Uchaguzi 2020 Polepole: CHADEMA walichapisha kura feki ili kuvuruga Uchaguzi Mkuu

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,844
15,364
Amani iwe nanyi

Mkuu wa idara ya itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi, shujaa Humphrey Polepole wakati akijibu swali la kukamatwa kura feki huko Kawe na baadae kuchomwa moto na wananchi amesema makaratasi hayo ya kura feki yalichapishwa na CHADEMA na baadae wakayasambaza wenyewe kwenye vituo vya kupiga kura na kisha wakayakamata wenyewe na kuyachoma moto wenyewe kwa lengo la kuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka huu!!

Polepole amehoji kama hizo ni karatasi kutoka NEC kwa nini wazichome moto? Kwa nini CHADEMA hizo kura feki hawakuzipeleka polisi kwa uchunguzi?

Hayo mabegi ya kura feki kwa nini aliyekuwa nayo walimkamata na kumwachia?
 
Eti shujaa hata Makonda alikuwa shujaa, tatizo mnaharisha halafu mnasahau kuchamba, hivi mnawafanya Watanzania vipofu?

uchaguzi mmeuvuruga na nina hakika wabunge wenu mliowapachika kama uyoga nao watakufa kama uyoga

Msije mkasema mmeuliwa maana kukataliwa nako kubaya.
 
Huu ni upuuzi sana na uongo wenye laana!

If and only if ilikuwa kweli, basi tuna mifumo ya kiusalama wa hovyo sana.

Huu ni upuuzi naufananisha na upuuzi wa yule kigogo wa Takukuru aliyesema masuala ya rushwa ndani ya ccm kinaachiwa chama kishighulikie? Serious?

So kesho red brigade na green guard wakitwangana wataachiwa wamalizane kivyama?

Mungu atunusuru na hawa wafia vyama.
 
Na kuna watu wanamuamini hahahaha! Human being's stupidity has no boundary.

CCM hua wanaona wananchi kama mazezeta flani vile, wanatamka ushenzi all the time, lile jinga jingine lilisema eti internet kilichotokea ni tatizo la mitambo tu sio kwamba wamezima kwa sababu ya uchaguzi,
 
Chadema walitoa wapi mihuli yamoto inayopatikana NEC?. Nakama nikweli kwa nini waliokamatwa police haikuwachukulia hatua hata kama ni CHADEMA wenyewe, na je kwa nini mwenyekiti wa tume alisema hakuna kura fake zilizokamtwa?.

Tukutane kesho tarehe 2 barabarani, hii ninchi yetu sote, nawala si ya ccm peke yao.

Una umri gani?
Labda tuanze na hilo.
🦁🦁🦁
 
Polepole aendelee kusema halafu walivyochapisha wakaweka tiki kwenye majina ya wagombea wa CCM kwa ngazi zote.

Polepole sasa amekuwa kama katuni, anajiropokea tu ilimradi asikike, binafsi nafurahi sana kwasababu sauti za wizi wa kura zimeshafika lumumba na zinaanza kuwakera na wanaona aibu.
 
Kama upinzani uta acha kujitathmini na kuamini walishindwa kwa kuibiwa kura kamwe hawata weza kuishinda CCM. Ata leo hii uchaguzi ukirudiwa Upinzani hauwezi kupata Viti zaidi ya Vitano, upinzani ni dhaifu sana.
Aaaaaaaah hhhaaaa

Hii ni chocolate flavor

Niambie Top C ndani ya sharobaro record

Sikia Hiii.

Haya mapenz na ogopa sana mimi
 
Halafu walivyochapisha wakaweka tiki kwenye majina ya wagombea wa CCM kwa ngazi zote.

Polepole sasa amekuwa kama katuni, anajiropokea tu ilimradi asikike, binafsi nafurahi sana kwasababu sauti za wizi wa kura zimeshafika lumumba na zinaanza kuwakera na wanaona aibu.
Nia ni kuvuruga uchaguzi na kudanganya wananchi kuwa Ccm imeiba. Ndio maana mliweka tick kwa wagombea wa Ccm.
 
Back
Top Bottom