SoC04 Sura mpya ya Tanzania: Manufaa kwa kizazi cha sasa na kinachokuja

Tanzania Tuitakayo competition threads

Nado boy

New Member
Jun 20, 2022
1
1
Imezoeleka katika chambuzi nyingi, watu husifia. Lakini ni vigumu sana kufanya uchambuzi kwa kuonesha makosa au udhaifu katika nyanja mbalimbali hususani katika jambo unalolifanyia kazi. Bila ya kukinzana na matakwa ya jukwaa hili zifuatazo ni hoja zinazoonyesha Matarajio au shauku ni kivipi itakiwa kuwa Tanzania ijayo, kwa manufaa ya watu wote. Ili uweze kupata Matarajio hayo lazima uonyeshe udhaifu wa sehemu Fulani au ufanye tathmini ya kukuza kilicho Bora.

Ni matumaini yangu kuwa Tanzania ijayo inapaswa kufanya mabadiliko katika nyanja za Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii. Kama ifuatavyo;

Mabadiliko katika nyanja ya Kiuchumi:
(a) Ziwepo Sheria na mazingira wezeshi katika kunufaisha makundi yote.
Kwani katika ofisi nyingi iwe za kiserikali au binafsi, siku hizi inaonekana Kuna mazingira yanayowabeba wanawake katika kuajiriwa au kufanya kazi, yaani idadi Yao imeongeka. Lakini Kuna kundi la vilema ambao mara nyingi Huwa hawatajwi, kundi hilo wapo ambao wamesoma mpaka vyuoni, lakini nafasi zao za ajira hazionekani. Hali hii huwarudisha nyuma sana kundi hili ambalo hujiona kana kwamba wametengwa katika kushiriki katika kukuza kipato Chao hata kwa Taifa.

(b) Mfumo wa familia katika masuala ya Kiuchumi.
Katika familia nyingi Baba pekee ndio huonekana anatoka na kwenda kufanya kazi bila kumshirikisha mke wake, hali hii humpelekea mama kuwa kama mzigo katika familia kwani Kila kitu hutegemea kutoka kwa Mume wake. Mfano, Mke haruhusiwi hata kuingia dukani kwa Mume wake. Hali hii hufanya akili za wanawake wengi aidha vijijini au Mjini kudhoofika na kuona hawawezi lolote, hivyo hutumia zaidi kuliko wanavyotengeneza pesa, hivyo basi, huleta Taifa lenye wategemezi wengi kuliko nguvu kazi.

Vilevile, wanaume wengi kwenye familia ambao hupambwa kama "kichwa cha familia", mara nyingi Huwa hawawahusishi watoto zao katika kufanya kazi za kuingiza pesa. Mfano watoto wengi hawahusishwi kwenye kazi mfano, za kibiashara. Wazazi wanaamini kuwa Bado wanasoma, hawapaswi kujua hata kufungasha mizigo ya dukani, hivyo vijana wengi hawana maarifa ya kijasiliamali au utafutaji pesa, na hivyo hutegemea elimu ya shuleni tuu. Na hivyo, baadaye huonekana kuwa mzigo kwa Taifa.

Mabadiliko katika nyanja za Kisiasa:
Inapaswa kufahamika kuwa siasa ndio injini ya nyanja zote nchini na hata Duniani. Mfumo mzuri wa siasa hupelekea mabadiliko ya kimaendeleo katika nyanja nyingine. Hivyo inabidi Kuwepo kwa vitu vifuatavyo Ili kubadilisha mfumo wa siasa nchini Tanzania;

(a) Nguvu ya mamlaka inabidi irudishwe kwa wananchi.
Kwani Ukweli ni kwamba Wananchi ndio waamuzi wa mamlaka ya serikali, na wao ndio wanaorasimisha na kuwapa ajira Viongozi wa Kisiasa serikalini. Lakini baada ya kuwapa ajira kupitia vituo vya kupigia kura, Viongozi huchukua madalaka yote na kuwakandamiza Wananchi. Hivyo wananchi wanapaswa kufahamu kuwa wao ndio wenye nguvu na hivyo wasijihisi kuwa sehemu tofauti na serikali Yao, na inabidi waweze kuwajibisha Viongozi pale wanapenda mrama.

Inabidi wawepo Viongozi wa Kisiasa hususani chama tawala ambao wanatambua nguvu ya wananchi kipindi wanapohitaji jambo lao, mfano, suala la katiba mpya au maboresho ya sera kuu, kwani ni lazima kusikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyia kazi.
Hivyo jamii inapaswa kutowaogopa wanasiasa na wanapaswa wawawajibishe pindi wanaposahau majukumu Yao, kwa mfano, kushinikiza wabunge kutoka madarakani.

(b) Kuwepo kwa nafasi, nguvu na uwezo wa kumshtaki na kumfungulia kesi Raisi wa Zanzibar au Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwenye vyanzo vya Sheria hususani katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Raisi haruhusiwi kushtakiwa au kufunguliwa kesi mahakamani.
Hali hii ni hatari sana kwa uvunjifu wa demokrasia na haki ya wananchi au baadhi ya wafanyakazi wa ngazi za chini. Kwani Raisi ni binadamu anaweza kukosea kama ambavyo Wanadamu wote hukosea, na hivyo anawajibu wa kusamehewa au kutumikia adhabu ya makosa yake. Lakini kwa Tanzania imekuwa tofauti kwani mtu yoyote haruhusiwi kumshtaki Raisi, hata akiwa amemaliza muhula wake wa uongozi.
Kwa mfano, Raisi anaweza kudhulumu Mali au maisha ya mtu au watu, hivyo anastahili kuwajibishwa kupitia chombo cha Sheria kulingana na makosa aliyoyafanya. Na mfumo huu utasaidia Raisi kutojifanya kuwa kama Mtu asiyekosea.

(C) Uwezo wa Mihimili mingine kuwa na nguvu ya kukosoa na kuwajibisha serikali kuu, Vilevile kukosoana.
Muundo wa Serikali ya Tanzania imeundwa kwa Mihimili mitatu yaani; Serikali kuu, Bunge na Mahakama. Kila Mihimili una haki na nguvu ya kukosoa Mihimili mwingine katika katiba, lakini katika uhalisia haki na uwezo huo haupo kabisa.
Kwani endapo kiongozi wa Mihimili huo akijaribu kukosoa maamuzi ya Mhimili mwingine hususani Serikali kuu, anakuwa katika hali mbaya, hata kupoteza nafasi yake.
Hivyo inapaswa Kuwepo kwa nguvu ya kikatiba kwa Mihimili hii miwili ambayo imefunikwa nguvu yaani; Bunge na Mahakama. Katika kuleta utawala Bora nchini Tanzania, vilevile maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii.

Mabadiliko katika nyanja za Kijamii:
(a) Kuwepo kwa dawati la utoaji PF-3 (Police Form 3)kwenye Hospitali.
Utoaji wa huduma hii ni kwa ajili ya wagonjwa waliopata ajali au waliojeruhiwa katika miili Yao kutokana na vifaa vyenye ncha Kali kama vile kisu, panga au hata risasi. Lakini utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa Hawa imekuwa ni shida sana, kwani wakipelekwa hospitali wanarudishwa mpaka uwepo ruhusa ya kituo cha polisi PF-3. Mara kadhaa wagonjwa hupoteza damu nyingi mpaka kufariki kwani zipo sehemu vituo vya polisi, vipo mbali sana na hospitali. Kwahiyo, ni Bora katika Kila hospitali Kuwepo na kitengo au dawati linaloshughulikia kutoa hizo PF-3 Ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi pindi wanapopata dharula.

(b) Utoaji wa ajira kutoka serikalini.
Imezoeleka kuwa ni aghalabu sana mtu kupata kazi kama hauna njia mbadala za upataji wa kazi hiyo, kwa mfano; kujiunga na chama tawala (CCM), kutoa rushwa ya ngono au pesa, vilevile uwe na mtu ambaye ana madaraka atakayekusaidia katika upatikanaji wa kazi hiyo. Vijana wengi wametumia muda wao mwingi na wengine wakiendelea kupata elimu shuleni au vyuoni, lakini ipo wazi kuwa wanaopata ajira wengi Wana watu wa kuwasaidia. Mfano, utoaji wa ajira nyingi serikalini unazingatia na "party affiliation", kwamba ni kwa namna gani umejiunga na chama, lakini kama upo chama tofauti na chama tawala huwezi kupata nafasi serikalini. Inaonekana Mabalozi wengi au wakuu wa Mikoa, wilaya na Wakurugenzi wengi ni wanachama kindakindaki wa chama tawala (CCM). Hivyo hali hii hunyima uhuru wa wananchi kwani wengine hawana vyama au hawataki kujihusisha na vyama,au vilevile wapo vyama tofauti na chama tawala. Na haiwezekani kupata nafasi kama upo chama cha upinzani. Kwani kuwa chama tawala haimaanishi ndio vigezo tosha kwa ajili ya kupata nafasi. Hivyo, inabidi utoaji wa ajira uzingatie vyama vyote vya siasa Ili kuleta utawala Bora na uwajibikaji.

(C) Kuwe na utaratibu wa kutoa elimu kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu baada ya kumaliza kidato cha sita.
Kwani wanafunzi wengi huiga au hufuata mkumbo tuu wa kuchagua course ya kusoma. Wanafunzi wengi hawajui hata katika course anayosoma anaweza kuwa nani au kufanya kazi gani baadaye, kwa sababu hakuna elimu kipindi wamemaliza kidato cha sita wanayoipata kuhusu uchaguzi wa course kulingana na masomo Yao. Uwepo utaratibu kipindi wakiwa jeshini kabla hawajachagua course au nyakati zao za mwisho wa kumaliza kidato cha sita, wapate elimu za course wanazotarajiwa kusoma.
Vilevile, vyuoni wanapaswa kuweka utaratibu wa kuwapa elimu vijana kuhusiana na course zao, kuwa ni kazi gani wanatarajia kufanya. Lakini inaonekana vijana wengi mpaka wanafika muda kwenda field hawaelewi wanaenda wapi, na hata wakitafutiwa sehemu hawajui wanaenda kufanya Nini katika vituo vya field.
 
Kwani katika ofisi nyingi iwe za kiserikali au binafsi, siku hizi inaonekana Kuna mazingira yanayowabeba wanawake katika kuajiriwa au kufanya kazi, yaani idadi Yao imeongeka. Lakini Kuna kundi la vilema ambao mara nyingi Huwa hawatajwi, kundi hilo wapo ambao wamesoma mpaka vyuoni, lakini nafasi zao za ajira hazionekani. Hali hii huwarudisha nyuma sana kundi hili ambalo hujiona kana kwamba wametengwa katika kushiriki katika kukuza kipato Chao hata kwa Taifa.
Nakubaliana na hija ya kwamba, tunataka taifa la HAKI, na sio linalojengwa kwa hurumahuruma. Kila kazi aipewe yule aliye mbora zaidibkwa kazi husika. Visipewe kipaumbele vigezo visivyohusiana na kazi husika, wazungu walosema MERITOCRACY
Katika familia nyingi Baba pekee ndio huonekana anatoka na kwenda kufanya kazi bila kumshirikisha mke wake, hali hii humpelekea mama kuwa kama mzigo katika familia kwani Kila kitu hutegemea kutoka kwa Mume wake. Mfano, Mke haruhusiwi hata kuingia dukani kwa Mume wake. Hali hii hufanya akili za wanawake wengi aidha vijijini au Mjini kudhoofika na kuona hawawezi lolote, hivyo hutumia zaidi kuliko wanavyotengeneza pesa, hivyo basi, huleta Taifa lenye wategemezi wengi kuliko nguvu kazi.
Hili naona ni familia na familia tu

, vyuoni wanapaswa kuweka utaratibu wa kuwapa elimu vijana kuhusiana na course zao, kuwa ni kazi gani wanatarajia kufanya. Lakini inaonekana vijana wengi mpaka wanafika muda kwenda field hawaelewi wanaenda wapi, na hata wakitafutiwa sehemu hawajui wanaenda kufanya Nini katika vituo vya field.
Basi hicho chuo kitakuwa hakijakamilika, maana dhumuni la chuo ni kufundisha hiyo kazi na kozi kwa ukamilifu wake
 
Back
Top Bottom