Tahadhari: Kwa hali ilivyo tusishangae kushuhudia kifo au vifo kwa wanagombania kupanda Mwendokasi

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
925
4,317
Last week ndugu yangu aliumia mgongo kwa kusukumwa akipanda Mwendokasi Kariakoo. Nilitoka Mwanza kwenda kumsalimia kisha nikaenda kujionea mazingira yaliyopelekea yeye kuumia.

Naomba niseme tu kwamba kwa hali ilivyo kituo cha Msimbazi na Gerezani sitashangaa kukatokea kifo.

Kwa namna watoto wanavyosukumwa na jinsi abiria wanavyogombania magari tutapata maafa.

Niwaombe viongozi wa Mwendokasi na viongozi wa serikali, itasikitisha sana kujitokeza kuomboleza vifo vya wanafunzi katika kituo cha Msimbazi, Kivukoni,Gerezani, DIT,Fire, Korogwe na Kimara. Naandika just kutoa taadhari nikitambua sikio la kufa alisikii dawa
 
Last week ndugu yangu aliumia mgongo kwa kusukumwa akipanda Mwendokasi Kariakoo . Nilitoka Mwanza kwenda kumsalimia kisha nikaenda kujionea mazingira yaliyopelekea yeye kuumia.

Naomba niseme tu kwamba kwa hali ilivyo kituo cha msimbazi na Gerezani sitashangaa kukatokea kifo.

Kwa namna watoto wanavyosukumwa na jinsi abiria wanavyogombania magari tutapata maafa.

Niwaombe viongozi wa Mwendokasi na viongozi wa serikali, itasikitisha sana kujitokeza kuomboleza vifo vya wanafunzi katika kituo cha Msimbazi, Kivukoni,Gerezani, DIT,Fire, Korogwe na Kimara. Naandika just kutoa taadhari nikitambua sikio la kufa alisikii dawa
Umaskini wa watanganyika ni furaha ya wachumia matumbo wa CCM.
 
Kwanini wananchi msipange foleni? Kuna kipindi pale kivukoni nilikuwa napanda kwa foleni, siku hizi imekuaje?
1. Utaratibu ule ulifanikiwa hapo awali wakati ulinzi ulikuwa ukisimamiwa na SUMA JKT, baada ya kubadilisha na kuweka kampuni binafsi ya ulinzi wanashindwa kudhibiti abiria kupanga foleni.

2. Utaratibu wa kupanga foleni unakuwa mgumu sababu unahitaji sana kuratibiwa na madereva wa mwendokasi ambaya anapaswa kudhibiti abiria kwa kuhakikisha mlango mmoja tu wa gari ndio unaofunguliwa, badala yake wakifika vituoni kama kivukoni wanafungua milango yote na kusababisha watu kugombania. Kwa kweli ni kero sana hakuna ustaarabu tena.
 
Last week ndugu yangu aliumia mgongo kwa kusukumwa akipanda Mwendokasi Kariakoo. Nilitoka Mwanza kwenda kumsalimia kisha nikaenda kujionea mazingira yaliyopelekea yeye kuumia.

Naomba niseme tu kwamba kwa hali ilivyo kituo cha Msimbazi na Gerezani sitashangaa kukatokea kifo.

Kwa namna watoto wanavyosukumwa na jinsi abiria wanavyogombania magari tutapata maafa.

Niwaombe viongozi wa Mwendokasi na viongozi wa serikali, itasikitisha sana kujitokeza kuomboleza vifo vya wanafunzi katika kituo cha Msimbazi, Kivukoni,Gerezani, DIT,Fire, Korogwe na Kimara. Naandika just kutoa taadhari nikitambua sikio la kufa alisikii dawa
Hoja yako isikilizwe na mamlaka husika na hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo.
 
Kwanini wananchi msipange foleni? Kuna kipindi pale kivukoni nilikuwa napanda kwa foleni, siku hizi imekuaje?
Kivukoni kola siku wapanda mwendokasi pale utaratibu wa foleni upo vile vile na milango unaofunguliwa ni mmoja tu ila kunakuwa na foleni mbili mmoja ya watu waotaka kukaa mwenye kiti hao huwa wanaanza kuingia foleni ya pili ni wenuye haraka waosimama
 
Mabasi yanaachana kwa Interval hadi ya Dakika 20 wakati mwingine.. Ni ngumu kuambia watu wapange foleni wakati mtoa huduma hana consistency na hazingatii muda.

Imebaki Abiria kugombania na kugombana tu.
Dar watu wake hawajastaarabika kwa kweli, wao kila kitu ni kugombania tu! Halafu hawa jamaa wa mwendokasi nao wangekuwa wanapishanisha mabasi hata dakika 10 ingekuwa afadhali. Sasa mtu unakaa kituoni mpaka nusu saa hujaona gari!
 
Niliwahi kaa gerezani toka saa kumi na moja na nusu jioni hadi kumi na mbili na dk 25,

Yani watu wanasimama hadi wanachoka wanaamua kukaa

Basi likija ni vurugu kila mtu anasema nilikuwa hapa wengine hawakubali mwisho wa siku line inavurugika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom