Sanjari na alivyokuwa akisisitza Nyerere (RIP):
"Tunataka kuona katika Taifa hili, vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga, akina "ndiyo bwana mkubwa", vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa"
8 Apr 2024 kuelekea kumbukizi ya kifo cha hayati Sokoine miaka 40, SUA Morogoro; bila kutarajiwa, Prof Shivji aliuvunja ukimya kuhusu ombwe la vijana hawa jeuri nchini, chanzo cha matatizo:
1. Yalisemwa mengi mema kabisa ya kumtofautisha hayati Sokoine kuelekea kumbukizi hiyo huko Morogoro:
2. Katika wazungumzaji wakuu, Joseph Warioba, Anna Makinda, Prof. Shivji, Prof. Mkenda, Dk. Biteko kuwataja wachache; walikuwa na mawasilisho bora kabisa yenye kuakisi uthubutu na ya kujifunza; yenye kumtofautisha waziri mkuu huyu, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 44; na wengi wengine.
3. Ikumbukwe Sokoine aliteuliwa kuwa wazIri mkuu kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 39.
4. Akichaguliwa kuwa mbunge akiwa na umri wa miaka 27, akateuliwa kuwa naibu waziri akiwa na miaka 29 na waziri kamili (ulinzi) akiwa na miaka 34!
5. Kwa hakika Sokoine hakuwa aina za vijana wale wa "hovyo" wa zama za kwetu.
6. Ombwe la vijana jeuri liliongelewa na wachokoza mada watatu; likianzishwa na kuchomekewa kwa ufupi, uchungu na uangalifu; na profesa nguli, Issa Shivji:
a) Shivji: ndani ya wasilisho lake alisema alijisikia ilikuwa ni muhimu sana kulisemea. Kwamba, hata hivyo angependa aepuke sana kumnyooshea mtu kidole.
kwamba:
(i) hili lilikuwa ni matokeo mabaya kabisa ya matumizi ya nguvu kubwa iliyopitiliza ya kuuuwa uhuru wa kujieleza na hasa kuuwa hamasa ya midahalo, kwenye taasisi za elimu na zaidi sana kwenye elimu ya juu.
(ii) Kukapotezwa dhana ya nguvu ya hoja na kuwa ni muhimu sana hoja kushindanishwa kupata iliyo bora.
(iii) Ubora wa hoja ukabinafshwa kuwa kwa matabaka. Ikawa wenye hoja bora ni wale au yule tu; bila kujali kasema nini; au wengine nao wanasema je.
(iv)Haya yakitokea, zaidi sana yakipewa msukumo mkubwa na serikali za ndani ya miongo 2 iliyopita. Ya kwamba tulipo tunavuna tuliyopanda.
(v) Akamaliza Shivji bila shaka akitupa jiwe gizani.
b) Prof. Mkenda: akisimama ikiwamo kumkaribisha mgeni rasmi alianza na kuligusia suala "chungu kumeza hili."
Akaanza:
(i) "Akilizungumzia tatizo la kuhusu midahalo mashuleni, nilimwona mwalimu wangu Prof. Shivji akiwa ananikazia macho mimi tu, humu ndani!" Kauli iliyoibua kicheko kikubwa kwa kila mtu ukumbuni, hadi kwa kina sisi tuliokuwa kwenye runinga: TBC, huko!
(ii) Akiendelea Mkenda akasema, "hata hivyo nimhakikishie mwalimu wangu kuwa, sisi kama serikali pia tumeliona na mimi kama waziri mwenye dhamana tumeshaanza kulifanyia kazi na tunakwenda kulifanyia kazi kwa ari zaidi!"
c) Dk. Biteko: kabla ya utangulizi wake rasmi, naye akaanza:
(i) Prof. Mkenda amesema wakati Prof. Shivji akilisemea hili, alikuwa akimwona akimkazia macho yeye tu. 'Kwa hakika nami niseme ukweli wangu, kwa maana msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.
(ii) Akaendelea Mh. Biteko:
"Mimi mbona ndiyo nilikuwa nimeona mkaziwa macho zaidi nilikuwa mimi...."!
Kauli iliyoibua kicheko kikubwa zaidi ya kile cha mwanzo!
6. Kwa hakika wenye akili zao tukawa tumewaelewa vyema hawa ndugu; na hasa ikizingatiwa:
"The guilty are always afraid "
7. Wale tulio soma Cuba tukawa tumawalewa vyema zaidi. Kwamba itakuwa kule kuibuka Kwa zile ajira zetu za laana, almaarufu kwa jina: machawa wa vyama na watu!
NB: Kwa hakika Mkenda ni Profesa. Kumbe hata kutokea jalalani na wengine wengi wapo!
"Excellent sense of humor."
Angalia Part 1 hapa:
Shivji: Chimbuko la wasiokuwa na Hoja au uthubutu wa Kuhoji, linalo ligharimu Taifa (Part 1)