SoC01 Suluhu ya kutumia takangumu kama mbolea asilia

Stories of Change - 2021 Competition

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,681
698,790
Tatizo la takangumu ni kubwa na lenye changamoto nyingi katika miji yetu... Manispaa nyingi hujaribu kwa kila namna kupambana na hili tatizo lakini juhudi bado hazijakidhi ukubwa wa tatizo.. Zipo kampuni zinazolipwa mamilioni kila mwezi kwa ajili ya kukusanya taka toka majumbani, kwenye masoko , sehemu za kutoa huduma mbali mbali, viwandani na hata maeneo ya biashara.

Kampuni hizi zikishakusanya hizi taka huzipeleka maeneo maalum ya kuhifadhia taka na huko huchomwa moto ambao nao huzua tatizo lingine la uchafuzi wa mazingira na madhara mengine ya kiafya kuazia kwenye ngozi, mfumo wa upumuaji na hata macho, kwakuwa taka hizi hubeba kila aina ya uchafu na mabaki na hazichambuliwi na kutengwa kulingana na makundi yake.

Natambua wazi kuna taka laini na taka hatarishi lakini hizi tatizo lake si kubwa kwakuwa zimewekewa utaratibu unaofanya kazi vizuri.

Kwenye taka laini kwa muktadha huu vinyesi, mikojo na maji machafu kuna madimbwi maalum ya kwenda kumwaga huko na kuna magari maalum kwa shughuli hiyo.. Na kuhusu taka hatarishi hasa zinatokoka kwenye mahospitali, viwandani, na kwenye maabara mbalimbali hizi nazo hukusanywa na magari maalum na kwenda kuchomwa kwenye matanuru maalum yajulikanayo kama incinerators..!

Sasa je unatambua ya kwamba unaweza kusaidia kutatua uchafuzi wa mazingira na hewa kwa kuzigeuza taka ngumu kuwa mbolea asilia, huku ukiongeza vipato kwa watu na kutoa ajira?

  • Ajira kwenye ukusanyaji
  • Ajira kwenye uchakataji
  • Ajira kwenye usambazaji
  • Ajira kwenye uuzaji na ununuzi
  • Ajira kwenye matangazo
  • Ajira kwenye vifungashio
  • Ajira kwa wenye vyombo vya usafiri
  • Ajira kwa wenye maghala
  • Ajira kwa wauza chakula na vinywaji
Nknk

Kama taifa tunaweza kuokoa mamilion ya fedha za kigeni na kuokoa uharibifu wa mazingira na kutunza ardhi yetu kama tukiamua kupitia mashirika, vikundi vya wajasiriamali na hata mtu mmoja mmoja kuwekeza kwenye mradi wa kuchakata taka ngumu na kuzigeuza mbolea asilia

Kinachotakiwa kufanyika ni hiki.. Yale maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka ngumu ..yanaweza kugeuzwa na kuwekwa viwanda vya mbolea, malighafi ya chuma na malighafi ya plastiki nk.. Badala ya kuzichoma moto taka na kusababisha uchafuzi wa mazingira na athari za kiafya..!

Viwanda hivi vikoje?
Unakuwa na mtambo wa kutenganisha taka kutokana na asili yake
Zinapofika dample humwagwa kwenye kinu kikubwa...kinu hiki kinakuwa na sumaku na mikanda inayotembea ( rolling pillars)

Sumaku itanasa vitu vyote vyenye asili ya chuma na bati na kuvidondosha kwenye mkanda wake na hivi vitapelekwa moja kwa moja mpaka sehemu yake..huko vinaweza kuuzwa kama chuma chakavu ama vikachakatwa na kuuzwa kama malighafi ya kutengenezea nondo nk

Mkanda w pili utakuwa na sensor za kuhisi(detect) vitu vyote vyenye asili na plastic..hivi navyo vitaelekezwa kwenye mkanda wake mpaka kwenye hifadhi yake(depositer tank) hapo vinaweza kuyeyushwa na kuwa malighafi ya kutengeneza vitu mbalimbali vya plastic

Mkanda wa tatu huu utakuwa mkanda mkuu ama mkanda jumuishi.. Huu utabeba takangumu zote zisizo na bati, chuma wala plastiki. Hizi zitasafirishwa mpaka kwenye hifadhi yake(deposit tank) na kufanyiwa mchakato wa kuzisaga ... Hapo unaweza kuongeza maji na kuziozesha kisha kuzikausha ama ukaziacha na kuzipaki tayari kwa matumizi ya kwenye mimea mbalimbali

Kwa namna hiyo taka ngumu zitakuwa malighafi hitajika tofauti na ilivyo sasa..huku mazingira yakitunzwa na kuokoa gharama kubwa za kuziteketeza na bado tukiokoa fedha za kigeni kwa kuacha kuagiza mbolea nje ya nchi, kuongeza wigo wa ajira na kutoa nafasi mpya za utafiti mpya kwenye nyanja za mbolea isiyo na sumu kwa faida ya kizazi kijacho.
 
Mtambo kama huu unaweza kuwa mradi wa manispaa kupitia vikundi vya vijana ama hata majeshi yetu (Magereza na JKT)ambayo yanajishughulisha na kilimo cha mazao ya muda mfupi na mrefu pia..na wanaweza kuokoa bajeti kubwa ya pesa ya mbolea

Kwa watu binafsi na vikundi vyenye mitaji midogo wanaweza kufanya hivi kwa kutumia mashine rahisi pia
Kupitia SIDO maeneo ya kwenye madampo yanaweza kugeuzwa sehemu ya ubunifu sanaa na ufundi kutokana na malighafi inayotokana na takangumu
Mashine za kuunda vitu
Milingoti ya plastiki
Mkaa wa karatasi
Vitendea kazi mbalimbali
Vitu vya ubunifu, sanaa, mapambo nknk
Yaani ni kuhakikisha kila anayeingia eneo la dampo hakosi kazi ya kufanya
1628085002292.jpg
 
Ajira nyingi zinaweza tengenezwa, Tanzania inahitaji mawazo makubwa kama haya hongera Mshana!
 
Kwenye taka kuna utajiri Mkubwa sana ndugu,nina mashine ya kusaga plastic nilikuwa nasaga mota ikafa nimesimama hasa baada ya kuingia kwenye uchimbaji madini lakini nategemea kurudi kwa kasi.
Kuna mchina anataka tani 300 kwa mwezi za plastic iliyosagwa tani moja ananua kwa milioni moja na laki 2.Niliunda mashine mwenyewe ya kusaga kwa kuangalia youtube japo haikufanya vyema lakini nategemea kurudi kwa nguvu kubwa na vifaa vya kisasa zaidi, mashine ya kusaga plastic,ya kumenya lebo za plastic,ya kuosha plastic,ya kukausha plastic ya kupika plastic na kutoa pellet yaani punje za plastic.
 
Lengo la project yangu ya plastic ni kutengeneza bidhaa zao la plastic mfano dizeli,petrol,mbao,vigae,tiles,tofali,pot za maua,nk.
Taka za masokoni mfano matunda na mboga zilizooza unaweza zalisha alcohol au spirit kwa ajili ya sanitizer.
Kutengeneza mbolea hai organic hizi soko la mbolea hizi ni kwenye mashamba ya maua na matunda na Yale ya kilimo hai awatumii mbolea za viwandani kwa ajili ya kulima matunda ya kuexport
 
Umetisha sana.kumbe jf humu kuna wenye sifa za hata kuwa mawaziri na wakaleta matokeo chanya aisee!
 
Ajira nyingi zinaweza tengenezwa, Tanzania inahitaji mawazo makubwa kama haya hongera Mshana!
 
Back
Top Bottom