Pugu: Rais Magufuli azindua ujenzi wa Reli, asema dereva mzuri hasikilizi maneno ya watu

Dereva mvuta bangi na mlevi anatuendesha kipombepombe na kibangibangi hatuwezi kunyamaza atatuingiza mtoni!
Tutamuondoa hapo natutaweka dereva mwingine ili tufike salama kwenye safari yetu
Hatuwezi kunyamaza kamwe tutakuwa wajinga
 
Daah...Prezdah yupo makini ktk yake...ni heriii aendelee kusimamia...lingine nasikia hela imeanzaa kuachiwaa tusubiriii.
 
Kwa mimi maendeleo ni mambo yanayohusisha ustawi wa watu katika aspects mbalimbali kama vile elimu bora, huduma bora za kiafya, miundo mbinu bora, upatikanaji wa maji safi na salama, kuimarika ulinzi na usalama pamoja na kuimarika kwa nguvu za kiuchumi za watu hao na taifa lao kwa ujumla etc.
(I STAND TO BE CORRECTED)
Elimu ndo jambo kubwa kwenye maendeleo,hayo mengine ni watoto wa elimu.
 
Jukumu lako ni kulipa nauli na kukaa kwny siti kufunga Mkanda na kusali sana tufike salama sio Kelele Mara piga honi, washa hazard Mara mteremko huo unautelezi twende taratibu mnamchanganya Suka!
si wanatuambiaga dereva akiwa anaenda mwendo mbaya tusikae kimya! tumuambie, akiwa anaongea na simu tumkataze, akiweka viroba kwenye chupa ya maji tumsimamishhe nna kumkamata. wametupa hadi namba za viongozi wa trafiki na sumatra.
 
Unaposafiri safari ndefu (mipango ya muda mrefu), dereva anahitaji abiria wanaoopiga kelele na stori, ziwe za furaha au huzuni, ziwe za kusifu au kukashifu maana bila hizo kelele dereva atalala usingizi kwenye usukani na safari kuishia njiani kwa gari kuacha njia. Tunakubali yeye ni dereva na sisi abiria, lakini hatukubali atupeleke tusikokujua na tusikotaka kwenda.

Dereva huyu atambue safari ni majaliwa. Kuna milima na mabonde. Kuna kukwama njiani, gari ikikwama njiani kwenye matope udereva wake hauna kazi-atawahitaji abiria washike wasukume gari. Kama angekuwa amewahi kwenda Mtwara tokea Dar kwa basi miaka 15 iliyopita, angeelewa.
Unayosema ni kweli, ila huyu dereva yuko makini kama dereva wa kisesa express, hata mlale wote yeye yuko macho na makini, tumetumia bil 10 kujenga majengo 20 yenye gorofa nne kila moja wapo waliosema hayatakamilika lakini yamekamilika na chenji imebaki. tulitumia us$ 8,000m kujenga bomba la gesi lenye umbali wa km 600 yeye anajenga reli tena ya kisasa zaidi duniani kwa us$ 187m kwa kilomita 300! huo ndio umakini wa dereva wetu. Wapo abiria walevi hata gari halijafika chalinze wanataka wachimbe dawa hawa ndio wataosababisha gari letu lisifike kwa wakati.
 
Kama kabeba vitunguu na maparachichi hapo ila hata trafiki wanasema pazeni sauti kuhusu madereva wazembe na wasiowajali walio wapakia
 
Hii safari tuliyoianza hatunaimani kama tutafika. Kwanza dreva hamsikilizi hata kindakta na Tandiboi wake. Watu tunaomba tushuke hata tukachimbe dawa dreva hasikii.

Kwanza dreva anapotupeleka siko kabisa. Wengine umesha tupitisha vituo.

Dreva huoni hata bumps. unapigwa toshi na unasimamishwa na Trafik hutaki kusimama.

Mi nishushe tu. Uko unakotaka kutupeleka mimi naomba nisifike uko. Nilipofika sasa pananitosha.
umejuaje kama umefika wakati uko ndani ya roli, ukipiga makelele polisi watajua uko kwenye tela kuna watu.
 
Wala hakuna anayetaka utekaji.

Hakuna anayetaka kiongozi Mungu mtu.

Hakuna anayetaka kiongozi anayedhani anajua kila kitu.
We unataka kiongozi mbumbumbu asiyeelewa lolote ili upate kiki na pa kutokea. Jpm hawapi nafasi hivyo amekaba kila mahali hamana upenyo. Mnasali mumpaye raisi kilaza ili mjitanue na akili na akili zenu finyu
 
abiria wanamwambia dereva tanki la gari linavujisha mafuta,
yeye kakazana kuangalia mbele tu alafu maskini aliweka lita tano tu...
embu ngoja tuone labda hili lori linatumia pia na upepo...:D
 
Daah...Prezdah yupo makini ktk yake...ni heriii aendelee kusimamia...lingine nasikia hela imeanzaa kuachiwaa tusubiriii.
Kumbe unajua kama kabana pesa miccm aisee sasa mlikuwa mnabisha nini,eti hela zipo shambani pigeni kazi .leo hii mnaproove wenyewe jamaa anaachia pesa
 
Ambaye hataikumbuka ni marehemu peke yake.hata yeye atakumbuka jinsi alivyoliza wananchi kwa muda huu mfupi
 
Back
Top Bottom