Rais Kikwete akutana na Wabwia Unga Ikulu Dar es salaam

Promo peak resonance!
Picha za nini muda huu ambapo nchi iko harijojo?
 
Last edited by a moderator:
Mnauza bidhaa wenyewe then mnataka watu waache tumia . Danganya toto
 
Rais Kikwete amefanya mazungumzo na vijana wabwia unga (Mateja) Ikulu jijini Dar es salaam na kuwataka waachane na tabia ya kubwia unga badala yake wawe raia wema kwa faida ya Taifa.

Mkutano huo wa JK na wabwia unga umefanyika jumanne Ikulu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mfadhili wa kituo kimoja cha kurekebisha wabwia Unga aitwaye Zacharia Hans Poppe.

Kweli Rais tunaye watanzania.
Kwahiyo hata huyo anaewauzia (Ridhwani) naye atakuwepo?
 
Enh mola !
Tulikutenda nini kiasi cha kuyastahili haya!
Tulikosea wapi kama nchi
tulifanya ovu gani kustahili laana hii
tunapaswa kufanya nini tujitakase tusirudie upofu huu
tulikiuka katazo gani itupase kuadhibiwa kiasi hiki
yarrabi tunusuru waja wako
tupe wepesi tulivuke hili aa kwa imani
tujalie nguvu tuitue nira hii!
 
Mkuu nguvumali hata wewe unamshabikia Kagame? Tuanze kufuatilia faili la urai wako?

mimi Kagame ni uchuro kwangu, lakini mkuu wetu wakaya nae afanye yake kwa VITENDO tuone nchi ikipaaa.

mimi situmii muda wangu kumsema jirani yangu ilihali kuna mengi yananingoja nyumbani kwangu.

huo muda wa kukaa na mateja angetumia kupambana na kuwapa motisha waliokatika vita ya kuusambaratisha mtandao hatari wa madawa hayo.

nashangaa hadi leo kashindwa kumtimua kazi mkuu wa usalama kiwanja cha ndege cha JKN ...HUWA SIMUELEWI MZALIWA WA MSOGA.
 
Kama walitimiza saa moja pale ikulu lazima aliwapatia kete yake kila mmoja, kwakua wengine hawawezi kukaa arosto muda wote huo.
 
hoja si kuongea na mateja hoja hapo ni yeye anapambana vipi na wauza hayo madawa nakumbuka enzi za mh amina chifupa alisha wahi kukabiziwa list ya wafanyabiashara wamadawa ya kulevya nashangaa amekaa kimya matokeo yake amina hatunaye tena baada tu ya kujitolea kupambana na wauza unga na baada tu ya amina kufariki imekuwa kimya nathubutu kusema kikwete ni mnafiki
 
...majina ya wauza unga JK anayo anashindwa kuyashughulikia...yeye anashughulika na waathirika....inasikitisha sana....Hii dhana ya kupambana na matokeo badala ya vyanzo vya matatizo ni tatizo kubwa kwa watawala wetu.....yaani badala ya kushughulika na chanzo cha ugonjwa (wauza unga)...we unashughulika na matokeo (mateja)...so sad yaani...
 
God Bless the PRESIDENT JK, God bless Tanzania.
In-ShaAllah Step by step tutafika na tutavuka maovu ya jangaa hili.
jamii tuungane pamoja kwa kila njia (kuomba Dua'a kwa mungu,kuzuia,kukaripia,Kuwasaidi,kukataza,kuripoti,kukemea,kuonya,kujitolea,kutafuta muarobaini, nk) Tuepushe balaa hili lisilokuwa na heri kwetu.
 
ni hatua nzuri, lakini kama kila kitu atafanya rais tu kweli, nini maana ya utitiri wa viongozi tulio nao hapa nchini? kuongea na hawa yaweza kutusaidia angalau kupata wapi tunaweza kumkuta muuza dawa za kulevya hadi yule mkubwa zaidi kwa njia ya snowball
 
bibikuku sikiliza,
kama huna uhakika na kitu unachokiandika usiwe unakurupuka kwa ajili ya
kuwapa watu hasira ili waelekeze lawana kwa rais.

Hivi moderators ........ Paw mnawezaje kuangalia mada kama hii inayoanzishwa ikiwa imepotosha kabisa lengo la rais kukutana na hawa jamaa ikulu jana.

Nazidi kufunguka kuwa mambo mengi yanayosemwa kuhusu rais ni ya uongo na uzushi.
copy Ritz

Haya sema wewe ukweli unaoujua ambao hutaki kuusema. Alikutana nao au hakukutana nao?? Hilo swala la malengo mie sijalizungumzia hapa umekuja nalo wewe
 
Wengi wao ni vijana wasio na kazi.Alichotakiwa ni kufanya uchunguzi wa sababu za vijana hao kujiingiza kwenye matumizi ya madawa hayo.Na katika uchunguzi,ndipo pia angefikia kwenye conclusion inayolenga pande zote,za hao aliopewa majina yao,pamoja na watumiaji kupewa counseling,reharbs na pia kujenga mazingira ya vijana kujiajiri ama kuajiriwa,na siyo kuspend pesa kudhibiti upinzani na nyingine kupeleka kwenye akaunti za nje.

Mkuu hili tatizo kalikuza yeye. Alitangaza kuwa anaorodha ya wauza dawa za kulevya na mpaka sasa hajawachukulia hatua yoyote matokeo yake anafanya vikao na wabwiaji wa unga akina Ray C na hao wengine. Sasa hapo si usanii mtupu. Anataka kujionesha kuwa ni mpambanaji wa madawa ya kulevya wakati anawakingia kifua wanaoendesha biashara hiyo. Anachotakiwa ni kutuonesha kuwa anawafanya nini hao wauzaji na sio kukutana na waathirika. Vinginevyo tunahaki ya kuhisi kuwa kwenye orodha yake kuna watu waliokaribu naye au nduguze ndio maana amekaa kimya!
 
Moja ya habari iliyosisimua wiki hii na humu JF ni ile ya rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete kukutana Ikulu na wabwia unga au mateja wanaodaiwa kustaafu shughuli hiyo. Hii ni mara ya pili sasa kwa rais kukutana na watu wa aina hiyo ikulu. Wa kwanza alikuwa ni mwanadada mwanamuziki maarufu kwa kuzungusha kiuno ambaye tumeambiwa rais aligharimia matibabu yake ya uteja na kisha kukutana naye ikulu. Kwakuwa hii inaweza kuwa njia ya kupunguza au kumaliza tatizo la madawa ya kulevya, namshauri rais sasa akutane na wasafirishaji na wauza madawa ya kulevya yaani wafanyabiashara wenyewe badala ya kukutana na waathirika tu. Bahati nzuri rais aliwahi kutangaza kuwa anawafahamu na anayo orodha yao. Tena alikwenda mbali zaidi na kusema hata baadhi ya viongozi wa dini wanajishughulisha na biashara hiyo. Akishafanya mazungumzo nao ikulu na wakakubali kuacha au kupunguza basi awasamehe kama alivyowasamehe wale wezi wa EPA kwani alisema watakao rudisha atawasamehe tatizo ni kuwa wale "waliorudisha" walimalizana kimya kimya hawakutangazwa kama hawa mateja ingawa tunahamu ya kuwajua waliorudisha na kiasi "walichochukua" na "walichorudisha" Lingekuwa ni jambo la kujivunia kama nao tungewaona wakiwa katika picha ya pamoja na rais Ikulu - mahali patakatifu!

Njia hii ya kukutana na wahalifu kama itaonekana inasaidia, basi rais aende mbele zaidi kwa kukutana na machangudoa ili kumaliza tatizo hilo linalochangia kuenea kwa UKIMWI. Baada ya hapo anaweza kukutana na majangili na kujadiliana nao kuona namna wanavyoweza kupunguza au kuacha kabisa kabisa shughuli za ujangili. Bahati nzuri pia upande huu nako kuna mwanga. Waziri wa maliasili naye ametangaza kuwa ana orodha ya majina ya majangili (Tanzania Daima 15/08/2013) hivyo orodha ya wauza dawa za kulevya na ya majangili zote zipo mikononi mwa rais na waziri wa mali asili. Kwa kupitia vikao hivyo itasaidia kupunguza gharama za kuwakamata na kuwafungulia kesi mahakamani. Hiyo nayo ikisaidia rais akutane na wanaowapiga risasi, kulipua mabomu kisha kuwajeruhi na kuwaua raia wasiokuwa na hatia katika shughuli za kisiasa, kidini na kiraia. Hiyo ikifanikiwa rais akutane pia na Pinda kujadili namna ya kurekebisha au kuifuta ile kauli ya kutaka vyombo vya dola kuwapiga raia wanaokaidi amri za vyombo hivyo badala ya kuwapeleka mahakamani. Kadiri tunavyoendelea tunaweza kugundua kuwa maovu mengi yanaweza kwisha kwa rais kukutana na wahusika ikulu. Na hili si jambo la ajabu kwani hata yule bosi wa Richmond ambaye rais wetu alisema hamjui na hana haja ya kumjua, alipokuja licha ya kuzuia kupigwa picha na waandishi wa habari alipokutana nao, alifika pia Ikulu ambako alionana na makamu wa rais Dk. Mohamed Bilali bahati mbaya rais alikuwa safarini nje labda angekuwepo ndipo "angemfahamu" kisha kufanya naye mazungumzo na kupiga naye picha. Huenda hata ile fidia ya mabilioni tunayotakiwa kuilipa Dowans kwa kuvunja mkataba isikuwepo. Hii ni tafakari yangu.
 
Tafakari nzuri. Inabidi pia akutane pale Ikulu na vibaka wanaoibia wananchi, ingawa najua hawakawii kumliza hapo hapo.
Pia akutane na wala rushwa na mafisadi ambao kwa bahati nzuri wengi kama sio wote ni wanachama wa ccm ambacho yeye kwa upande mwingine ni Mwenyekiti.
 
Back
Top Bottom