SoC04 Pazia limekuwa kuukuu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Surgeon huyu

New Member
May 2, 2024
1
0
Safina Inayozama

"Ni majira ya saa 10 jioni kikao kinakaliwa cha kuweka mikakati wa maendeleo kwa miaka 5 hadi 25 ijayo, lakini kinachowashangaza wazee wa Kijiji cha Wafagiliaji Wanashangazwa na ongezeko la wazee kwenye kikao cha kujadili kesho yao huku vijana wasio wasomi wanaojishughulisha na shughuli zisizo rasmi wakiwa wamekaa viti vya mbele kabisa kuchangia maendeleo ya nchi yao. Wazee wakiwa katika hali ya butwaa na minong’ono ya hapa na pale wakilalama kwanini vijana walio na elimu kubwa za hapa na ng’ambo tena waliowasomesha Kwa gharama nyingi, wKiwa bize mitandaoni wakisutana na kushikana ughoni hawajafika kwenye kikao na hawahangaiki kulipambania taifa lao.

Mwenye mamlaka (anasimama) na kusema: “ kaeni kimya mimi ndiye mwenye hii nchi, naweza amuachochote na hamanifanyi chochote”. (Anataka kukaa, kisha anasimama tena Anatoa mwongozo)“Yule mwenye hoja za kulijenga taifa letu asogee hapa mbele, na waandishi wa hababri acheni kuandika unoko na uzushi”. (Waandishi wa habari wakiduwaa)

Kijana 01.

Anasimama kijana mmoja (anaonekana kama kijana wa mtaani), anakohoa kisha anawasalimu “nawasalimu kwa jina la nchi ya Wafagiliaji”, Wanainchi wanaitikia kwa miitikio mbalimbali wanasikika wazee wakisema “Ufagiliaji uendelee” Kijana 01. Ndugu zangu kwa maisha niliyoishi hapa duniani na kwa mvua hizi 28 nimeona mambo yafuatayo ambayo Viongozi wangu myaweke kwenye mipango ya muda mfupi au mrefu.

A; Kuwekeza kwenye vizazi (watoto). Serikali yetu inatakiwa kuweza katika watoto kuwajengea watoto uwezo mkubwa wa kuja kuwa matunda kwa taifa letu katika mambo yafuatayo; Elimu; Je elimu yetu inajibu Vilio vya Ukosefu wa ajira kwa vijana wetu, je inajibu uhitaji wa wafanyakazi wanaohitajika kwenye jamii yetu. Ni vyema masomo ya sanaa yakapunguzwa na tukaongeza masomo ya sayansi na teknolojia ili tuwe na vizazi vya kuunda dhana na sio watengenezaji dhana.

Bado hatujachelewa watoto kulelewa kwenye ndoto zao kwa kujenga shule na vyuo kulingana na ndoto zao, hakuna haja shule moja kuwa na sayansi na sanaa tena wanachangia walimu na madarasa tunaua ndoto. Vyuo na shule za sayansi na sanaa vitenganishwe, na mazingira yawe tofauti. Kuongeza Ufanisi na nguvu kwenye vipaji na talanta za vijana na watoto wetu. Kwa maisha ya sasa viapaji vimekuwa msaada mkubwa sana kupunguza ongezeko la Ukosefu wa ajira, hapa Yafanyike haya - Kujenga shule na vyuo vya vipaji angalau viwili au vitatu nchini kwetu, ili nchi yetu itoe wanamichezo machachari na wasanii wa viwango vya juu.

B; Mfumo wa kuendesha serikali yetu. (kitabu) “ Hapa wazee wanainuka na kupiga mayowe” anatulia kisha anasema, “Mfumo wa nchi ndio nguzo kuu ya uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wetu hivyo napendekeza ubadilishwe ili kila mwanainchi hapa ajivunie nchi yake, uongozi jiwe na mawimbi haufai, uongozi uliojaa nyasi na vichaka ni anguko la siasa za kweli na kikwazo cha maemdeleo, huleta mwanya wa mambo meusi na yasiyo na manufaa kwetu sote, kwasasa naona tunamfumo kichaka, watu wanaogopa hata kukatiza haufai, tubadilishe mistari na vituo kwenye kitabu chetu ili kila anayetuletea giza akutane na mwanga wa mionzi aungue afe.”

Wanapiga yowe wanakijiji ……kiongozi anasimama na kusema “ keleleni Wajinga nyie, manasadiki kushadadia maneno ya chuki haya”, huku akiwawageukia waandishi wa habari, “Ole wenu mrushe maudhui haya , tutawafuta…“ kijana anamaliza na kupigiwa makofi kama yote 2. Kijana 02. Anakohoa kisha anarusha dongo kwa vijana wenzake.anasema kwa sauti kali “Acheni kuwa makoti , kutwa kuwapamba viongozi nje na huku mnajua ndani ni mbwa mwitu , Tumekuwa wa ovyo sana ilitakiwa tuwe mfano na msaada kwa taifa letu”.

Kisha akaiomba serikali: “ Naomba serikali yangu vijana wapewe kipaumbele katika fursa za uwekezaji maana ndio chanzo kikuu cha kodi kwa rasilimali watu, taasisi za fedha za serikali zikae na vijana kwa ajili ya kuwapatia mambo yafuatayoKuwapatia elimu ya uwekezaji na fursa zilizopo. Kuwapatia mikopo rahisi na riba nafuu kwa vijanaVijana wanasimama kwa shangwe, wakipiga kelele “ tumekwama kwenye kilimo, hatuana kazi mijini, tunaishi kama makoti, kazi kusifia watu , tunahangaika , tupeni mikopo ya riba nafuuu……Mkutano wote unajawa nderemo na vifijo.

3. Kijana 03. Akiwa ameshikilia kamera yake, anasema “mimi kama mwandishi wa matukio nina langu jambo, sisi waandishi tuache kutumiwa na hao wenye mbawa, ila tujikite kutafuta taarifa sahihi ili tuwe daraja kati ya uongozi na wananinchi.
a) Tuongee ukweli daima wala tusinyamaze
b) Kamwe tusikubali kutumiwa na watu binafsi
c) Tuwafikie wanakijiji huko waliko,
d) tuandae makala zinazosaidia wanainchi kujua fursa za harakati za viongozi katika maendeleo. Watu ni kama hawajamuelewa kwasbabu hawajaon aumuhimu wa waandishi wa habari katika kuleta maendeleo zaid ya kuripoti matukio ( Elimu ya utambuzi inahitajika).

4. Mzee mmoja anasimama, Mkutano unatulia kwa kitambo wakisubiri hekima za mzee huyu Anakohoa kisha anaongeza yafuatayo kwa uchungu sana, ANASEMATangu nimezaliwa sijawahi ona vijana wa ovyo kama wa kizazi hiki. Wanashindwa vilabuni kila wakati, wanaingia makazini wakiwa wamelewa. Naomba sheria za uuzaji wa vileo zichunguzwe tuatakuw na nchi ijayo ya hovyo. Nchi inapoteza pesa kuhudumia vijana wadogo magonjwa ya figo na ini kisa unywaji hovyo wa pombe.

Tumesomesha vijana wengi tangu uhuru, ni wakati sasa wa kujifungia nchini kwetu na kuzalisha bidhaa nyingi, huku tukiagiza bidhaa chache toka nje . kama imeshindikana, basi tuwe mabingwa wa uuzaji wa mazao adimu duniani yanayopatikana tanzania, kama vile karafuu, kahawa, mkonge, mchele safi, kakao na madini tanzanite. Kuwa na mikataba ya uwekezaji yenye tija na maendeleo ya taifa, niwaombe wasomi wotesaidieni nchi yenu kuwa na uwekezaji wenye maendeleo kwa taifa letuNamalizia katika suala la Uwajibikaji na Uzalendo, watu wawajibike kulijenga taifa lao, Rushwa na ufisadi upigwe vita daima….kelele zinarindima mkutano mzima.

Wanainchi wakipiga Kelele “Uhuru wa kujieleza ndio chanzo cha uwajibikaji,” Mwenye Mamlaka anasimama na kusema “mmmhhh Mnajisumbua tu” Wanainchi wanapiga kelele tena “Uhuru wa vyombo vya habari ndio chanzo cha uwazi kiutendaji”Kelelel zinakuwa nyingi, Polisi wanaamua kuingilia kati na kunymazisha mkutano.Kikao kinafungwa huku haukuna muafaka hakika………………………
 
Mwenye mamlaka (anasimama) na kusema: “ kaeni kimya mimi ndiye mwenye hii nchi, naweza amuachochote na hamanifanyi chochote”
Hahahahaaaaaah 😁


; Kuwekeza kwenye vizazi (watoto). Serikali yetu inatakiwa kuweza katika watoto kuwajengea watoto uwezo mkubwa wa kuja kuwa matunda kwa taifa letu
Hakika, umenena tunajenga kuanzia chini kwenda juu. Na siku zote misingi ndiyo ya msingi. Mtoto wa miaka 1-7 ndiye anajenga mtu mzima aweje

kujenga shule na vyuo kulingana na ndoto zao, hakuna haja shule moja kuwa na sayansi na sanaa tena wanachangia walimu na madarasa tunaua ndoto. Vyuo na shule za sayansi na sanaa vitenganishwe, na mazingira yawe tofauti.
Hapa nina swali kwako, je tutajenga vipi umoja wa kitaifa ikiwa unasisitiza kila fani itengwe na wenzake. Maana hata mtu akiwa kiongozi atapaswa ku 'orchestrate' vikundi mbalimbali ili kufikia lengo. Je mtoa mada huoni kwamba itapendeza mtu akipata uzoefu wa kuishi watu tofautitofauti tangu mapema?


Mfumo wa kuendesha serikali yetu. (kitabu) “ Hapa wazee wanainuka na kupiga mayowe” anatulia kisha anasema, “Mfumo wa nchi ndio nguzo kuu ya uadilifu na uwajibikaji wa viongozi wetu hivyo napendekeza ubadilishwe ili kila mwanainchi hapa ajivunie nchi yake, uongozi jiwe na mawimbi haufai, uongozi uliojaa nyasi na vichaka ni anguko la siasa za kweli na kikwazo cha maemdeleo, huleta mwanya wa mambo meusi na yasiyo na manufaa kwetu sote, kwasasa naona tunamfumo kichaka, watu wanaogopa hata kukatiza haufai, tubadilishe mistari na vituo kwenye kitabu chetu ili kila anayetuletea giza akutane na mwanga wa mionzi aungue afe.”
Well said, perfecto. Yaani hakuna la kuongeza hapa.

Kijana 03. Akiwa ameshikilia kamera yake, anasema “mimi kama mwandishi wa matukio nina langu jambo, sisi waandishi tuache kutumiwa na hao wenye mbawa, ila tujikite kutafuta taarifa sahihi ili tuwe daraja kati ya uongozi na wananinchi.
a) Tuongee ukweli daima wala tusinyamaze
b) Kamwe tusikubali kutumiwa na watu binafsi
c) Tuwafikie wanakijiji huko waliko,
d) tuandae makala zinazosaidia wanainchi kujua fursa za harakati za viongozi katika maendeleo. Watu ni kama hawajamuelewa kwasbabu hawajaon aumuhimu wa waandishi wa habari katika kuleta maendeleo zaid ya kuripoti matukio ( Elimu ya utambuzi inahitajika).
Habari zote zingekuwa na dhima kuu ya KUJENGA NCHI YETU SAFI tunafanikiwa. Mimi sio msahaulifu. Ninakumbuka enzi za Magufuli hii ndiyo ilikuwa dhima kuu ya habari zote na mafanikio tulianza kuyaona, morali za wananchi zilienda juu sana.

Ni wakati sasa wa kujenga taifa kwa habari za kiuchunguzi za kujenga. Anayetangazq ubomoaji tu, naye ni sehemu ya wabomozi. Na anayesifia tu naye ni sehemu ya upotoshaji. Tunataka wanaojenga kwerikweri 🙅‍♂️

Nchi inapoteza pesa kuhudumia vijana wadogo magonjwa ya figo na ini kisa unywaji hovyo wa pombe.
Na ndiyo maana uchangiaji gharama(cost sharing) za matibabu usisitishwe kwa namna yoyote ili kuibakiza jukumu binafsi kwa afya (personal rwsponsibility, acountability)
 
Tumesomesha vijana wengi tangu uhuru, ni wakati sasa wa kujifungia nchini kwetu na kuzalisha bidhaa nyingi, huku tukiagiza bidhaa chache toka nje . kama imeshindikana, basi tuwe mabingwa wa uuzaji wa mazao adimu duniani yanayopatikana tanzania, kama vile karafuu, kahawa, mkonge, mchele safi, kakao na madini tanzanite. Kuwa na mikataba ya uwekezaji yenye tija na maendeleo ya taifa, niwaombe wasomi wotesaidieni nchi yenu kuwa na uwekezaji wenye maendeleo kwa taifa letuNamalizia katika suala la Uwajibikaji na Uzalendo, watu wawajibike kulijenga taifa lao, Rushwa na ufisadi upigwe vita daima….kelele zinarindima mkutano mzima.
Ahsante sana, umeliweka kiufasaha saana hili jambo.

SOKO, SOKO SOKO LA KIMATAIFA KWA BIDHAA ZETU.
 
Back
Top Bottom