Swalha na Said walishakubali ndoa imekufa ila wadananda wakaendelea kuishinikiza kwa manufaa yao binafsi

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,181
2,945
Dada mdogo wa marehemu mke amesema dada yake alimwambia kashachoka kutukanwa na mumewe na hadhani kama ndoa ina manufaa, mdogo mtu aliendelea kumshinikiza amalize mgogoro kwani yeye anaona wanagombania kitu ambacho hakipo hivyo rahisi kusuluhisha. Mdogo mtu alikuwa anaishi kwenye nyumba nzuri ya shemeji na gari la dada alikuwa analitumia kupigia misele mjini.

Marehemu mume alishamwambia mzazi mwenzie waliyeachana warudiane kwani hamuelewi mkewe, mwezi March Said alimpeleka mzazi mwenzie nyumbani kwake anapoishi na Swalha, alipomuuliza mkeo yuko wapi akasema amerudi kwao.

Said alimwambia mama yake wiki moja kabla ameshika sanda na akazimia papo hapo, usiku huo huo baba mkwe akapata mganga na kwenda 'kumuagua'. Ni ndoa iliyokuwa inasongeshwa mengi.

Hata sababu ya mke kwenda mara kwa mara kwao ni dalili nyumba ilishamshinda.

Watu mpaka wamelazana hospitali kwa kipigo bado mnang'ang'aniza waendelee!

Wazazi, mashemeji na mawifi, wahusika wakichemka tusishinikize mambo yaendelee. Wahuska ndio wanajua zaidi yaliyomo ndani mwao.

Swalha.jpg
 
Maelezo yao tayari wanajichanganya na ni bora wangekaa kimya kipindi hichi kipite, wanaona wanamtetea kumbe wanamvua nguo marehemu. Kuna mahali mama mtu alieleza na ukitafakari wazi unaona mwanae alikuwa tatizo. Bora wanyamaze hawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom