Siasa zimezidi The Law School of Tanzania. Hiki chuo kimulikwe!

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
28,179
36,156
Kwa hakika hii nchi ni ngumu sana. Mambo yote hata yasiyopaswa yamegeuzwa kuwa siasa siasa tu.

Hili la law school nalo kwa hakika ni shida.

Examination Results

Hiyo ni "site' yenye matokeo yaliyotoka tangia jumatano 5/10 lakini hayafunguki.

Waliofeli, watatakiwa kwenye supplementary zitakazoanza jumatatu 10/10.

"Watajua vipi wanafunzi waliofeli kuwa wamefeli na kujiandaa tokea kokote waliko Tanzania, kufika kwenye mtihani Dar kwa wakati?"

Hayupo anayejali ila kukusanya pesa za ada tu.

Mass failures ni jambo la kawaida kwenye chuo hiki. Takwimu zinaonyesha si nadra wanafunzi 30 tu kufaulu baina ya wanafunzi 400. Kwa uhalali upi?

Wanafunzi hawa huwa ni wahitimu wa shahada za kwanza, wengine wakiwa na shahada za uzamili na hata za uzamivu. Walimu Law School ni hawa hawa wanaofundisha UDSM na vyuo vingine.

"Iweje wanafunzi hao kufeli law school wanapokuja kusoma kwa mwaka mmoja tu, kwa walimu hao hao?"

Mazingira wezeshi kabisa kwenye zile rushwa zetu pendwa za ngono na mauzo batili ya notes.

"Iweje kitabu 'original' kilichoandikwa na mwalimu husika kuruhisiwa kuingia nacho kwenye mtihani, lakini siyo photocopy ya kitabu hicho hicho?"

Kwa hakika kuna mengi ya kuangaliwa kwenye vyuo hivi vinavyoendeshwa na walimu miungu watu.

Pia soma:
Dokezo - Tuhuma za Siasa chafu "Law School of Tanzania" wahusika wajitokeze kuzijibu

 
Mada yako kuihusianisha na siasa nakubaliana nawe, namfahamu mwalimu mmoja hapo Law School aliwahi kupewa shavu na JPM enzi zile, akawa wakili wa serikali, hivyo tabia za kisiasa kuwepo kwenye utendaji wa hicho chuo sishangai.

Hii elimu ya Law School huwa naona kama imelazimishwa kuwa ngumu kwa manufaa ya wachache, siku hizi imegeuzwa kufaulu mitihani yao kuwa kama kushinda bahati nasibu.

Huo mfano uliotoa wa idadi ya wanafunzi wanaofaulu huku wengi wa wanaofeli wakiwa wametoka vyuo vile vile vinavyofundishwa na walimu walewale, ni jambo la kushangaza zaidi, nieleweke; sio kwamba nalazimisha wafaulishe wengi ili kuturidhisha, lakini kwa trend ilivyo ya ufaulu kila mwaka hairidhishi.

Wale jamaa zangu ni kama wamejigeuza "miungu watu" wanajua wao ndio wameshika funguo zenu kuwa mawakili, hivyo lazima wafanye namna ya kuwapunguza kwa kila njia ilimradi siku ya mwisho viwango vya wafaulu viwe chini.

Lakini hawajui kwa kufanya kwao hivyo, wanaitia jamii mashaka juu ya uwezo wao wa kiufundishaji, kwanini wanafunzi wengi wanafeli kila mwaka zaidi ya wanaofaulu? sasa "Law School" imegeuka kuwa "School of future Failures"?!

Huwa nahisi kama wana mpango maalumu wa kuhakikisha wana "regulate" idadi ya mawakili Tanzania, kwamba isiwe kubwa na kupunguza soko lao, hasa ukizingatia "unyeti" wa fani yao [wakili msomi].

Au kama tatizo ni ufinyu wa muda wa masomo unaosababisha kufeli kwa wingi basi waongeze muda, iwe course ya miaka hata miaka miwili, au mitatu.

Huo mfano wa kuingia kwenye chumba cha mtihani na kitabu OG uliotoa, huku wenye photocopy wakibanwa, nao ni kielelezo cha ujanja ujanja wanaofanya hao walimu, lakini niwape angalizo tu...

Hata hao wanaoingia kwenye chumba cha mtihani na kitabu OG, bado wasijiamini, wajiandae kwa lolote, hapo kinachoangaliwa na muuza kitabu ni biashara yake pekee, ufaulu wako haumuhusu, matokeo ya hilo somo yakitoka mtu akafeli licha ya kuwa na kitabu kwenye chumba cha mtihani msishangae, maisha yenu sio mepesi hivyo.
 
Je kwa Tanzania mitihani ya law school ifutwe au iboreshwe ili tupate fursa ndani na nje ya nchi

2 February 2019
Kampala, Uganda

Legal experts disagree on removing LDC pre-entry exams



Over the years, scores of people have failed the pre-entry exams for the Law Development Centre bar course. Last year, the debate in many circles on whether these exams are a necessity raged on after Parliament passed a resolution to have the examinations suspended. The President of the Uganda Law society Simon Peter Kinobe does not agree with the call to scrap the pre-entry exams.

Source: NTVUganda
 
Hiyo ndiyo dawa wewe andika utanikumbuka

Mkuu kukubali kutishwa na miungu watu siyo suluhu. Haya ya kuhofia kulipiziwa visasi ndiyo yanayoukomaza ubaradhuli.

Woga na hofu nyingi zilizotujaa watanzania ndizo zilizotufikisha hapa tulipo. Kila mtu anaogopa kuchuma janga asije kula na wa kwao.

Nchi imejaa opportunists.
 

THE LAW SCHOOL OF TANZANIA : Taasisi ya Uanasheria kwa Vitendo



Kuandikishwa ktk daftari kama mawakili binafsi walioonesha umahiri kupitia mitihani yao hivyo wanaweza kuwawakilishi wateja katika mahakama za wilaya na mahakama kuu mahakama ya rufaa....
 
VIWANGO VYA KIMATAIFA NA KIKANDA

Lini wanasheria waTanzania wanaweza kuruhusiwa kuwa mawakili wa mahakama kuu za Kenya, nini tatizo mawakili wetu hawawezi kuruhusiwa kuingia 'Bar' Kenya lakini kina LPO Lumumba wao wana leseni ya kutetea mteja ktk mahakama kuu za Tanzania. Tatizo ni nini ? Viwango, lugha au fursa mawakili wetu hawazioni ?

African Academy of Sciences
https://www.aasciences.africa › fellow
Patrick Loch Otieno Lumumba | The AAS - African Academy of Sciences

Prof Patrick Lumumba is an eloquent Kenyan legal practitioner and an Advocate of the High Courts of Kenya and Tanzania.


EALA MPs criticize Kenyan decision barring Ugandan law students from enrolling for Kenyan bar course

Members of the East African Legislative Assembly have spoken out against a decision by Kenya School of Law to block non-Kenyans admission for the bar course in Kenya. On 17th November, the Director of Kenya School of Law issued a directive to that effect but the EALA representatives say this is not in the spirit of East African integration. Francis Jjingo filed this report from Nairobi Kenya where the regional assembly is currently in session.
Source : NTVUganda
 

THE LAW SCHOOL OF TANZANIA : Taasisi ya Uanasheria kwa Vitendo



Bila kujali mwanafunzi kasoma wapi na ana shahada gani, bila kufaulu law school ni kazi bure.

Hali halisi ya mitihani Law School ni kama ilivyo kwenye mada.

Hii nchi ni ngumu sana. Siasa mtindo mmoja.

Kwa hakika kupatikana haki hapa nchini tutasubiria sana.
 
MHITIMU WA DEGREE YA SHERIA AKIJITAYARISHA KUFANYA MAFUNZO YA ZIADA ILI KUKUTOA HUDUMA BORA YA KAZI YA UWAKILI KWA WATEJA

20 May 2021
Nairobi, Kenya

KENYA SCHOOL OF LAW

CynthiaUNTAMED| Ready for Kenya School of Law



Ready for Kenya School of Law: This is the last step towards my admission to the bar as Advocate of the High Court of Kenya. Ready for this and going in with a positive attitude. Get ready with me.
Source : Cynthia Nyongesa


Source : Cynthia Nyongesa


More info :

Kamusi Ya Maneno Na Misemo Ya Kisheria​


 
Kwa hakika hii nchi ni ngumu sana. Mambo yote hata yasiyopaswa yamegeuzwa kuwa siasa siasa tu.

Hili la law school nalo kwa hakika ni shida.

Examination Results

Hiyo ni "site' yenye matokeo yaliyotoka tangia jumatano 5/10 lakini hayafunguki.

Waliofeli, watatakiwa kwenye supplementary zitakazoanza jumatatu 10/10.

"Watajua vipi wanafunzi waliofeli kuwa wamefeli na kujiandaa tokea kokote waliko Tanzania, kufika kwenye mtihani Dar kwa wakati?"

Hayupo anayejali ila kukusanya pesa za ada tu.

Mass failures ni jambo la kawaida kwenye chuo hiki. Takwimu zinaonyesha si nadra wanafunzi 30 tu kufaulu baina ya wanafunzi 400. Kwa uhalali upi?

Wanafunzi hawa huwa ni wahitimu wa shahada za kwanza, wengine wakiwa na shahada za uzamili na hata za uzamivu. Walimu Law School ni hawa hawa wanaofundisha UDSM na vyuo vingine.

"Iweje wanafunzi hao kufeli law school wanapokuja kusoma kwa mwaka mmoja tu, kwa walimu hao hao?"

Mazingira wezeshi kabisa kwenye zile rushwa zetu pendwa za ngono na mauzo batili ya notes.

"Iweje kitabu 'original' kilichoandikwa na mwalimu husika kuruhisiwa kuingia nacho kwenye mtihani, lakini siyo photocopy ya kitabu hicho hicho?"

Kwa hakika kuna mengi ya kuangaliwa kwenye vyuo hivi vinavyoendeshwa na walimu miungu watu.

Kuna kipindi kimoja waliwahi kumdhalilisha Mwalimu mmoja wa chuo kikuu alienda kusoma pale law school. Walimuuliza mwanafunzi swali darasani, yule mwanafunzi akashindwa kujibu, basi wakamuuliza Mwalimu wako aliyekufundisha ni Nani?., akamtaja mwalimu wake kumbe naye ni mwanafunzi happy darasani, basi yule Mwalimu akasimamishwa darasani ajibu swali, akashindwa basi alipigwa madongo humo darasani mpaka akaona aibu.
 
Je mwanachama wa chama cha wanasheria Tanganyika anaweza kufungua kesi ili kutetea wahitimu wa degree ya sheria wasitahiniwe katika shule ya sheria ili kutambulika kama mawakili waliofikia viwango ?

Na ikiwa hawatafanya mitihani ya shule ya sheria, wahitimu hawa kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania tutajua vipi ubora wao wa kuweza kutuwakilisha sisi tusiojua sheria wala misamiati na lugha ya kiswahili / kiingereza ya sheria?


02 February 2022
Dodoma, Tanzania

SIKU YA SHERIA

Tanganyika Law Society TLS ambacho kilikuwa chama huru cha wanataaluma ya sheria kukubali kuhamia Dodoma makao makuu huku kikiwa na jengo lake la Wakili House jijini Dar es Salaam walilolijenga kwa juhudi zao kama wanataaluma ni hatua mojawapo ya kujitumbukiza ktk kibano cha mhimili wa dola.


Source : Wakili TV

TLS kuwa omba omba kiasi sasa serikali leo tarehe 2 February 2022 kutambuliwa na serikali kuwa TLS hii siyo ile iliyokuwa huru chini ya viongozi madhubuti kama kina Tundu Lissu, Fatma Karume, Dr. Rugemeleza Nshala, Rwechungura kwa kuwataja kwa uchache haliopigania TLS kuendelea kuwa huru.

Mwaka 2020 mwezi January serikali ilianza zoezi la kuizonga na kuimaliza pumzi ya TLS kwa kuwasilisha muswada ulipingwa na kambi ya upinzani bungeni na wadau wengine watetezi wa uhuru

Strong reactions greet Tanganyika Law Society new law​

Thursday January 30 2020​

Dodoma. Parliament has passed a law through the government Miscellaneous Amendments Act, which among other things, ‘curtails’ Tanganyika Law Society (TLS) autonomy.

Under the Bill, which was tabled in Parliament on Tuesday evening by Attorney General Prof Adelardus Kilangi, the government will have a mandate to appoint its representatives to the TLS annual general meeting, where important issues about the Bar including the election of the association president, are made.

If the Bill is assented to by President John Magufuli, then Constitution and Legal Affairs minister will also have powers to appoint government representatives in TLS meetings.

The Bill drew strong reactions from Opposition lawmakers, who argued that the Bill was passed in order to restrict TLS and lawyers’ powers.

Some of the MPs, who spoke during the debate, claimed that the Bill was tabled in order to impose the Executive powers on the Judiciary.

Parliament also turned down some of the recommendations from TLS, which included extension of president’s tenure to three years. Currently, TLS president’s tenure expires after a year READ MORE : Strong reactions greet Tanganyika Law Society new law
 
KUKIMBILIA MUHURI WA UWAKILI

Wakili mwandamizi / senior legal counsel Rwechungura : Mbivu na Mbichi za Biashara ya Law Firm kwa Mawakili

Jinsi firm inavyowakuza vijana katika fani ya uwakili, senior counsel Charles Rwechungura anatufungua macho taaluma hii inayoheshimika na kuaminika inavyopikwa ikapikika ... kutambua skills alizonazo na kuzielezea .... kuna kuandika FB attorneys hutoa maandiko ... vijana tengenezeni website ili kuonessha umahiri upate kujulikana ... msuguano wa mawazo .... baadhi ya vijana hawana uvumilivu wa kujituma wanataka mambo ya haraka tofauti na senior counsels walivyokuwa wanajifua kuwa mahiri ....
Source : wakili tv
 
Back
Top Bottom