Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI: SINGANOJR.

SEHEMU YA 43.
Hamza aliwahi kutoka kazini kuliko kawaida ili kuwahi miadi na Prisila , mrembo huyo alikuwa ameshamtaarifu ni wapi amkute hivyo alisogea mpaka Mlimani City na ndani ya dakika tano tu kupita Prisila alitokea , siku hio alikuwa akitumia gari nyingine kabisa aina ya Bentley.
“Inaonekana ni kama nilivyotarajia , unajali muda “Aliongea Prisila huku akimwangalia Hamza na kuonyesha ishara ya kuridhika.
“Umependeza mno Prisila , unaonekana kama wale warembo ma’model’ maarufu?”.Aliongea Hamza na kumfanya Prisila kutabasamu.
“Halafu hili gauni nimelinunua muda mrefu sana , lakini sijawahi kupata ujasiri wa kulivaa”Aliongea akiwa na tabasamu.
“Kwanini umepata huo ujasiri leo , kwangu mimi uzuri wako naona hautokani na mavazi”Aliongea.
“Nimepata ujasiri wa kuvaa hivi kwasababu nipo na wewe mbele ya Classmate wangu wa kitambo ”Aliongea na kumfanya Hamza kushangaa.
“Unamaanisha nini?”
“Namaanisha leo unakwenda kuigiza kuwa boyfriend wangu mbele ya wanadarasa zangu wangu wa Highschool , tuna Reunion leo na nimewaambia nina boyfriend”Aliongea Prisila akiwa siriasi , hakuwa hata na aibu kuongea hayo maneno na ndio kitu kilichomshangaza zaidi Hamza.
“Mwanamke mrembo kama wewe unakosaje mpenzi au ndio unapanga kuniingiza kwenye matatizo?”Aliuliza Hamza , aliona haya maswala ya kufanywa boyfriend feki na kila mtu yanaanza kumchosha , swala la kujiingiza kwa Regina lishaanza kumuumiza kichwa kuhusu usalama wake,lakini tena Prisila anamwingiza.
“Ndio ujue sina ,ndio maana upo hapa , kama ningekuwa nae ningehangaika vyote hivi , kabla sijaondoa gari fanya maamuzi hapa hapa, je upo tayari kuigiza kuwa bofriend wangu kwa leo tu?”Aliuliza na kumfanya Hamza kuanza kukuna kichwa.
“Sikia Prisila mimi kazi yangu sio kuigiza kuwa boyfriend feki , nina mpenzi tayari, kwa urembo wako sidhani kama unaweza kukosa mtu ambae anaweza kufanya unachotaka , nipo tayari kulipa fadhila ila sio kwa njia hii”Aliongea Hamza na palepale alifungua mlango wa gari kutoka.
“Huyo mpenzi wako anajua unaigiza kuwa mpenzi wa Regina?”Aliuliza na kumfanya Hamza kusita kwanza na kumgeukia.
“Kwahio kwasababu bosi wako ameniajiri kuwa mpenzi feki na wewe unataka kufanya hivyo, haiwezekani kwa kila mtu , nilichokifanya kwa bosi wako ni shauku ilionifikisha hapa , lakini sio kurudia tena kwa mtu mwingine, kuhusu mpenzi wangu kujua ama kutokujua hili ni swala ambalo lipo juu yangu, nadhani unajua siwezi kuendelea kuwa na bosi wako kwa muda mrefu”Aliongea Hamza.
Prisila alijikuta aking’ata meno , aliamini ingekuwa rahisi kwa mwanamke mrembo kama yeye kukubaliwa na Hamza hata kimaigizo tu, lakini mawazo yake yalikuwa tofauti kabisa , Hamza anamkatalia tena akiwa siriasi kabisa.
Upande wa Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyo anawaza ndio aliona ni muda wa kuondoka na alishuka kwenye gari na kuanza kupiga hatua akitaka kuvuka barabara kurudi kwenye kampuni maana hakufika hapo na gari.
Prisila alijikuta akifumba macho kwa dakika kadhaa na kisha alifungua mlango haraka na kutoka.
“Hamza wait!!!”
Aliita akimaanisha Hamza amsubiri na Hamza ambae tayari alikuwa ashaanza kupiga hatua kuvuka barabara alisimama akimsubiria.
Ijapokuwa alimkatalia mrembo huyo lakini mara baada ya kushuka kwenye gari muonekano wake ulizidi kumfanya kuonekana mrembo , Prisila alikuwa mwanamke mzuri sana pengine alikuwa akishika nafasi ya pili baada ya Regina.
Hata watu waliokuwa karibu na eneo hilo walimkodolea macho na kwa jinsi ambavyo alimwita Hamza ni kama ilidhidhirisha kuna kitu kinachoendelea baina yao.
Prisila alikaza mwendo na kumsogelea Hamza , awamu hio alikuwa mpole kuliko mwanzo.
“Hakuna namna unaweza kunibadilisha mawazo”Aliongea Hamza.
“Unakumbuka asubuhi ulichosema kwenye simu , upo tayari kufanya hicho kitu baadae , hii ni ahadi umeweka, kosa lako ni kutokuuliza , kwanini unanikatalia sasa hivi ilihali sina mbadala?”Aliongea.
“Na wewe kosa lako ni kuamini naweza kukubali kila utakachoniambia na nifanye, hata kama ni kujishusha thamani na kukubali ombi lako”Aliongea Hamza akiwa na uso usiokuwa na hisia zozote. Lakini kauli yake ilimfanya Prisila kushangaa na kujikuta akisugua meno, ilikuwa ni dhahiri alitaka kusema yaani mwanamke mrembo kama yeye kuigiza nae kuwa mpenzi ni kujishusha thamani.
“Basi naomba unisindikize , sina chaguo lingine, nitakutambulisha kama rafiki yangu wa kawaida tu”Aliongea katika hali ya kujishusha , lakini kilichomshangaza ni baada ya kuona Hamza anacheka.
“Unacheka nini .. umekubali au?”Aliuliza .
“Ukweli ni kwamba nilikuwa nishakubali tokea asubuhi , katika kitabu changu cha kumbukumbu sijawahi kushindwa kulipa deni hata liwe kubwa vipi?”Aliongea na palepale alimpa mkono Prisila ambae alikuwa akimshangaa, alipokea kiwasiwasi na wakaanza kupiga hatua kuelekea kwenye gari na awamu hio Hamza hakumwingiza upande wa dereva bali alimzungusha kwenye siti ya abiria na mara baada ya kumfungulia mlango aliingia ndani.
“Kama ulikuwa umenikubalia kwanini ulikuwa ukinizungusha , ulikuwa unanijaribu?”
“Huwezi kusema nilikuwa nikikujaribu , unaonekana kuwa mtoto unaepndwa na kupewa kila kitu, lakini kumbuka huwezi kupata kila kitu unachohitaji”
“Nani kakuambia napewa kila kitu , ni kweli napendwa na wazazi wangu lakini wakati wao wa kunipa kila ninachohitaji ushaisha na sasa natafuta ninachotaka , nilitaka wewe kuigiza kuwa boyfriend wangu kwa leo kwasababu unanilipa na baada ya hapo kila mtu anajua mambo yake , ningeweza kupata mwanaume yoyote ndio lakini hakuna ninaemdai hivyo watakuwa wananidai , unadhani mimi mtoto wa kike nitakuwa nalipa kwa njia ipi , watataka mahusiano na mimi na mengineyo, labda hujui tabia yangu , napenda kudai kuliko kudaiwa ndio maana najitahidi kufanya kila namna niwe nadai watu na sio kudaiwa”Aliongea na kumfanya Hamza kutoa tabasamu.
“Kwahio mpango wako ni kunitengenezea deni tokea mwanzo na sio kunisaidia?”
“Nadhani ushaanza kunielewa sasa , lakini katika watu niliowadai wewe ndio nimekupa namna ya kunilipa kirahisi lakini unaleta ujeuri”Aliongea huku akivuta mdomo.
“Hehe… ingekuwa miezi kadhaa iliopia nisingekuzungusha hata kidogo”
“Unamaanisha nini?”
“Ninachomaanisha sikuwa na mpenzi hata wa maigizo , sasa hivi nazungukwa na warembo ni kawaida kwangu kuringa kidogo”Aliongea na kumfanya Prisila kutabasamu.
“Endesha kuelekea Kunduchi Prima hotel”Aliongea na Hamza alikata kulia kwake na kuichukua barabara ya Bagamoyo Road kutoka Sam Nujoma.
Dakika chache mbele walikuwa washafika katika hoteli ya Kunduchi , ilikuwa hoteli ya kisasa na ukweli ni kwamba Hamza hajawahi kufika katika hoteli hio licha ya kwamba sio mara yake ya kwanza kuwa katika hoteli kubwa.
Prisila alikuwa akiungana na wanafunzi wenzake aliosoma nao High school, alikuwa amesoma shule za hela nyingi hivyo ilikuwa ni sawa kukutana katika eneo la hadhi ya juu kama hilo.
Mara baada ya kuingia katika hoteli hio ya rangi nyeupe , Hamza aliweza kuona bango ambalo lina maandishi makubwa yaliokuwa yakitambulisha hoteli hio, lakini kuna kitu ambacho kilimshangaza sana Hamza , ilikuwa ni picha chini ya maandishi ambayo ilitumika kama Logo ya hoteli hio.
“Mbona unashangaa , unaangalia nini?”Aliuliza Prisila kwa shauku.
“Hamna tu”Aliongea na kisha alisogeza gari mpaka eneo la maegesho na wakatoka, ile wanaanza kuzipiga hatua waliweza kuona wenza wengine ambao mwanamke alikuwa amening’inia katika mkono wa mwanaume wakiingia, walionekana kuwa romantic.
Mwanaume alikuwa amevalia shati la mikono mirefu chapa ya Fendi na saa ambayo haikuonekana kwa ukaribu ni ya kampuni gani lakini ilionekana ya thamani.
Mwanamke upande wake alikuwa amevalia gauni la Chanel la mkato wa chini , alikuwa amebeba begi kwenye mikono yake chapa ya Hermes, licha ya kutokuwa mrembo sana lakini alikuwa akivutia na kuonyesha ni wale wanawake wa hadhi ya juu.
“Lidya!!”Aliita Prisila , alionekana kumtambua huyo mrembo.
Mwanamke yule mara baada ya kugeuka kwenye macho yake kulionekana aina flani ya wivu lakini alibadilisha na tabasamu bandia.
“Wow! , Kama kawaida yako Prisila , unazidi kuwa mrembo siku hadi siku”
Aliongea lakini upande wa yule mwanaume mara baada ya kumuona Prisila macho yake yalichanua na ilionekana ilikuwa ngumu kuacha kumkagua Prisila juu hadi chini.
“Lidya na huyu ni rafiki yako uliesoma nae?”Aliuliza yule mwanaume huku akiendelea kumchunguza Prisila.
“Ndio jina lake anaitwa Prisila ila alikuwa akifahamika zaidi kwa jina la Pria , Prisila huyu ni mchumba wangu anaitwa Bahati”
“Mchumba!, aisee hongera zako , naona unaenda kuolewa”Aliongea Prisila akionekana kuwa na furaha juu ya Lidya.
“Bahati wangu usimuone hivi , ni mtoto wa Mzee Mtei mmiliki wa makampuni ya Mtei Enterprise , ijapokuwa huwezi kumuweka katika kundi la vijana matajiri kama Saidi , lakini ni bilionea kibongobongo, nadhani kuwa kwetu pamoja imepangwa”Aliongea Lidya akitoa taarifa ambao hazikuhitajika kabisa na baada ya kusema hayo aliinua uso wake na kumwangalia kijana mtanashati anaejiita Hamza Mzee.
“Na huyu kaka ni..?”Aliuliza na kumfanya Prisila kusita kumtambulisha Hamza, sio kama hakutaka kumtambulisha bali hakujua amtambulishe vipi.
“Niite Hamza ni zaidi ya rafiki kwa huyu mrembo”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
“Hamza!!, nakumbuka mara ya mwisho wakati tunakutana Prisila ulisema mpenzi wako amesharudi kutoka nje ya nchi na kwasababu alikuwa bize hakuweza kuhudhuria , Mr Hamza unaweza kutuambia kwanini ukamuacha mrembo kama huyu kuja peke yake , wengi tulidhani huna mapenzi ya kweli kwa Prisila”Aliongea.
“Nadhani wakati mnakutana ndio kipindi ambacho joto la Dar lilikuwa kali sana , hivyo kazi za kutengeneza AC zinakuwa nyingi”Aliongea Hamza.
“Wewe ni fundi wa kutengen4eza AC?”Aliuliza akiwa mshangao na Hamza alitingisha kichwa kukubali.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kusikia mtu alietoka nje ya nchi kuwa fundi wa kutengeneza AC , Are you for real?, unanifanya nitamani kucheka”Aliongea huku akichanganya kiswahili na kingereza.
“Sorry , Prisila nadhani unaijua tabia yangu ya kuropoka, hehe..”Aliongea lakini wanasema ndege wanaofanana huruka pamoja , hata kwa Bahati Mtei alikuwa na tabasamu lililojaa kejeli.
“Lidya hutakiwi kucheka , unajua fika AC zikiharibika kuna hitajika fundi, hivi ni vitu ambavyo hatuwezi kufanya sisi wenyewe”Aliongea.
“Ndio mpenzi , una akili sana”Aliongea
Prisila alionekana kutopenda jambo lile na alikuwa akitaka kusema kitu lakini Hamza alimzuia kwa kumtingishia kichwa akimwashiria asibishane nao.
Hakuona haja ya kubishana nao , ili mradi ashajua tabia zao hilo lilikuwa likitosha hivyo kucheza ngoma yao ni kujishusha.
“Sioni sawa kuchekana kwasababu ya vipato vyetu , hakuna aliezaliwa nacho , wote tunatafuta”Aliongea Prisila.
“Prisila sioni tatizo kwa wao kucheka na kudharau wa chini yao , sio wa kwanza , ni jamii ndio ilivyo, unaweza usiongee waziwazi lakini ubaguzi wa kipato umeshamiri kila kona, hata hili kusanyiko nadhani halijalengwa kukutana na kukuumbushiana habari za shule bali ni kuvimbiana nani ana kipi zaidi ya mwingine”Aliongea Hamza.
“Unanifanya nisitamani kuingia kabisa”Aliongea Prisila.
“Ushafika , haina haja ya kujificha , ukiondoka watakuonna ni muoga na utawapa sababu za kuendelea kuongea, isitoshe kila aliekuja ni kwa ajili ya kuonyesha anaendelea vizuri kimaisha , hivyo sidhani ni swala baya pia”Aliongea na kumfanya Prisila kumwangalia usoni.
“Unaonekana kuwa mtu mzima na mwenye kujiamini”Aliongea Prisila na kumfanya Hamza kutabasamu.
Kwasababu Lidya na mpenzi wake wameshatangulia kuingia na Hamza na Prisila walianza kuzipiga hatua kuingia ndani pia , lakini Hamza alisimama ghafla mara baada ya kuhisi kuna mtu alikuwa akimwangalia na macho yake alikuwa ameyakazia upande mwingine wa maegesho ya watu mashuhuri na alikodolea macho gari ya Roll Royce na kwasababu kioo cha upande wa kulia kilikuwa kimeshushwa aliweza kuona aliekuwa yupo ndani.
“Twende Hamza , mbona umesimama tena?”Aliuliza Prisila na kumshitua Hamza.
“Ulikuwa ukiangalia nini , ni mara ya pili nakuona unashangaa”
“Hamna kitu, nadhani utanashati wangu unafanya watu kuniangalia sana, kuna mtu alikuwa akinikodolea macho”Aliongea huku akiwa na tabasamu na kumfanya Prisila kutingisha kichwa chake kwa masikitiko.
Walipokewa na mhudumu wa hoteli ambaye aliwaongoza moja kwa moja mpaka katika chumba binafsi ambacho kilikuwa na meza kubwa iliojaa wanaume na wanawake.
Watu wale mara baada ya kumuona Bahati na Lidya akiingia walianza kuongea chini kwa chini wao kwa wao na baada ya kuonekana kwa Prisila walizidisha.
“Prisila!!”
Mwanaume mrefu wa mita kama moja na nusu hivi aliita , na alionekana kumwangalia Prisila kwa sekunde kadhaa kabla ya kuhamishia macho yake kwa Hamza.
Prisila aliishia kutoa tabasamu na waliingia ndani na alichukua nafasi hio kumtambulisha Hamza na walionekana kuridhika nae , pengine ni kwasababu ya mavazi yake , lakini upande wa Lidya hakuwa na kifua.
“Oteeni kazi anayofanya mpenzi wa mrembo wa darasa”
“Kwa muonekano wake nadhani anahela za kutosha , sio watu wa kawaida wenye kudumu mavazi ya bei hio, muonekano wake unaongea kila kitu”
“Ahah , muonekano wapi , ni fundi wa kurekebisha AC zilizoharibika”Aliongea Lidya.
“Nini!!?”
Watu wote waliokuwa ndani ya eneo hilo walionekana kushangaa, sio kwamba walikuwa wakishangaa kazi ya Hamza bali walikuwa wakishangaa Prisila mwanamke ambae alikuwa mrembo wa darasa wakati wakiwa shule kuwa na mpenzi ambae ni fundi wa kawaida na wengi walianza kumwangalia Hamza kwa kejeli.
Asilimia kubwa ya waliokuwa hapo ndani walikuwa wametokea katika zie familia za matajiri , ijapokuwa Prisila famiia yake ilikuwa na pesa lakini hawakuwa matajiri , baba yake ambae ni profesa hakupata mshahara wa kuitwa tajiri, hivyo ni kama yeye ndio ambae familia yake ipo kinyonge zaidi.
“Mbona mnashangaa , hamjawahi kusikia wala kuona mafundi?”Aliongea Prisila huku akionyesha kukosa utulivu.
“Haha.. usituelewe vibaya Prisila , kwa urembo wako na hadhi uliokuwa nayo wote tulitegemea mpenzi wako kuwa wa hadhi ya juu, nilitarajia ungekuja na Chriss mtoto wa tajiri Gabusha labda ndio maana tulikuwa na hamu ya kumjua”Aliongea mwanaume ambae alikuwa akiitwa Dismasi.
“Umejuaje nina mawasiliano na Chriss?”Aliuuliza Prisila.
“Karibia marafiki zote wa Chriss wanajua nyie ni wapenzi , nimeshangaa kuona ukimtambulisha mtu mwigine”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia Prisila.
“Hata kama , sina mahusiano na Chriss ni mwanaume ambae ananifuatiia ila hana kigezo cha kuwa mpenzi wangu”Aliongea.
“Prisila unamaanisha nini hana kigezo, ni kipi ambacho huyu Hamza wako kamzidi , kama ni ushombeshombe hata Chriss anao na kubwa zaidi ndio mtoto wa pekee wa Mzee Gabusha hivyo mali zote za baba yake ni za kwake”Aliongea Lidya huku akiona kabisa Prisila anajaribu kujikweza mbele yao, Lidya alijiambia kama Chriss yupo tayari kutoka nae kimapenzi basi angeachana na Bahati saa hio hio bila huruma yoyote.
“Hivyo ni vigezo vyako usitake kila mmoja avitumie katika kuchagua watu sahihi, unaongea kama vile Hamza hana vigezo , unamjua vizuri au kisa umnemuona leo ndio unaanza kumhukumu?”Aliongea Prisila alionekana kukasirika mno , angejua hilo lingetoka asingekuja kabisa na Hamza.
Aliona amemleta mtu wa watu kwa ajili ya kupokea vichambo , lakini mara baada ya kugeuza macho yake pembeni kumwangalia Hamza ambae anasemwa , alionnekana kuwa bize na chakula ambacho kimeandaliwa.
Hamza hakutaka kuwa na hasira , aliona kuwa na hasira ni kujishusha kuwa katika levo sawa na wao, kwake hali hio ilikuwa ikimfurahisha sana kwani aliona ni kama vichaa wamekutana na kuanza kulumbana.
“Jamani haya mambo yametoka wapi , hii ni mara ya kwanza kwa Prisila kumtambulisha mpenzi wake kwetu , tunachoongea hakina umuhimu kabisa , kazi yake inahusiana vipi , isitoshe hata kazi yake ni muhimu pia, nani kati yenu anajua kutengeneza AC?”Aliongea Saidi kijana tajiri zaidi ambae ndio kiongozi wa kuandaa mkusanyiko huo wa wanafunzi wenzake kila mwaka.
Kundi hilo la watu walicheka na kukubaliana nae , huku wengi wakijikomba kwake kwa kumpamba kama mtu mwenye busara.
Gharama zote za kukutana zilikuwa juu ya Saidi Mohamed na vyakula vya bei ghali viliandaliwa na kubadilishwa kila dakika na jambo hilo liliwafanya watu wote kuendelea kuwa chawa kwa kumsifia sifia na kujipendekeza.
“Nimesikia kutokana na wateja wengi kuipenda hii hoteli , mmiliki ametengeneza mfumo wa kutoa kadi za uanachama kwa baadhi ya watu wa hadhi ya juu tu, hivyo kukaa hapa lazima uwe mwanachama na si vinginevyo, nasikia bosi wa mahoteli yote ya Prima ni mwanamke”
“Sio hivyo tu , nasikia pia asilimia kubwa ya wanachama ni wale ambao wanafahamiana na mkurugenzi , Bro Side mpaka kutupatia nafasi ya kukutana katika hii hoteli lazima uzito wako baada tu ya kurudi Tanzania umeongezeka”Aliongea Lidya.
“Hivi ni kweli hii hoteli ipo chini ya Prima Real Estate , nilichosikia Boss Yulia anatokea katika familia kubwa tu hapa nchini”Aliongea Dismasi.
“Haishangazi sana , ulimwengu wa kitajiri ni wa tofauti sana na watu wa kawaida”Aliongea bwana aliefahamika kwa jina la Jimmy.
“Nasikia kampuni ya Prima licha ya kuwa na sifa za kuingia katika soko la hisa ilishindikana kutokana na asili ya wanaoimiliki , lakini kama ingeingia katika orodha ya soko la hisa ingekuwa moja ya kampuni yenye thamani kubwa sana kimtaji, ijapokuwa kuna usiri mkubwa juu ya familia anayotokea Yulia lakini hata mimi naamini atakuwa na koneksheni kubwa ndani ya serikali”Aliongea mwingine.
“Boss Side , umewezaje kupata kadi ya uanachama ndani ya hii hoteli , utaratibu wao wa kutoa uanachama huwa unakuwaje?”Aliuliza Lidya.
“Ilikuwa kama bahati tu nikakutana na Mkurugenzi na ndio alinialika kwa kunipatia kadi ya uanachama”Aliongea Saidi na muda uleule aliingiza mkono kwenye koti lake la suti na kuchomoa kadi na kumpatia Lidya.
“Aiyaa .. kadi inapendeza kweli , Bosi Side hebu tuione na sisi”Waliongea huku wakigombania.
Lakini upande wa Side alionekana kama vile hajaridhika mara baada ya kuona Prisila hakuwa akijali kabisa jambo lile.
“Jamani ilivyokuwa nzito , nadhani imetengenezwa kweli na madini ya dhahabu kama walivyosema”
“Ni Gold kweli , Lidya hebu acha kukaa nayo muda mrefu , nipe na mimi nione”Aliongea mwingine
“Subirini kwanza , bila ya kapicha hili halipiti hivi hivi”Aliongea huku akitoa simu yake ya I phone na kuanza kupiga selfie.
Bahati mpenzi wake alionekan kutoifurahia tabia ya mpenzi wake kumpapatikia Saidi, aliona ni kama vile anapotezewa licha ya yeye pia kuwa tajiri.
Lidya hakuishia kupiga picha akiwa ameshikilia ile kadi, lakini vilevile alipiga Selfie akiwa na Bosi Side na dakika ileile aliposti huku akiandika Caption
“It feels so good to have a meal with Director Said Mohamed of Vodocum Corporation”
Mara baada ya kuona Lidya alichokuwa akifanya wanawake waliokuwa hapo pia walitumia nafasi hio kupiga picha na Saidi Mohamedi , Mkurugenzi mtendaji wa kampuni kubwa ya mtandao ya Vodocum.
“Prisila angalia na wewe , ni watu wachache sana wanabahatika kushika kadi kama hizi kwenye maisha yao yote”Aliongea mwanadada aliefahamika kwa jina la Phina.
“Nishaiona tayari , mnaweza kuendelea tu kuiangalia”Aliongea Prisila akiwakatalia.
Bahati licha ya kuwa bosi wa kampuni ndogo hakutaka kujishusha lakini hata hivyo hakutaka kukaa kizembe kutotumia fursa hio na palepale alitoa kadi yake ya biashara.
“Mkurugenzi mimi ni GM kutokea kampuni ya Mtei Enterprise.tafadhari naomba upokee kadi yangu ya biashara kwa ajili ya mawasiliano”Aliongea lakini Bosi Side aliishia kuipokea na kuiweka juu ya meza.
“Uniwie radhi ndugu , tupo hapa kwa ajili ya kukutana na sio kuongea maswala ya kazi , hivyo hatuwezi kubadilishana mawasiliano.”
“Haina shida , umekuwa role model wangu katika maswala ya kibiashara sio rahisi kuongoza kampiuni kubwa ya mabilioni ya fedha kwa umri mdogo , baba pia mara nyingi amekuwa akiniambia niige mfano kwako, ni juzi tu kutokana na mwelekeo wa kampuni yako tulikuwa tkipanga kuwekeza kwa kununua hisa Vodocum”
“Nadhani tule kwanza , tutaongea baadae kama tutapata nafasi hio”Aliongea akimkatisha.
“Oh .. basi hakuna shida”Bahati alijikuta akinywea , alitamani kuwa na ukaribu na mtu mzito kama Side katika orodha ya mawasiliano yake,alitamani hata kuwa na namba yake tu ili kwenda kujigamba kwa wenzake, lakini Side alionekana kumkataa mbele ya watu.
“Side hebu fanya hivyo kwa ajili yangu bwana na kumpokea Bahati kwa mikono miwili , Mtei Enterprise sio kampunni ndogo naamini baadae itakuja kuwa kubwa, kwasasa kampuni yao ina thamni ya bilioni kumi, sidhani kama inaweza kuitwa kampuni ndogo”Aliongea Lidya.
“Lidya naona mchumba wako anatokea katika familia ya kitajiri , hongera sana ukiolewa na wewe moja kwa moja unakuwa tajiri”Aliongea Phina kwa wivu na kauli ile ilimfanya Bahati kuona angalau sasa na yeye ameanza kuonekana.
“Ukiilinganisha kampuni yetu na Vodocum sisi ni kama sisimizi tu”Aliongea akijaribu kwa mara ya pili kuwa chawa.
Ki ufupi kusanyiko hilo halikuwa na ile hali ya kuvutia kwani kila mtu alikuwa akiongea kile alichokuwa nacho na walichokamilisha huku wengine wakiwa chawa na walisahau hata kula.
Upande wa Hamza alikuwa bize na Kambakochi ya bei ghali ambayo imeandaliwa na alimwangalia Prisila na kuona mwanamke huyo alikuwa na wasiwasi mno.
“Prisila huna njaa , kula hata kidogo?”Aliongea Hamza na kumfanya Prisila kutoa tabasamu baada ya kuona Hamza hakuathirika na kilichoendelea na angalau alipata hamu ya kuanza kula japo kidogo.
“Prisila ombi langu la mara ya mwisho juu ya kuja kufanya kazi katika kampuni yetu bado lipo hai , lakini sijasikia majibu yoyote kutoka kwako?”
“Boss Side unataka Prisila kwenda kufanya kazi katika kampuni yenu , nasikia licha ya Dosam kuwa kampuni kubwa na kulipa vizuri lakini kwa Vodocum ni habari nyingine”
“Vodocum ni kampiuni Kongwe ina matawi Afrika nzima , kuna rafiki yangu mjomba wake licha ya kuwa kitengo cha kawaida lakini ana maisha”
“Prisila uwezo wake ni mkubwa sana , makampuni mengi yanamhitaji kwa ajili ya kufanya nae kazi , si jambo la ajabu kuombwa na sisi aje afanye kazi Vodocum Tanzania na kutokana na thamani yake kuwa juu nipo tayari kwenda juu zaidi katika mshahara wake kuliko anaopata pale Dosam”
“Boss tupo wafanyakazi wenye uwezo zaidi ya Prisila mbona , au kuna sababu za kutaka kumuajiri yeye tu ,unampenda nini tajiri?”Aliongea mmoja wapo lakini Side alimpotezea.
“Kwasasa niseme napenda kazi yangu katika kampuni ya Dosam ,Bosi Side uniwie radhi sipo tayari”
“Hakuna shida , una muda wa kutosha wa kufikiria”
“Prisila unasita sita nini , kufanya kazi ndani ya kampuni ya Vodocum sio swala la mshahara tu, unajitambulisha kimataifa, pili ndio nafasi pekee ya kuwa karibu na bosi Side , unajuaje tunaweza kukuita Mrs Side haha..”Baada ya baadhi yao kusikia kauli hio waliishia kutoa tabasamu la kinafiki, lakini kauli ile ilikuwa ni kama imemkera zaidi Prisila.
“Nyie mkiendelea kuongea ujinga , nitakasirika”Aliongea Prisila akiwa siriasi.
“Acheni kumtania Prisila ,ninachofanya ni kuhakikisha Prisila hadhi yake inapanda ndio maana , hakuna zaidi ya hilo”Aliongea Side.
“Prisila usimuangushe bosi , ni bahati ujue kufuatwa na bosi mwenyewe kutaka kufanya nae kazi, unaweza kuona sio maamuzi sahihi lakini kumbe ulioshikilia ndio maamuzi mabaya”Aliongea Lidya.
“Lidya kuna haja gani ya kuzunguka zunguka , unamlenga Hamza , kwanini usimwambie moja kwa moja “Aliongea Dismasi.
“Sijataja mtu jina ,mnikome”Aliongea na kufanya watu kuanza kucheka kinafiki huku wakimwangalia Hamza , hakuna ambae anajali kama Hamza anaweza kukasirika au Lah na jambo lile lilimchosha Prisila na kumshika mkono Hamza.
“Tuondoke , siwezi kuendelea kukaa hapa”Aliongea na kumshitua Hamza ambae alikuwa akimalizia kubeba kipande cha mwisho cha nyama.
“Umekasirika kwasababu ya wao kunicheka?”Aliuliza Hamza.
Prisila hakutaka kumfanya Hamza kujisikia vibaya , ijapokuwa alikuwa akitafuta hela kwa shida , lakini hakuona ni tatizo tofauti na hao watoto wa matajiri ambao wanadhani pesa ndio kila kitu.
Upande wa Hamza licha ya kwamba hakuwa akijali , lakini alihisi furaha mara baada ya kuona Prisila hataki kuona akiendelea kuchekwa.
“Nisisikie mtu anamuongelea tena Hamza , huyu ni braza wangu kuanzia leo hii”Aliongea Side , shida yake ilikuwa ni kutokumfanya Prisila asiondoke maana alikuwa akifurahi kumwangalia.
‘Prisila usikasirike , leo ni siku nzuri na tumekutana na kumjua mpenzi wako hivyo anapaswa kupewa heshima yake”Aliongea na kauli yake iliwafanya wote sasa kutulia.
Prisila alikuwa bado anasita sita kuendelea kubaki , lakini kwasababu Side ndio kaongea aliamua kutulia.
Sasa dakika hio hio mlango wa chumba hicho ulifunguliwa na wafanyakazi waliovalia sare nadhifu walitengeneza njia huku wakionyesha heshima juu ya mwanamke ambae alikuwa akiingia.
“Nini tatizo , mbona kama nahisi kuna mtu anataka kuondoka tayari?”Aliongea kwa kingereza , alikuwa ni mwanamke mchangamfu.
Alikuwa amevaa shati la mikono mirefu la michirizi myeupe na mieusi huku akiachia vifungo kadhaa kifuani , huku chini akiwa amevalia suruali ya rangi ya kahawia akimalizia na koti la surti ya rangi ya kahawia , mavazi hayo yalimfanya kuwa mrembo sana na kuchora umbo lake la kuvutia.
Alikuwa amesuka nywele zake kwa mtindo wa Crochet na kumfanya nyuzi nyuzi ndefu kumwagika begani , alikuwa na weusi angavu rangi ya chocolate, hadhi yake ilikuwa ni ile ya mwanawake wa daraja la juu.
Alikuwa mrembo mno tembea yake kutumia viatu vya skuna na harufu ya marashi yake ya bei ghali ilifanya wanaume kumeza mate.
Kingine cha kuvutia zaidi ni kwamba namna yake ya kuongea ilijaa mapozi na cheo kwa wakati mmoja, ni aina flani ya haiba ambayo mwanamke wa kawaida hawezi kuwa nayo, ni haiba ambayo mtu hufunzwa na sio kuzaliwa nayo.
Mwanamke pekee ambae alikuwa na uwezo wa kushindana nae katika muonekano ni Prisila peke yake , lakini bado haiba yake na utulivu wa macho hakumfikia.
Kitendo cha Hamza kumuona mwanamke huyo akiingia muonekano wake ulibadilika na kuonekana wa usiriasi kidogo na ghafla ni kama amekumbuka kitu alichosahau kuona na kujikuta akitoa tabasamu ambalo limejaa uchungu.
Tatizo pekee ambalo aliliona ni moja tu na kujiuliza imekuwaje huyu mwanamke akawa Tanzania tena katika mazingira kama hayo.
Upande wa mwanamke macho yake yote yalikuwa yamemkazia Hamza , huku akionyesha ishara flani ya kuzuia hisia zake.
Upande wa watu waliokuwa hapo ndani pia walikuwa katika hali ya mshangao , walishangazwa na kivuli cha mwanamke huyo kilivyokuwa na nguvu na kuwasabibishia msisimko.
Alieanza kusimama kwa heshima alikuwa ni Saidi Muhamehd au bosi Side.
“Bosi Yulia! , sikutarajia kama utakuwepo leo?”Aliongea Saidi.
Wengine wote mara baada ya kusikia jina la Bosi Yulia walielewa ni nani anaongelewa na walijikuta wakisimama mara moja , huku maswali yakiwavaa ,wakijiuliza inamaana huyu ndio moja ya mataikoni wa kike ndani ya taifa la Tanzania, mmiliki wa makampuni ya Prima.
Hakuna ambae ashawahi kudhania bosi Yulia angeonekana kuwa kijana na mrembo hivyo, isitoshe wanawake ambao walikuwa ni matajiri hawakuwa na muonekano wa kuvutia tofauti ya Regina na Yulia.
Kila mmoja alionyesha heshima , huyo alikuwa ni bosi zaidi ya Saidi .
Bahati alikuwa na furaha mno kiasi kwamba hakujua ni wapi aweke mikono yake , moyo wake ulikuwa umejaa furaha , mwanzoni mpango wake ulikuwa ni kumtumia Lidya ili kujenga ukaribu na Tajiri Side ndio maana akalazimisha kushiriki kusanyiko hilo lakini sasa anamuona Yulia shabaha yake ilibadilika mara moja.
Muda huo wanadarasa hao walikuwa wakimuonea wivu Saidi mno kutokana na kuwa na ukaribu na bosi mkubwa kama huyo tena mrembo.
“Kwahio kumbe ni wewe bosi Side ndio umeandaa hii party , mniwie radhi kwa bughuza”Aliongea kwa lugha ya kingereza. Na maneno yake mbele ya wasomi hao yaliwashangaza , ilikuwa ni kama wanajiuliza inamaana amefika kwa ajili ya kuangalia party ambayo imeandaliwa na Saidi , lakini sasa kilichotokea mbele kiliwashangaza.
Bosi Yulia alizipiga hatua na kumsogelea Hamza huku akimwemwesa lipsi zake kama mtu aliekosa kujiamini.
“Sikuwahi kuwaza nitakuja kukutana na wewe hapa , nilidhani sitokuja kukuona kamwe”Aliongea na kulikuwa na ishara ya uchungu katika sauti yake.
“It real is fate”Alijibu Hamza kwa lugha ya kingereza akimaanisha ni majaliwa huku akitoa tabasamu.
“Yaani , nilipokuona pale kwenye maegesho ya gari nilijiuliza ninaota au, hata kuja hapa sijaamini kama ni wewe, nimekuja kuhakiki , lakini ni wewe kweli?”Aliongea bila ya kupepesa jicho.
“Bosi Yulia , unafahamiana na Hamza muda mrefu?”Aliuliza Saidi na kufanya kila mtu kutegemea jibu.
“Hamza!! , kumbe ndio jina lako?”Aliongea yulia na kufanya watu kuzidi kushangaa huku wakijiuliza wanafahamina vipi huku hawajuani majina au Hamza hakuwa na jina hapo kabla.
“Ndio”
“Umefika lini na kwanini Tanzania?”Aliuliza Yulia.
“Ni stori ndefu”Alijibu Hamza na kumfanya Yulia kutabasamu.
“Niambie taratibu taratibu , sio rahisi kukutana na wewe hapa , awamu hii nadhani haitakuwa haraka , bado hata sijakushukuru kwa kilichotokea wakati ule kama isingekuwa wewe ning….”
“Miss Yulia , its not convinient to talk about it here “Aliongea Hamza akimaanisha kwamba sio vizuri kuongelea hilo hapo.
“Nini tatizo , kwanini umebadilika sana , wewe katika kumbukumbu zangu sio mpole hivi”Aliongea Yulia.
Watu wote waliokuwa hapo walijikuta wakishangaa kwa kuwaangalia wawili hao na maongezi yao , ilionekana ni kama vile Hamza amemfanyia Yulia kitu cha ajabu nje ya nchi , ndio walivyotafsiri.
Yulia alionekana kuelewa na hapo hapo alimsogelea Hamza karibu kabisa, huku akiona hali hio aliokuwa nayo Hamza inamvutia mno , walisogelena karibu kiasi kwamba mpaka pumzi zao zinagusana ngozi ya kila mmoja.
“Then do you want to come to my house ?, just me and you alone , we can have a good chat”Aliongea akimaanisha au anataka aende nae kwake wakiwa wawili tu na kufanya maongezi yawe mazuri zaidi.
Alichokuwa akifanya Yulia ni kumpagawisha Hamza mazima tena bila ya kificho.
Sasa fikiria bosi mkubwa kama Yulia anamfanyia hivyo Hamza ambae sisi tunamjua ni mzembemzembe.
Kauli hio ilimfanya Prisila na wenzake wote kutoa midomo kiasi kwamba ukiwawekea yai linapita.
Walijiuliza Hamza ana nini mpaka mwanamke wa aina hio kumwalika kwa kimitego namna hio.
Tajiri Side hata yeye muonekano wake ulibadilika , ulikuwa muonekano mzito , hasa baada ya kupotezewa kabisa na Yulia.
“Just who is Hamza!!?”Ndio swali ambalo lilimvaa mara moja.
Prisila alikuwa akimjua Yulia vizuri kwa kumsikia , lakini kitendo cha mwanamke huyo kumfahamu Hamza ilimfanya awe na shauku ya kutaka kujua kwanini Hamza anafahamiana nae , ukweli ni kwamba hio ni mara ya pili kwa Hamza kumsahngaza , mara ya kwanza ilikuwa ni mwanasayansi nguli wa hisia za kibinadamu wa taasisi ya Felizi yaani Frida na leo ni tajiri Yulia.
Kitendo cha Hamza kuwa katika hali kama hio na mwanamke tajiri na mrembo kama huyo ilikuwa ni vibao chapuchapu kwa kila mtu ambae alikuwa akimbeza kuwa fundi.
Watu hao ambao waliona hawawezi hata kukaa meza moja kula chakula na Yulia na sasa walikuwa wakimbeza mwanaume ambae alionekana ana historia nae.
Wale wote ambao walicheka sana walianza kumwangalia Lidya kwa macho ya hasira, walijiambia kama sio Lidya kuongea upuuzi wake na umbea umbea wasingejiweka upande mbaya na Hamza na pengine wangeweza kupata walau nafasi ya kujipendekeza kwa Yulia.
Upande wa Hamza hakuwa na mawazo hayo kabisa , alijua kama Yulia ataendelea kuropoka itamletea shida kabisa hususani katika matukio ambayo yamekwisha kupita
Hivyo Hamza bila kujifikiria mara mbilimbili alimshika Yulia mkono na kisha akamvuta kumtoa katika chumba hicho.
“Niufuate” Aliongea.










SEHEMU YA 44.
MASAA KADHAA NYUMA.
Jaususi Mstaafu Amosi hakutaka kuchelewa hata dakika moja mbele ya Kanali Dastani , alijua akifanya kosa tu atawahiwa ndio maana usiku huo huo mara baada ya kumuwekea kirusi Kanali katika chumba cha Pub ile moja kwa moja alianza kufanya uchunguzi juu ya wapi ataweza kumpata Mchuku, mkuu wa Gereza.
Katika ujasusi wake kuna mambo makuu mawili ambayo alipata , kwanza alijua kuna mfungwa ambae amehusika na kesi ya Sedekia ambae yupo gerezani , jambo hili hakuwahi kulisikia hapo kabla licha ya kwamba ni swala ambalo lilitokea wakati yeye akiwa kitengoni , hakujua kwanini swala hili lilifichwa sana.
Swala la pili nin mahusiano ya Tresha Noah na Kanali , alikuwa akijua fika Mheshimiwa Raisi ambae anakwenda kumaliza muda wake alikuwa ni raisi ambae anapenda warembo , hili lilikuwa swala la wazi mpaka kwa watanzania , licha ya kwamba Raisi Elias alifanya makubwa katika uongozi wake lakini udhaifu wake ilikuwa ni wanawake , tokea siku ambayo alifiwa na mke wake akiwa madarakani ndio aliongeza moto.
Ukweli ni kwamba wakati wa kifo cha First Lady kinatokea sekeseke liibuka huku ikiaminika ni raisi huyo kumuua mke wake baada ya kumsaliti na moja ya tajiri Mkubwa aliekimbia nchi na kuishi uhamishoni kwa muda mrefu.
Wengi wanaamini kutokea kwa kifo cha First lady kulimfanya azidi kubadilika tabia na kuendekeza ngono, lakini kwanzia hapo Raisi Mbilu alikuwa makini sana na wanawake ambao anatembea nao , hata kama hakuwa akiwapenda lakini hakutaka wamsaliti , pengine ilikuwa ni Trauma aliopata kutoka kwa mke wake ambae inasemekana alimpenda sana.
Sasa Amosi kujua swala la mwanamitandao ya kijamii maarufu Tresha Noah kuwa na mapenzi ya siri na Kanali ilikuwa ni kete ambayo kwake aliona itafikia muda atatakiwa kuicheza vizuri na sio kwa kurupuka.
Kutokana na swala la mfungwa huyo kuwa siri , hakujua moja kwa moja atakuwa yupo gereza gani na njia pekee ambayo aliona inaweza kumpa majawabu ya haraka haraka ni kupitia kitengo cha TISA(Tanzania inteligence service Agency).
Lakini hata hivyo asingeweza kupata taarifa hio ya siri kwa uharaka bila ya kutumia mtu mwenye madaraka na pia katika mazungumzo ya Kanali Dastani alisikia Waziri akihusishwa hivyo moja kwa moja aliona sio jambo jepesi.
“Shit.. nimesahau kitu muhimu Mchuku ni mkuu wa Gereza hivyo ni rahisi kufuatilia anahudumu katika gereza lipi kupitia Mkuu wa Magereza”Aliwaza Amosi huku akijiona mjinga,kwanini hakufikiria njia nyepesi hio.
Dakika ileile baada ya wazo hilo kumwingia alisimamisha IST yake pembeni na kulitafuta jina la moja ya Askari polisi ambae aliamini lazima atakuwa na taarifa ya wakuu wa Magereza kwa upande wa jiji la Dar es salaam, alienda kwenye majina mpaka akalifikia jina la Afande Chika na kupiga simu lakini jibu ambalo alipata lilimkatisha tamaa , simu yake haikuwa hewani , lakini hata hivyo aliona haina haja ya kukata tamaa , alitafuta namba nyingine , jina lilikuwa ni Sajenti Ulimboka na alipiga na simu iliita dakika chache na kupokelewa na kuanza kusikia makelele.
“Amosi nipigie baadae , nipo eneo la tukio’Sauti upande wa pili ilisikika na kumfanya Amosi kukunja ndita.
“Ulimboka namuulizia Afande Chika, hapatikani hewani kupitia namba yake ya kawaida”Aliongea Amosi kwa haraka haraka.
“Amosi unaemtafuta jeshi la polisi pia linamtafuta , sijui kwanini unamtafuta ila kwasasa nipo kwenye majukumu ya kazi, nipigie asubuhi”Aliongea Ulimboka na kabla hata hajampa maelezo Amosi ya kueleweka simu ilikatwa palepale na kumfanya Amosi kutamani kutoa tusi.
Mpaka hapo koneksheni yake polisi ilikuwa ishafika mwisho , Amosi licha ya maisha yake mtaani kuonekana kama vile ni ya kihalifu hakuhitaji kujuana na askari wengi polisi , alihitaji afande mmoja tu mwenye nguvu na ambae anaishi kifisadi na huyu alikuwa ni Afande Chika.
Asichokijua Amosi ni kwamba Afande Chika aliingia katika mikono ya Chatu na haieleweki alifichwa wapi mpaka kutokuonekana kwake au amekufa au lah.
Baada ya kukosa jibu la haraka haraka aliona amuhusishe bosi wake wa kazi ,yaani Brigedia Doswe , ilikuwa ndio njia yake ya mwisho kutaka kupata kile anachohitaji tena mapema mno.
Hakujali muda ni saa ngapi na ingeonekana ni ukorofi wa namna gani kumpigia Brigeida muda huo lakini kwasababu jeshi ni kazi ya wito pia, hakujifikiria mara mbilimbili na kupiga simu na iliita kwa muda mrefu bila ya kupokelewa , alipiga mara nyingine na haikupokelewa na aliamini moja kwa moja Brigedia huenda amelala hivyo aliona labda afanye asubuhi asubuhi , jambo la uhakika tu ni kwamba Brigedia angeona missed call zake angempigia.
Amosi kinyonge alirudi garini na kuliwasha kisha taratibu aliliingiza barabarani huku mpango wake ni kurudi nyumbani kwa ajili ya kupumzika, akiwa njiani alikuwa akifikiria kauli ya Ulimboka juu ya DCP Chika kutafutwa na polisi, ilikuwa kichekesho kwake , yaani polisi anatafutwa na polisi wenzake, alijua lazima kuna kitu kinachoendelea.
Wakati akiwa katika mataa ya Mwenge ili aelekee Mikocheni kwenye apartment yake simu yake ilianza kuita na alipoangalia anaepiga ni Brigedia , palepale alipunguza mwendo wa gari na kupokea simu.
“Jambo Afande “
“Jambo ,Amosi habari za usiku , kuna taarifa yoyote?”Aliongea Brigedia na sauti yake iliashiria haraka na Amosi alilitambua hilo.
“Nimepata uelekeo wa ile kazi ya Wabrazili , nilimfuatilia Kanali na nimemsikia akiwa katika mazungumzo na moja ya wakuu wa Magereza wakizungumzia juu ya Mfungwa aliehusika na kifo cha Sedekia…”
“Amosi hebu acha kuendelea kuongea kwanza , Umesikia wapi hio taarifa nyeti hivyo ya daraja la kwanza kitengoni?”
“Mkuu ni kama nilivyosema nilisikia mazungumzo kutoka kwa Kanali Dastani..”Aliongea Amosi huku akijiuliza mbona amekasirika baada ya kusikia hilo swala , inamaana hata yeye alikuwa akijua na ameupiga kimya.
“Amosi kuhusu swala hilo ni sehemu ya siri za taifa kwa kushirikiana na washirika wetu wa nje , ni swala linalogusa diplomasia ya nchi , niambie unachotaka nikusaidie ni nini kwenye uchunguzi wako , ila achana na swala kabisa la mfungwa , sitoweza kukuepusha tena na kifo uking’ata zaidi ya usichoweza kumeza”
“Nataka kujua Afande Mchuku ni Mkuu wa gereza lipi Afande , nimejaribu kuwasiliana na Afande Chika lakini hapatikani hewani…”Aliongea na upande wa pili ulikuwa kimya na kumfanya Amosi kusimamisha gari mkabala na hoteli ya Krebyss.
“Amosi nipo na Afande Mafulu hapa CP wa mkoa , kama unaemzungumzia ni Afande Kigo Mchuku taarifa za kifo chake zimeripotiwa sasa hivi kwa wakati mmoja na za DCP Chika , kuna uwezekano unachotaka kufuatilia kwa Mchuku ndio kimemuua akiwa chooni huko Fulu Dozi Bar Segerea , alikuwa kaimu mkuu wa gereza la Segerea baada ya Afande Simba kupalalaizi , Amosi kesho fika ofisini kwangu nadhani tuna la kuongea, kwasasa nakata simu nipo kwenye kikao”Aliongea na simu ilikatwa palepale
Amosi alijikuta akitoa macho , yaani ndani ya dakika kumi tu mtu ashapoteza maisha , akili ilijaribu kumwambia pengine ni Dastani lakini iligoma kabisa, Japo Kanali Dastani aliaminiwa kwa uwezo wake wa akili na ushapu lakini sio kwa namna hio ,kuna kitu tayari alikihisi pengine kuna muhusika mwingine , lakini swali liliibuka palepale , kwanini Mchuku afariki ndani ya dakika chache baada ya kuwasiliana na Dastani , akili yake ilimjibu lazima alichorekodi kina taarifa ya kutosha , swali lingine kama ameuwawa je alichorekodi kimechukuliwa na muuaji jibu hakupata na kwa haraka haraka aling’ata meno kwa hasira na kujiambia anapaswa kuwahi Fuludozi Bar eneo la tukio kabla ya taarifa hazijamfikia Kanali Dastani , aliamini lazima angepata kitu.
*******
Upande mwingine nusu saa mbele lango la nyumba ya mapumziko ya Mheshimiwa raisi lilifunguliwa na gari aina ya V8 iliingia na palepale alitoka mwanaume mwenye muonekano mgumu kidogo mwenye masharubu.
Kama Amosi angekuwepo angemfahamu mara moja , ndio mwanaume ambae alimpiga risasi ya ubavuni mpaka kumpelekea kulazwa siku kadhaa katika hospitali ya jeshi.
“Nipo kwa ajili ya kuonana na mheshimiwa”Aliongea bwana huyo mara baada ya kuzuiwa na bodigadi namba moja wa raisi.
“Mheshimiwa ametoa taarifa hataki usumbufu”Aliongea bodigadi yule akiwa na sura isiokuwa na utani , hakuwa na dalili yoyote ya kumpisha, sio kama hamjui alikuwa akimjua lakini alizingatia itifaki za ki usalama kwa mheshimiwa, hususani muda huo wa usiku.
“Ni swala muhimu Afande , napaswa kuripoti mara moja kwa mheshimiwa na kupotea”
“Kama nilivyosema Mheshimiwa kapumzika, hakuna namna ya kuonana nae sasa hivi, kama una maagizo yoyote yaache hapa nitayafikisha”Aliongea na kumfanya bwana yule kumwangalia kwa macho makali kidogo na alionekana kutulia kidogo na aliingiza mkono mfukoni lakini kitendo chake kilifanya walinzi wote kukoki bastora na kumnyooshea wakidhani anatoa siraha licha ya kumkagua getini, lakini bwana yule alinyoosha mkono juu kwa ishara ya kujisalimisha huku mkononi akionekana ameshika kitu.
Afisa huyu mkuu wa kitengo cha Itifaki mara baada ya kuona kitu kilichokuwa kwenye mikono ya yule bwana alinyoosha mkono na kuchukua.
“Ni taarifa ambayo nilipaswa kumpatia mheshimiwa moja kwa moja , kazi alioniagiza nimemaliza”Aliongea na Kanali Ashrak alimwangalia bwana huyo kwa macho ya umakini na kisha aliwapa ishara wenzake kushusha siraha chini.
Unajua nyumbani kwa raisi unaweza ukaruhusiwa kuingia getini lakini ukashindwa kupita mbele ya kitengo cha itifaki ya kumuona Raisi ambacho huongozwa na ADC mwenyewe , hiki ndio kilichomkuta.
“Bundi najua ukaribu wako na mheshimiwa na naheshimu hilo lakini kwasasa hali ya usalama kwa mheshimiwa imeimarishwa ni vizuri ukipotea mpaka pale mheshimiwa atakapokuhitaji yeye mwenyewe. This isn’t personal” Aliongea ADC na Bundi alitingisha kichwa kuelewa na kisha alisindikizwa na kutoka nje kabisa.
Kanai Ashrak aliishia kuangalia ile flashdrive na kisha alitoa tabasamu na kuiweka mfukoni na baada ya pale alitoa ishara kadhaa kwa wenzake na kuingia ndani, pengine alikuwa akipeleka ujumbe ule kwa mheshimiwa lakini mara baada ya kuingia ndani haikuwa hivyo , mmoja kwa moja alielekea katika chumba kingine ambacho ndani yake kilikuwa na tarakishi.
****
Kilichowaacha midomo wazi zaidi ni kwamba Yulia hakuleta ukinzani na zaidi sana alionyesha kufurahi kushikwa mkono na kutolewa nje, lakini kitendo cha Hamza kumtoa Yulia mpaka kwenye Korido mabodigadi waliingilia kati na kumzuia.
“Mkuu muachie bosi wetu , vinginevyo usitulaumu tukichukua hatua”Aliongea mmoja wapo lakini kauli yao ilimfanya Yulia uso wake kujikunja na kuwafokea.
“Ondokeni njiani , yoyote atakaemchokoza huyu mwanaume awe makini maana nitamtimua , kingine msinifuate”Aliongea na kufanya wafuasi wake kuangaliana kwa mshangao , hawakuwahi kumuona bosi wao kuwa legelege mbele ya mwanaume kama hivyo.
Hamza alimpeleka Yulia mpaka floor inayofuata upande wa balkoni sehemu ambayo aliona ni tulivu.
Mara baada ya kusimama alijikuta akivuta pumzi nyingi na kumwangalia mwanamke huyo , upepo wa bahari ndio uliowapuliza na kufanya nywele za kizungu za Hamza kupepesuka.
Hamza alikuwa akimchunguza mrembo huyo na kitu pekee alichoona ni kwamba hakuwa amebadilika kabisa , alikuwa mrembo vilevile kama alivyomuacha.
“Unaniumiza bwana mkono wangu”Aliongea na palepale alimfanya Hamza kukumbuka kumbe amemshikilia mkono huyo mrembo.
“Sorry”Aliongea Hamza na kumuachia.
“Usiwaze unaweza kuendelea kunishika mpaka uchoke , kwasababu miaka saba iliopita ulikuwa muhuni zaidi ya hivi , kunishika mkono tu kuna tatizo gani?”
Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akimeza mate mengi na kutoa tabasamu.
“Hehe ,, mpaka leo unakumbuka”Aliongea Hamza lakini mrembo huyo ambae macho yake ni kama yamejaa maji aliendelea kumwangalia Hamza huku akionekana kuwa mbali kihisia.
“Imekuwaje upo hapa Tanzania, sehemu ambayo sijawahi kuiwazia utakuwepo hata mara moja?”
“Kuna mambo yalitokea na kunifanya kuchoka maisha niliokuwa nayo, nikaona nibadilishe mazingira na kwasababu ya kuijua lugha ya kiswahili vizuri Tanzania ndio niliona mahala sahihi”
“Unajua kiswahili?”Aliongea , ukumbuke hapa muda wote walikuwa wakitumia kingereza.
“Najua ndio”Aliongea Hamza kwa kiswahili na kumfanya Yulia kushangaa.
“Sikutegemea kama ungejifunza kiswahili na kuongea kama mzawa”Aliongea.
“Mimi ni Mzawa hivyo najua kiswahili vizuri tu siwezi kukuambia chochote lakini jua hivyo”Aliongea Hamza.
“Mwisho wa siku licha ya kuwa hapa nchini hujajua kilichotokea na kukutana kwetu ni kwa bahati mbaya tena, wakati ule hukutaka kunipatia hata mawasiliano yako na sasa unaanza kunificha pia”
“Ni kwasababu mambo yangu hayahusiani kabisa na wewe , Madam unapaswa kujua sasa hivi mimi ni mfanyakazi na mwanachuo tu , hivyo yaliopita tuyaache yapite”
“Mwanachuo?, Mfanyakazi?”Aliuliza kwa mshangao , ilikuwa ni kama vile amegundua uwepo wa sayari nyingine katika mfumo wa jua kwa mshangao wake.
“Nipo Dosam pale msaidizi wa karibu kabisa na CEO?”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu la kejeli ni kama vile nafasi hio haikuwa ikimtosha, Regina na hasira zake za karibu angekuwepo pengine angemtukana.

“Nini..isijekuwa umempenda bosi wa kampuni ya Dosam , Regina Wilsoni namfahamu vizuri alivyo mrembo”
“Hehe… najua CEO wetu ni mrembo lakini haimaanishi kwamba nimempenda nipo kikazi zaidi”
“Siwezi kuamini , kwa uwezo wako si ni rahisi sana kupata pesa , isitoshe sidhani kama Regina anakufaa inasemekana ni mgonjwa wa aki…”Alitaka kuongea lakini alisita.
“Ni mgonjwa wa nini..??”Aliuliza Hamza akiwa siriasi na kumfanya Yulia kuonyesha kujutia palepale mdomo wake , lakini alijua ni kwasababu ya furaha kubwa aliokuwa nayo.
“Sina maelezo ya kutosha , taarifa hizi ni za siri pia , nimesikia ni mgonjwa wa akili wa nafsi mbili , itakuwa vizuri zaidi ukifuatilia kwa upande wako”Aliongea Yulia na kumfanya Hamza kushangazwa na jambo lile mno.
“Kuna mwingine anaejua kuhusu hili?”
“Sidhani kama kuna anaefahamu , lakini niamini mimi taarifa hii ni ya siri mno hata familia yake hakuna anaejua kasoro bibi yake pekee, ninachomaanisha ugonjwa wake ukimpata hata kama anaweza kukupenda akiwa na nafsi ya Regina akibadilika anaweza akakupotezea moja kwa moja”Aliongea na kumfanya Hamza kuwaza lakini muda huo Yulia alitumia kumsoma Hamza kimawazo na kuna kitu alichogundua lakini hakutaka kukiweka wazi.
“Kuhusu hili nitafuatilia , kama umesema ni la siri naomba liendelee kuwa siri , mimi kama msaidizi wake wa karibu chochote kikimpata nitawajibika”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Yulia kuwa na wivu wa wazi.
“Yulia ninachomaanisha usije ukaruhusu mawazo yako yakaenda mbali , nipo ndani ya kampuni ya Dosam kwa ajili ya kutengeneza pesa kama watu wa kawaida , mimi sio mtu ambae umekutana nae miaka saba iliopita”
“Kama huo ndio mpango wako , kwanini usijiunge na kampuni yetu ya PRIMA? Nitakupa nafasi ya kuwa bodigadi wangu, haijalishi Regina anakulipa kiasi gani nipo tayari kulipa zaidi yake”
“Hapana haiwezekani , nimeshasaini nae mkataba , isitoshe kwa ulichosema nadhani anahitaji ulinzi zaidi kuliko wewe”
“Unanionaje , nipo tayari kukuliipa milioni ishirini kwa mwezi , kama haitoshi nitajie kwa ajili yako nipo tayari kulipa kiasi chochote”Aliongea na kumfanya Hamza kuona Yulia anachagua cha kujibu maneno yake na kumfanya acheke.
“Yulia tulikutana kwa muda mchache sana Zurich , hivi unadhani kuniona vile ndio kunijua , ukweli ni kwamba hujui chochote kuhusu mimi halafu unataka niwe bodigadi wako?, mbona kama unaniamini sana kupitiliza”
“Mimi ninachojua wewe sio mtu mbaya , kama kweli ungekuwa ni mtu mbaya usingeniokoa katika dakika zangu za mwisho za uhai”Aliognea huku awamu hio akilegeza sauti na mikono yake kuiweka katika mabega ya Hamza.
“Au upande wako mwingine unakufanya kuwa mbaya , kama ni hivyo nakufaa zaidi ya Regina”Aliongea huku aking’ata lipsi zake kwa namna ya kukonyeza na pumzi yake kuizuia na kufanya jicho kulegea.
Matendo yote ya Yulia yalimfanya Hamza mwili wake kuwaka moto, Yulia alikuwa akijua anachokifanya katika kumpagawisha.
Hamza mara baada ya kuona yanakwenda kumshinda alimshika kwenye shingo kwa spidi ya hali ya juu na kwenda kumbana kwenye ukuta na kusogeza mdomo wake karibu zaidi huku Yulia akiendelea kumwangalia kwa macho ya kumruhusu lakini yaliojaa waswasi kwa wakati mmoja.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTINZI: SINGANOJR

SEHEMU YA 45
ILIPOISHIA
“Yulia ninachomaanisha usije ukaruhusu mawazo yako yakaenda mbali , nipo ndani ya kampuni ya Dosam kwa ajili ya kutengeneza pesa kama watu wa kawaida , mimi sio mtu ambae umekutana nae miaka saba iliopita”
“Kama huo ndio mpango wako , kwanini usijiunge na kampuni yetu ya PRIMA? Nitakupa nafasi ya kuwa bodigadi wangu, haijalishi Regina anakulipa kiasi gani nipo tayari kulipa zaidi yake”
“Hapana haiwezekani , nimeshasaini nae mkataba , isitoshe kwa ulichosema nadhani anahitaji ulinzi zaidi kuliko wewe”
“Unanionaje , nipo tayari kukuliipa milioni ishirini kwa mwezi , kama haitoshi nitajie kwa ajili yako nipo tayari kulipa kiasi chochote”Aliongea na kumfanya Hamza kuona Yulia anachagua cha kujibu maneno yake na kumfanya acheke.
“Yulia tulikutana kwa muda mchache sana Zurich , hivi unadhani kuniona vile ndio kunijua , ukweli ni kwamba hujui chochote kuhusu mimi halafu unataka niwe bodigadi wako?, mbona kama unaniamini sana kupitiliza”
“Mimi ninachojua wewe sio mtu mbaya , kama kweli ungekuwa ni mtu mbaya usingeniokoa katika dakika zangu za mwisho za uhai”Aliognea huku awamu hio akilegeza sauti na mikono yake kuiweka katika mabega ya Hamza.
“Au upande wako mwingine unakufanya kuwa mbaya , kama ni hivyo nakufaa zaidi ya Regina”Aliongea huku aking’ata lipsi zake kwa namna ya kukonyeza na pumzi yake kuizuia na kufanya jicho kulegea.
Matendo yote ya Yulia yalimfanya Hamza mwili wake kuwaka moto, Yulia alikuwa akijua anachokifanya katika kumpagawisha.
Hamza mara baada ya kuona yanakwenda kumshinda alimshika kwenye shingo kwa spidi ya hali ya juu na kwenda kumbana kwenye ukuta na kusogeza mdomo wake karibu zaidi huku Yulia akiendelea kumwangalia kwa macho ya kumruhusu lakini yaliojaa waswasi kwa wakati mmoja.

ENDELEA
Yulia alikuwa amekabwa kisawa sawa ukutani , umbali kati yao ilikuwa ni sentimita tatu tu.
Muonekano wa Hamza ulikuwa ni ule wa usiriasi , hakukuwa na ishara yoyote ya uzembe , alionekana kama vile ni mtu wa karne nyingi zilizopita na aliinua mkono wake wa kushoto na kukiinua kidevu cha Yulia kwa kukibetua kwa juu.
“Niachie bwana, unaniumiza ujue?”Aliongea akilalamika na hio yote ni mara baada ya kuona macho ya Hamza yalivyokuwa na usiriasi usiokuwa wa kawaida hata kidogo , ule ujasiri wake mbele ya Hamza ulimpotea na sasa alikuwa ni kama Panya mbele ya paka.
Muda huo alikuwa ashapoteza ule muonekano wake wa hadhi ya ubosi , aligeuzwa ghafla tu na kuonekana kama msichana mdogo ambae amekosa msaada.
“Unaonaje ukiondoka hapa Tanzania?”Aliongea Hamza huku akiwa na tabasamu lililojaa uovu na kumfanya Yulia uso wake kuwa wa moto huku mboni za macho yake zikicheza cheza.
“Usije kujaribu kunichezea na kujaribu kuniwekewa mtego , maana nikigundua sina uhakika kama utaendelea kuwa salama”Aliongea Hamza.
“Hmmm..”Yulia aliishia kutingisha kichwa akikubali.
Alikuwa akiamini, kuwa kwake ndani ya jiji la Dar es salaam sehemu aliozaliwa na kuijua vizuri basi angeweza kuwa na uwezo wowote mbele ya wanaume na kuwasumbua , lakini hakuamini Hamza alishajua alichokuwa akiwaza tokea muda mrefu.
Yulia alikuwa akisita kukubali lakini kutokana na muonekano wa kutisha wa Hamza alijikuta akikubali kishingo upande , kwasababu Hamza hakuwa na dalili yoyote ya kutania.
Hamza mara baada ya kuona mwanamke huyo ameshika adabu yake na ameogopa alimwachia.
“Usije kuthubutu kuongea chochote kilichotokea baina yetu jijini Zurich , sitotaka kujiingiza kwenye matatizo kwasababu yako”
“Nimekuelewa , lakini je naweza kukutana na wewe?”Aliuliza Yulia, hakuwa mwanamke mpumbavu asielewe nia ya Hamza.
“Kwanini unataka kukutana na mimi?”Aliuliza .
“Mbona nahisi kama unanichukia?”
“Haipo hivyo , lakini hakuna chochote kati yetu , nilifika Zurich kwa misheni maalumu ya kukuua na nikakuta umeshatekwa tayari nikakuokoa , kama nilichofanya kinachukuliwa kama kuokoa uhai wa mtu basi nitakuwa nimeokoa maelfu ya watu , itakuwa ni kujichosha kuanza kukutana na kila mmoja kwasababu hio tu”Aliongea.
“Sio kweli , hukuniokoa tu , lakini vilevile umenisaidia kulipiza kisasi kwa kundi lote la watu waliomuua mama yangu na mdogo wangu , ni wewe ulienisaidia kulipiza kisasi na ukaenda mbali kunipa nauli ya ndege kurudi nyumbani kwa kunitoa katika lile giza licha ya mbinu yako kuwa rafu”Aliongea huku muda uleule akiinamisha macho yake chini.
“Kwa kipindi chote tokea nirudi nyumbani , nimetumia kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kutuma watu kukutafuta , lakini ilikuwa ngumu kwangu kwani sikuwa nikilifahamu jina lako na unapoishi”
“Ulikuwa ukituma watu kuja kunitafuta?”Aliuliza Hamza huku akicheka.
“Ulitaka kufanya nini baada ya kunipata , usiniambie mpango wako ni kunilipa kupitia mwili wako?”Aliuliza Hamza na kumfanya Yulia kumwemwesa lipsi zake , macho yake yalikuwa yamejaa matarajio.
“Kama nipo tayari utaniruhusu?”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia huyo mrembo na kisha akavuta pumzi na kuzishusha.
“Ijapokuwa ombi lako linavutia sana , nataka kuendelea kuishi maisha ya amani , nikijihusisha kwa namna yoyote na wewe nina uhakika nitajipalia tu makaa na kuingia matatizoni, isitoshe mimi siwezi kurudi na kuwa wa zamani tena”Aliongea.
“Inaonekana mpango wako ni kukaa Tanzaniwa kwa muda mrefu , kama ni hivyo je naweza kukutafuta japo mara moja moja?”
“Yulia kwa hadhi yako na nguvu ya familia yako , hata kama unataka kupata bodigadi mwenye uwezo wa juu ni kitu chepesi sana , kwanini iwe mimi?”
“Umejuaje ukubwa wa hadhi ya familia yangu , au ulinifanyia uchunguzi kabla?”
“Haina haja ya kuigiza najua mambo mengi kuliko unavyofikiria , katika bango linalotambulisha hoteli yenu , ile Logo inayotambulisha kampuni yenu ni maalumu ambazo zinatolewa kwa familia zenye hadhi na kufanya isitumike kutambulisha biashara za watu wengine duniani , kampuni yako ni kubwa hivyo ni rahisi kukutambulika kimataifa , huwezi kutumia Logo ile bila ya kujua nguvu yake, hivyo moja kwa moja inaniambia familia yako imesajiliwa GREL na kupewa hadhi ambayo inatambulishwa na ile Logo, familia zote ambazo zina usajili wa hadhi ndani ya GREL hupewa alama zinazofanana lakini tofautishi kama ile”Aliongea Hamza.
GREL kirefu chake ni Global Registry of extraordinary lineages. Sio sahihi kuiita GREl kama umoja hadharani kwani haijawahi kutangazwa hivyo bali kwa nje ni kama jarida tu au kitabu cha kutambua hizo familia , lakini kwa siri ni umoja tena wenye nguvu.
Familia ambazo zipo katika orodha ya GREL ni kama vile familia ya Rockfellers , familia ya Rothchild , familia ya Al Saudi kutoka Saudi Arabia, familia ya Fujiwara kutokea Japani na kuendelea.
Kwa lugha nyepesi unaweza kusema familia hizi ndio zenye mizizi ya kihistoria , kiuchumi na ushawishi ndani ya taifa husika au kwa bara zima, yaani ndio sehemu ya familia ambazo zipo ndani ya Deepstate.
Sasa inasemekana wazo la kupatia kila familia yenye nguvu nembo(Logo) lilitoholewa kutoka katika utaratibu wa kifamilia wa familia za damu ya kifalme hususani katika mataifa mengi ya bara la Asia , mfano China na Japani ambapo familia kama vile Tang ina alama yao ya upekee kabisa ambayo haitumiwi katika biashara yoyote ndani ya taifa hilo.
“Wewe ni nani , kwanini unayajua haya yote , umejuaje ile logo ipo katika GREL?”Aliuliza Yulia kwa mshangao.
“Napenda kujifunza vitu vingi nisivyovijua , hivyo niliweza kujua mara moja”Aliongea Hamza.
“Ni kweli familia ninayotokea ipo katika GREL lakini hili linahusiana vipi na wewe kuwa bodigadi wangu?, wewe ndio muokozi wangu nakuamini ndio maana, nimekusubiria kwa muda wote huo , kwanini hunionei huruma?”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia kwa macho ya kichokozi.
“Haya yameisha , naonekana kuchoka wakati wewe hujachoka , nakubali uwezo wako wa kuigiza ni mkubwa , kwanza umeuchukua uhusika wa mwanamke anaeongojea mwanaume wake kwa muda mrefu kukutana nae na kumlipa kwa kutumia mwili wake , tena sasa hivi umetoka katika uhusika huo na unaigiza kuwa mwanamke kama bikra ambae anaogopa na anahitaji mwanaume wa kumlinda , ki ufupi hakuna ukweli wowote kuhusu wewe , hebu niambie umeweza vipi kunitafuta na ni kipi unataka kutoka kwangu?”Aliuliza Hamza na kumfanya Yulia muonekano wake kubadilika na kuwa wa kikauzu.
Mwishowe Yulia alitoka katika ule muonekano wake wa mapozi na kuwa mwanamke mrembo kauzu ambae amesimama kama roboti.
“Umejuaje nakugizia tokea mwanzo , nadhani nilipaswa kuwa makini zaidi”Aliongea
“Uwezo wako wa kuigiza ni mkubwa mno , miaka saba iliopita wakati nakuokoa nilikuwa nishajua muonekano uliokuwa nao ni wa kimaigizo tu”
“Kwanini?”Aliuliza huku akiwa na mshangao , hakuamini Hamza wa miaka saba iliopita aliweza kumtambua mara moja undani wake ukoje.
“Wazazi wako wote na wadogo zako waliuliwa na wale maninja , nilikuokoa na kisha nikakurudisha hotelini , unakumbuka ni kitu gani uliniambia cha kwanza?”
“Nimesahau , nilisema nini?”
“Ulisema una kiu mno ya maji , yaani mtoto ambae mama yake , baba yake na mdogo wake ndio wametoka kufariki unarudi hotelini na kitu cha kwanza baada ya kulia kwa lisaa limoja ni kumuomba mtu usiemjua maji?,watu wengine wanaweza kuona ni kawaida , lakini kwa upande wangu sikuona kitu kile ni cha kawaida, katika moyo wako hukuwa na machungu kabisa ya familia yako kupoteza maisha , uliweza kupotezea kwa muda mfupi sana hisia za huzuni ulizokuwa nazo na kuanza kufikira hatua inayofuata”Aliongea na kauli ile ilimfanya Yulia kushangaa.
“Inaonekana sikuwa msiri vya kutosha mbele yako”Aliongea Yulia.
“Makisio yangu ni kwamba na wewe pia una ugonjwa wa akili wa Protesting personality Disorder , nakosea?”Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu.
“Hakika una uelewa mkubwa sana , tofauti na mama yangu wewe ni mtu wa pili kuijua siri yangu , ningekuwa na uwezo wa kukuua basi ungekufa leo hii”Aliongea akiwa siriasi.
“Duhh!, ili kutimiza malengo yako unataka kumuua kwanza aliekuokoa , yoyote yule anapaswa kufa hata kama ni kwa kumtishia , hizo ndio dalili za ugonjwa wako”Aliongea Hamza kwa upole.
“Huu sio ugonjwa , ni Mungu ambae ameniumba kwa kutoniwekea uwezo wa kuwa na hisia , ili nisisumbuke na hisia ambazo hazina maana”Aliongea.
Unachopaswa kuelewa ugonjwa ambao anauzungumzia Hamza ni aina ya ugonjwa wa akili ambao mtu anazaliwa nao na tabia yake kubwa ni kwamba mtu akiwa na ugonjwa huu huwezi kumkuta akiishi katika uhalisia wake , maisha yake mwanzo mwisho ni maigizo tu pili hata kama anahitaji msaada na akaupokea kamwe hawezi kukubali alisaidiwa na njia pekee ni kumuua aliemsaidia ili kulinda siri ya kusaidiwa , dalili nyingine ni kwamba watu wa aina hii hawana hisia kabisa, yaani wapo kama maroboti yalivyo , yaani hawahisi maumivu wala furaha tofauti ni kwamba utawakuta wanaigiza kuhisi maumivu au furaha , au kupenda, ndio walivyo, haijawahi kufahamika unasababishwa na nini lakini kitaalamu unaendana na ugonjwa wa akili unaofanana na Munchausen Syndrome.
“Kama hivyo ndio unavyowaza , basi hakuna tatizo , ila usijali siwezi kuwaambia watu kuhusu tatizo lako”Aliongea na kumfanya Yulia aliekuwa kama roboti kupiga hatua moja mbele na kumwangalia Hamza usoni.
“Kama ulijua tokea mwanzo kuhusu tatizo langu kwanini bado ukaendelea kutoa ushirikiano kwangu?”
“Kama ilivyokuwa miaka saba iliopita , tulikutana kwa bahati mbaya , hivyo haina haja ya kuongea chochote kuhusu mimi ili mradi hatutokutana tena , sitaki kujua wewe ni mtu wa aina gani na kipi unafanya, ki ufupi sitaki kujua chochote kuhusu wewe?”
“Kwanini bado naona unaonekana kujali maisha yangu , mpaka kuijua siri yangu?”
“Hapana , ninachomaanisha ni kwamba sitaki kupitia maigizo yako unitumie na mimi kama kete yako kwenye mipango yako , kwa kusema hayo siwezi kuwa bodigadi wako au mtu yoyote kwako”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfanya Yulia midomo yake kupinda kwa tabasamu lililojaa uovu.
“Ijapokuwa sijui ni hisia gani ambazo wanawake wanapata wakimpenda mwanaume lakini mimi nahisi nakupenda”Aliongea na kumfanya Hamza kutoa tabasamu huku akijihisi huu upendo utaanza kumbadilisha muda si mrefu.
“Lakini hata hivyo , kuna kitu kimoja ambacho hujapatia”Aliendelea kuongea
“Oh! , ni kitu gani hicho?”
“ Sijakutana na wewe kwa kukutafuta , ni kwa bahati tu tumeonana ndio maana natafsiri kama majaliwa”
“Kama ni hivyo nadhani nilipangiwa kupatwa na hili janga?”
“Ndio , hili ni janga kwako, lakini kwasababu unajua siri yangu basi kwanzia leo hatutojihusisha kwa lolote kati yetu , vinginevyo wewe ufe au mimi nife”Aliongea Yulia na kumfanya Hamza kugeuka na kuzipiga hatua kurudi alikotoka.
“Nadhani pia unapaswa kuomba sana isije ikatokea siku moja nikaliharibu ua kwa ukatili”Aliongea Hamza na kutokomea
Kitendo cha Hamza kupotea katika macho yake , Y ulia alitoa simu yake katika mfuko na kubonyeza namba.
“It’s me .. Go find someone Called Hamza , I want all his information..”Aliongea kwa lugha ya kingereza
Baada ya kumaliza kutoa maelekezo aliweka nywele zake sawa pamoja na nguo zake na kurudia muonekano wake na kutoa tabasamu la kimaringo na mapozi na kwa madaha alizipiga hatua kurudi ndani.
Hamza na Yulia walitumia zaidi ya dakika kumi kwenye kuongea tu , lakini kwa watu ambao walikuwa ndani ya chumba binafsi , walikuwa na hisia mchanganyiko kana kwamba ni muda mrefu sana umepita tokea watoke , ikiwemo kwa Prisila ambae ni kama alianza kushikwa na wivu.
Lidya na Bahati walikuwa wakijutia maneno yao kiasi kwamba utumbo wao ulikuwa ukijinyongorota na kufanya nyuso zao kuonekana mbaya.
“Prisila hivi ni kweli Hamza ni fundi wa kawaida tu?”Aliuliza Saidi na kwa upande wa Prisila ukweli ni kwamba alimjua Hamza juzi tu hivyo hakuwa na taarifa za kutosha.
“Alikuwa fundi ndio , lakini sasa hivi ana kazi yake nzuri tu”Aliongea Prisila akilenga Hamza kuwa boyfriend feki wa Regina na pia msaidizi wake.
Ijapokuwa Prisila aliongea hivyo lakini hakuna ambae aliweza kuelewa kile alichomaanisha haswa , ilikuwa ni kama kauli yake ni nyepesi sana kwa swali gumu ambalo ameulizwa.
Muda huo wakitaka kumchimba zaidi ndio muda ambao Hamza alirudi na mara baada ya kundi lote kuona hakuna anaekula zaidi ya kuonekana kama watu wanaesubiria mtu alijikuta akishindwa kujizuia na kutoa tabasamu.
“Nyie mnafanya nini , mbona kama mpo kwenye kikao?”Aliuliza. lakini ilikuwa ndio nafasi ya kila mmoja kuanza kumuuliza maswali Hamza.
“Hamza kwanini hukutuambia unafahamiania na bosi Yulia?”
“Hamza umefahamiana vipi na bosi Yulia?”
“Bro Hamza , Kaka mkubwa , hebu kwanza kunywa hii Wine nadhani itakidhi radha ya ulimi wako?”
Yaani ki ufupi bila aibu kila mtu alianza kuwa chawa kwa kujipendekeza kwa Hamza
Lakini Hamza hakuwa na mudi ya kuendelea kula tena na alichotaka ni kuedelea kumpa kampani Prisila hivyo aliwapotezea kabisa , isitoshe alijua kabisa taifa hili lazima lipo chini ya Yulia , hivyo chochote atakachofanya kinaweza kumletea shida.
“Prisila vipi chakula ni kitamu?”Aliuliza Hamza na Prisila kwa kumwangalia tu Hamza ni kama kuna kitu amekisoma.
“Ni kitamu ila nimeshiba , unaonaje tukitangulia kuondoka , nahitaji kwenda kupumzika”
“Hakuna shida nitakusindikiza”Aliongea na muda huo huo wote walisimama ili kuondoka na watu hao waliona aibu kwa kuona kwamba Hamza amechoshwa na kujipendekeza kwao.
Muda huo ambao Hamza anataka kuondoka Yulia alirudi na kuingia na mara baada ya kuona Hamza anaondoka alitoa tabasamu la kumuaga.
“Hamza , siku nyingine ukiwa na muda jaribu kuja hata mara moja moja basi , haina haja ya kuwa mpole mbele yangu”Aliongea na Hamza alitoa tabasamu hafifu.
Muda uleule Yulia alichukua kadi ya madini ya dhababu kutoka kwa msaidizi wake.
“Hii ni kadi ya daraja la juu kabisa ya uanachama wa hoteli zetu, ndani ya jiji hili wanazo watu wasiopungua kumi , ichukue na unaweza kuja hapa muda wowote ndani ya masaa ishirini na nne na hutoweza kulipia hata shilingi”Aliongea
Lidya, Bahati na tajiri Saidi mara baada ya kuona hio kadi macho yao yaliwatoka kwa matamanio na wivu , hata kadi ya unachama ya Bosi Side haikuwa ya daraja la juu kama hio, kadi hio ilimaanisha unaweza kuingia ndani ya hoteli hio na kupata huduma bila ya kulipia hata shilingi.
Sasa walijiuliza kadi ya hali ya juu ya namna hio inakuwaje Yulia anampatia Hamza, lakini sasa wakati kila mtu akiitamani upande wa Hamza aliikataa.
“Nashukuru sana , lakini haina haja”
Lidya na wenzake kichaa kilitaka kuwapnda , ni kama walikuwa wamesikia tofauti hata kwa bosi Side alijikuta akikunja ndita bila ya kupenda.
Ukweli ni kwamba maana halisi ya kadi hio sio kwa ajili tu ya kupata huduma bure katika mahoteli yote ya Prima , bali ilikuwa ikiashiria hadh, sasa inakuwaje Hamza hataki kadi kama hio tena kwa kumkatalia mtu mwenye nguvu kama Yulia.
Upande wa Yulia licha ya kukataliwa waziwazi hakujali sana , alijua Hamza alikuwa akifanya hivyo ili kumuepuka , lakini sasa kadri ambavyo Hamza alijifanya kumkataa ndio alivyozidi kumtaka.
“Upo sahihi , kwasababu tunafahamina huitaji uthibitisho , unaweza kuja hapa muda wowote , au kuja makao makuu ya kampuni yangu au nyumbani , wewe nipigie tu simu”Aliongea huku akiwa na tabasamu.
Na watu nyuma ya Yulia walijikuta wakishindwa kupumua vizuri , ukweli ni kwamba Yulia hakuwahi hata kumjali raisi wa Jamhuri iweje leo aoneshe udhaifu mbele ya Hamza.
Hamza alijua kabisa huyo mwanamke hakuwa na mpango wa kumuacha kirahisi , lakini alijiambia ili mradi havuki mpaka basi atamuacha aendelee kuongea anavyotaka.
Wakati Hamza akiingia katika gari na kuliondoa ndani ya hoteli hio watu wale wote walijipanga mstari kwa ishara ya kumsindikiza,pengine walifanya hivyo kwasababu Yulia alikuwepo pia akisindikiza gari ya Hamza kwa macho.
Hamza mara baada ya kufika barabara ya kuingia Salasala aliingiza gari katika moja ya mgahawa, alifanya hivyo kwani alijua kabisa Prisila alikuwa na njaa na pia muda ulikuwa umeenda.
Prisila alijikuta akifurahi kuona Hamza alikuwa na uwezo wa kuona ishara ndogo ndogo na kuzifanyia kazi , mfano kujua alikuwa na njaa na kumleta mgahawani.
Muda huo ndio sasa Prisila alipata ujasiri wa kumuuliza Hamza kuhusu Yulia , imekuwaje kuwaje amefahamiana nae , maana njia nzima alikuwa kimya.
“Umefahamiana vipi na Yulia ?”
“Tuliwahi kukutana mara moja na nilimsaidia , sio kama nafahamiana nae sana ile tu kwasababu ya msaada wangu ndio maana kanichangamkia”Aliongea.
“Kumbe..”Aliongea Prisila huku akiona kabisa Hamza kuna vitu anaficha , mwanamke huyu kuna muda alikuwa akiwaza imekuwaje Hamza ndio ambae alikubali malipo kwa kuwa boyfriend feki , maana yeye ndio alibandika lile Tangazo.
“Imekuwaje mara baada ya kuona tangazo kule kwenye mtandao ukaamua kutuma ujumbe wa kuwa tayari?”Aliuliza Prisila na kumfanya Hamza kucheka.
“Kama nitakuwa na jibu basi naweza kusema baba yako alichangia kwa kiasi kikubwa”
“Nini, Baba yangu, kivipi?”Aliuliza Prisila kwa mshangao , alikuwa akijua Hamza alikuwa chini ya profesa Singano ambae ni baba yake chuoni.
“Unajua tokea niujue mtandao wa JamiiFroum , nimekuwa nikipenda sana kusoma maoni ya hapa na pale wakati ambao nakuwa sina kazi , sasa siku naona lile Tangazo siku iliofuata baba yako ndio alifundisha kuhusu shauku”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.
“Kwahio ulikuja PM kwasababu ulikuwa na shauku ya kujua kama aliebandika tangazo yupo siriasi?”Aliuliza a Hamza alitingisha kichwa na kumfanya Prisila kutabasamu.
“Mimi sio mtumiaji sana wa mtandao wa JF , ila baba ni mtumiaji mkubwa na ameanza kuutumia muda mrefu tu”
“Unaonekana kabisa , mtandao wako pendwa utakuwa ni Insta na Tiktok?”
“Mimi napendelea Insta na Linkedin , sina akaunti Tiktok ila muda mwingine natumia”Aliongea na kumfanya Hamza kuelewa.
“Ila mpaka Regina kukupa kazi ya kumtafutia mchumba feki , inaonekana anakuamini sana?”Aliuliza Hamza.
“Sio kuniamini tu namwamini pia , Regina sijafahamiana nae kazini , tulicheza wote tukiwa wadogo?, nimeweza kumfanya rafiki licha ya tabia yake yake ya kupenda kuwa peke yake , nakumbuka hakuna ambae aliweza kufanya nae urafiki kati yangu wakati analetwa na babu yake, alikuwa mpole mno na Bibi Mirium ndio alikuja kwetu kuniomba nicheze na Regina kumchangamsha”Aliongea Prisila akiwa katika tabasamu kana kwamba anakumbuka matukio ya utoto.
“Ulifanya kazi kubwa kwelikwel?”Aliongea Hamza na kumfanya Prisila kucheka sana kana kwamba anajua anachomaanisha.
“Ndio maana siwezi kuondoka katika kampuni ya Dosam , kwasababu ni mimi pekee ambae anaweza kunifungukia kuhusu anachojisikia”.
“Namini nikuulize swali , ilikuwaje katika wote waliotuma maombi ukachagua jina langu?”Aliuliza Hamza.
“Niseme tu licha ya watu kutoa lugha chafu katika maoni yao lakini kulikuwa na maombi zaidi ya mia tano?”Aliongea
“Zaidi ya Mia tano!?”Aliuliza Hamza na palepale alijikuta akicheka.
“Ndio , hata mimi nilishangaa na nilikesha sana kupitia”
‘Sasa ilikuwaje ukanichagua mimi?”
“Regina ndio alikuchagua , ukweli ni kwamba aliangalia nani aliandika ujumbe mfupi zaidi na unaoeleweka na ulikuwa ni wa kwako na akaniambia niwasiliane na wewe niweke miadi, alionekana kuwa na uhakika utamfaa, nadhani ilipangwa lakini kila nikifikiria ni uchizi unajua siku Regina alivyoniambia nimtafutie boyfriend feki”Aliongea huku akianza kucheka na kumfanya kupendeza mno, Prisila alionekana kujiachia mno mbele ya Hamza kiasi kwamba alijishangaa.
Mpaka wanakuja kutoka walitumia saa moja kamili na Hamza kwasababu hakuwa na usafiri ilibidi aite Uber mpaka mawasiliano ili achukue gari yake hivyo aliagana na Prisila ambae anaishi Makongo juu.
****
Upande mwingine ndani ya gari aina ya Porche Cayenne, Bahati na Lidya walikuwa ndani .
Ukweli ni kwamba kitendo cha Hamza na Prisila kuondoka ni kama ile vibe ilipotea na kufanya hata bosi Side kukosa mudi ya kuendelea hivyo kila mtu alitawanyika.
Sasa wawili hao walikuwa wakirudi nyumbani na walikumbana na foleni ya magari mengi barabarani kuliko isivyokawaida na kufanya waonyeshe kukosa uvumilivu.
“Hivi nini kinaendelea kuhusu yule Hamza?”Aliuliza Lidya huku akiwa amekunja uso .
“Haijalishi kilichotokea , ilikuwa ni makosa yako kuanza kumdharau tokea mwanzo na kuniweka katika hali tatanishi namna ile , ki ufupi leo tumedhalilika sana”Aliongea Bahati
“Kwa misingi gani unanibebesha lawama zote mimi , usijione mtakatifu sana wakati muda wote ulikuwa ukimkodolea macho Prisila unadhani sijaona , kama umempenda si useme tu?”Aliongea Lidya kwa hasira.
“Unaongea upuuzi gani hebu acha kubadili topiki”Aliongea Bahati
“Sikia bahati usije ukanionyeshea dharau ukidhani nimekosa soko , naweza kuolewa muda wowote , wapo wanaume kibao wanaonitaka , halafu kama sio mimi usingeweza hata kukaa meza moja na Side”Aliongea Lidya huku akionyesha maringo.
Upande wa Bahati aliishia kumdharau kimoyomoyo Lidya na alikuwa akijiuliza kama kuna uwezekano wa wao kuendelea na swala lao la ndoa au ndio mahusiano yao yamefika mwisho , ukweli hakuona uwezekano wa kuweza kuishi na mwanamke kama Lidya, mwanzoni alimtongoza kwasababu aliona kuna ukaribu kati ya Lidya na Side lakini baada ya kilichotokea leo kwa Side kumpotezea alimdharau zaidi Lidya na moyo wake ulizidi kubadilika mara baada ya kumuona Prisila, akili zake zilimwambbia kabisa anahitaji mwanamke kariba ya Prisila, mstaarabu ambae hababaishwi na vitu vya kupita.
Wakati akiendelea kuwaza namna ya kumalizana na Lidya , kioo cha gari kiligongwa kwa nje na kufanya Lidya na Bahati wote kugeuka na kuangalia na walishangaa mara baada ya kuona sura ya polisi
“Ndugu afande kuna tatizo gani?”Aliuliza Bahati.
“Simamisheni gari pembeni , nahitaji kuwahoji”
“Kutuhoji! , kuna kosa lolote ambalo tumefanya?”Aliuliza Bahati kwa mshangao.
“Sio kuhusu nyie , tunafanya uchunguzi juu ya mwanaume anaefahamika kwa jina la Hamza Mzee, nadhani mnaweza kutusaidia kwa kujibu maswali yetu mawili matatu”Aliongea Polisi yule na kumfanya Lidya na Bahati kuangaliana na mwishowe walikubaliana.
Kitu ambacho hawakujua ni kwamba kila mtu ambae alifika katika hoteli ile ukimtoa Prisila alihojiwa na polisi hao , lakini ukweli ni kwamba sio polisi bali ni watu waliovalia mavazi ya kipolisi.
Kitendo cha polisi kuwahoji kiliwafanya waone kabisa kuna kitu ambacho kinaendelea katika maisha ya Hamza na jambo hilo liliwafanya kuwa na waswasi nae.
******
Upande mwingine katika moja ya Bar iliokuwa ikipatikana ndani ya eneo la Masaki alionekana Chriss akibugia bia mfululizo kama hana akili nzuri huku macho y ake yakiwa mekundu.
Pembeni yake alikuwepo Amosi Jasusi mstaafu ambae alikuwa akimwangalia Chriss kwa macho yaliokuwa na mashaka.
“Bwana Chriss nadhani kwa hali hii hatuwezi kuendelea na maongezi yetu”Aliongea Amosi.
“Sikia Jasusi bado sijalewa tunaweza kuongea , niambie uchunguzi wako umefikia wapi?”Aliongea Chriss huku akiongea kwa sauti ya juu kiasi cha kumfanya Amosi kugeuka na kuangalia nyuma kama kuna watu wamesikia kauli yake.
“Nimepoteza muda wangu kuja hapa , ukiwa sawa kiakili tutaongea”Aliongea Amosi huku akisimama kuondoka.
“Sikia Mzee Amosi nishasema sijalewa bado , akili yangu inafanya kazi , au na wewe pia unanidharau , mimi sijalewa kaa chini tuongeee”Aliongea kwa nguvu lakini Amosi alijua kama akiendelea kubakia katika eneo hilo basi siri ya uchunguzi anaofanya itabumbuluka hivyo maamuzi ni kumuacha.
“Prisila nitamfanya mbaya huyo boya uliemtambulisha leo , Mimi ndio Chriss Gabusha, uwezo ninao na nia ninayo , Ma**na zako Prisila unaniumizaje kiasi hichi , ni mwaka wa ngapi huu nimekufuatilia na kutaka uwe wangu….”Chriss aliendelea kuongea kwa hasira kiasi kwamba watu walishaelewsa bwana huyo alikuwa ametoswa , wanawake waliokuwa hapo ndani ambao walikuwa wkaimfahamu Chriss walishangaa na kujiuliza ni mwanamke gani anaweza kumuumiza mwanaume mtanashati na tajiri kama Chriss , lakini licha ya maswali yao huo ndio ukweli kwamba ametoswa , Prisila hakuwa akimpenda na hicho ndio kilichomuumiza maana alikuwa amemfuatilia msichana huo kwa miaka miwili mfululizo bila ya mafanikio.
Sasa habari za Prisila kumtambulisha mpenzi wake katika kusanyiko lao zilimfikia kutoka kwa Saidi huku akienda mbali kumwambia mtu ambae ametambulishwa anaonekana kuwa na ukaribu na Yulia, huku akimbeza kwa kumtania kwamba maneno yake yote yalikuwa ni bure , Side alifanya hivyo kwasababu alikuwa akimpenda pia Prisila na alikuwa na kinyongo na Chriss ambae alimuona kama mwanakauzibe.
Muda huo wakati bwana huyo akiendelea kufakamia kilevi Alex na James waliweza kuingia na kusogea katika meza aliokaa Chriss huku wakimwangalia kwa mshangao na kisha waliangaliana.
“Chriss hebu punguza kunywa bwana , unajiabisha ujue”Aliongea Alex huku akimpokonya Chriss chupa ya Whiskey.
“James , yule boya wako aliekuchukulia mwanamke wako amemchukua na wangu”Aliongea Chriss na kumfanya James kushangaa.
“Chriss unamaanisha nini , ongea vizuri nikuelewe?”
“Nimesema boya wako kamchukua na demu wangu fullsto…p”Aliongea na dakika ileile alijilaza kwenye meza na haikueleweka alikuwa usingizini au pombe zimemzidia na kupoteza fahamu.
“Anamaanisha nini huyu mpuuzi?”Aliuliza James na kumfanya Alex kutingisha mabega.
“Mimi najuaje , hebu tumbebe tumrudishe home”Aliongea Alex na James alikubali na walianza kumkokota Chriss na kumtoa ndani ya Bar hio.
Upande mwingine mara baada ya Amosi kutoka ndani ya Bar ile akiwa ameshindwa kuongea na Chriss aliingia kwenye gari lake kama kawaida , lakini sasa kitendo cha kuvuta pumzi alijikuta akinasa harufu ya marashi ambayo imeongezeka ndani ya gari yake na palepale alihisi hatari lakini hata hivyo alichelewa kwani kabla hata ya kugeuka alijikuta akifunikwa na Helmet zito kichwani na kumfanya kukosa pumzi na kupoteza fahamu.
******
Hamza akiwa njiani kuelekea nyumbani aliweza kupokea simu kutoka Amiri rafiki yake akimuulizia juu ya lile swala la lugha na Hamza ukweli ni kwamba hakuweza kulipatia ufumbuzi kabisa.
Amiri upande wake anasema Mellisa anazidi kubadilika kitu ambacho kinampa mawazo , ijapokuwa hakuongea anabadilika kivipi lakini Hamza alielewa na kuona ngoja alifanyie kazi.
Baada ya kufika nyumbani aliweza kugundua nyumba yote ilikuwa kimya ikiashiria hakukuwa na mtu nyumbani , ilikuwa ni bahati tu Hamza alikuwa na kadi pamoja na nywira za kufungulia mlango hivyo hakupta shida ya kuingia ndani.
Mara baada ya kuingia katika chumba chake tu , jambo la kwanza alilofanya ni kuwasha laptop aliopewa na Regina na kisha alihamisha lile faili la Amiri kutoka kwenye simu yake na kulituma kwa njia ya Email kwenda kwa barua pepe ambayo aliijua yeye.
Baada ya kufanya hivyo alijiunga kifurushi cha kimataifa na kuingiza namba ya nje ya nchi na kupiga simu na hazikuchukuwa dakika nyingi sauti ya mwanamke aliekuwa akitumia lugha ya Kiswedish ilisikika.
“My Prince hatimae umenitafuta baada ya kimya cha muda mrefu”Sauti ilisikika hivyo huku ikionekana upande wa pili alikuwa akijaribu kuzuia hisia zake.
“Niwie radhi sana Sally sio makusudi”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu kana kwamba alifurahia kusikia sauti hio.
“Haina haja ya kuomba radhi najua umechoka na ulihitaji kupumzika”
“Naomba radhi kwa kukuachia matatizo na kufanya uyafanyie kazi , utakuwa umechoka sana kurekebisha makosa yangu”
“Sio kweli , kuniamini kwako na kuniachia familia yako niiangalie ni heshima kubwa kwangu, kwanini nichoke?”
“Huwa navutiwa sana na ukamilifu wako , ni wewe pekee ambae najua unaweza kunisaidia mambo mengi , vipi hali ya ndugu zangu?”Aliuliza Hamza.
“Kila mtu yupo bize na mambo yake , wewe ndio uliwaambia wasikutafute na wamejitahidi kupotezea mawazo ya kukumbuka kwa kujiweka bize , kila mtu yuko sawa..”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka kidogo
“Ungenifuata pengine sasa hivi ungekuwa na maisha magumu sana , angalau kuwa nao karibu kunakufanya upumue”
“Ukiongea hivyo unakosea , maisha yangu yote natamani kuwa karibu yako katika mazingira yoyote yale”Sauti ilisikika na kumfanya Hamza kutoa tabasamu la uchungu.
“Anyway , nimekutafuta kwasababu kuna kitu nataka ujaribu kukifanyia uchunguzi?”
“Nielekeze tafadhari”
“Nimetuma faili la sauti kupitia barua pepe yako , hebu sikiliza lugha iliotumika nataka kujua ni sehemu gani duniani wanazungumza lugha hio , nitafute ukiwa na majibu ya uhakika”Aliongea
“Hakuna shaka nitampa kazi mtu wa lugha kufanyia kazi , naamini mpaka wewe kushindwa kuijua hio lugha basi itakuwa ni ngeni kwenye masikio yako”
“Nadhani umenielewa , Sally nashukuru kwa kila unachofanya kwa ajili yangu..”Aliongea Hamza na hakusbiri jibu upande wa pili na hio ni mara baada ya kusikia sauti za viatu kutoka chini.
Hamza mara baada ya kushusha pumzi na kujituliza alitoka kwenye chumba chake na kushuka chini sebuleni , ilikuwa ni kama alivyohisi Shangazi na Regina walikuwa wamerudi.
Kilichomshangaza Hamza ni kwamba baba yake Regina na mke wake walikuwepo pia na walikuwa wakisukuma kiti cha magurudumu ambacho kimekaliwa na mwanamke mzee.
Bibi huyo licha ya kuonekana kuwa mzee lakini alikuwa na muoekano wa hadhi. Licha ya sura yake kujikunja lakini mpangilio wa uso wake ilionyesha alikuwa ni mwanamke mrembo wakati wa ujana wake.
Hamza hakuwa na haja ya kujua bibi huyo ni nani , alijua fika atakuwa ndio bibi yake Regina, hivyo alimsogelea na kumsalimia.
“Nimefurahi kukutana na wewe bibi , jina langu naitwa Hamza mzee , Mpenzi wa Regina”Alisalimia bila ya kumjali mzee Wilsoni na mke wake.
“Kwahio wewe ndio Hamza , sio mbaya , sio mbaya , unaonekana kuwa mtoto mzuri , ushakula chakula cha usiku?”Aliuliza.
“Ndio bibi , vipi wewe umeshakula?”
“Wote tumekula”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa na alisimama na kumwangalia Regina.
“Vipi hali ya bibi , mbona anaonekana kuchoka sana?”
“Sijachoka kabisa , baada ya kuona ni kweli Regina kapata mchumba nimefurahi mno , sijachoka kabisa”Aliongea.
Upande wa Regina alijikuta akizungusha macho yake mara baada ya kuona namna Hamza alivyokuwa akiongea na bibi yake bila wasiwasi.
“Bibi unapaswa kupumzika mapema , kesho utaendelea kufanyiwa uchunguzi wa afya yako”Aliongea Regina.
Kiasili familia ya walikuwa wakiishi Mkoani Tanga Wilaya ya Bumbuli, ni umbali mrefu kidogo mpaka mpaka kufika Dar es salaam , hivyo kwa mzee kama huyo atakuwa amechoka sana.
“Regina kwanini unataka kunipumzisha mapema ,bibi yako nataka kuongea kidogo na Hamza”Aliongea
“Mtoto masikini kama huyu utaongea nae nini?”Aliongea Lamla.
“Wewe Lamla unaongea nini , baba mkwe wako alikuwa masikini pia wakati akianza kufanya biashara kutoka chini , kwahio unanidharau na mimi kuolewa na mwanaume masikini?”Aliongea na kumfanya Lamla uso kumuiva.
“Mama sijamaanisha hivyo?”
“Miaka mingi imeenda lakini sioni mabadiliko yako , Vipi kwanza Frank anafanya nini siku hizi?”
Alikuwa akiulizia mdogo wake Regina yaani mtoto wa Lamla na Mzee Wilson, na swali lile lilimfanya Lamla sura kuwa mbaya.
“Frank yupo bize siku hizi kufanya Research yake , ndio maana hajaweza kufika ndani ya muda”Aliongea
“Mtu sio kama anasomea nje ya nchi , yaani hapo UDSM tu ameshindwa kuja kumsalimia mtu alietoka Tanga?”Aliongea huku akionyesha kutoridhika kabisa.
“Hapana mama , ni kwamba tu yupo bize ,kila siku anasema atakuja kutembelea lakini imekuwa ngumu kutokana na ratiba za chuoni”
“Hebu acha kumtetea , lini alikuja kunisalimia, inamaana hata kupiga simu kumshinda?, kwanini anashindwa kuwa na tabia ya Regina , licha ya umri mdogo lakini ameweza kuendeleza alipoishia babu yake na kuwa bosi wa kampuni lakini bado anapata muda wa kunitafuta”
“Mama nitamrekebisha Frank , hajui hata anachofanya kama anakosea”Aliongea Mzee Wilsoni.
“Mnaweza kuondoka sasa , nitalala hapa nyumbani kwa Regina”Aliongea
“Mama , hebu fikiria vizuri , tumeshakuandalia chumba chako cha siku zote”Aliongea Mzee Wilsoni kwa uchungu.
“Nimekuja Dar mwenyewe na nitaishi ninapotaka kuishi , rudini nyumbani mkamuadabishe mtoto wenu”Aliongea akiwa siriasi na kwasababu walimjua hakawii kukasirika , Mzee Wilsoni na mke wake walishia kumwangalia Regina kwa dakika na kisha wakaondoka.
“Mariposa hebu nipeleke chumbani kwangu”
“Sawa Madam”Aliongea Shangazi na kumwendesha bibi kuelekea katika chumba chake
Kulikuwa na chumba kikubwa cha Master floor ya kwanza , ni kwa ajili ya wageni lakini kutokana na kwamba ni ngumu kumpandisha juu hivyo chumba hicho kilimfaa bibi yake Regina.
“Dokta Ronicas hajakuambia ni wapi tunapaswa kuonana nae kwa ajili ya kuonana na bibi?”Aliuliza Regina.
“Ni hospitali ya Muhimbili , kaalikwa kutoa hotuba kwa wanafunzi katika chuo cha MUHAS, baada ya hapo ataingia hospitalini”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia kwa maswali.
“Asante kwa hili?”
“Huna haja ya kunishukuru , isitoshe tunakaribia kuzeeka ndani ya ndoa yetu”Aliongea Hamza akijaribu kumtania.
“Unaongea upuuzi gani , nani anakaribia kuzeeka?”Aliongea huku akimkodolea Hamza na kujiambia kadri wanavyozidi kuzoeana ndio ambavyo Hamza anazidi kushindikana.
Muda huo Shangazi aliweza kutoka na kuwaita Hamza na Regina.
“Regina na Hamza mnaitwa , Bibi yenu anataka kuongea na nyie”Aliongea na kufanya Hamza na Regina kushangaa , Regina alijiuliza ni kitu gani ambacho bibi yake anataka kuongea maana ni kama wameongea kila kitu njia nzima.
Baada ya kuingia Bibi Mirium alikuwa ameshalala tayari na alionekana kuchoka.
Kwa kuangalia tu Hamza aliweza kuona bibi huyo yupo katika hatua za mwisho za ugonjwa wake.
Ijapokuwa hakuwa daktari lakini alijua fika kwa hali ambayo amefikia hakuna kitu ambacho Flora anaweza kufanya kumtibia, labda kuwe na teknolojia mpya.
“Bibi kwanini usipumzike kwanza ni kitu gani unataka kuongea?”Aliuliza Regina akikaa pembeni ya kichwa cha bibi yake.
“Sidhani kuna haja ya mimi kupumzika haraka haraka , isitoshe ninakwenda kupumzika kwa muda mrefu siku chache zijazo”
“Bibi usiongeee hivyo , hakuna kitakachokutokea , kesho utakutana na Dokta Ronicas , ni dokta namba moja dunia nzima anaeaminiwa hata kutibia wafalme , nina uhakika ataweza kukuponyesha”Aliongea Reigna lakini Bi Mirium hakuona haja ya kuongea zaidi na alimshika mkono Regina.
“Kama kweli unataka niishi japo kwa siku chache , unapaswa kunipa tumaini…”
“Nipo tayari Bibi , ni kipi nifanye?”
“Nataka muoane haraka iwezekanavyo , nikishaona umebeba ujauzito sitotaka kuondoka kwa haraka mpaka nimuone mjukuu wangu ili nikikutana na babu yako niwe na stori nzuri ya kumwambia”Aliongea

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom