matukio kama haya si kwamba huyu mama ndo wa kwanza kufanyiwa, hata mababu zake walishafanya mchezo kama alioufanya mumewe, sema tuu hajajua kama amejidhalilisha, kamdhalilisha mumewe, watoto wake na familia zao kwa ujumla. Mtu mwenye kazi yake au biashara zake na akiwa busy kulea watoto hawezi pata muda wa kumpiga mgoni wa mumewe wala kuita waandishi wa habari wakaweka zogo nyumbani kwako. Huku ni kuwa idle au mambo ya uswahilini, mwanamke mwenye staha anamaliza mambo yake na mumewe bila watoto wala majirani kujua nini kinaendelea. Kama wamefikia level ya kulala vyumba tofauti basi wanatakiwa kila mtu awe na time zake wasisumbuane na kudhalilishana mitandaoni, kesho na keshokutwa anakuja jutia alichofanya.
Sasa mama kama huyu akiwa na binti yake atamfunda avumilie ndoa kweli au atumie akili, maarifa au hekima gani kunusuru ndoa yake?
Kweli ndoa sio siku ya harusi tuu ndoa ni kuishi na kukabiliana na kila linalotokea kwenye ndoa vinginevyo ukiwa na roho ndogo usioe wala usiolewe. Wengine ndo tushakuwa manunda nasubiria kichanga wa Obama tuu azaliwe kanavoruka huko tumboni balaa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.