Points 10 za ujenzi: Hawa ndiyo wataalam muhimu wa ujenzi

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,099
1,886
Leo katika sikukuu hii ya wafanyakazi duniani, nimeona itakuwa ni vyema kujuzana juu ya wataalam muhimu katika katika tasnia ya ujenzi.

Hapa nalenga zaidi ujenzji wa Majengo madogo,yaani
  • Nyumba za chini mpaka ghorofa mbili
  • Frame za maduka
  • Zahanati
  • Shule
  • Majengo ya ofisi

1.AFISA MIPANGO MIJI
Kabla ya ununuzi wa eneo lolote ,hawa ndiyo hupanga na kuratibu mipango ya matumizi na maendeleo ya ardhi
  • Husanifu muonekano wa mji/jiji
  • Hubainisha matumizi ya ardhi katika maeneo husika (manispaa/miji/jiji)
  • Hutunga sheria za ujenzi

2.MSANIFU RAMANI
Hufanya kazi zifuatazo
  • Kusanifu ramani ya jengo lako.
  • Kuandaa maelezo ya kitaaluma juu ya hatua za ujenzi katika hatua husika na sehemu husika za jengo (specifications)
  • Ushauri kwenye matumizi ya eneo lako
Ukihitaji Msanifu: 0718315764 na 0715654227
0719873434

3.MHANDISI UJENZI
Huusika na kazi zifuatazo
  • Kuandaa michoro na nyara za mhimili
  • Kusimamia ujenzi
  • Hupima ubora wa ardhi ya eneo lako
Ukihitaji Mhandisi :+255759417051,+255765739115

4.MKADIRIAJI GHARAMA UJENZI/QUANTITY SURVEYOR
Katika mradi wako,unaweza muajiri ili afanye kazi zifuatazo.
  • Kukasirika gharama za ujenzi
  • Ukaguzi wa fedha na matilio matumizi (kwa wale mnaohisi kuibiwa na mafundi).
  • Kuandaa mikataba ya wafanyakazi wako wote.
Ukihitaji huduma : 0688232069, 0719688606

5.MHANDISI UMEME
Nao hufanya yafuatayo
  • Kuandaa ramani za mfumo wa umeme
  • Kuainisha matilio/vifaa ya kwenye umeme
  • Kuingiza mfumo wa umeme
Ukihitaji huduma : 0719885622 ,0623085454
+255758375940

6.FUNDI MABOMBA
  • Huandaa ramani ya mfumo wa mabomba ya maji safi na maji taka ndani na nje ya jengo
  • Huainisha matilio zinazohitajika na gharama zake
  • Huweka mfumo wa maji safi na maji taka katika jengo
Ukihitaji huduma : 0713669803

7.MSANIFU MANDHARI
Hujishughulisha na yafuatayo
  • Husanifu ramani ya muonekano ya mazingira ya jengo lako
  • Kusimamia ujenzi wa mazingira
Ukihitaji huduma:0626010945

8.MSANIFU WA MUONEKANO WA NDANI/INTERIOR DESIGN
  • Huandaa ramani za muonekano wa ndani wa jengo
  • Hupamba jengo na kulipa muonekano wa kipekee
  • Hupangilia rangi na matilio zinazopaswa kutumika ndani
Ukihitaji huduma : +255716015544

9.FUNDI MWASHI +MSAIDIZI+FUNDI GYPSUM
huusika na
  • Kubeba matilio na kujenga boma la jengo lako
  • Kujenga paa
  • Kujenga mashimo ya vyoo
  • Kuweka dari
  • Urembo
Ukihitaji huduma: +255628819698 (Gypsum),0715738625 ujenzi
+255686446497 ujenzi


.FUNDI SEREMALA + FUNDI VYUMA+ALUMINIUM
  • Huandaa Milango na madirisha
  • Huandaa sehemu za ngazi
Ukihitaji huduma : 0655309830
0654878672

10.MLINZI
  • Husimamia ulinzi wa mali za eneo la ujenzi
  • Huorodhesha watu wanaoingia na kutoka eneo la ujenzi
  • Huorodhesha mali zinazoingia na kutumika katika ujenzi.
Namba nilizo ziweke hapo ni wataalam/mafundi wenye uwezo haswa katika kutekeleza majukumu ya kazi zao.



Heri ya siku ya wafanyakazi...🙋‍♂️
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom