuwa mdogo na kukatika katika kwa umeme maeneo hayo.

TANESCO inawaomba Wananchi kwa ujumla, kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha Miradi ya uboreshaji umeme
zikiwa zinakaribia kukamilika.
 
mkuu tutaomba kujua kama umeshachukua fomu na kulipia. je umelipia gharama ya nguzo au bila nguzo bila kusaau ni tarehe ngapi kama ulilipia. tutafurah kama tutapata mawasiliano yako pia.

usiku mwema
Mbona hunijibu kuhusu hili

Nawashukru kwa huduma hii, Mi niko Mwanza nina tatizo kama la ndugu hapo juu nimelipia TANESCO-NYAKATO nguzo mbili tangu Tarehe 6 Septemba 2016 hadi leo sijaletewa nguzo, kila siku madai ni hakuna nguzo sasa mi kama mteja hamuoni kama mnanionea?

Ikumbukwe hadi kulipa hiyo pesa kuna huduma niliamua kutozifanya ili nipate huduma ya umeme, badala yake nimekosa huduma zote mpaka leo huku nyie pesa yangu mkiifanyia biashara.

Naomba nipewe ufafanuzi kuhusu jambo hili.

Natanguliza shukrani zangu.
 
Huku Tarime umeme umekua ni kero, leo tu toka asubuh umekatika zaid ya mara 4...Mtatuunguzia vifaa vya umeme
 
Back
Top Bottom