SI KWELI Picha ya Rais wa Senegal, Diomaye Faye akiwa shambani na mke wake

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Picha hii inadaiwa kuwa ya Rais Mteule wa Senegal, Diomaye Faye akiwa na mke wake.

JamiiCheck naombeni ufafanuzi maana nimewahi kuiona sehemu fulani sikumbuki ni wapi, lakini ilikuwa inamzungumzia mtu mwingine kabisa.

SI KWELI 212334566.jpg
 
Tunachokijua
Machi 28, 2024, Ukurasa wa Instagram wa Times FM ulichapisha picha inayodaiwa kuwa ya Rais mteule wa Senegal, Diomaye Faye akiwa shambani mke wake enzi hajawa Rais.

Picha hii iliambatana na ujumbe unaotoa nasaha za kuheshimiana kama binadamu pasipo kujali hali zetu za maisha ya sasa kwani hatujui mbeleni itakuwaje.

"Rais mteule wa Senegal,Diomaye-Faye akiwa shambani na 'Festi Ledi' (mkewe), nyakati hizo. Ni Mungu pekee anayejua kesho yake mwanadamu yeyote. Heshimu kila mtu kwenye maisha kwa sababu huwezi kujua" walisema Times FM.

Hadi kufikia Aprili 4, 2024, chapisho hili lilikuwa limepara likes 4354 na comments 199.

Ukweli wa Picha hii
Utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google Image Search umeonesha kuwa pamoja na Times FM, kurasa zingine kadhaa za mitandao ya kijamii zilichapisha pia picha hii kwa nyakati tofauti.

Mathalani, picha hii ilichapishwa pia na ukurasa huu, huu, huu, huu na huu.

Pamoja na kuchapishwa siku tofauti, picha hii ilikuwa na maneno yenye ujumbe unaofanana, ukibainisha kuwa ilikuwa ni sura ya Rais wa Senegal na Mke wake.

Kupitia utafutaji huu, JamiiCheck imebaini kuwa picha hii siyo ya Rais Diomaye Faye kama inavyodaiwa.

Kwa muda mrefu, Picha hii imekuwa ikichapishwa ikiwa na maneno tofauti. Hata hivyo, inaonekana kuchapishwa mtandaoni kwa mara ya kwanza Novemba 21, 2021 na ukurasa wa Mtandao wa Facebook wa Zambia Reports ikiwa na ujumbe unaosema ni nani anaweza kufanya jambo hili na mpenzi wake?

Ukurasa huo ulichapisha tena picha hiyo Aprili 5, 2022.

Pia, Rais Faye ameoa wake wawili, Marie Khone Faye na Absa Faye lakini picha hii haitaji hata jina la mwanamke anayedhaniwa kuwa ni mke wake.

Kwa kurejea maoni ya wachangiaji wa picha, ni dhahiri kuwa picha husika haina uhusiano wowote na Rais wa Senegal na wanaoichapicha wanapotosha.
Asante kwa ka uchunguzi na ufafanuzi wakuu wa JamiiForums . Inasikitisha chombo cha habari cha Times FM kupotosha taarifa kwa lengo la kutafuta kiki uchwara. Tunaomba serikali, kupitia TCRA, iwafungie wapuuzi hawa kwa kuupotosha umma kwa maskusudi ili liwe fundisho kwa wapumbavu wengine wenye tabia kama hii.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom