Safaricom yaweka rekodi Africa Mashariki kufikisha mapato ya dollar billion 1 kwa mwaka

Nimeishi kenya miaka mitano. Hakuna tofauti kubwa sana ya kimaisha kati ya kenya na Tanzania.

Tanzania uchumi wake haujulikani vzr kwa sababu mambo mengi ya kimaendeleo na kiuchumi yapo nje ya Mfumo unaoeleweka.
Lakin mambo mengine ya hali ya kimaisha, poverty, rushwa, ufisadi nk...mambo ni yale yale nchi zote mbili

Hio ni mtizamo wangu lakini.
Kenya wana
Shule nzuri sana za serikali,
Hospitali bora na nyingi hadi vijijini,
Airports na bandari zenye ufanisi mkubwa.
Urasimu mdogo kulinganisha na Tanzania.
Ubunifu mkubwa wa teknolojia na utoaji huduma.
Urahisi wa kufanya biashara mkubwa
Mzunguko wa pesa mkubwa.
 
Vodacom wamalioa kodi kidogo kuliko hata Airtel. Wakati wao voda ndiyo waba wateja na revenue kubwa kuliko airtel

Huwa nawaelewa sana tigo na voda kugoma kujisajili DSE. Soko la mawasiliano ya mobile bongo lina siri nyingi sana
 
Kenya wana
Shule nzuri sana za serikali,
Hospitali bora na nyingi hadi vijijini,
Airports na bandari zenye ufanisi mkubwa.
Urasimu mdogo kulinganisha na Tanzania.
Ubunifu mkubwa wa teknolojia na utoaji huduma.
Urahisi wa kufanya biashara mkubwa
Mzunguko wa pesa mkubwa.
Nimeishia hapo uliposema Urasimu ndogo kuliko Tanzania.

Itakuwa huijui kenya wew.
Kwa Africa nzima sidhani kama inakosa top 3 kwa Urasimu na Rushwa. Hata miradi yap mikubwa ya barabara SGR nk kuna upigaji sio wa kawaida.
Au kuna kenya nyingine sio hii.

Hospital na shule kenya labda useme za private ila za public usitupange aisee. Ni hivyo sana.

Gap kati maskini na Tajiri ni kubwa sana huko kenya. Kuna maeneo mengine nasa ya kilimani na westlands watu wa kawaida hawaruhusiwi kukanyaga.
Kule Eastleigh wasomali wakijenga maghorofa wanapangisha wasomali tu. Mweusi hukai kule.

Kenya wanamatatizo mengi at hand kulinganisha na Tanzania aisee usitupange.

Tanzania uongozi ukiwa bora na watu sahihi. Inapiga hatua haraka sana. Basi tu viongozi ni wazembe na wabinafsi
 
Nimeishia hapo uliposema Urasimu ndogo kuliko Tanzania.

Itakuwa huijui kenya wew.
Kwa Africa nzima sidhani kama inakosa top 3 kwa Urasimu na Rushwa. Hata miradi yap mikubwa ya barabara SGR nk kuna upigaji sio wa kawaida.
Au kuna kenya nyingine sio hii.
Sitajielekeza kujibu hizo porojo nyingine ila nikujibu hizi mbili tu,
1. Ripoti ZOTE za utafiti kuhusu nchi zenye urasimu mdogo na wepesi wa kufanya biashara Africa Mashariki zinaiweka Rwanda ya kwanza na Kenya ya Pili, pia ripoti zote hizo zinaziweka Rwanda na Kenya katika nchi 10 zenye mazingira bora ya kufanya biashara Africa, Tanzania hatumo.
2. Kenya haiko hata top 20 ya Rushwa katika Africa, huo ni uhakika na sio dhana.
Kinachokuzuzua ni kwa sababu Kenya ina uchumi mkubwa kwa hiyo hata Rushwa zake zitaonekana kubwa tu, pia ni kwa sababu ya uhuru wa vyombo vyao vya habari ndio maana unapata taarifa na kelele zao nyingi kuhusu Rushwa, nchini mwako vyombo vya habari muda wote vinajadili mpira, betting na udaku wa kina diamond na mwaijaku saa ngapi utasikia habari za Rushwa.
 
Vodacom waanzishe pochi la biashara kama ilivyo Safaricom. Kila mtu atumie hiyo Kulipa kwa Mpesa kama ilivyo kenya. Unaweza ishi Nairobi mwezi mzima bila kushika hela ni Kulipa kwa Mpesa tu. Kuanzia Daladala, mama ntilie, bodaboda nk.
Wakianzisha hiyo lazima voda impige chini Safaricom na kurahisisha maisha ya watz kwenye kutafuta chenji na kupunguza magonjwa ya kuambukiza
Hizi tu lipa kwa simu makato hela ya mboga kula na familia kabisa.

Tanzania tunafaida ya kuwa na idadi kubwa ya watu, warahisishe hizi huduma na kufanya gharama ziwe rafiki tu.

Kwa sasa ni nafuu kutembea na cash kwa matumizi madogo ya mara kwa mara kuliko kutumia hizi lipa namba.

Binafsi ni mtumiaji mkubwa wa hizi lipa kwa simu, ila maumivu ya makato nikimuwazia anayeungaunga, hawezi tumia.

Kampuni za simu kuwekewa hela tu humo kwao ni faida kubwa sana, watujali wateja basi.
 
Moja ya Sababu ya Safaricom kufanya vizuri katika huduma yao ya M-PESA ni sera nzuri ya Benki kuu ya Kenya, mfano halisi ni rahisi kuintergrate malipo na online wallet kuliko ilivyo kwa M-pesa Tanzania.
Nina mwaka wa tatu huu nipo Bongo ila natumia M-pesa Kenya kwenye international money transfers.
BOT wana restrictions kibao ambazo ki uhalisia zinafanya huduma ya pesa kimataifa ya mitandao ya simu kutoweza kuwa flexible.
Lack of competition.... ni hilo tu
 
Wiki hii kampuni ya simu ya Safaricom ya Kenya imefikisha mapato ya dollar bilioni 1.07 kwa mwaka na kuifanya kampuni ya kwanza katika ukanda wa Africa Mashariki kufikisha na kupita kiwango cha mapato ya dollar bilioni kwa mwaka.
Mkuu vipi baada ya makato kama kodi wanabaki na faida ya dollars ngapi?
 
Moja ya Sababu ya Safaricom kufanya vizuri katika huduma yao ya M-PESA ni sera nzuri ya Benki kuu ya Kenya, mfano halisi ni rahisi kuintergrate malipo na online wallet kuliko ilivyo kwa M-pesa Tanzania.
Nina mwaka wa tatu huu nipo Bongo ila natumia M-pesa Kenya kwenye international money transfers.
BOT wana restrictions kibao ambazo ki uhalisia zinafanya huduma ya pesa kimataifa ya mitandao ya simu kutoweza kuwa flexible.
Hii nayo ni point isiyo zungumziwa mdau. Sis bado tupo pale pale, ni lack of vision maybe
 
Back
Top Bottom