White party
JF-Expert Member
- May 5, 2015
- 1,021
- 1,151
Nawasalimu kwa kina la Jamhuri ya Muungano,
Kumekuwa na utaratibu wa serikali tangu mwaka 2017 kuajiri walimu wa sayansi na hesabu tu,ikitokea arts imeguswa basi ni Kiingereza pekee hali hii imefanya idadi ya walimu wa masomo mengine ya arts kuzidi kupungua mashuleni na hata kama hawapungui wanafunzi wanazidi kuongezeka kila kukicha kwa sababu ya elimu bure.
Mwaka 2016 hadi 2018 tumepitia uhakiki na walimu kibao wametumbuliwa,serikali haikuajiri kuziba pengo hilo badala yake walimu wa sekondari wakashushwa Shule za Msingi na bado hao wa Sekondari pengo halikuzibwa.
Mhe. Rais, Waziri wa TAMISEMI, elimu na utumishi tunaamini mnalijua hilo naomba msilifumbie macho, hali sio nzuri mashuleni, Shule ina walimu wawili au mmoja wa kiswahili au Historia sekondari! Ni mzigo mkubwa hasa Shule za Vijijini.
Tafadhali tunaomba muajiri walimu wa masomo yote angalau kupunguza pengo mliloacha wakati wa uhakiki, pengo linaloachwa na wastaafu, kufariki, kuacha kazi nk
Nawasilisha.