Ndugu zangu,
Nahofia tunachanganya na kushindwa kutofautisha kati ya dini, siasa na siasa za vyama.
Mengi ya kila siku maishani yana siasa ndani yake lakini si lazima yawe na siasa za vyama. Kiongozi wa kiimani anapaswa kuwa huru kuzungumzia kwa ujumla wake masuala ya kijamii kwa lengo la kuelimisha na hata kuasa.
Kiongozi wa kiimani kwenye kusanyiko la waumini wenye itikadi tofauti si vema na busara kumtafuta kondoo wa dhambi wa kunyoshewa kidole na waumini kwa mtazamo wa siasa za vyama.
Na viongozi wa kiimani wanaweza mioyoni mwao kuwa na mitazamo binafsi ya kiitikadi na hata mapenzi kwa vyama vya siasa, lakini, hawapaswi kuyaonyesha hayo mbele ya waumini wao na jamii kwa kupitia majukwaa ya kiimani.
Kutokufanya hivyo, tutafika mahali tutawaona waumini nao wenye kuonyesha hisia zao za kiitikadi kwenye nyumba za ibada. Hapo tutakuwa tumepotea njia.
Maana, kwa kiongozi wa kiimani, waumini wote ni wake, bila kujali tofauti zao za kiiitikadi.
Na hakika, ni busara na hekima, kwa mwanadamu kutambua na kuheshimu mamlaka iliyopo na zaidi, inayotokana na watu.
Kutambua na kuheshimu mamlaka inayotokana na sheria, kanuni na taratibu za mahali husika, hivyo basi, mamlaka inayotokana na Katiba ya wakati huo.
Na mwanadamu huyo, midhari amefanya mawili hayo, ana lazima ya kufanya jambo la tatu; kuyaenzi mamlaka hayo.
Tafadhali Usininukuu."
Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)