Season 3: Kila binadamu ni kichaa, tunachotofautiana ni asilimia za uwendawazimu, njoo ujifunze namna ya kukokotoa asilimia zako

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,774
9,536
Kuna msemo maarufu hutumiwa na watu wengi usemao hasira hasara huu msemo umebeba mambo mengi. Je kwa siku unakasirika mara ngapi? Na hasira zako hudumu kwa dakika nagapi?

Tafakari kidogo kuhusu hayo maswali kisha twende taratibu.

Kichaa huwa anasifa (dalili) zifuatazo kuongea peke yake, kupiga watu, kuvunja vitu au kuharibu vitu (uharibifu), hasira za haraka, kuona, kunusa, kusikia au kuhisi vitu ambavyo havipo yaani wengine hamvioni, kuona tofauti na uhalisia mfano mbuzi unamuona ni fisi, kushindwa kujisimamia ktk mambo madogo madogo mfano usafi binafsi, kushindwa kufanya kazi yaani unakuwa hauna mzuka, kuchanganyikiwa, kujitenga, kupoteza hamu ya kuishi n.k . Sio lazima uwe na hizi dalilizote.

Mtu kuwa kichaa anaweza akawa na dalili mbili au tatu kati ya hizo yaani atleast dalili mbili.

Kuna baadhi ya mambo yanaweza kuifyatua akili ya mtu (ku triger) na kumfanya apate dalili moja wapo kati ya hizo hapo juu mfano ulimnunulia mke wako i phone ya milioni mbili ghafla umekuta sms za kumsifia kijeba mwingine jinsi alivyo mpa penzi tamu yaani unajikuta tu umeitamiza simu umeenda umemvagaa mke wako unampiga makofi ngumi mitama na unajikuta umeua unaona haitoshi unatamiza tv chini unavunja dressing table, unawapigia simu wazazi wake unawatukana wote kisha baadae fahamu zinakurudia unaona huo ni msala utafia jela unaamua kuiteketeza kwa moto maiti yake kwa kuichoma na magunia ya mkaa yapatayo kumi na mbili, mfano wa pili ni daktari kakupima haraka haraka kakuambia una ukimwi bila yeye kukupa kwanza ushauri na nasaha ile hali itakayokukuta ndio ukichaa wenyewe, biashara yako imefirisika ghafla, umedisco chuo, umepata msiba wa ghafla ile hali inayokukuta ndio ukichaa wenyewe hivyo basi utapata dalili mbili au zaidi kumbuka safari ndefu huanza na hatua fupi fupi hata safari ya ukichaa kamili huanza na dalili ndogo ndogo.

Jinsi ya kukotoa asilimia za ukichaa/wendawazimu wa mtu.
Angalia akili inapofyatuka mtu anakaa na hasira au dalili tajwa hapo juu kwa dakika ngapi (hali ya kuchanganyikiwa)

Mfano MR X akichanganyikiwa kwa wivu wa kimapenzi hukaa na hasira kwa dakika 30 kisha anakua sawa

Formula

% kuchanganyikiwa = muda aliochanganyikiwa(ktk masaa)/24 hrs × 100%

=[{30÷60} ÷24] × 100
=2%

Mke wako ukimkorofisha angalia reaction yake na muda atakao nuna na kuwa na tabia za ajabu ajabu kama vile kugoma kupika n.k kisha kokotoa na ufanye tathimini.

Kuna wengine hua wanaamka na ukichaa yaani asubuhi tu anaamza kupiga watoto na kupiga mayowe bila sababu wewe mhesabia dakika kisha kokotoa fanya tathimini

Kuna wengine wakilewa huanzisha ugomvi, hupiga watu hulala na wanawake hovyo fahamu zikirudi wanaanza kujilaumu wewe muhesabie dakika kokotoa fanya tathmini

Kichaa kamili ana score kuanzia 70 mpaka 100% yaani tukisema 100% namaanisha yuko out of mind 24 hrs.

Haya mambo yapo na yanatokea kila siku, refer case za UDOM wanafunzi kujirusha gorofani yaani anapanda kule juu kisha anajirusha.

Ikumbukwe kuwa mambo yanayoweza kufyatua akili yapo mengi sana ambayo ni mambo ya kimaisha na vitu kama Bangi, pombe, cocaine n.k

Kufyatuka kwa akili maarufu kama dishi kuyumba kunaweza kukutokea kwa sekunde, dakika, masaa kadhaa, siku, mwaka au miaka. Asilimia kubwa huwa ni kwa muda fulani kisha anakaa sawa wengi ni dakika 5, 30 au lisaa limoja kisha anakuwa sawa.

Kila mtu ni kichaa ila tunachotofautiana ni asilimia za ukichaa. Harakati za kimaisha zinaweza kukufanya ukawa kichaa kamili.
 
Mfano wa matukio unayoweza kiyachukulia powa, lakini yana gharimu uhai wa watu na shida kubwa huanzia kichwani kwa akili kigyatuka na waliokaribu kushindwa kukotoa na kufanya tathimini mapema
GridArt_20240427_153511988.jpg
 
Back
Top Bottom