News Alert: Tabia ambazo Wanawake wanatakiwa kuziacha kwa ustawi wa jamii bora

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,638
Hizi ni tabia ambazo zimeanza kuwa sugu kwa watoto wa kike ambazo kwa bahati mbaya hazina faida na ndizo chanzo kikubwa cha watoto wa kike wa miaka hii kufeli katika mahusiano na kuwa na maisha yasiyo na direction ya kueleweka katika jamii hata pale wanapokuwa na mafanikio.

Ukipita huko mtaani utakuta kuna watoto wa kike wakilalamika sana na kuona kama kuna ubaya wanafanyiwa na wanaume ila hata maneno ya busara husema kuwa, kabla haujalaumu mtu kukusababishia tatizo jiulize wewe una mchango gani juu ya hilo tatizo.

1. Tabia ya kujilinganisha na jinsia ya kiume.

-Hapa ndipo nuksi zinapotafutwa. Kwa miaka mingi kampeni za kifeminist na wanaharakati wa nchi za magharibi ambao wameambukiza na wanaharakati wa mataifa yanayochipukia kama Tanzania zimelenga katika kumshusha mwanaume katika nafasi yake na kumuweka mwanamke badala ya kutetea haki za kimsingi za mwanamke. Kimsingi wamepoteza lengo la msingi.

Miaka hii wanawake wanatia jitihada katika kushindana na kujilinganisha na mwanaume badala ya kuwa wao kama wao. Hii huwa mo dosari kubwa sana kwa mwanamke, maana hakuna mwanaume wa kueleweka atakuja kukusogolea mwanamke kiburi au unaemletea jeuri za kujishindanisha nae.....hapo hakuna heshima hata kidogo.

2. Kutoheshimu miili yao.
- Mwili wa mwanamke anayejisitiri na kuuficha machoni pa walafi wa ngono huwa una usalama na mvuto wa heshima. Leo hii wanawake wengi wao hawaheshimu miili yao kwa wao wenyewe kusababisha hivyo.

Aidha kupitia mavazi yasiyo na staha (wao huyaita mapigo), ambayo huvaliwa kwa kuexpose maeneo ya miili yao na kuwavutia wanaume wapenda ngono na si wanaume ambao hutaka utulivu na upendo katika maisha. Tabia hii imesababisha vilio vingi vya kuchezewa, au kusalitiwa au kutumiwa na wanaume wapenda ngono kisha lawama zikaelekezwa katika kada yote ya wanaume.

3. Tamaa ya mali na vitu vya mpito

Wanawake wengi ni wahanga wa tamaa ya vitu vya kidunia ambavyo hupotea na muda. Hii imepelekea wengi kutokuwa na misingi imara ya upendo wa dhati na badala yake wameambukizana kasumba ya kupenda vitu badala ya mtu na mwishowe wameonekana takataka mbele ya wanaume wenye pesa zao na kushuka thamani kwa wanaume wenye mapenzi ya kweli.

4. Kujirahisi
Watoto wa kike wengi miaka hii wamekata tamaa sana juu ya future zao. Unaweza kuta binti anawasiliana kimahaba na wanaume zaidi ya kumi na yeye anajionea sawa tu hakuna shida. Hili linajidhihirisha kwa namna wanavyokuwa wepesi kujitongozesha au kutoa nafasi kwa wanaume zaidi ya m'moja kwa wakati kwa kisingizio kuwa mahusiano hayadumu, au wanatafuta faraja ya muda pale ambapo mahusiano yao yanapitia misukosuko ya kawaida au tu basi kujiruhusu kuwa na tamaa ya kutumika miili yao kwa mtu zaidi ya m'moja. Hii imeshusha thamani ya watoto wa kike wengi.

5. Kutokuheshimu vitabu vya MUNGU.
- Katika hali ya kawaida, kwa mtu yoyote anapojiweka mbali na mafundisho mazuri ya MUNGU ambayo hutumika kutulinda na pia kama muongozo wa mienendo yetu, then mtu huyu huwa katika hatari ya kupotea maisha yake yote na kujikuta pahala sio.

Kujifunza na kutii maneno ya MUNGU huwa ina mpa mtu ulinzi wa kuepuka na maovu pamoja na watu waovu na kumpa sura na haiba nzuri mbele ya jamii. Hata wale wanaume waovu hawatakuwa na ushawishi juu yake wakutaka kumtumia na kumharibia maisha yake.

Ila hali halisi haipo hivyo. Kwasasa mabinti wengi wanapata miongozo yao kupitia post za social media kama Instagram, Facebook na hata whastapp. Kwamba hizo ndizo zimekuwa ni bible zao kwa sasa na wanazifanyia kazi kweli kweli maneno ambayo yametungwa na kutengenezwa na binadamu wenzao. Usishangae kwann wengi leo hii kuharibikiwa katika maisha imekuwa ni swala la kawaida sana. Na lawama hutupiwa wanaume wote ila ujiulize ni mwanaume ndie aliyekuzuia kumjua MUNGU na kuheshimu maandiko yake.

6. Kutokuwa wawazi wa hisia na kuwa na michezo ya hisia.
- Miongoni mwa shida ya watoto wa kike now days ni kupenda michezo ya hisia wakati wa kufanya maisha serious.

Watoto wa kike wa leo anaweza kuwa na hisia na ww na asikwambie akitaka tu uhangaikie kujua yeye anajiskiaje juu yako. Hii huwakatisha tamaa watoto wa kiume wengi ambao tofauti na zama za wazazi wetu, wa kisasa wana mambo mengi kichwani na ni ngumu kubalance upuuzi na mambo ya msingi.
Unakuta binti anasumbua akili kisa tu anataka amuonyeshe mwanaume kuwa yeye sio mwepesi, ila cha ajabu binti huyo huyo, akija diamond atamla siku hiyo hiyo bila kumtongoza......hapo ndipo huwa hawaeleweki hawa viumbe....


Tabia zipo nyingi sana......siwasemi hapa ili mjisikie vibaya na kujibu, ila nawasema ili mjitafakari na kurejea misingi yenu ili tuokoe jamii yetu ambayo kwa sasa inaharibika kwa kasi sana.....

Tufanye kushare na zinginezo ambazo zikuzigusia hapa ili hawa viumbe wajifunze na kurekebisha....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo Ujinga ndio maana Baba wa Taifa alisema tuna maadui watatu MARADHI , UJINGA na UMASIKINI sasa kipindi hiki asilimia kubwa ni WAJINGA na ukishakuwa mjinga lazima uwe masikini na utapata MARADHI


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kweli tupu, hii inapelekea kuumizana kimapenzi na kusababisha wengi kuathirika kisaikolojia. Mwisho wa siku jinsia moja kuona wote wa jinsia ya pili kuwa ni wanyama hata ikitokea amependwa kiukweli hathamini kwa sababu ya historia ya maumivu aliyopata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli kabisa, hasa hiyo tabia ya kutaka kuwa juu ya mwanamme kimaamuzi ilinifanya kuachana na mabinti kadhaa niliowahi kuhusiana nao kabla ya kuoa.


Hata humu JF wamo wanawake wa tabia hii, Urafiki wa kawaida tu ila atakupangia masharti magumu utafikiri unataka kupanda AIR FORCE ONE.
 
Ukweli kabisa, hasa hiyo tabia ya kutaka kuwa juu ya mwanamme kimaamuzi ilinifanya kuachana na mabinti kadhaa niliowahi kuhusiana nao kabla ya kuoa.


Hata humu JF wamo wanawake wa tabia hii, Urafiki wa kawaida tu ila atakupangia masharti magumu utafikiri unataka kupanda AIR FORCE ONE.
Nilikuwa na mmoja huyo ilikua serious relation ..nilikiwa nimemzidi kipesa ,kikazi,kiakili lakin anajifanya mjuaji sana.. masharti kibao.. akawa ana force ndoa kwa nguvu.
Nikaona siwez ishi namwanamke mbishi ndani ya nyumba. Nikafukuza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na yoooote kuna vitu huwa havibadiliki na vitabaki kuwa hivyo daima dawamu...mwanaume atabaki kuwa mtu mume na mwanamke atabaki kuwa mtu mke,.hivyo nafasi hizi mbili haziwezi kulinganishwa,kila nafasi itabaki kwa jinsi yake..muhimu ni kila mtu kufanya wajibu wake kama mwanamke na mwanaume kwa nafasi zao..

Kujua thamani na kujitambua kwa msichana ni jambo muhimu la kulijua na kujifunza,maisha yanabadilika kila iitwapo leo na wakati haumngoji mtu,.muhimu ni kujipanga na kujua nn unastahili katika haya maisha baasi,.

Kukosa staha,kujilinganisha, uvivu,kujirahisi,kuwa na tamaa ya vitu pengine viko nje ya uwezo wako,kukosa utii na maadili ni shida inayotukumba wadada lakini hayo yote tunaweza kuyakwepa kwa kutambua THAMANI NA WAJIBU wetu kama wanawake werevu..

Rasilimali muhimu tuliyopewa wote ni MUDA tukiutumia vizuri hata Mungu hatosita kututegea sikio tukimuita...tukubali kubadilika na kuendana na wakati la sivyo vilio,ghadhabu,sononi na mambo ya kuumiza mioyo hayatoisha kamwe.
 
Tabia mojawapo ya kuacha ni ile ya Kuipenda CCM haalfu baadae wanatuigia makelele
 
Mkuu umeongea kweli tupu ila kwa kizazi hiki cha dot.com ni kama unampigia mbuzi gitaa
 
Back
Top Bottom