Rai: Bangi na gongo vihalalishwe

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,678
698,787
1473923328325.jpg
Ifike mahali tuachane na unafiki! Hivi vitu ni chanzo kimoja kizuri sana cha mapato kama kikiwekewa utaratibu maalum na kuongezewa thamani yake kwa kufanya mchujo wa kitaalam na ufungaji pia
Hivi ni vyanzo vinavyotoa ajira kwa maelfu ya vijana...ni vyanzo ambavyo wengi wanaendeshea maisha yao ikiwemo kusomesha matibabu na hata ujenzi...lakini kile ambacho kingepaswa kuingia serikalini kinachukuliwa na wachache wanausalama wetu hasa jeshi la polisi
1473923337729.jpg

Kesi za bangi na gongo ni nyingi sana huko vituo vya polisi na mahakamani, hawa wanaokamatwa wangetengenezewa utaratibu maalum TANZANIA ya viwanda ingeanzia hapa
1473923350078.jpg

Kwenye hii operation ya kukamatwa hii mitambo askari kibao nao walikamatwa
 
Kuendelea kutozitambua hizi bidhaa ni kuendelea kupoteza ajira nyingi na mapato mengi mengi
Tafiti nyingi zimethibitisha kuwa bangi ikitumiwa kwa kiwango cha chini ni tiba kwa magonjwa mengi hata kwenye ushirikina
Vile vile Vinywaji vingi vikali formula zake haitofautiani na gongo kwanini tusiwekeze huku?
 
Ngoja waje watokwa povu wakushambulie mkuu Mshana jr. Hata huko uingerezea juzi kati hapa bunge lao lilizungumzia hili swala.
 
Ngoja waje watokwa povu wakushambulie mkuu Mshana jr. Hata huko uingerezea juzi kati hapa bunge lao lilizungumzia hili swala.

Yawezekana mtoa mada ni mvuta bangi.
Mimi ni mpinzani no moja wa kupinga matumizi ya mmea hata post nilishawahi kuweka lakini kila kitu sio negative kivile tunaangalia maslahi mapana ya Taifa
 
Hizi mambo siku zikihalalishwa basi hata watumiaji watapungua, hulka yetu wanadamu ni kupenda kitu kinachokatazwa(hasi, haramu).
Kule uholanzi, bangi na uchangudoa vimehalalishwa na serikali ya huko inapata kodi mingi tu kupitia mmea huu. Pesa hizo hizo, tunazipata kama msaada. Sioni mantiki ya kukubali misaada kutoka nchi hio yenye kipato tunachoamini ni haramu.
 
Hata mimi nakubaliana na wewe, waruhusu pia Malaya kujiuza ili mradi wawekewe utaratibu wa kupimwa mara kwa mara na kulipa kodi, kwa hili nadhani tutapata uungwaji mkono wa baadhi ya wabunge wa ccm akiwemo msukuma
 
Mkuu umeongea ukweli mzito,familia nyingi zinasomesha kupitia hizi bidhaa.
Baadhi ya Polisi wana uhakika wa kupata chochote toka kwa kina mama muuza.
TFDA na TBS vyema washirikishwe kwenye huu mpango mkakati wa urasimishaji
Mateja watapungua kwani watapata kitu mbadala cha kuwastimusha.
 
Kuna mapato mengi sana yanapata hapa na kwa mfano mmea una mpaka wateja ambao ni prominent leaders
 
Ok coz nchi za wenzetu ni biashara kubwa sn inayoongeza pato la taifa lakini lazina zitungwe sheria elekezi ili kuzuia magonjwa na mambo mengine
 
Ok coz nchi za wenzetu ni biashara kubwa sn inayoongeza pato la taifa lakini lazina zitungwe sheria elekezi ili kuzuia magonjwa na mambo mengine
Kwa hili kidogo kwangu naweza kusema lisubiri kidogo kwakuwa linajumuisha mambo mengi
 
Back
Top Bottom