Serikali ifanye udhibiti wa uuzaji wa spare za magari ya Serikali na Mafuta; Tunaomiliki garage tunaumia sana mfanyacho

Madereva nao wamejiongeza. Kama mabosi wao wanakula kwa urefu wa kamba zao, nao pia wanajinafasi katika sehemu zao za kazi.

Kama tatizo ni kubwa kiasi hicho, basi kuna haja ya magari ya serikali kuwekewa vifaa maalumu ili nyendo zake ziweze kufuatiliwa kwa urahisi. Ufuatiliaji kupitia "motor vehicle tracking devices" ni wa kawaida sana ambapo serikali haishindwi kuugharamia na kuutumia.
 
Serikali inapaswa kununua magari ya Ambulance, polisi, Rais, PM, Spika, IGP, CDF na Mkuu wa UT tu, wakurugenzi wa mashirika, mawaziri, Wakuu wa mikoa na watumishi wengine wote wakopeshwe magari na/au wapewe bajeti ya mafuta.
 
Hii nchi ni ngumu sana kuongoza. Yaani unashindwa kuelewa hizitaasisi zote za usalama wa taifa zinafanya nini?. Huo wizi ulianza siku nyingi tu. Nilimaliza Chuo kikuu na kuanza kufanya kazi kwenye Wizara ya Ujenzi katika mwaka wa 88. Kuna kijana tuliokuwa tunasoma wote akaishia form four Div 4, alikwenda kusomea store keeper mwaka mmoja na akaajiriwa depot ya mafuta ya Serikali Kurasisni. Sikuamini maisha niliyomkuta nayo maana yalikuwa ya kifahari sana. Alikuwa amenunua mpaka bus ya kwenda kijijini kwao. Kuna mambo ambayo yapo kwenye hii Serikali ya CCM yanaumiza sana watu. Anyway kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake lakini yanaumiza wengi na ni wachache wanaofaidi kwa kutumia kodi zetu.
 
Mabosi kwa kutumia sheria mbovu wanafuja fedha za kodi za wananchi kununua magari badala ya kuchimba visima vya maji n.k

Toka maktaba :
Mkurugenzi ajitetea manunuzi ya gari


Hili ndilo gari aina ya V8 lenye thamani ya shs. Mil. 400 alilonunuliwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita ambapo Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amedai kuwa ununuzi wa gari hilo ni ufujaji wa fedha za umma.


Mkurugenzi huyo wa Halmashauri hiyo, Mhandisi Modest Apolinary amejibu tuhuma hizo na kusema kuwa gari hilo lilinunuliwa kwa kufuata utaratibu na waliomba kibali kutoka kwenye ofisi ya Waziri Mkuu na walipewa kibali hicho.

1700732560359.png
 
Naomba kutoa Rai kwa Serikali kujiwekea utaratibu mzuri wa kuwadhibiti madereva. Hali ya sasa siyo nzuri sana mtaani na kwenye vijiwe. Yawezekana kweli uchumi siyo mzuri na maslahi ya madereva siyo mazuri kivile kutokana na elimu zao. Lakini pamoja na umaskini walionao haileti maana kufungua spear za magari mapya na kuziuza kisha kufunga spear zilizokufa. Haileti maana kufungua matairi mazuri yenye TBS na kufunga tairi zilizopitwa na wakati . Ni hatari sana kwao, kwa wanaowabeba na hata familia zao.

Lakini haya yote yanatokana na ukweli kwamba hakuna usimamizi wala anayefuatilia ufanisi wa vyombo vya usafiri vya Serikali. Nikifuatilia sana aliyepewa dhamana ya kuwasimamia madereva ana masters na wakati mwingine hata Phd. Analipwa fedha nyingi lakini pia kwa ubosi wake siyo mtu wa kwenda garage kufuatilia. Baadhi hata vifaa vyamagari hawavifahamu hivyo kujua kibovu na kizima kwao kizungumkuti. Baadhi wamepewa dhamana hiyo kama adhabu huku baadhi wakiwa na mgongano wa maslahi kwa kushirikiana na madereva kuhujumu Serikali kwenye matengenezo na mafuta.

Hali hii ya wizi wa mafuta na vipuri imekuwepo muda mrefu ila kwa sasa imezidi. Dereva anakuja na gari garage anawapa vijana wafungue vifaa na kufunga vibovu hadharani bila hata kificho. Naandika kwa uchungu kwani magari mengi haya yananunuliwa kwa kodi zetu huku machache tukipewa msaada.

Kwa upande mwingine wapo madereva wanafungua vifaa hasa tyre za gari za umma na kufunga kwenye magari yao. Unajiuliza huyu Dereva akipata ajali na tyre mbovu nani atakayekuwa? Udhibiti wa kodi zetu upo wapi?

Nadhani Serikali inaweza ikawa imelifumbia macho ila sisi tuliopo mtaani kwenye vijiwe na wamiliki wa garage tunaona. Hata kesho serikali ikitoa namba za whatsapp special watu watume picha za uhalifu huu watu watatuma. Siyo Busara magari ya kodi zetu yakafa kwa sababu ya watu wachache wanaonenepesha familia zao.

Leo tembelea ofisi za Serikali uone magari yaliyopaki, ni mapya kabisa ila wameyakwapua vifaa vya ndani na kuuza kisha wameyaweka juu ya mawe. Kila ofisi ukienda magari ya Serikali mapya yamepaki lakini huku mtaani hakuna bosi yeyote ambaye amepaki gari means watumishi wa umma wana pesa za kutunza magari kuliko Serikali? Hapana, wanayaua makusudi kwa kuuza spear na kunenepesha miili yao.

Last time tuliona Mtanda akiwa huko Kaskazini anaenda ofisi ya mkurugenzi magari yamepaki kwa kifaa cha milioni moja; yakikaa baada ya muda wanaanza kuiba kifaa na kwenda kuuza......huu ndio uhujumu uchumi.

Ni yapi maoni yangu kwa Serikali na jamii?
1. Maafisa usafirishaji Serikalini wawe wataalamu wa fani ya usafirishaji waweze kusimamia vyema mali za umma ikiwemo pikipiki na magari.

2. Dereva atakayebainika ameiba au kuuza kifaa cha Serikali afukuzwe kazi kulinda uhai wa anaowabeba akiwemo bosi wao

3. Magari yote mapya yaliyopaki kwenye ofisi za umma viongozi wa hizo taasisi wawajibishwe ikiwemo kufukuzwa kazi kwa kuhujumu uchumi wa wananchi. Gari ya milioni mia mbili inapaki hadi kufa kwa kukosa huduma ya milioni moja au mbili?

4. Garage itakayobainika ina spear zilizotolewa kwenye gari za Serikali mmiliki awajibishwe ikiwemo kuthibitisha alipotoa spear husika.

5. Serikali ipige marufuku gari za Serikali kuingia garage zisizo rasmi na pale zinapopaki au kuingia pawepo na kibali maalum cha kufanya hivyo.

6. Serkali itoe namba maalumu kwa umma ya kusaidia kuripoti matukio ya hujuma kwa mali za umma.

7. Utaratibu wa kuwauzia watumishi hasa viongozi wa umma magari uangaliwe upya kwani unachangia wao kuua magari kwa lengo la kujiuzia.

Zidumu fikra za watu wazalendo, zidumu hoja zenye tija, lidumu jukwaa la great thinkers.
Nilishangaa siku engine ya hilux double cabin ilipo vuliwa na kuwekwa kwenye gari binafsi na ile ya gari binafsi yenye knock ikafungwa kwenye ya serikali ndipo nilipo ona serikali inajua kununua na sio kusimamia.

Magari mengi sana ya serikali yamebadilishwa usajili na kumilikishwa watu binafsi.
 
Kauli za Hangaya kumnanga Simba wa Yuda na kumdhalilisha marehemu kwenye Mkutano Mkuu wa CCM ilikuwa ndo mlango wa haya yote.

Nchi imewashinda, kilichosalia ni kusaka na kuua watu wanaowapinga waziwazi.

Tuendelee kula nyama mtori upo chini
Simba wa yuda au shetani yule
 
Naomba kutoa Rai kwa Serikali kujiwekea utaratibu mzuri wa kuwadhibiti madereva. Hali ya sasa siyo nzuri sana mtaani na kwenye vijiwe. Yawezekana kweli uchumi siyo mzuri na maslahi ya madereva siyo mazuri kivile kutokana na elimu zao. Lakini pamoja na umaskini walionao haileti maana kufungua spear za magari mapya na kuziuza kisha kufunga spear zilizokufa. Haileti maana kufungua matairi mazuri yenye TBS na kufunga tairi zilizopitwa na wakati . Ni hatari sana kwao, kwa wanaowabeba na hata familia zao.
Ni watumishi wote wa kipato cha chini
  1. Makarani wanauza sana stationery
  2. Polisi ndiyo usiseme rushwa imeshamiri
  3. Wakuu wa shule nao wanabuni mbinu kila kukicha
  4. Madereva wanauza sana mafuta (sijui wanayatoaje kwenye matank) na vipuri
 
Back
Top Bottom