Lancashire
JF-Expert Member
- Sep 20, 2014
- 14,062
- 10,354
Nawatakia heri wafanyakazi wote.
Mh. Rais nachukua fursa hii kukumbusha tu tangu uingie madarakani baada ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli haujaanzisha mradi wowote mkubwa wa kimkakati. Kazi inaendelea kukamilisha miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na marehemu Magufuli ambayo ni ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme SGR , Bwawa la umeme la mwalimu Nyerere, Ujenzi wa vivuko, madaraja pamoja na miradi mingine midogo midogo.
Nakukumbusha tu kuwa mpaka sasa unatembelea nyota ya marehemu John Pombe Joseph Magufuli. Unahitaji kuweka alama yako. Aidha nikupongeze kwa kuwaongezea watumishi mishahara, kujenga madarasa, kuongeza vifaa tiba na ujenzi wa vituo vya afya. Watanzania bado tunakusubiri.
Nakutakia utekelezaji mwema.