UZUSHI Rais Museveni amteua mwanaye Natasha Museveni kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimeona taarifa hiyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa mwanaye huyo ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda.

Wengi wamehusisha uteuzi huo kuwa ni kuimarisha familia yake ambapo Mkewe Mama Janet Museveni ni Waziri wa Elimu kwenye Serikali, Mwanaye wa Kwanza Muhoozi ni Mkuu wa Majeshi ya Uganda.

Museveni.jpg
 
Tunachokijua
Natasha Museveni alizaliwa mnamo 1976, ni mtoto wa pili kati ya watoto wanne wa Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museni.

Natasha Museveni(Natasha Karugire) ni mbunifu wa mitindo na mshauri, ameolewa na Edwin Karugire. Katibu wa Kibinafsi wa Rais wa Uganda wa Masuala ya Makazi(kaya)
GIczCbLXgAA2oly

Watoto wengine wa Museni ni:-
  • Jenerali Muhoozi Kainerugaba - Alizaliwa mwaka wa 1974, ni Mkuu wa Majeshi ya Uganda
  • Patience Rwabwogo - Alizaliwa mwaka wa 1978, kasisi wa Kanisa la Covenant Nations
  • Diana Kamuntu - Alizaliwa mwaka wa 1980
Kumekuwa na taarifa inayosambaa mitandaoni ikimuhusisha Natasha Museveni kuwa ameteuliwa na Rais Museveni kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda, taarifa hizo zilianza kusambaa kupitia kwa baadhi ya raia wa Uganda tangu Aprili 1 2024.

Pia mnano Aprili 2 taarifa hizo zilichagizwa zaidi na Mbuvi Gideon Kioko Maarufu kama Mike Sonko ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Nairobi akichapisha kwenye mtandao wa X ujumbe wa kumpongeza Natasha kwa kuteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda.

1712287810103-png.2954113

Je, uteuzi huo una ukweli wowote?

JamiiCheck,
imefuatilia suala hili kutoka katika vyanzo rasmi mbalimbali vya habari na taarifa vya Uganda na kukuta hakuna taarifa yoyote rasmi inayomuhusisha Natasha na uteuzi wa kuwa Gavana wa benki Kuu ya Uganda kama inavyodaiwa.

Pia, JamiiCheck imetazama kwenye akaunti rasmi ya Ikulu ya Uganda, State House Uganda, akaunti rasmi ya Serikali ya Uganda, Government of Uganda na katika akaunti rasmi wa Benki Kuu ya Uganda, Bank Of Uganda kote hakuna taarifa yoyote ya kuteuliwa kwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda.

Vilevile The Media Observer ambao hujihusisha na kuhakiki habari, wamechapisha taarifa kuwa, wamewasiliana na wanahabari wanaoaminika wa Uganda, ambao waliifafanulia Media Observer kuwa ni kweli kumekuwa na uvumi huo wa Natasha kuteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda, ila taarifa hizo si za kweli, ni uzushi uliochapishwa mtandaoni na raia wa Uganda siku ya Tarehe 1 Aprili kwa lengo kusherekewa siku ya wajinga.

Taarifa zinabainisha kuwa tangu Gavana Emmanuel Tumusiime Mutebile alipofariki mnamo January 23, 2022 hakuna uteuzi wowote wa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda uliokwisha kufanyika.

Kutokana na kutokuwepo kwa taarifa zozote rasmi zinazothibitisha kuwepo kwa uteuzi wa Gavana wa Benki Kuu ya Ugabda, JamiiCheck imejiridhisha kuwa taarifa za Natasha kuteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Uganda ni Uzushi.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom