Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,865
- 4,693
Mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta athari katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha, baada ya baadhi ya nyumba kufunikwa na kuzingirwa na maji, hivyo baadhi ya wananchi kukosa makazi.
Kutokana na changamoto hiyo, wengine wamelazimika kwenda kutafuta nyumba za kupanga, wengine wakienda shule na baadhi kuhamia kwa ndugu na jamaa zao.
Akipotafutwa na Mwananchi Digital kuzungumzia athari za mvua hizo, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dadi Kolimba amesema yuko msibani na kwamba atatoa taarifa baadaye.
Mvua hizo zilizonyesha tangu wiki iliyopita zinatajwa kuathiri maeneo mbalimbali wilayani humo, ikiwemo Kata ya Qurus na Karatu.
Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Aprili 16, 2024, baadhi ya wananchi wameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia kwa haraka kabla madhara hayajawa makubwa.
Jeneth Mfanya, mkazi wa Mtaa wa Bwawani amesema amelazimika kwenda kuupanga kutokana na nyumba yake kujaa maji.
Amesema mvua hiyo iliyoanza kunyesha tangu wiki iliyopita imeleta athari kubwa kwao, kwani mbali na nyumba yake kujaa maji, pia saluni aliyokuwa anaitegemea kama kitega uchumi nayo imejaa maji na amefanikiwa kuokoa vifaa vichache.