Operesheni Zinduka 14 - Alipo Hatupo, Tuliko Hayupo - Wasikilize na Waone Hawa

Mkuu MMK mi nadhani kuliko kupambana na Lowasa heri mgepambana na Mbowe aliyemleta,inashangaza hamdeal na Mbowe

Mkuu si unajua Dada yake kakosa u first Lady? make jamaa ni shemeji wa Dr
 
pole sana kwa mission impossible,hata usemeje ntampigia kura Lowassa japo mimi ni ccm
 
EL aka Jambazi Sugu hawezi kuwa rais wa tano wa nchi hii whatever the case, na ni wakati wa kuwashughulikia kina Mbowe et al ambao siasa zao ni za kimalaya. Wote wanaowadhulumu walipa kodi wa nchi hii ni lazima wachukuliwe hatua, hatuwezi kuwaacha wakafikiri sisi ni mpira wa kupigwa kule wanakotaka kila wanapochagua kufanya hivyo. As for Chadema kina kufa rasmi baada ya uchaguzi huu. Mwisho wa kulamba peremende umefika.
 
Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Mahojiano na mtangazaji wa BBC, Zuhura Yunus yamehitimisha kile ambacho viongozi wakuu wa CHADEMA walikuwa hawataki tukifahamu.

Lowassa is good for nothing, incompetent, unfunctional, corrupt and weak!

Eti kupambana na ufisadi ataanzisha one stop centre.

Eti Ufisadi wa viongozi serikalini itabidi akae na kutafakari jinsi ya kupambana nao. Mpaka apewe Urais ndiyo atafahamu njia ya kupambana na ufisadi wa viongozi.

Nadhani hafamu hata maana ya ufisadi au tofauti ya rushwa na ufisadi.

Amesema hawezi kusema kama alishauri serikali kuanzisha elimu bure kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu! Hana kumbukumbu!

Lowassa ni msanii!

Kumbuka kiapo, "sitatoa siri za baraza la mawaziri."
 
Last edited by a moderator:
Mkuu si unajua Dada yake kakosa u first Lady? make jamaa ni shemeji wa Dr

Mi nimeshangaa sana hata Dr slaa alipofanya press alimchafua sana Lowasa,huku anamsifia mbowe as if Lowasa aliingia kwa nguvu chadema,hawaongei chochote kuhusu mbowe na viongozi wengine kama kina lissu lakini wao wanamchafua tu lowasa ambaye alikuja,au aliletwa na kina mbowe,hapo kosa lingekuwa la uongozi wa chadema hasa mbowe,wangedeal na mbowe siyo lowasa
 
Tatizo la wanajiita wachumbuzi ni kuwa mbali na hao wanaowachambua. Unaongea kama kijana wa Masaki
 
Mi nimeshangaa sana hata Dr slaa alipofanya press alimchafua sana Lowasa,huku anamsifia mbowe as if Lowasa aliingia kwa nguvu chadema,hawaongei chochote kuhusu mbowe na viongozi wengine kama kina lissu lakini wao wanamchafua tu lowasa ambaye alikuja,au aliletwa na kina mbowe,hapo kosa lingekuwa la uongozi wa chadema hasa mbowe,wangedeal na mbowe siyo lowasa

Mkuu hapa tunamjadili mtu anayetaka kuwa mkuu wa nchi ......
 
Bi'ismihi ya Jabbaru, kujibu huu wajibu,
wasokujua qaharu, vema ni bora watubu,
wanazifanya kufuru, kukushiriki Wahhabu,
sijitie ubahau, na kujitoa akili.

Ulumbapo na walumbe, uchunge usikuvuke,
vina sio upelembe, kutunga povu utoke,
ushairi sio pombe, hata ukutoke ute,
sijitie ubahau, na kujitoa akili.

sijitie ubahau, na kujitoa akili,
ungezijua nahau, sio kusuka ukili,
mapenzi hayasahau, uitimize kauli,
sijitie ubahau, na kujitoa akili!

kula mtenda hutenda, hapo ndipo kisirani,
kibovu sana kupenda, jaa kusifu machoni,
twajua unakoenda, rushwa iko mkononi,
sijitie ubahau, na kujitoa akili,

nalikwamba tangu kale, zikichopoka chutama,
umebaki vilevile, wana wanakutazama,
uliandika tangu kule, huna jipya huna jema,
sijitie ubahau, na kujitoa akili.

twakujua zakutosha, toka lini hamnazo?
alivoja jifurusha, wajua huna mawazo,
ushemeji hupofusha, ukageuka kikwazo,
sijitie ubahau, na kujitoa akili.

kuishi ukimbizini, ukajisifu jabali,
chakula kutia inzi, huku ukitakabali,
majisifu makunyanzi, hayo hatuyakubali,
sijitie ubahau, na kujitia akili.

kura zetu kwa Lowassa, na wa UKAWA WABUNGE,
sana utajipapasa, bora hata ujinige,
kamba upige msasa, hata bure ujinyonge,
sijitie ubahau, na akili kujitoa.

namshukuru maulana, kunipa huu wasaa,
kuwaona wenye lana, wenye akili usaa,
nilishasema hapana, sio siku hata saa,
sijitie ubahau, na akili kujitoa.

wenzo waenda na pingu, wewe waja na ushanga,
siasa sio virungu, mungeacha kujipinga,
msijitie uungu, hawako mtaovunga,
sijitie ubahau, na kujitoa akili.

usijelazimu watu, watende ukitakacho,
wanajua wao utu, si kile ukipatacho,
twaijua yako kutu, hatutaki chako hicho,
sijitie ubahau, na kujitoa akili.

mbele sana sitokwenda, wakati nikamaliza,
sauti kama za punda, sana tutazisikiza,
makosa sana kupenda, akili ukatoboza,
sijitie ubahau, na akili kujitoa.
 
Mamamaye! U-mnikulu ndo ukawa umeota mbawa vile! Pole sana kiongozi ulitamani sana na wewe ukale shavu pale magogoni, lakini bahati haikuwa upande wako!! Umechelewa sana maana raia tayari walishaamua!! Ni Lowassa tu hiyo trh 25/10/2015.
 
EL aka Jambazi Sugu hawezi kuwa rais wa tano wa nchi hii whatever the case, na ni wakati wa kuwashughulikia kina Mbowe et al ambao siasa zao ni za kimalaya. Wote wanaowadhulumu walipa kodi wa nchi hii ni lazima wachukuliwe hatua, hatuwezi kuwaacha wakafikiri sisi ni mpira wa kupigwa kule wanakotaka kila wanapochagua kufanya hivyo. As for Chadema kina kufa rasmi baada ya uchaguzi huu. Mwisho wa kulamba peremende umefika.
Wacha1, hii itakuwa part time.,.. Ni Njaa au ni nini mkuu. Ufanani na Lumumbafc.

Still nakuadmire
 
Last edited by a moderator:
Ila unapomjadili lowasa na unaonyesha ubovu wake bila kumjadili aliyemleta msingi wa hoja yako unaweka wapi

Huyo aliyemleta tulimsema hatua za awali kabisa.....baada ya uchaguzi tutajua mbivu mbichi ....kwasasa acha tuwajadili wagombea ambao wanataka ukuu wa nchi ....
 
Ila unapomjadili lowasa na unaonyesha ubovu wake bila kumjadili aliyemleta msingi wa hoja yako unaweka wapi

Afadhali ww umeprove kua Dr slaa hakumleta huyo fisadi hapo CDM.....nakushauri ufuatilie OZ 2,3,4 utaona jinsi MMM alivyompa za uso political entrepreneur Mbowe.....
 
Afadhali ww umeprove kua Dr slaa hakumleta huyo fisadi hapo CDM.....nakushauri ufuatilie OZ 2,3,4 utaona jinsi MMM alivyompa za uso political entrepreneur Mbowe.....
Mkuu bado sijaprove kwamba Dr slaa hakuhusika na sijui kama alishiriki au hakushiriki kumleta lowasa,but how comes kamati kuu yote ya chadema yeye ndo ajiengue,pia inawezekana ni mroho wa madaraka,wenzake wameafiki akaona yeye hasimamishwi kuwa mgombea heri awakomoe kwa kujiengua ili aue chama.
 
Magufuli anafaa Lowasa anakubalika, Magufuli ni maziwa ya mgojnwa (nchi yetu inaumwa magonjwa mengi), Lowasa ni pombe (itakayolilewesha taifa letu life likiwa usingizini). NI HIARI YETU WAPIGA KURA TUMPE MGONJWA MAZIWA AJENGE SIHA YAKE AU TUMPE POMBE ALALE ASISIKIE MAUMIVU NA KUFA.
Lowassa hata akiwa ICU nampa kura yangu
 
Waachwe wananchi wachague mtu wamtakae. Wewe MM usitupangie sisi wapiga kura we beba box tu huko ya huku hayakuhusu
 
Back
Top Bottom