Simba misimu 3 makocha 7 anatafutwa kocha wa 8, mna uhakika kuwa shida yenu ni makocha?

Majok majok

JF-Expert Member
Aug 3, 2023
621
1,577
Hii sio afya kwa mafanikio ya wenzetu mbumbumbu, muda mwingine inabidi kuwapa ushauri tu ambao mnaweza kuchukua ama kuuacha ikiwapendeza kwa maana akuna Yanga Bora bila Simba imara na akuna Simba Bora bila yanga imara!

Aiwezekani makocha ndio wawe mbuzi wa kafara Kila mara pindi mambo yanapokwenda mama Kila msimu, mpaka Sasa ndani ya misimu 3 Simba amefukuza makocha 7 na anatafutwa kocha wa 8 kuja kupokea kijiti Cha BENCHIKHA aliyeamua kusepa baada ya Kuona mapichapicha ambayo ayaeleweki kwenye klabu!

Swali ni kivipi awa makocha wote ndio wanakuwa mbuzi wa kafara?
Ina maana Kila kocha anakuwa ameshindwa kuifundisha Simba? Kila kocha Hana mbinu? Tatizo la msingi pale Simba ni makocha? Hapana nakataa jambo hili kwa nguvu zote, umemleta BENCHIKHA akufikishe nusu fainali ya klabu bingwa vipi vitendea kazi alivyoomba awafikishe pale mnapopataka mlimpa?

Angewafikisha nusu fainali akiwa na wakina jobe? Fred? Onana?
Angewapa ubingwa wa ligi kuu akiwa na aina ya wachezaji wasiokuwa na Kasi Wala akili kubwa ya mpira?

Vipi kuhusu fungu la usajili linatoka kusajili wachezaji ambao makocha hao walihitaji ili kufikia malengo ya makocha husika kimbinu na kiufundi?

Matatizo ayo yote yanaangukia kwa viongozi, ambao ndio wanatakiwa watimize mahitaji ya kocha kwa ufasaha ili ata akiondolewa aondolewe kihalali lakini kwa viongozi wa Simba wote awako smart kusema na ukweli!

Kuanzia kwa Mo ambae ni mwekezaji ni kirusi namba moja pale Simba, Mo amekuwa na Tabia ya kihindi tunayoijua wengi, Tabia Ile waliokuwa wanaitumia wakoloni ya divide and rule! Mo amekuwa mchonganishi kwa viongozi na wanachama wao, kwa vyanzo vyangu vya ndani Mo amekuwa atoi pesa ya kutosha kuendesha klabu na mzigo mkubwa amekuwa akiubeba Try again kupambana kutafuta pesa uku na uko ili klabu isonge mbele!
Lakini kanjibhai amekuwa anakurupuka uko mafichoni na kutweet kuwa anatoa pesa, jambo ambalo limekuwa linampa wakati mgumu try again mbele ya wanachama na mashabiki maana wanahoji Kama pesa inatoka inakuwaje usajili unakuwa ni WA magumashi hivi?

Wanaletwa wachezaji wa Bei ndogo na viwango vya chini kiubora?
Kwa maana iyo uyu bwana Mo anakuwa anatafuta kujikosha kwa wanachama aonekane yeye anafanya kazi yake ya kutoa pesa ipasavyo lakini viongozi ndio wanazitafuna!!! Na try again amekuwa Misri wa kumfichia bossi wake uhuni wake ili asitoe Siri za taasisi matokeo yake anajishushia heshima yake!

Nawaambia wanachama wa Simba tatizo la kwanza la Simba ni Mo! Kabla amjadili na makocha Kila msimu muangalieni kwanza uyo mwekezaji wenu ni kirusi!

Tatizo la pili ni viongozi wenyewe na wanachama wenu, Kuna mpasuko mkubwa uliozaliwa kwenye uchaguzi uliopita, Kuna wanachama awakufurahishwa na uongozi ulioingizwa madarakani kupitia mlango wa nyuma, na kumuweka mangungu pale, mgawanyiko huu auwezi kuwaacha salama ata kidogo.

Tatizo la Tatu ni katiba yenu mliyoipitisha Ina mapungufu mengi sana ambayo yataendelea kuwatafuna sana, inakuwaje mwekezaji mwenye hisa 49% anakuwa na nguvu kuliko wanachama wenye hisa 51%?
Apo ndipo utapoona mangungu analaumiwa bure maana yeye kazi yake ni kufungua na kufunga vikao Hana mamlaka yoyote Wala nguvu, mwenye nguvu ni Try again ambae Yuko upande wa mwekezaji!
Na ilikuwaje katiba yenu ikaruhusu mwekezaji mmoja tu kwenye klabu?

Jambo hili litawatesa sana kwa maana uyu kanjibhai ndio maana anafanya anachojisikia kufanya akiamua kuzira anazira anajua mtamfata kumlamba miguu na kumpigia magoti mgejifunza katiba ya yanga ilivyo imenyooka Kama rula ingewasaidia kuiga kizuri Cha mwenzako sio kosa!

Kwa maana iyo Simba matatizo sio ya makocha wanaofukuzwa Kila uchwao Bali matatizo ya msingi ni ayo wakirekebisha uko watakaa sawa maana Kuna wanachama Wana vinyongo awawezi kukubali Simba ipate mafanikio watafanya Kila njia waiferisha kutokana na mpasuko uliopo na katu timu aiwezi kufanikiwa kwa stahili iyo!
Umoja na mshikamano ndio Siri ya mafanikio kwenye hivi vilabu vya Simba na yanga tofauti na hapo ni ngumu!
 
Hiyo hisa ya 51% ni kwa wanachama wangapi? Kwenye biashara yule mtu mwenye hisa nyingi ndiye mwenye kauli . 51 % ni total hisa divided among say 4 million fans each with different views on how to run the club.
 
Unaposema makocha 7 ndani ya misimu mi3 inabidi uwataje hao makocha na miaka waliyohudumu
 
Kiuhalisia, Simba hawajui tatizo liko wapi, ni kama wanabahatisha. Hela wanazo, hivyo shida sio uchumi. Kila msimu wanaibua nadharia tofauti.

Mara waseme shida ni Matola, jamaa akaenda zake kusoma ila bado tabu ikaendelea kuwepo. Wakamsema ni Mgunda, nae akaondoka, wakamsema ni kocha, nao wameshatimua sana. Sasa hivi wanasema shida ni uongozi. Hapo kwenye uongozi, wengine wanasema ni kina Mangungu, wengine wanasema ni mwekezaji. Ndio maana nasema ni kama wanabahatisha. Ila kuna upande nao unashida sana, ila hakuna anayeuonyooshea vidole, nao ni mashabiki.

Mashabiki wa Simba kuna muda nahisi wengi wao ni kama hawana akili vizuri. Hivi unawezaje kuletewa Manzoki kwenye mkutano, ukashangilia sana wakati sio mchezaji wako na hatokuwa na msaada wowote?
 
IMG-20240428-WA0020.jpg
 
Hivi vitimu masikini kama Simba na Yanga vinabidi vijifunze kitu kutoka kwenye timu kama Leicester city kuchukua ligi kuu na timu ya taifa ya ugiri kuchukua euro. Ili timu hizi masikini angalao kuchukua champions league ni wachezaji na kocha kuelewana Kwa muda mrefu ila kama Kila msimu mnabomoa timu na kufukuza kocha mtasubiri milele. Naona mwanga Kwa utopolo japo nasikia na pacome kumbe na yeye kizungumkuti
 
Hivi vitimu masikini kama Simba na Yanga vinabidi vijifunze kitu kutoka kwenye timu kama Leicester city kuchukua ligi kuu na timu ya taifa ya ugiri kuchukua euro. Ili timu hizi masikini angalao kuchukua champions league ni wachezaji na kocha kuelewana Kwa muda mrefu ila kama Kila msimu mnabomoa timu na kufukuza kocha mtasubiri milele. Naona mwanga Kwa utopolo japo nasikia na pacome kumbe na yeye kizungumkuti
Screenshot_20240428_200450_X.jpg
 
Miaka waliyohudumu hajaweka
1. Zoran 2022 (julai -septemba akatimuliwa)..
2. Pablo Franco ( november 2021 - may 22 akatimuliwa)
3. Didier Gomes (January 2021 - October 21 chali)
4. Robertinho ( January 2023 - November 2023 chali)
5. Benchika ( December 2023 - April 2024 mweleka)
6. Hitimana ....list goes on Bado wale wakushikishwa na kupokonywa Guardiola mnene na matola... Ni noma sana
 
Ingawa mimi ni mwana Yanga, kwa hili ninawalaumu sana Yanga. Kuwakanda watani wao wa jadi mabao matano katika prime time bila huruma kuliwaathiri sana viongozi wa SImba kisaikolojia kiasi kuwa mpaka sasa hawajapona. Sasa kuwaongezea mengine mawili wakati wa marudiano ilikuwa ni kutonesha kidonda. Waliutakiwa watoe sare wakati wa marudiano na wasiweke mabango tena ila sasa Yanga kwa kukera wakazidisha nyundo.


Baada ya kuona pich hii nilijua ni swala la muda tu

1714330550599.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom