Swali fikirishi: Kanda ya Kaskazini ingelikuwaje endapo utawala wa kimajimbo /Kikanda ungeruhusiwa Tanzania?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
5,196
7,071
Tetesi zisizo rasmi ni kuwa baadhi ya watawala wa Tanganyika walikuwa wakiwahofia watu wa ukanda huo! Sina uhakika kama hayo ni ya kweli au ni porojo tu.

Hata wengine wameenda mbali kwa kidiriki kusema kuwa Nyerere alilazimia kutokuruhusuKanda hiyo kumtoa Rais wa Tanganyika.

Ingawa yote hayo yasemwayo yanaweza uasiwe na ukweli, lakini ni kweli kuwa Kanda ya Kaskazini ni kati ya maeneo yenye maendeleo nchini. Na siri kubwa ya mafanikio yake ni kukumbatia Elimu.

Unafikiri, utawala wa kimajimbo ungeruhusiwa Tanzania, hivyo kila Kanda inakuwa huru kusimamia na kutumia rasilimali zake bila kuingiliwa na Serikali Kuu, Kanda ya Kaskazini ingekuwa na hali gani kwa sasa? Ingekuwa imeendelea zaidi ya ilivyo sasa?

 
Tungekuwa na ubaguzi na tishio kubwa bora hata sasa amani imetawala, na shukrani kwa mwamba kutoka Mara ambaye aliweka misingi ya nchi hii

Hao jamaa wangepata kiti sipati picha tungekuwa na nchi ya aina gani
 
Back
Top Bottom