Rais Kikwete akutana na Wabwia Unga Ikulu Dar es salaam

Rais Kikwete amefanya mazungumzo na vijana wabwia unga (Mateja) Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka waachane na tabia ya kubwia unga badala yake wawe raia wema kwa faida ya Taifa.

Mkutano huo wa JK na wabwia unga umefanyika jumanne Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mfadhili wa kituo kimoja cha kurekebisha wabwia Unga aitwaye Zacharia Hans Poppe.

Kweli Rais tunaye watanzania.

bibikuku, vipi ratiba ya wale wa bongo movies ndo nafasi imechukuliwa na mateja?

Yaani huwa najiuliza ni lini wahadhiri wa vyuo vikuu watakwenda ikulu au lugha zao ni tofauti?
 
Rais Kikwete amefanya mazungumzo na vijana wabwia unga (Mateja) Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka waachane na tabia ya kubwia unga badala yake wawe raia wema kwa faida ya Taifa.

Mkutano huo wa JK na wabwia unga umefanyika jumanne Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mfadhili wa kituo kimoja cha kurekebisha wabwia Unga aitwaye Zacharia Hans Poppe.

Kweli Rais tunaye watanzania.

2015 ifike tupumzike jamani !
 
Amekutana na wateja wake,maana nimesikia naye jina lake (jk) lipo kwenye list ya wauza sembe na ndio maana haitoi
 
wameenda kuongea na mshua...adhani walienda wakiwa kamili hawana arosto....au waligawiwa happo hapo..nayule riz
 
ona sasa vijana kwa wazee wasivyojitambua.
wanafanywa kuwa miradi ya watu bila wao kujitambua.

angalia walivyokaa mkao wa kutojielewa ktk maisha ya ulimwengu huu.
vijana acheni kufikiri kwa akili ya kuambiwa.

oneni madhara ya mihadarati yanavyowadharilisha mpaka kufikia hatua ya kufungashwa kama mizigo mpaka ikulu na jamaa anawainjoy tu kama vikatuni vile.
wito: msiwe wepesi wa kukurupukia kila jambo bila kujua mwanzo na mwisho wake.
 
Rais Kikwete amefanya mazungumzo na vijana wabwia unga (Mateja) Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka waachane na tabia ya kubwia unga badala yake wawe raia wema kwa faida ya Taifa.
Exactly how are they to become good citizens? ukitoa labda vijana wachache waliotoka familia zenye angalau kwenye jamii na kuweza kupewa msaada wa kifamilia kukimbia mazingira.

Tatizo sugu hapa ni ajira people are idle kuanzia asubuhi mpaka jioni, there is nothing to stimulate young people hata waliomaliza chuo hawana ajira, hivi unategemea mteja arudi kwenye mazingira yaleyale na madawa yanapatikana vilevile asirudie tena tabia yake hii itakuwa maajabu ya dunia.

Tatizo la madawa ya kulevya linaelekea kuwa sugu na tegemezi kwenye jamii bila ya long term solution ya kulimaliza, madawa yenyewe inavyoonekana tayari yanamchango mkubwa kwenye uchumi maana ni large network sasa ina depend na madawa hilikuishi Tanzania, where is the alternative ya watu hawa bila ya ajira au sera za kuwawezesha kuishi wote wauzaji, wasambazaji na watumiaji.

Kijana wa chini ndio kiashirio people are desperate na kukosa matumaini ya mbele kama ujawa machinga, ujajipendekeza kwa mtu (naanza kuelewa hata hapa JF kwanini wengine wanafikiria ni muhimu, inaonyesha jinsi gani ubunifu ulivyobado kwetu na hali halisi ya maisha ilivyo), au huna ajira where is hope?.

Maana mpaka mtu afikie kuvuta hivyo vitu na wanajua athari zake ujue wamekesha kata tamaa na maisha. Halafu raisi anasema wawe raia wema how? isitoshe yeye mwenyewe ana diriki kusema anawajua waletaji hila hawezi wataja, sasa anadhani hao watu bidhaa zao wanaenda zipeleka wapi kama sio kuwauzia vijana hao hao anaowaomba wawe raia wema.

Kuzuia tatizo ameshindwa in the first place, kutoa alternative ameshindwa sasa anaomba miujiza begs the question does he know what he is doing in the first place.
 
Rais Kikwete amefanya mazungumzo na vijana wabwia unga (Mateja) Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka waachane na tabia ya kubwia unga badala yake wawe raia wema kwa faida ya Taifa.

Mkutano huo wa JK na wabwia unga umefanyika jumanne Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mfadhili wa kituo kimoja cha kurekebisha wabwia Unga aitwaye Zacharia Hans Poppe.

Kweli Rais tunaye watanzania.

Tunaomba picha za hao wasitaafu wa Unga tuzione
 
Rais agewataja wauzaji wa sembe aliosema anawajua na kuwachukulia hatua za kisheria angeokoa wengi kwenye janga hili! Kuwaita ikulu mi sioni kama ni kutatua tatizo. Wengine watatumia ili waarikwe ikulu. Rais akate mizizi ya madawa aache siasa kwenye swala hili nyeti
 
Middle+finger+erection_306992_4263683.jpg
 
Roho inauma jamani.... Ulaaniwe wewe unaefanya biashara ya madawa ya kulevya. Eee weweee wewee
 
8E9U3935.jpg
Kijana Jimmy Changchuu alieachana na matumizi ya dawa za kulevya akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete picha aliyochora yeye na kijana mwenzake wakati vijana hao walimpomtembelea Rais Ikulu jijini Dar es Salaam leo.Vijana hao wanalelewa katika kituo cha Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam

8E9U3986.jpg

Vijana walioachana na Matumizi ya dawa za kulevya kutoka katika kituo cha Pilli Missanah Foundation kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.Kulia pembeni ya Rais ni Mwanzilish Kituo hicho Bi.Pilli Missanah na watatu kushoto ni mfadhili mkuu wa kituo hicho Bwana Zacharia HansPoppe
(Picha na Freddy Maro)
 
Back
Top Bottom