Pesa uzalishwa wapi ?

idiomer

Member
Aug 15, 2012
53
18
Pesa au fedha Uzalishwa wapi??
Pesa ni chombo cha kubadilishana bidhaa na huduma katika ya watu.
Katika lugha ya kiswahili. Chombo hicho kina majina kaza wa kaza
Fedha, mshiko, chapaa, na mengine mengi
Baada ya kutafuta taarifa kwa kina hatimaye nimepata majibu ambayo wengi pia wanaweza kuwa nayo na pia zipi athari za kuzalisha fedha zako mwenyewe katika nchi yako pia ungana nami uweze kujua zaidi na zaidi.
Kwanini nchi nyingi hasa mataifa yanayoendelea Africa hazizalishi nchi zake zenyewe?
1. Kuwa na teknolojia duni. Uzalishaji wa fedha unapitia mchakato ambao utakuwa mgumu kwa mtu kuweza kuzalisha fedha bandia. Hivyo ukitaka kuzalisha fedha lazima uwe na mitambo ya kisasa sana. Kampuni kubwa la kuzalisha noti la muda mrefu De La Rue ambalo limeanza kazi hiyo karne ya 18 mpaka sasa lina uzoefu wa kutosha. Unaweza kuangalia video na kuona fedha zinavyozalishwa nimekuwekea link hapa.
View: https://www.youtube.com/watch?v=SKq1UnuVijA
2. Usalama ni sababu ya pili. Asilimia kubwa ya nchi nyingi hasa Africa suala la Rushwa ni kubwa sana. Hivyo kuzalisha fedha ni kutumia fedha. Lazima uwe na bajeti ya kuzalisha labda noti bilioni moja au zaidi kwa mwaka. Sasa ndugu yangu kama wewe unaweza kuweka zako hapo milion 100. Ila kama zinazalishwa UK na mtu ambaye hajawahi kufika hata Liberia na analipwa mshahara mzuri kazi yake anaifanya kwa uaminifu.
3. Siri. Makampuni haya ya kuzalisha fedha yana usiri mkubwa sana. Sasa asilimia kubwa sisi katika hali ya usiri inapotea kila kukicha juzi tu afisa mmoja katembea na house girl habari imesambaa kila kona. Afisa ametumbuliwa na Rais akiwa nje ya nchi. Sisi hatuna siri kabisa na hii inapelekea kutoaminiana. Mtu wa kuzalisha fedha kama ni ndugu yako yupo hapo kivukoni anampigia mchepuko wake leo tumezalisha kiasi cha noti milion 100 za elfu kumi kumi, Nami nimeweka zangu milion 10 za elfu moja moja usijali mambo ni kula bata.
4. Uchumi. Kwa uchumi wa nchi nyingi za Africa ni vema kuzalisha fedha nje. Kwa maana kampuni la fedha linatakiwa kuzalisha fedha kila mwaka sasa ukiwa na machine kwa ajili ya kuzalisha fedha zako tu ni hasara. Kuna kampuni zinazalisha fedha za nchi hata 20 hadi 50. Kwa hiyo ni biashara nzuri na zinaaminika. Hata BBC walijaribu kuuliza badhi ya kampuni je mnazalisha fedha za nchi ipi na ipi kampuni hizo hazikuweka wazi kwa sababu ya usalama. Sasa unaweza kuona jinsi gani wanalinda na kuheshimu kazi yao. Unaweza kusoma zaidi nimekuwekea link hiyo usome. Why countries print money outside their borders . Hizi ndio sababu kubwa nafikiri na pengine unaweza kuja na nyingine ukiwa na kiu ya kujua zaidi.
ATHARI ZA KUZALISHA FEDHA NJE YA NCHI.
1. Kupotea kwa thamani za fedha au kupata mtikisiko wa kiuchumi. Mfano Libya ilitoa zabuni ya kuzalishiwa noti zanye thamani takribani bilioni 900 na kampuni uingereza lakini fedha hizo zilichelewa na kusababisha kupata shida kidogo ya kiuchumi kwa nchi ya Libya. Japo baadae walizipata.
2. Fedha zinaweza kuchelewa na ni hatari kusafirisha fedha nyingi kwenye ndege kwa sababu wanaosafirisha nao wanakuwa wanazitaka.
Pengine watu wengi tunajua fedha za kila nchi zinazalishwa nchi moja , uswizi la hasha. Hapa si kweli Nchi kama USA na CHINA wanatengeneza Fedha zao wenyewe. Inakadiriwa USA hazalisha karibu noti bilioni moja kwa mwaka.

LAKINI PIA KUJUA FEDHA YENYE THAMANI ZAIDI AFRICA?.
Fedha ya Tunisia ndio fedha ambayo ina thamani kubwa kuliko fedha yoyote Barani Africa. Na Euro 1 = Tunisia Dinari 3.36. Us dollar 1 = Tunisian Dinar 3.15
Nchi ambayo fedha yako ina thamani ndogo sana barani Africa ni Sierra Leone. Ambayo 1 USD = 19,995 SLL. Sawa na kusema 1 USD ni sawa na 20,000 fedha ya siera Leoni. Katika nchi ambazo fedha zake zina thamani ndogo Sierra Leone nin ya kumi na katika kumi za mwisho Tanzania ni ya saba hivyo tukipambana tunaweza kutoka huku kama wenzetu Kenya.
Nchi hizo naziweka hapa uweze kuzitazama na pengine kabla ya kuziweka wewe unajua kama pengine mtanzania ndugu yetu Uganda kwa M7 ni kibonde wetu.
Kutoka Mwisho yaani thamani ndogo kwenda kwenye unafuu.
1. SIERRA LEONE
2. GUINEA
3. MADAGASCAR
4. UGANDA
5. BURUNDI
6. CONGO
7. TANZANIA
8. RWANDA
9. MALAWI
10. SOUTH SUDANI
Nchi Tano ambazo sarafu zao zina nguvu Zaidi. Tunisia, Libya, Morocco, Ghana na Botswana
Nchi gani imepoteza kiasi kikubwa cha fedha uwanja wa ndege zikiwa zinaletwa baada ya kuzalishwa ughaibuni na kiasi gani cha fedha kimeibiwa? Nchi nii ni Liberia imepoteza kiasi cha USD milion 104 kiasi hicho kimepotea katika mazingira ya kutatanisha uwanja wa ndege.
Kwanini India imesitisha ya zabuni yake ya kuzalisha noti nchini China? India ilisemekana kutaka kuingia mkataba na kampuni la kichina kutengeneza rupia ila kwa sababu za usalama na ugomvi wa kimipaka na China ikasitisha.
Mwandishi
CALVIN MMARY mmarycalvin@rocketmail.com ,
 
Wacongo wenyewe,hela zao wanaoza Kwanza .

Sasa sijui zinaingiaje kwenye mfumo halali !

Sorry kutoka nje ya mada.
 
Back
Top Bottom