Siasa za ajira za GPA na hatma ya vyuo vyetu vya Madaktari Tanzania

kibaravumba,
hili ni wazo zuri sana, tena wanafunzi wenyewe wanaofundishwa wapewe uzito zaidi katika vetting hiyo! Interview ihusishe mtu kufanya kazi kwa mwezi mmoja akifundisha somo husika na wanafuzi wawe sehemu ya vetting hiyo itakuwa safi sana!
 
Kuna msemo ulikua una vuma sana vyuoni...."GPA does not matter" au "GPA sio issue, issue ni connection"!

Na misemo hii ilitumiwa sana na wale wasio penda kusoma japo walipenda sana kwenda clabu na kuangalia series!
Kwa kweli elimu ya Tanzania inakatisha tamaa sana. GPA haiwezi saidia mtu kuwa competent & Innovative maana mwanafunzi wanaweza kuwa na GPA kubwa lakini akawa na uwezo mdogo kwa mfano Mwanafunzi aliyepewa mtihani akapa GPA ya juu lakini hana hiyo competence!
 
Nina mdogo wangu ambaye kwa kweli ana sifa zote za kubaki pale Muhas lakini sababu ya ujinga huu yupo mtaani tu!
Olevel aliongoza masomo ya sayansi Tanzania nzima! Alevel pia alikuwa among the best student pale Ilboru! alipofika Muhas kajitahidi masomo yake amepata A na B+ ila kwa sbabu hakufikisha GPA ya 3.8 alipata kama 3.6 amekosa sifa hizo..ila kijana yuko vizuri sana kwenye Anatomy na mambo ya surgery mno.
Kwakweli wajiangalie upya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichoongelea wewe ni "uwezekano" lakini si kweli kwamba wenye GPA kubwa hana uwezo kikazi!
 
Tanzania tuna watu wanaobabaikia mavyeti kuliko ujuzi!

Ubaya ni kwamba, hata wenye vyeti hawaakisi umahiri unaostahili.

Tunababaika sana na makaratasi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kwa sbb hiyo watu wanapapatikia vyeti kwa nguvu zote na kwa gharama yoyote badala ya ujuzi/umahili!
Hapo kuna kutoka kweli. Huu mtazamu finyu huu inabidi tufikie pahala tupige stop! Mtu apimwe kwa uwezo wake na siyo mafyeti tu!
 
Ulichoongelea wewe ni "uwezekano" lakini si kweli kwamba wenye GPA kubwa hana uwezo kikazi!
Kama hiyo GPA imepitia std za viwango linganishi na za yule aliyepata GPA ndogo hapo unaweza kuwa sawa kabisa, lakini kiukweli mazingira na viwango vinavyopelekea watu kutoka vyuo mbalimbali kupata matokeo husika havilingani.

lakini hata hivyo nilichokuwa nasemea ni kuweka vigezo kwa wakufunzi wa vyuo vya madaktari visivyoakisi uhalisia. Shule ya udaktari asikuambie mtu, hizo GPA ni za kusadikika. kinachotakiwa tumpime mtu kwa somo analoomba kufundisha kama yupo vizuri, na endapo kuna jingine pia iwe malupulupu sio msingi wa kumuajiri.

Hii ni ktk kuokoa hali mbaya ilivyo mavyuoni kwa sasa!
 
Ni ubinafs tu mkuu....ndo mana watu wanafake GPA.Nilikataliwa chuo kisa nimepata GPA 3.9 MA badala ya 4.0
Mimi sina tatizo kutumia GPA kma kipimo cha ufaulu ziko fair zaidi ya kutumia marks kwani zina angalia uzito wa somo kitu ambacho marks kwa kawaida haifanyi. Tatizo ninalo liona ni kwenye cut-off points za mtu kukubalika kazini. Degree ya kwanza mainly ni by course work hata wale wanaofanya special project hizi bado zinahesabiwa kama course work hivyo gpa ni kipimo kizuri. Sasa unapokuja Masters nafikiri iitakiwa kuwe na weighting ya Research component lakini uzito mkubwa inapewa GPA, actually mimi ningefuata system ya zamani kuangalia kama mtu amefaulu masters yake inatosha. Nimeshasikia GPA hizo zikipigwa randa ili zifanane na 4.0 vinginevyo mtu anarudishwa. Ukichukulia kuwa kuna masters by research amabazo hazina GPA inayo eleweka unaona shida iliyopo kutumia GPA kumbakiza mwalimu chuo. Naona huko tuendako sitashangaa kudaiwa GPA ya PhD.
 
Tangu lini degree za human medicine na veterinary medicine zikawa classified, ukishahitimu kama daktari ni daktari tu hakuna mambo ya GPA, labda kwenye ungwini ndo wanafukuzana na GPA
Hadi sasa kwa uwelewa wangu hakuna classification ya hizi degree (inayowekwa kwenye lile gamba). Lakini for the purpose of graduate studies GPA ni index nzuri zaidi ya performance than marks peke yake. Problem ni kwenye kuamua criteria za kutumia.
 
Yaani pale home MUHAS unaingia kipanga lakin wazee wanakuburuza unatoka na gpa kilaza japo skills tunazo.
Na kwa kuwa kibongo bongo kinacho matter ni vyeti basi product nyingi za muhas tuanonekana hatukidhi vigezo.
Wazee waache unaa.
Nina mdogo wangu ambaye kwa kweli ana sifa zote za kubaki pale Muhas lakini sababu ya ujinga huu yupo mtaani tu!
Olevel aliongoza masomo ya sayansi Tanzania nzima! Alevel pia alikuwa among the best student pale Ilboru! alipofika Muhas kajitahidi masomo yake amepata A na B+ ila kwa sbabu hakufikisha GPA ya 3.8 alipata kama 3.6 amekosa sifa hizo..ila kijana yuko vizuri sana kwenye Anatomy na mambo ya surgery mno.
Kwakweli wajiangalie upya

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina mdogo wangu ambaye kwa kweli ana sifa zote za kubaki pale Muhas lakini sababu ya ujinga huu yupo mtaani tu!
Olevel aliongoza masomo ya sayansi Tanzania nzima! Alevel pia alikuwa among the best student pale Ilboru! alipofika Muhas kajitahidi masomo yake amepata A na B+ ila kwa sbabu hakufikisha GPA ya 3.8 alipata kama 3.6 amekosa sifa hizo..ila kijana yuko vizuri sana kwenye Anatomy na mambo ya surgery mno.
Kwakweli wajiangalie upya

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nasema, kama huyo mdogo wako kwa mfano, ana 'A' au 'B' ya Anatomy na amependa kuwa mkufunzi ktk somo hilo, basi atathminiwe kwa uwezo wake ktk somo husika badala ya kutafuta mara biostatistic/biochemistry alipataje! Maana ili upate cheti cha kumaliza udaktari lazima masomo yote upate sio chini ya C!
 
Hadi sasa kwa uwelewa wangu hakuna classification ya hizi degree (inayowekwa kwenye lile gamba). Lakini for the purpose of graduate studies GPA ni index nzuri zaidi ya performance than marks peke yake. Problem ni kwenye kuamua criteria za kutumia.
GPA inayo mazuri yake hata mimi sikatai, lakini kwa hili la kupata wakufunzi wa madaktari GPA imetuhujumu sana saana! Ndio maana nilisema na kumuunga mkono mkuu hapo juu alipochangia juu ya vetting kwa somo husika. Mtu anayekwenda somea Bachalor of art (major Kiswahili) kwa mfano, huyu wa kiswahili, akija na GPA ya 4 wala siwezi shangaa, maana mzigo wake hauwezi lingana na MD. Na akija amepanga A zake hapo na MD na makalayi yake bado naamini huyu wa MD mziki wake ni mzito zaidi.
 
Yaani pale home MUHAS unaingia kipanga lakin wazee wanakuburuza unatoka na gpa kilaza japo skills tunazo.
Na kwa kuwa kibongo bongo kinacho matter ni vyeti basi product nyingi za muhas tuanonekana hatukidhi vigezo.
Wazee waache unaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie nafikiri, kigezo cha GPA kwenye medical school kiangaliwenkwa upya!
 
kibaravumba, umeongea ukweli na pendekezo lako lina mashiko.
1 .vetting itumike.
2 wenye GPA ndogo au grade score ndogo kwenye somo husika lakini wamepublish(peer review journal) kwenye topic zinazohusiana na somo husika pia wawe considered for admission for Master na Ph.D
 
Mimi sina tatizo kutumia GPA kma kipimo cha ufaulu ziko fair zaidi ya kutumia marks kwani zina angalia uzito wa somo kitu ambacho marks kwa kawaida haifanyi. Tatizo ninalo liona ni kwenye cut-off points za mtu kukubalika kazini. Degree ya kwanza mainly ni by course work hata wale wanaofanya special project hizi bado zinahesabiwa kama course work hivyo gpa ni kipimo kizuri. Sasa unapokuja Masters nafikiri iitakiwa kuwe na weighting ya Research component lakini uzito mkubwa inapewa GPA, actually mimi ningefuata system ya zamani kuangalia kama mtu amefaulu masters yake inatosha. Nimeshasikia GPA hizo zikipigwa randa ili zifanane na 4.0 vinginevyo mtu anarudishwa. Ukichukulia kuwa kuna masters by research amabazo hazina GPA inayo eleweka unaona shida iliyopo kutumia GPA kumbakiza mwalimu chuo. Naona huko tuendako sitashangaa kudaiwa GPA ya PhD.
unajua ndio maana waafrica bado tupo nyuma sana, na tunaweza baki nyuma kwa miaka mingi ijayo tusipojitathmini na kuchua hatua. Huko majuu, wenzetu walioendelea mwanafunzi hahangaiki kulundikiwa mzigo wa masomo. Anaweza yeye kujichukulia vijisoma vyake vichache tu anakwendanavyo na kupata Ba, honor, MSc na PhD zinazong'wara. lakini sisi huku tunamlundikia mwanafunzi masomo lukuki tukimtaka afaulu yote, na mwishowe tunaweka cut-off GPA ya masomo yote hayo. Hii haiko sana. Ndio maana wabobezi wa kuingia 'deep' ktk fani zetu huku ni nadra sana. Unamkuta mtu anajua mambo mengi juu juu tu! Ndio maana tunakuwa wasindikizaji wa fumbuzi zinazotokea duniani!
 
Unawezakua na hoja nzuri sana

Na pia pamoja na class struggle,mnyukano wa madaraja ya kimaisha nyie wachanga msije kuchukua nafasi zao,nk

Tunarudi kwenye uchumi wa nchi,ni mdogo mno nafasi ni chache

Hivyo concept iliyopo ni cut off iwe kali zaidi

Nchi ingekua mtambuka na nafasi za ajira zipo kwa wingi na uwekezaji kwenye sekta ni kubwa vya kutosha watu wote then viwango vya GPA lazima vishuke,hii ni normal law of economics!

Pamoja na yote hayo hawa jamaa huenda wakawa sawa maana wanaangalia international standards na sio below!

Wakisema GPA ni 3.8 ni kweli 3.8 na kuna sababu kabisa!

Umeniua nguvu eti unapofananisha GPA za Political Science ni rahisi na zenu ni ngumu hivyo msamehewe zichukuliwe hivyo hivyo ndogo

Hoja hiyo ni mufilisi kabisa kwasababu huwezi fananisha Udaktari na Political Science ndio maana ni machungwa na maembe japo ni binadamu walewale wanazisoma,ila tofauti n amount of energy kupata hizo cut offs...Udaktari una demand 3.8 and not below kwasababu lukuki

Umeng’ang’ania eti mna practical skills sana GPA sio issue sana,unaongea as if ni practicals tu zinatakiwa,inatakiwa analytical skills ambayo inataka higher brain power na sio practicals tu

Na tukija kwenye masomo ya practicals umefaulu basi viwango vile husika basi?

Jibu ni hapa hivyo unakimbilia huruma ya GPA huku ukifananisha na PA ambazo ni mbingu na ardhi

Cha msingi mtu achague PA kabisa medical school aache

Hii maneno eti mi najua sana kazi sijui sana mambo ya mitihani,how do we believe you wakati hata vyeti vyako havitoi hiyo suggestion?

Tunakupimaje sasa?Tukupe mtu umkate utumbo u-prove your point kua wewe ni mkali wa kazi na sio mitihani?

Hatutaki robots,tunataka mtu analytical anaejua kunyambua matatizo ya utatibu na kutoa proper decisions analytically then hiyo ma operations na mambo ingine watakuja kufanya maroboti

Mtu daktari hata hujui kuandika email au ku-analyze issues na kutoa real michanganuo kitaaluma na kutoa majawabu kwa kutumia ubongo kwa kisingizio eti nilikua sipendi mitihani nataka practicals tu which is of course nonsense!

Mi nafikiri tuwaache waliopata 3.8-5.0 wachukuliwe wafanye wanachoajiriwa

Wa 2.0-3.7 wafanye practicals wanazopenda huku hawana anylticak brain to reason anything wafanye yao,basi!

Hizi hoja za kushusha GPA sidhani kama zina mshiko yoyote!

Hazina in a nutshell!

Tuelewe kua GPA kubwa ina suggest huyu mtu ana reasoning capacity kubwa na ana uwezo wa ku analyze information nyingi kwa usahihi kwa muda mfupi,practical kama yupo chini sio tatizo sana!

Practicals by the way in 10 years from now ni robots tu zitafanya,ila brain power bado ni more valuable mzee,tusidanganyane!
 
Back
Top Bottom