Sani Abacha: The economic figure in Nigeria

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
SANI ABACHA, MBABE WA MAPINDUZI NIGERIA, UTAWALA WAKE ULIGUBIKWA NA UFISADI, MAUAJI,UKATILI NA UKIUKAJI MKUBWA WA HAKI ZA BINADAMU: LAKINI NI KIPINDI CHAKE NIGERIA ILISHUHUDIA MAGEUZI MAKUBWA YA UCHUMI.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Sartuday -3/11/2018.
Dumila, Morogoro- Tanzania

Nigeria ilipata uhuru wake tarehe 1 Oktoba 1960 kutoka kwa Uingereza. Nigeria ni nchi ya Afrika ya Magharibi inayopatikana kwenye pwani ya Bahari ya Atlantiki, Mji mkuu ni Abuja uliyopewa hadhi ya kuwa makao makuu ya taifa hilo mwaka 1991 baada ya kuhamishwa kutoka Lagos mwanzoni mwa mwika ya 1991. Rais wa sasa ni Muhammadu Buhari ambae ni rais wa 15 toka taifa hilo lilipo pata uhuru mwaka 1960 na kuwa jamuhuri rasmi mwaka 1963.

Demokasia nchini humo ilianza mwaka 1993 ambapo mwaka huo uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wenye misingi ya demokasia uliitishwa, uchaguzi huo ndio ulichochea mvurugano wa kitaifa kufatia matokeo ya uchaguzi huo kufutwa baada ya Chief Abiola kutoka upinzani kushinda. Uchaguzi huo ulitaka kuirejesha Nigeria kwenye historia mbaya ya machafuko na mparaganyiko wa kitaifa kama yale machafuko ya Kati ya mwaka 1966-1970.

Sintofahamu ya kutaka kuzuka machafuko nchini Nigeria kufatia mgogoro mkubwa wa kisiasa ulio anza mapema tarehe 12/6/1993 baada ya serikali ya Jeneral Ibrahim Babangida kufuta matokeo ya uchaguzi ambao ulikuwa umempa ushindi Chief Abiola, ushindi huo ndio ulimfanya mbabe wa siasa na mapinduzi ndani ya Nigeria kuibuka tena nchini humo, sio mwingine ni Sani Abacha huyu ni kiongozi mwenye kuratibu mapinduzi yote nchini humo kuanzia yale ya mwaka 1983 yaliyo muingiza madarakani Muhammadu Buhari na yale ya mwaka 1985 yaliyo mfurumusha Buhari tena madarakani.

Huyu Abacha ndie aliyefanikisha kumuingiza madarakani Ibrahim Babangida kupitia mapinduzi ya mwaka 1985, hatimae mwaka 1993 akaratibu mapinduzi baridi yaliyomuondoa Babangida na baadae akafanya mapinduzi kuionndoa serikali ya muda ya Ernest Shonekan na kujitawaza kama kiongozi wa taifa hilo, haraka sana akajipandisha vyeo na kuwa Jeneral mkuu wa majeshi ya taifa la Nigeria. Kufatia hatua hiyo ikamfanya kuwa askali wa kwanza Nigeria kupata cheo kamili cha Jeneral bila kupitia vyeo vingine vya chini (attain the rank of full General without skipping a single rank).

Utawala wa Sani Abacha ndio utawala katili na wa kidikteta kuliko tawala zote zilizo pita nchini humo japo kupitia yeye ndio ilikuwa mwanzo wa demokasia kufunguka nchini Nigeria mpaka leo. Utawala wake umeacha majeraha na maumivu makubwa pengine kuliko watawala wengine wowote wa nchi hiyo toka uhuru.

Huyu Sani Abacha alizaliwa September 20 1943 huko katika mji wa Kano jimbo la Kano Nigeria, alikuwa ni mzaliwa kutoka kabila la Borno kutoka eneo la Kanuri, Kano. Mwaka 1963 alijiunga na chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Nigeria (Nigeria military training college) na baadae kuhamishiwa chuo cha Mons Officer Cadet school huko Uingereza ambako huko alitunukiwa cheo cha lieutenant daraja la pili alipo rejea Nigeria alijiunga na jeshi huko Kaduna.

Abacha aliingia madarakani kwa kufanya mapinduzi baridi yaliyo muondoa madarakani Ernest Shonekan kufatia mitifuano ya kisiasa baada ya uchaguzi uliofanyika 1993 chini ya utawala wa Babangida, Uamuzi huo wa Babangida kufuta matokeo wakati kila kitu kikiwa wazi kuwa mshindi ni Chief Abiola, kilisababisha vurumai kubwa. Wananchi waliandamana na kupaza sauti kuwa Babangida alikuwa anafanya jaribio la kuzuia demokrasia kuchukua nafasi. Pamoja na shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, waliotaka Chief Abiola atangazwe mshindi, Babangida hakukubali. Matokeo yake aliamua kujiuzulu urais na kumteua mwanasheria Ernest Shonekan ili aongoze nchi kipindi machafuko hayo yakiendelea.

Kufatia hatua hiyo Shonekan aliongoza Nigeria kwa miezi mitatu yenye presha kubwa kutoka kwa wananchi. Baada ya hali kuwa tete, Jenerali Sani Abacha, wakati huo akiwa mnadhimu wa jeshi, alimpindua Shonekan. Abacha akifahamu kuwa sababu aliyoitumia kumpindua Shonekan ilikuwa machafuko yaliyotokana na wananchi kutokukubaliana na Abiola kunyimwa ushindi wake, yeye ndiye aliharibu zaidi.

Kwani baada ya mategemeo kuwa hali ya mambo kupoa ndio nchi iliendelea kuchafuka zaidi baada ya mivutano kuongezeka baina ya Abacha na Chief Abiola kuendelea kuvutana, maana baada ya uchaguzi Abiola alitaka kupewa haki yake baada ya ushindi. Alitegemea ujio wa Abacha ungeheshimu demokrasia ya WaNigeria, lakini ilikuwa tofauti mno kwa Abacha maana Abacha hakufanye yale walio tegemea.

Abiola katika kutafuta haki yake baada ya kuona hakuna juhudi zozote za Abacha kuheshimu demokrasia ya WaNigeria, alizunguka nchi mbalimbali na kwenye jumuiya za kimataifa. Kote alipokwenda aliona kuna hali ya kusuasua, hivyo Juni 11, 1994, alirejea Nigeria kisha akafanya mkutano wa hadhara, Epetedo, Lagos na kujitangaza kuwa Rais kisheria. Alipokuwa anajitangaza Rais, Abiola alisema kuwa alishawishika kuingia kwenye siasa ili kuwakomboa Wanigeria, wafurahie uhuru wa nchi yao kwa kuhakikisha anapigania upatikanaji wa Serikali ya kidemokrasia. Alisisitiza kuwa katika hilo hakuwa tayari kunyamaza mpaka demokrasia ionekane ndani ya maisha ya Wanigeria.

Kwa tangazo hilo, Jeneral Abacha aliona amechokozwa mpaka mwisho. Akaagiza magari 200 ya kijeshi yaliyojaa askari kwenda kumkamata Abiola. Sababu ya kutumia nguvu kubwa hivyo ni imani kuwa Abiola alikuwa akipendwa sana na watu, kwa hiyo kitendo cha kumkamata kingeweza kuibua rabsha na wananchi. Abiola alikamatwa na kufunguliwa kesi ya uhaini. Kuanzia alipokamatwa, Abiola hakuwahi kuachiwa. Alihamishwa gereza moja hadi lingine mpaka Julai 7, 1998, saa 10 alasiri, Serikali ya Nigeria ilipotangaza kuwa Abiola amefariki dunia kwa matatizo ya moyo. Kabla ya kifo cha Abiola hiyo tarehe 7/7/1998, tayali Jeneral Abacha alikuwa amesha fariki dunia siku 29 nyuma yani June 8 1998. Kifo cha Abacha na Abiola walitofautiana siku 29 na wote vifo vyao viligubikwa utata.

Abacha alifariki mwanzoni wakati mitifuano baina yake na Abiola ukiendelea wakati huo Abiola alikuwa gerezani, kifo cha Sani Abacha kilizua Utata baada ya wengine kusema aliuawa kwa kuwekewa sumu na makahaba, awali ilielezwa Abacha alionekana akiwa na wanawake wawili wenye asili ya India kutoka Dubai,lakini taarifa ya serikali ilipinga madai hayo na kueleza kifo chake kilitokana na shinikizo la damu baada ya matumizi ya vidonge vya viagra, baada ya kifo chake Abacha ,Jenerali Abdulsallmi Abubakar alishika madaraka kabla ya kurejesha utawala wa kiraia chini ya Rais Olusegun Obasanjo.

Huku pwani pana msemo wa kiswahili usemao "kila pana lenye ncha lina mwisho" hivyo Abacha alivuma Nigeria nzima akasikika dunia nzima jina lake likatajwa kila mahali kuwa ni fisadi, mwizi, dikiteta na kiongozi mfujaji pesa, huku upande mwingine akitajwa kama kiongozi aliye ipaisha Nigeria kiuchumi. Kufatia haya yote sasa turejee mpaka Kwenye viunga vya Villa Park Ikuru ya Nigeria kwenye jiji la Abuja ili kumuangazia kwa upana na undani kiongozi huyu wa kijeshi Sani Abacha.

Abacha mzaliwa wa kabila la Borno kutoka Kanuri, sehemu kubwa ya maisha yake alikulia katika mji wa Kano, Nigeria. alikuwa Rais wa 10, wa Nigeria kuanzia mwaka 1993-1998 ,Kwenye utawala wake Abacha inaelezwa aliiba zaidi ya dola millioni 350 na kuzificha kwenye mabenki ya uswizi na nchi nyingine za ulaya. Abacha alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha yaliyoacha maswali mengi kuliko majibu, mbali na kifo chake cha utata cha juni 8, 1998 lakini pia aina ya utawala wake imeacha majeraha na maumivu makubwa pengine kuliko watawala wengine wote wa nchi hiyo walio mtangulia na walio mfuata baada yake.

Mara kwa mara alijikuta akinyooshewa vidole na jumuiya mbalimbali za kimataifa. Lakini pia kutochukua juhudi zozote za kukomesha vitendo vya rushwa huku naye akitajwa kama kiongozi mla rushwa hatari wa kupindukia, kulimfanya kuchukiwa zaidi ndani na nje ya Nigeria utawala wa Abacha ulishutumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huku mwenyewe akipuuza kila aina ya upinzani dhidi yake. Uamuzi wake wa kumnyonga mwandishi na mwanaharakati Ken Sarowiwa ulishutumiwa vikali ndani na nje ya nchi, pia alipuuzia mbali ombi la kutowafunga Moshood Abiola na Olusegun Obasanjo, Abacha anadaiwa kujilimbikizia mali nyingi ikiwa ni pamoja na kutorosha pesa na kuziweka kwenye akaunti yake binafsi nje ya nchi akishirikiana na kijana wake mkubwa aliyeitwa Mohammed Sani Abacha.

Wakati wa utawala wa Abacha ambao uligubikwa na tuhuma kubwa za ukiukaji wa haki za binadamu, unyanyasaji na mauaji ya waandishi wa habari huku wanasiasa wakitiwa kashikashi za kisiasa. Katika utawala wake watu walio onja kaa la moto katika makali ya utawala wa Sani Abacha ni Olesegun Obasanjo na Chief Abiola. Huyu Obasanjo ndie aliyekuja kuwa rais baadae. Huku huyu Abiola alikuwa mwanasiasa aliye mhenyesha Abacha kufuatia mtifuano ule wa kisiasa uliotokea kisha Abiola akakamatwa na kufunguliwa kesi ya uhaini.

Kuanzia alipokamatwa, Abiola hakuwahi kuachiwa. Kufatiwa kukamatwa kwa Abiola siasa nchini Nigeria ikapamba moto mashinikizo ya kutaka Abiola achiwe huru yakaongezeka, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, Rais wa Afrika Kusini wakati huo, Nelson Mandela na viongozi mbalimbali, walisafiri mpaka Nigeria kuonana na Abacha ili kumuomba Abacha kumwachia huru Abiola bila mafanikio.

Huku aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa John Paul II pamoja na mshindi wa tuzo ya Nobel, Desmond Tutu, nao pia walimwomba Abacha kumwachia huru Abiola lakini Rais huyo wa kijeshi alikataa. Juni 9, 1995, mke wa pili wa Abiola, Alhaja Kudirat Abiola, aliuawa. Sababu ya kuuawa inatajwa ni msimamo wake wa kuwa mstari wa mbele kumtetea mume wake. Aliyekuwa msaidizi wa Abacha, Meja Hamza Al-Mustapha ndiye anatajwa kumuua Kudirat kwa maagizo ya Abacha. Vilevile, familia ya Abiola, walisumbuliwa, kuwekwa mahabusu, kubadilishwa magereza na kuachiwa mara kwa mara kipindi chote Chief Abiola alipokuwa gerezani.

Kipindi chote Abiola akiwa gerezani, Abacha alitoa sharti kuwa angeweza kumwachia huru kama Chifu Abiola angeutangazia umma kuwa yeye siyo Rais na kwamba hakushinda uchaguzi wa Juni 12, 1993. Sharti hilo ndilo ambalo Abiola alilikataa. Abiola alisema kuwa kutamka maneno hayo ni kuwasaliti wananchi ambao kwa wingi wao, mshikamano na imani kubwa, walimchagua na wamekuwa naye pamoja hata kipindi yupo gerezani.

Wakati hayo yakiendelea kwa Abiola kwa kuonja makali ya utawala wa Abacha pia mwanaharakati mwingine aliyeitwa Ken Sarowiwa ambae aliyekuwa mwanahabari mashuhuri alikutana na mbinyo wa Abacha. Huyu Ken sarowiwa alikuwa ni mwandishi mashuhuri na mwanaharakati wa Nigeria, aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa na utawala wa kijeshi wa Nigeria chini ya Jenerali San Abacha, Ken Sarowiwa alipigwa risasi akiwa na wenzake wanane Novemba 10 ,mwaka 1995 saa 7:30 mchana katika gereza la Port Harcourt kwa makosa ya kubambikiziwa kesi.

Kama ilivyo kuwa kwa Abiola, Ken Sarowiwa aliongoza harakati za kudai kodi dhidi ya mrahaba wa mafuta yanayochimbwa katika eneo la ardhi ya watu wake, yaani waogoni. Hawa watu wa kabila la Waogoni walipinga kwa nguvu serikali ya Jenerali Sani Abacha kuipa kampuni ya kigeni la Royal / Dutch Shell, kuwa na hisa kubwa ya mafuta yatokayo katika eneo lao. Wakati wazalendo wa eneo hilo wakiwa duni mno Kiuchumi na umasikini wa kutupwa. Kufatia hatua hiyo watu walioishi katika Delta ya Mto Niger ,waliazimia kufanya mapambano ya kudai mrahaba wa haki Katika mgawanyo wa mapato yatokanayo na mafuta yaliyochimbwa katika eneo lao, wakati wao hawana barabara ,hawana Maji, madawa, shule ,zahanati ,hospitali na hata tone la mafuta hapo kwao huku bei ya mafuta eneo lao yakiuzwa kwa bei kubwa.

Asilimia 90 ya mauzo ya nje Nigeria, yalitokana na mafuta yatokayo katika hiyo delta ya mto Niger, Nigeria ni miongoni mwa mataifa ya daraja la kwanza duniani yanayosafirisha mafuta kwa wingi. Waogoni na Waijaw, raia wa maeneo hayo walikuwa duni sana, walilazimika kusafiri hadi mjini wa Port Harcourt makao makuu ya jimbo hilo la Niger delta State kutafuta mafuta ya kutumia huku yakiwa na bei kubwa.

Ken Sarowiwa ambaye alikuwa mtoto wa chifu Beeson Sarowiwa wa kijiji cha Bane, hakuona furaha kuishi kwa taabu katika eneo lenye Utajiri wa mafuta yanayochimbwa na makampuni ya kigeni ya ulaya na marekani wakati watu wake wakiwa fukara wa kupindukia. Wakiishi huku rasilimali walizopewa na mungu zikigawanywa na utawala wa kijeshi wa Sani Abacha na hao rafiki zake wa kibepari na kampuni zao zilizoungana za Royal Dutch Shell. Lakini kila walipojaribu kusema walipigwa virungu na polisi waliolipwa mshahara na kampuni hizo na walipewa sare za jeshi na viatu.

Sarowiwa akajitoa kuwaokoa waogoni ,kama Nabii MUSA alivyofanya kuwakomboa waisrael utumwani ,Misri. Maana yeye aliuona utajiri ulitoka katika ardhi yao ,lakini wakabaki hawana elimu ,walisalia masikini waliolazimika kutoa rushwa kwa askari wa Abacha ambao walizagaa mitaani kila kukicha ili kuwalazimisha raia wawape rushwa. Rushwa ilitolewa kwa hawa askari wa Abacha, sio mpaka ukosee bali kama ulijipitia barabarani na Jembe lako begani asubuhi wakati unapokwenda shambani ukikutana na askari wa Abacha, lazima uwape mshiko au utakamatwa bila sababu.

Kutokana na unyanyasaji kuzidi Sarowiwa na wenzake walianzisha chama chao cha ukombozi cha Movement for Survival of the Ogoni People ( MOSOP) ili kupinga unyonyaji na uzandiki katika eneo zima la Delta ya Mto Niger. Mafuta ,ambayo yaliunemeesha utawala wa Sani Abacha na hizo kampuni za kigeni ,wakati huku raia wa kawaida wakibaki masikini.Waogoni wapatao 500,000 walisalia fukara katika ardhi tajiri ya rasilimali ya mafuta. Huko Nigeria ,mapipa ya mafuta zaidi ya milioni 634 yenye thamani ya dola za marekani takribani bilioni 30 yalichimbwa mahali hapo kila mwezi. Mapipa hayo yalitoka katika mtandao wa visima takribani 100 vilivyounganishwa katika vituo vitano. Huku Shell petroleum Development Corporation ( SPDC) waliendesha uchimbaji mafuta kwa ubia na shirika la mafuta la Nigeria ( MNPC), AGIP na ELF.

Serikali na wawekezaji waliendelea kupuuza kilio cha waogoni bila kuwapa mrahaba wa haki yao ili waondokane na kero zao. Wakati rasilimali hiyo ikitoka kwenye ardhi yao, Abacha alipewa gawio, askari wake walilipwa mshahara na watoto wao walisomeshwa ughaibuni na wengine walikuwa wakurugenzi katika mashirika hayo. Wakalipwa mshahara mizuri, nyumba na masurufu mazuri. Kutokana na vuguvugu la wadai haki basi mara moja utawala wa Abacha ukaanza kuwashughurikia wanaharakati wote wa MOSOP, akiwemo na kiongozi wao Ken Sarowiwa mwanzoni walianza kutishiwa kwa kufunguliwa mashitaka ya kubambikizwa kufatia hatua hii wanachama wengine wa chama hiki walikimbilia uhamishoni.

Abacha ambae ndie alikuwa mkuu wa nchi akawakamata vinara wa kikundi hicho cha MOSOP na kuwashitaki huku yeye akiwa ndie mshtaki, Abacha akajifanya hakimu na mwendesha mashtaka, shahidi na mlalamikaji kwa pamoja huku akilenga kuwaua wote. Kufatia shinikizo kutoka kwa Jeneral Sani Abacha hatimae wanachama wa MOSOP walihukumiwa kifo katika mahakama za kiini macho (kangaroo court) akiwemo Mwanaharakati kinara wa eneo hilo Ken Sarowiwa. Kupitia mgogoro huo watu wake Ken Sarowiwa yaani watu wa kabila la Ogoni walifungua kesi mjini New York kuishtaki kampuni ya Royal /Dutch Shell kwa kumuua Sarowiwa huku madai hayo yakipamba moto japo dai lao halikuwahi kufanyiwa kazi kwa uzito wake mpaka pale Abacha alipo fariki dunia na kulipeleka vuguvugu hilo kupoa kidogo

Nje ya tuhuma za udikteta na ukadamizaji haki za binadamu pamoja na ufisadi mkubwa katika utawala wa Abacha kumbukumbu nzuri pekee inayokumbukwa ya utawala wake ni kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza mzigo wa madeni ya nje kutoka dola za kimarekani bilioni 36, mwaka 1993 kufikia dola billioni 27 mwaka 1997 ,aliongeza pato la nchi kupitia fedha za kigeni kutoka dola millioni 494 mwaka 1993, hadi dola bilioni 9.6 mwaka 1997. Alipunguza mfumuko wa bei kutoka asilimia 54 enzi za Ibrahimu Babangida hadi asilimia 8.5 kati ya 1993 na 1998. Pamoja na rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu Sani Abacha anatajwa kama kiongozi pekee katika historia ya Nigeria aliyefanikiwa kuleta mageuzi makubwa sana ya uchumi wa nchi hiyo.

Utawala wa Abacha ambao ulitawala toka mwaka 1993 mpaka juni mwaka 1998 ndio ulio fungua mlango wa ukuaji wa uchumi wa taifa hilo ambapo leo taifa hilo linashika nafasi ya pili kwa uchumi mkubwa Afrika. Uchumi huu tunaouona sasa Nigeria ambao unakua kwa kasi na kuifanya Nigeria kuwa moja ya mataifa yenye nguvu za ukuaji kiuchumi duniani huku likiwa na uchumi wa pato ghafi la dola 0.37 trillion ikiwa imeshikilia uchumi wa Afrika kwa asilimia 47% na kuwa taifa muhimu linaloamua mwenendo mzima wa uchumi wa Afrika. chanzo cha ufufukaji wa uchumi huo ni utawala wa Jeneral Sani Abacha.

Abacha ambae utawala wake ulionwa kama mwiba ndani ya shilikisho la Nigeria huku ukiwa imesheheni vituko, mauaji, ufisadi, ukatili na mageuzi ya uchumi ndani ya Nigeria hatimae dunia ilitaalifiwa kuwa Abacha alifariki dunia Juni 1998 katika Ikulu ya Villa ,mjini Abuja na kuzikwa siku hiyo hiyo.

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
IMG_20190507_095524_650.jpeg
 
Magwiji wote walishindwa kumshawishi, Papa, Mandela na Kofi Anan hakika alikuwa na kibri
 
Nakumbuka enzi hizo vyombo vyote vya kimataifa ni Jen. Sani Abacha. Enzi zile anataka kumnyonga Ken Sarowiwa ilikuwa stori Kubwa sana. UN, VATICAN, na viongozi mashuhuri sana duniani walimuomba jamaa asimmuue. Jamaa alitia pamba masikioni na kumuua mchana kweupe... Ama kweli hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Alitawala miaka mitano tu kama Jiwe letu. Tofauti Jenerali Abacha yeye alipaisha uchumi wakati Meko wetu yeye aliuharibu uchumi kwa kuwa na tamaa ya kuwa na miradi mingi kwa wakati moja.
 
Nakumbuka mwaka 97 hadi 98 asubuhi saa 12:00 au saa 12:30 hivi nikisikia habari za Sani Abacha kupitia Redio One, wakati huo nipo kwenye harakati za kujiandaa niwahi namba shuleni.
 
Back
Top Bottom