Kenya 2022 Pongezi kwa Rais Samia kuwa 'Neutral' kwa Uchaguzi Mkuu wa Kenya. Pole kwa Museveni na Kagame kwa 'Kumsapoti' anayeenda Kuangushwa

Kenya 2022 General Election

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,050
110,067
System ya Tanzania ilishausoma mapema Mchezo na kujua kuwa Ruto ataenda (na mpaka sasa GENTAMYCINE nasema ameshashinda) na Kumshauri Mama kutoonyesha Upande wake Wowote kati ya Ruto na Odinga.

Nazilaumu mno Systems za Uganda na Rwanda kwa Kukurupuka kwao na kudanganywa na Rafiki yao Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta kuwa Mtu anayemtaka Raila Odinga ndiyo atashinda na wao Marais Museveni na Kagame Kuingia 'Kichwakichwa' na waziwazi huku Wakijiamini wakisema wanamuunga mkono Raila Odinga.

Mpaka muda naandika huu Uzi ni kwamba asiyetakiwa na System ya Kenya na Adui Mkuu wa Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta Mgombea na aliyekuwa Makamu Rais William Ruto ameshashinda huu Uchaguzi.

Kinachofanywa sasa na System ya Kenya kwa Kushirikiana na Watu wa IEBC (Tume ya Uchaguzi Kenya ) ni Kumuibia Kura Mshindo William Ruto na kumpa Raila Odinga Ili atangazwe Mshindi.

Na endapo Mbinu hii itaonekana ni Hatari (Haifai) na Watu wa System ya Kenya kwa labda Kuhofia italeta Machafuko makubwa kinachoenda Kufanyika (Kufanywa) ni Kulazimisha 'Kubalansi' Matokeo ili kuwe na Marudio ya Uchaguzi na waweze Kumpiga (Kumuibia) vizuri Hustler William Ruto anayeonekana Kukubalika zaidi na Vijana hasa Wasio na Ajira na Wenye Maisha Magumu ya Kiuchumi.

Na karma kutakuwa na Marudio ya Uchaguzi huu basi bado Rais Uhuru Kenyatta atatakiwa kuwa Madarakani kwa Siku 90 (takriban Miezi Mitatu) na MImi GENTAMYCINE namshauri Hustler William Ruto kuwa kama anajipenda basi afanye kila awezalo ndani ya Siku hizi 90 asiwe Kenya na kama akiwa Kenya basi ajitahidi awe na Ulinzi mkubwa na mkali kwani najua nini Kitajaribiwa kufanywa Kwake ili kumdhoofisha au kumuua Nguvu kwani tayari System ya Kenya haimtaki kwakuwa imeshajua kuwa Ruto akiwa Rais wa Kenya ataanza Kulipiza Kisasi kwa Adui yake Mkuu Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta na pia atataifisha Mali zake nyingi na 'Kumpurula' kila Kitu Uhuru Kenyatta ambaye siyo Siri kuanzia Marehemu Baba yake na hata Yeye wameiibia mno Kenya ( hasa Ardhi ) na Wamejitajirisha sana kwa kuwa na Mali nyingi Ndani na Nje ya Kenya.

Pongezi nyingi tu Kwako Rais Samia.
 
Punguzeni mahaba na muuface ukweli kwamba Raila Odinga ndiye Rais mtarajiwa wa Kenya.

Screenshot_2022-08-11-07-50-09-285_com.android.chrome.jpg
 
Ahaa haaaah mtaani wangu bhana, unajua sana kucheza na akili za watu. Umejiweka ktk position ambayo utakuwa mshindi, yaani kama Agwambo, Baba akishinda basi kaiba kura. Usisahau huyo Hussler Ruto ni mafia vilevile, hashindwi kitu hata kuiba ana uwezo kwani naye ni 'Sonko', Mdosi ile mbaya. Pia swala la ukabila linambeba kwani anatoka kwenye Jamii ya Karenjin yenye watu wengi sana. Na huku Wakikuyu wakimpa support kwa vile running mate wake ni Mkikuyu. Vyovyote vile lolote linaweza tokea. Ila sisi wa kanda ya ziwa tungependa 'Omugaya' Raila ashinde kwani ana unasaba zaidi na ndugu zetu wa Rorya.
 
Mkuu hakuna anae kuchukia. Wewe ni kivutio ndio maana tunapenda kusoma.post zako.

Halafu wakurya hawakimbiliagi polisi mkuu. Kwa kukimbilia kwako polisi ume wa aibisha Wana mara wenzako.

Wewe hupendi challenge kumbe?

Anyways mada yako uliyo andika haina mashiko.

Unaweza kuweka uthibitisho kwamba Kagame na Museveni Wana msapoti Raila?

Hujui unafanya jambo la hatari sana kuwazushia viongozi wanao heshimika kama Kagame na Museveni?

U put jf into jeopardy kwa kuandika tuhuma za uzushi uzushi dhidi ya viongozi wanao heshimika

Acha utoto mkuu
 
Mkuu hakuna anae kuchukia. Wewe ni kivutio ndio maana tunapenda kusoma.post zako.

Halafu wakurya hawakimbiliagi polisi mkuu. Kwa kukimbilia kwako polisi ume wa aibisha Wana mara wenzako.

Wewe hupendi challenge kumbe?

Anyways mada yako uliyo andika haina mashiko.


Unaweza kuweka uthibitisho kwamba Kagame na Museveni Wana msapoti Raila?

Hujui unafanya jambo la hatari sana kuwazushia viongozi wanao heshimika kama Kagame na Museveni?

U put jf into jeopardy kwa kuandika tuhuma za uzushi uzushi dhidi ya viongozi wanao heshimika

Acha utoto mkuu
 
Kwenu Uongozi wa JamiiForums huyu Mtu hajaanza leo kuwa na tabia ya Kunichokoza na kupenda kwa Makusudi Kuharibu Mtiririko wa ama Threads zangu au Posts zangu hapa JamiiForums.

Yeye anachojua ni Kunidhihaki na kwa Makusudi kabisa Kunichokoza ili nihamaki na nijibizane nae kwa Lugha ya Ukali ili Moderators wenu wakiona wanipe BAN kitu ambacho Yeye na Watu wa Kundi lake wenye Chuki zisizo na Kichwa wala Miguu na Mimi ndicho wanakitaka Kutwa.

Na kinachonishangaza hasa ni Kitendo cha Members hapa Kumchekea na Kufurahia Uchokozi wake na Dhihaka zake za kila mara dhidi yangu kwa Kumnyamazia ila GENTAMYCINE nikiamua tu Kupambana nae kwa Lugha niijuayo Mimi ambayo inaumiza zaidi ndipo utawaona Wao ( Members ) wengi Wanafiki wakiongozwa na Tate Mkuu na Bila bila wanajitokeza Kunilaumu na Kuhoji kwanini namjibu Kiukali ila ninapokuwa Nachokozwa na Nadhihakiwa nae huwa hawasemi Kitu na wala hawamsemi.

Kilichonishangaza zaidi na ambacho kila Siku nasema hapa kuwa huyu LIKUD ni Mmoja wa Moderators na pia anasapotiwa na baadhi yao ni kwamba Juzi tu tumetoka Kujibizana nae kwa Maneno Makali na siyo ya Kupendeza na nina uhakika Moderators waliona hilo Tukio na walijua kabisa kuwa Yeye ni Mchokozi na amekuwa na tabia ya kufanya hivyo Kwangu kila Siku hapa JamiiForums walichokifanya Moderators ni Kufuta zile Posts zetu za Majibizano yetu Makali na Kumuachia hadi Leo tena ameibuka na Utamaduni wake ule ule wa Kunichokoza.

Narudia tena na nina uhakika kuwa kuna Kikundi cha Watu ( Members ) hapa tena huenda wanasaidiwa ( Wanasapotiwa ) na Moderators ( baadhi ) kwa Roho zao Mbaya na Chuki Kwangu kutokana na Uwasilishaji wangu wa Kipekee wa Mada, Mvuto na Umaarufu wangu umekuwa ni Chukizo Kuu Kwangu GENTAMYCINE hivyo waneanzisha Mkakati Maalum wa Kunichokoza na Kunidhihaki kwa Makusudi ili Nihamaki ( kwa kujua nina Hasira za Karibu ) na Kuwajibu kwa Maneno yangu Makali ili Mada zangu ziwe zinaharibika Kimaudhui na ziwe Chafu ( kwa kujaa Majibizano yetu ya Lugha Kali ) na haraka sana GENTAMYCINE nipigwe BAN jambo ambalo ndilo wanalitaka liwe linanyika ( linafanywa ) dhidi yangu Kutwa hapa Jamiiforums.

Hata katika hii Post ambayo Mimi nimechangia tu kwa Mtazamo wangu kama walivyofanya Wengine ila amekuja tena Kunichokoza na Kunidhihaki ili nihamaki na tujibizane kwa Maneno Makali ili Lengo lake litimie na ninyi Moderators mkasirishwe nami kisha haraka mnipe BAN za Mwezi au Miezi Mitatu Mitatu kama ambavyo mmekuwa mkinipa na Mkakati wao Maalum dhidi yangu Utimie.

MImi ni Mvumilivu sana na mno halafu sina Unafiki wala Uoga na mpaka leo ( Usiku ) huu mnaona nimeandika hiki ( hivi ) jua nimechoka. Na asidhani kuwa kwa Kunichokoza na Kunidhihaki Kwake hivi anaweza Kushindana nami kwa Vita ya Maneno Makali ila nimeamua tu kuwa Mstaarabu kwa Kutomjibu vile anavyotaka na Kukusudia kwa Kuwaheshimu Members na kwa Heshima ya huu Mtandao ambao wengine umetusaidia Kutupa Maarifa na Kutukomaza zaidi Kifikra japo kwa Wengine umewasaidia Kuwaonyesha jinsi walivyo Majuha na Wendawazimu kwa Kuwekeza zaidi muda wao kwa Kunishambulia, Kunichokoza na Kunidhihaki GENTAMYCINE utadhani kuna chao chochote nilichokula au nina Deni nao.

Na namalizia kwa kusema huyu huyu Mtu hana tu hii ID Moja tu bali nina ID's zake zaidi ya Nne ( 4 ) ninazozijua ambazo kutokana na Upumbavu wake huwa ananishambulia, ananichokoza na kunidhihaki kwa Lugha hii hii Moja inayofanana. Na kuna Siku alinichoko:a Kimakusudi na nilipomjibu Vikali akaniambia ( narudia akaniambia ) atanipiga BAN na kweli ndani ya muda mchache tu nikapigwa hiyo BAN.

Mwisho naomba hii Post yangu ya Malalamiko kumhusu huyu Member isifutwe kwani kumekuwa na tabia ya pale tu GENTAMYCINE nikilalamikia Jambo hapa na nikimtagi ( Tag ) JamiiForums Founder Maxence Melo na huyu Cookie upesi sana hiyo post yangu inafutwa na sijui huwa ni kwanini inafutwa.

Posts za huyu Member LIKUD na Wengine wanaonichokoza, Wanaonidhihaki na Wanaonishambulia Kutwa hapa huwa zinaachwa na hazifutwi, ila nikiwa najibu Mapigo kwa Maneno yangu Makali au nawataja hawa akina Maxence Melo na Cookie haraka unaona post yangu inafutwa.

Na kila mara nasisitiza hapa JamiiForums kuwa kama unaona HUNIPENDI au HUNIKUBALI kwa namna yoyote ile GENTAMYCINE na Kwako Mimi sina THAMANI yoyote ya Kiuwasilishaji basi cha kufanya ni rahisi sana cha Wewe kuamua tu KUNIBLOKU ( IGNORE ) ila cha Kushangaa ni kwamba 99% ya Wanaojinasibu Kutwa hapa Jamiiforums kuwa WANANICHUKIA na HAWANIPENDI ndiyo hao hao Wanaoongoza kwa KUNIFUATILIA, KUNISOMA na hata baadhi yao ni 'FOLLOWERS' wangu Jambo ambalo huwa sielewi ni kwanini. Hivi Logically Yule unayemchukia unaweza ukapoteza muda wako 24/7 Kumfuatilia? Hili kama siyo tatizo Kubwa la Akili linalowakabili litakuwa ni nini tena? Wao wameshaona Mimi nikihangaika nao au hata kupoteza muda wangu Kuwasoma na hata tu Kuwafuatilia?

Kama mnamtuma semeni tu nijue.

Inakera.

Cc:. Moderator, Active, JamiiForums, Paw, Cookie and JamiiForums Founder Maxence Melo

Kama Kawaida yenu na nilikitegemea Jana Usiku baada ya Kuandika post hii hii haraka sana mkawahi Kuifuta na Kufuta comment yake LIKUD na najua hata hii nayo mtaifuta muda si mrefu ili Kumlinda na Kuonyesha Kufurahia Kwenu anavyonichokoza, anavyonidhihaki na anavyonishambulia Kutwa hapa Jamiiforums. Na kamwe sitochoka Kuwalaumu na Kuwalalamikieni juu ya hili na huyu Member.
Mtani acha ufalla unajitetea kama wa kike ...acha mara moja wewe wakiume alaaa🤣
 
Odinga kuwa Rais maana yake nchi iko mikononi mwa Kenyata, Odinga hana akili za kuiongoza Kenya bali kinachofanyika ni kuwafurahisha wajaluo na kubalance mambo. Mwisho wa siku Odinga atakuwa ceremonial tu na gizani atakuwepo Kenyata.

Nakuunga mkono Genta, kama system itacalucate na kuona kumtangaza Odinga hali inaweza kuwa mbaya basi kitakachofanyika ni maridhiano na Odinga anaweza kuwa makamu huku Ruto akiwa mwenyekiti.
 
Mods wa humu kuna watu wanaamua kuwalinda kwa makusudi ,hata mimi kuna member Kazi yake ilikuwa kutafuta kila post yangu kutoa dislike na pamoja na kucomment matusi tena makubwa au kuweka picha chafu akicomment post zangu cha ajabu mods walikua wanaacha tu bila kufuta na mara moja wakiona lugha kali zaidi wanafuta tu bila kumuadabisha muhusika.

Mimi nikaamua kumpuuza kutomjibu kwa chochote sasa hivi amechoka na kuiacha kampeni yake ya kunidhalilisha kwa kuona simpi ushirikiano.
Dini imekukaa,jibu ni kuuchuna tu😘
 
Back
Top Bottom