🚨Shikamoo Mpemba

Samatime Magari

Senior Member
Feb 10, 2017
106
405
1667808327137.png
1667808341276.png

.
Ilikua December Mwaka jana 2021 Ijumaa Usiku Boni alinitext WhatsApp, Akanambia anatafuta Toyota Harrier ya mkononi Tako la nyani yenye hali nzuri. Akasema budget yake ni Million 18 Net hapandi wala hashuki, akipata white au silver itakua safi..
.
Akasema yuko Dodoma ila ikipatikana hata sasa hivi anakuja kuchukua machine, Basi baada ya kusoma hii text na kuona how serious he is nikamvutia wire tuongee kwa undani zaidi, tukaongea akanambia ana prefer hizo rangi sababu ya vumbi na jua kali la Dodoma..
.
1667808549391.png
1667808560982.png
1667808630444.png

.
Na ikipatikana ndani [interior] ikiwa cream au gold itakua safi, Baada ya kumaliza kuongea nae na mimi nikamvutia uzi Jamaa angu Manase tunae fanya nae hizi kazi nikampa hitaji la mteja, Manase akanambia gari ipo anayo Mudi pale Magomeni mapipa lango la jiji imenyooka..
.
NIkaomba picha zikaja kuona gari ina sifa zile zile anazotaka Boni mixer ndani ni cream na rangi sio Black wala white hafu body safi, Nilivyoona picha tu nikamwambia Manase weka conference call kwanza tuongee na Mudi atupe taarifa zaidi za hii gari, Ikawekwa conference call..
.
Mudi kuulizwa taarifa za gari akasema hii gari ni ya mpemba ana wake wawili, Mdogo Magomeni mkubwa Kijitonyama na ana duka Kariakoo. Route za gari ni Kariakoo, Kijitonyama na Magomeni basi gari iko vizuri sana Iko sawa na haina tatizo lolote kama mnavyoina kwa picha..
.
1667808796296.png
1667808823372.png

.
Kwenye Bei akasema na mpemba anataka million 19 anatoa laki 5 na gari iko Magomeni maana week hii ni zamu ya mke mdogo kama vipi kesho njooni mkague, Binafsi kusikia hivi nikauliza una hakika Mudi gari iko poa, akasema acha maneno kesho Asubuhi njoo ukague gari Mzee..
.
Nikamwambia kuna ndugu yangu anaitaka ila ana 18M vipi inafaa, Mudi akasema njooni mkague gari hatuwezi shindwana, Mi kusikia hivi nikajua hii gari 18M inatoka na inatoa maji, Basi bila hiyana na roho nyeupe nikamrudia Boni nikamtumia picha na details za gari..
.
Nilipoona picha zime bleutikiwa nikavuta wire nikamwambia gari ndo hiyo, Nimeambiwa machine iko poa ni kutekenya tu safari imo hakuna cha kurekebisha. Boni kusikia hivi akanambia basi by J pili asubuhi nitakua hapo kuna gari yetu inaleta matikiti Dar usiku huu nakuja nayo..
.
1667809264114.png
1667809286869.png

.
Na akasema Jumatatu anatakiwa awe shambani dodoma so muda alionao ni Jumapili tu, Baada ya kusikia hivi ndo nikajua kumbe Boni ni mmoja wa wakulima wa matikiti hapa nchini na Jumatatu mapema sana alikua anahitajika shambani sababu Bibi Shamba ana ziara shambani..
.
Nikamwambia sawa we njoo Mungu ni mwema kila kitu kitaenda sawa, Simu ikakatwa then nikarudi kwa Mudi nikamwambia Mteja anakuja kesho asubuhi so weka vitu sawa. Mudi akasema gari iko magomeni mda wote ni wewe tu Mi nikalala asubuhi Jumapili hiyo by saa 1 niko Magomeni..
.
Kufika pale nikampigia simu Mudi nikaelekezwa gari ilipo, Kufika kwenye gari nikakuta inaoshwa basi nikaikague pale kwa nje na ndani nikaona machine iko safi kabisa upande wa body na interior, Jamaa anayeosha kumuuliza mwenye gari yuko wapi akanambia mpemba bado amelala..
.
Na huwa anaamka saa 4-6 siku za weekend akiwa kwa mke mdogo. Mzee nikasogea pembeni nikampigia Simu Boni kujua amefikia wapi, Akanambia alishafika Dar sema alipita kusalimia sehemu anakuja.. . Binafsi nikamwambia nimeshafika nimekagua gari body na interior ziko sawa..
.
1667810203754.png
1667810261459.png

.
Sema sijaiendesha njoo upige gear mwenyewe ujionee, akasema poa, Ile namsubiri Boni, Mudi yule dalali wa Mpemba nae akaja, Akaipamba pamba gari pale na kuzidi kunihakikishia machine iko safi. Akasema kama budget ni 18M atafanya namna mpemba atoe 500K ya wapambanaji..
.
Kama baada ya nusu saa hivi Boni akafika naye akakagua body na ndani machine, akasema ngoja aendeshe kidogo, Mudi akasema ngoja mpemba aje kabisa tukitoka hapa ni moja kwa moja. Basi tumekaa kidogo Mpemba akaja tukasalimiana na kutambulishana then tukaingia ndani ya gari..
.
Boni na Mimi tuko mbele, Mpemba na dalali wake Mudi wako nyuma, Boni akawasha gari akaanza kuendesha [test drive] na akaanzia na rough road kusikiliza miguuu, Gari ikapitishwa rough road iko vizuri, ubaridi upo unapiga safi kabisa tukaingia kwenye barabara ya lami.
.
1667810766148.png
1667810793167.png

.
Mpemba akasema twende kama tunaelekea Mliman city, Akasema hii gari haina shida so itest njia ya kwenda Bank Mlimani hapo. Basi Boni akapiga gear mbele kidogo akasikia kama kuna kitu kinapiga kelele Mpemba akamwambia ni chini ya steering kuna kitu kimeisha gharama ni Ni 45,000 na atampunguzia kwenye bei,..
.
Basi tukafika mlimani city, Tukapark gari then tukaenda bank ili Boni afanye malipo ageuke na gari yake Dom, Boni kufika Bank akakuta bonge la foleni sema akatumia ID yake kukwepa foleni ili kuokoa muda awahi kurudi zake shambani..
.
Wakati tuko maeneo ya nje pale Bank picha linaanza simu Yangu ikaanguka kwenye tiles kioo kikafa, nikavuta kinokia cha torch chap Na Mudi alisema Mpemba atatoa 500K nikaona hii pesa nitengenezee simu tu nirudi Whatsapuni, Basi Boni akamaliza kufanya muamala akakabiziwa chuma..
.

1667811129205.png
1667811144068.png
1667811310623.png

.
Wakati tunaondoka Mpemba na Mudi wakasema si tutangulie tu wao wanaendelea na mambo yao, Sasa Boni alisema anapita pale lumumba kwa jamaa ake kupimp gari kidogo. Basi nikasema kama vipi twende na Mimi uniache pale Mitaa ya Aggrey Kariakoo nitengeneze simu, tukaanza safari..
.
Ile tumetoka Mliman tuko njiani tumepitia Mabibo gari ikazingua AC na hapo ishakua mchana joto limekubali tukahisi labda setting bofya bofya pale wapi tukaona isiwe kesi tukashusha vioo tule upepo wa Mungu. Boni akasema ngoja afike Lumumba then aangalie shida nini..
.
Akaniacha pale Aggrey kwa mafundi simu yeye akaenda Lumumba, Mi nimebaki pale aggrey namsikilizia fundi simu amalize anipe simu mara simu ikaita kuangalia hivi ni Boni nikasema nini tena mbona mapema Kupokea tu Boni akanaambia hebu njoo hapa Lumumba one time maana sina hata nguvu za kuongea..
.
Nikawaza jamaa wamemuibia gari au ? Basi nikachukua punda chap niko Lumumba kufika pale gari ninayoiona na ile tuliyokagua iko tofauti.. . Kwanza picha linaanza gari imeungwa chassis yani chassis imechomelewa kabisa na ukifungua bonnet unaiona..
.
1667811482978.png
1667811493713.png

.
Yani ilishakula mzinga mkubwa then wakakata wakaunga kipande kingine, Kuangalia taa za mbele zimelegea hazina hata lock, ile label ya harrier nayo imeegeshwa, ukifungua milango inapiga kelele kama imepinda hivi Gari engine ina leakages na ina matatizo ya umeme kuna saa Unawasha indicator inapiga horn na matatizo madogo madogo ya hapa na pale. .
.
Mwenyewe kuona hivi nikachoka aliyetoa Pesa ndo akawa amechoka kabisa, Jamaa ake Boni wa pale Lumumba akamtia moyo kidogo Boni akapata nguvu. Marekebisho yakafanyika pale + service ili Boni arudi Zake Dom shambani, muda wote huu mpemba hajapigiwa simu Boni akaona alibebe kama lilivyo.. .
.
1667811644930.png
1667811662526.png

.
Basi by jioni gari ikawa sawa mi nikarudi zangu Kigamboni home. Boni akaanza safari ya kurudi Dodoma jioni ile na mimi nimefika home nikamsimulia mama chanja yaliyotukuta.. Mama Chanja akaishia kunicheka tu na kuniambia najifanyaga najua magari leo nimekutana na wanayoyajua zaidi. .
.
Sasa niko home usiku mida ya saa 7 usk hivi Boni akanipigia simu akanaambia gari inachemsha yuko kijiji flani anatafuta msaad, Mi nikamshaauri afanye anachoweza Afike Dom then kesho tutawasiliana tujue cha kufanya, akasema sawa haina mbaya. .
.
1667811814224.png
1667811830454.png

.
Kesho asubuhi nikawaweka conference call kuhusu hili, hapo ni Mimi, Manase, Mudi + Mpemba. . Nikawaeleza mapicha picha ambayo gari imeleta, Mpemba nae eti akawa anashangaa anasema si mlikagua lakini..
.
Nikamwambia ndio tulikagua lakini pale kulikua na nguvu za ziada sio bure na nikawaambia Mlima matikitiki amesema anapandisha gari kwanye zile gari zao kubwa anairudisha dar. Hili la kurudisha Jamaa alisema kweli anairudisha Mpemba kusikia hivi + Jamaa ni mkulima wa Matikiti tena kwenye shambani kwa number 1 akaingia ubaridi..
.
Mpemba akauliza kwani gharama za kuirekebisha zikoje, Basi nikamrudia Boni nikamwambie atupe brake down ya matengeneze Boni akashare pale vitu vinavyohitajika na ufundi tukakuta gari inahitaji compressor na radiator mpya..
.
1667811950125.png
1667811964635.png

.
Pia inahitaji body work kidogo na vitu vingine, tukashare gharama na mpemba akakubali kulipa, Wapambanaji nao margin yao ikaguswa kufukia mashimo. Sema baadaye tulikaa na kutafakari yaliyotokea pale tukasema kuna kitu kiliendelea pale sio Bure..
.
Any way siku nyingine mkiwa mnataka kufanya manunuzi makubwa mtangulizeni Mungu, Kuna time unaweza nunua kitu na usijue hata kwanini umenunua ila ndo unajikuta umeshanunua. Sema chombo ilirudi sawa na Boni nae baadaye akaisukuma kwa mtu mwingine akapambane nayo..
.
1667812098563.png
1667812118126.png
1667812411647.png
1667812435064.png

.
Kama unahitaji kuagiza gari Japan , UK, Singapore, Thailand, etc karibu.. . Tuko na network ya trusted dealers nje, dealers wanaotupa gari zenye ubora wa juu kwa bei safi, Tutafanya mchakato wako wa kupata gari kuwa rahisi salama na unaojali muda wako..
.
Simply tupigie au njoo WhatsApp [0714547598] au ofisini Posta Mpya Phoenix House mkabala na Mkapa tower tutaku assist + kukushauri, Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu, utatupa hitaji lako tutakupa then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice..
.
Utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo, Natumaini umejifunza kitu kama jibu ni ndio basi usisahau kushare kwa ajili ya wengine..
.
Asante
Samatime
0714547598
 

Attachments

  • 1667812130611.png
    1667812130611.png
    30.7 KB · Views: 36
Mpemba aliimwagia maji ya ubani mashtaka gari kabla ya kuiweka sokoni. yaani ukiiona inaita ukishainunua tu halahaulaa.
 
Kwani gari huwa inakaguliwaje mpaka mtu anunue??
Yani ni masaa kadhaa tu mwamba karidhika na kutoa M18 kiroho safi kabisa.
 
Sasa mkuu biashara yako ni kuuza magari na inaonesha kuna mtu ulimuingiza mkenge kwa utetezi kwamba Mpemba alifanya mambo meusi, ingawaje kuna kasoro kibao zinaonekana wewe ulifanya (maana gari haikukaguliwa kiufundi, TRA n.k), uliamini mali kauli pekee...

Mwisho wa thread unatangaza biashara yako ya uagizaji magari, je huoni kama habari ya mwanzo inatia doa kazi yako ya msingi?
 
Huu mtiririko wa story hii mara nyingi hutokea Sana kuna madalali wanafanya biashara Kwa kutumia kiini macho hata huku mitaa ya chamazi kuna watu wanaitwa "Jenga uza" hawa jamaa wanauza nyumba na viwanja Kwa kutumia style hii..
ogopa Sana madalali wa Lumumba sio watu kabisaa sikuzote ukitaka kununua gari mikononi nenda na mafundi wako wakague kila kona
 
Back
Top Bottom