Parachuchi kupukutika

bhakamu

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
798
774
Jamani nisaiidieni mwongozo nipulize dawa Gani maana miparachichi yangu inapukutisha matunda yangali machanga!
 
Nitumie kiwatilifu kipi kupunguza athari!
Kama ni organic farmer anahitaji kiwatilifu kilicho organic, lakini kama mchangiaji aliyesema yana stress za maji au joto ni kufuata ushauri wa experts.
 
Jaribu hii (VOEMA) orgn from south Africa kwene baadhi yamikoa kuna mawakala wao bei yake imechangamka kidogo lita moja 80kView attachment 2976962
20240429_173653.jpg
View attachment 2976963
View attachment 2976973
 
Jamani nisaiidieni mwongozo nipulize dawa Gani maana miparachichi yangu inapukutisha matunda yangali machanga!
Matunda kupukutisha maua kuna sababu kadhaa na utatuzi wake.
1. Lishe duni yaani ukosefu wa baadhi ya madini muhimu katika maua na matunda mfano calcium,Zinc,Boron na Potassium. Hizi mara nyingi zinawekwa kwa kupulizwa kwenye miti kutumia mashine na zinaweza kuwa organic au synthetic zipo zote. Hapa ndio chance ya tatizo huwa tunaweka 50%.

2. Wadudu,japo sio mara nyingi wapo wadudu wanaokula maua na matunda na kuyapukutisha na mara nyingi hawa huwa wanaleta magonjwa ndani yake hasa hasa ni wale sucking insect pests na Chewing insect pests mfano vidukari na panzi. Taadhali ichukuliwe. Hii inaweza kuwa kati ya 25-30%

3. Kiu ya maji au stress kwa maana kuna madini hayawezi kutembea kwenye mmea bila maji na ni muhimu katika hii hatua ya maua/matunda mfano ni Calcium. Maji sio kwamba unamwagilia mwagilia tu,elewa parachichi ni mti ambao una ubaguzi sana wa maji. Maji ya chumvi ni tatizo na jitahidi walau uweke Lita 20+ kwa wiki hadi 40. Kumantain usalama wa miti yako.
 
Back
Top Bottom